Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!

wakuu wapya wa wilaya


Kikwete afyeka
Wakuu wilaya 51
·      Ateua wengine wapya 70
·      Wamo wana habari saba
·      Pinda amkejeli aliyejiuzulu


Na Charles Misango

RAIS Jakaya Kikwete amewafyeka wakuu wa wilaya 51 kwa sababu mbalimbali, zikiwemo za kinidhamu, katika uteuzi mpya uliotangazwa jana na kuwaingiza wana habari saba kuwa miongoni mwa wakuu wa wapya wa wilaya.

Kadhalika, serikali imemkejeli aliyekuwa Mkuu wa Wialaya ya Mbozi mkoani Mbeya, Kimolo ambaye hivi majuzi alitangaza kujiuzulu wadhifa huo kwa kile alichodai kutoridhishwa na mwenendo wa utendaji wa serikali ngazi ya mkoa na wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Akitangaza uteuzi huo mbele ya waandishi wa habari jana, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kati ya wakuu wa wilaya 114, waliobaki  katika nafasi zao ni 63 na wengine wakienguliwa kwa sababu nyingi za msingi zikiwemo nidhamu mbovu, ugonjwa na kustaafu.

Bila kutaja majina ya walioachwa, Pinda alitangaza majina 70 ya wakuu wapya, wakiwemo wanahabari wakongwe. Hao ni pamoja na aliyekuwa meneja wa kampeni wa Kikwete katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge mwaka 2010, Muhingo Rweyemamu anayekwenda wilaya ya Handeni.

Wanahabari wengine ni Naibu Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Jacqueline Liana anayekwenda kuwa mkuu wa wilaya ya Magu.

Wanahabari wengine ni, Seleman Mzee Seleman aliyekuwa kituo cha televisheni ya Taifa, anayekuwa mkuu wa wilaya ya Kwimba, Novatus Makunga aliyekuwa mwakilishi wa ITV, Arusha ambaye sasa atakuwa mkuu wa wilaya ya Hai, watangazaji wawili wa zamani wa Radio Tanzania, Ahmed Kipozi, anayekwenda Bagamoyo na Suleiman Kimchaya ambaye pia amewahi kuwa mbunge, anayekwenda Tabora. Wa mwisho katika safu ya wanahabari ni Lucy Mahenga ambaye pia ni Mbunge viti maalum (CCM) atakayekuwa Uyui.

Mboni M. Mgaza(Mkinga) Hanifa M. Selungu (Sikonge) Christine S. Mndeme(Hanang) Shaibu I. Ndemanga      (Mwanga) Chrispin T. Meela (Rungwe) Dk. Nasoro Ali Hamidi (Lindi) Farida S. Mgomi (Masasi) Jeremba D. Munasa (Arumeru) Majid Hemed Mwanga(Lushoto) Mrisho Gambo (Korogwe), Elias C. J. Tarimo     (Kilosa) na Alfred E. Msovella (Kiteto). Wengine wapya ni Dk. Leticia M. Warioba (Iringa) Dk. Michael Yunia Kadeghe (Mbozi), Mrs. Karen Yunus (Sengerema), Hassan E. Masala (Kilombero), Bituni A. Msangi (Nzega), Ephraem Mfingi Mmbaga (Liwale), Antony J. Mtaka         (Mvomero), Herman Clement Kapufi (   Same) na  Magareth Esther Malenga (Kyela)

Wapo pia Chande Bakari Nalicho (Tunduru), Fatuma H. Toufiq (Manyoni) Seleman Liwowa (Kilindi), Josephine R. Matiro (Makete),       Gerald J. Guninita (Kilolo) Senyi S. Ngaga         ( Mbinga), Mary Tesha (Ukerewe), Rodrick Mpogolo (Chato), Christopher Magala, (Newala), Paza T. Mwamlima (Mpanda), Richard Mbeho (Biharamulo), Joshua Mirumbe (Bunda), Constantine J. Kanyasu (Ngara), Yahya E. Nawanda       (Iramba), Ulega H. Abadallah(Kilwa), Paul Mzindakaya, wilaya mpya ya (Busega), Festo Kiswaga (Nanyumbu), Wilman Kapenjama Ndile (Mtwara) na Joseph Joseph Mkirikiti (Songea).

Wengine ni Ponsiano Nyami (Tandahimba), Elibariki Immanuel Kingu (Kisarawe), Dk. Charles O. F. Mlingwa (Siha), Manju Msambya          , wilaya mpya ya Ikungi, Omar S. Kwaangw’(Kondoa), Venance M. Mwamoto    (Kibondo), Benson Mpesya (Kahama) Daudi Felix Ntibenda (Karatu), Ramadhani A. Maneno (Kigoma) Sauda S. Mtondoo (Rufiji),  Gulamhusein Kifu(Mbarali), Esterina Kilasi wilaya mpya ya Wanging’ombe, Subira Mgalu (Muheza) na Martha Umbula (Kongwa).

Wamo Rosemary Kirigini (Meatu), Agness Hokororo (       Ruangwa),  Regina Chonjo (Nachingwea), Wilson Elisha Nkhambaku (     Kishapu), Amani K. Mwenegoha (Bukombe), Hafsa M. Mtasiwa (Pangani), Rosemary Staki Senyamule (Ileje), Lt. Col. Ngemela E. Lubinga, wilaya mpya ya (Mlele) na  Iddi Kimanta (Nkasi).


Wakuu wa wilaya waliyobaki na vituo vyao katika mabano ni James K. O. Millya (Longido),  Mathew S. Sedoyeka (Sumbawanga),  Fatuma L. Kimario (Igunga)
James C. Yamungu (Serengeti),  Abdallah A. Kihato (Maswa), Sarah Dumba (Njombe), Jowika W. Kasunga (Monduli), Elizabeth C. Mkwasa (Bahi), Issa E. Njiku (Misenyi),  John B. Henjewele (Tarime), Elias W. Lali (Ngorongoro), Raymond H. Mushi (Ilala), Francis Miti (Ulanga), Evarista N. Kalalu (Mufindi) na Mariam S. Lugaila (Misungwi).

Wengine ni Anna J. Magowa(Urambo), Anatory K. Choya (Mbulu), Fatma Salum Ally (Chamwino), Deodatus L. Kinawiro (Chunya), Ibrahim W. Marwa, wilaya mpya ya Nyang’hwale, Norman A. Sigalla (Mbeya), Moshi M. Chang’a, wilaya mpya ya Mkalama, Jordan M. Rugimbana (Kinondoni), Georgina E. Bundala wilaya mpya ya   Itilima , Halima M. Kihemba (Kibaha), Manzie O. Mangochie (Geita)  Abdula S. Lutavi (Namtumbo), Zipporah L. Pangani (Bukoba), Ibrahim H. Msengi  (Moshi), Col. Cosmas Kayombo, wilaya mpya ya Kakonko, Lembris M. Kipuyo (Muleba) na Elinasi A. Pallangyo (Rombo).

Wanaoendelea na ukuu wa wilaya wamo pia Queen M. Mlozi (Singida),  Juma S. Madaha (Ludewa), Angelina Mabula        , wilaya mpya ya Butiama, Hadija H. Nyembo, wilaya mpya ya Uvinza, Ernest N. Kahindi, wilaya mpya ya Nyasa, Peter T. Kiroya (Simanjiro), John V. K. Mongella (Arusha), Baraka M. Konisaga (Nyamagana), Husna Mwilima, wilaya mpya ya Mbogwe, Sophia E. Mjema (Temeke), Francis Isaac, wilaya mpya ya Chemba, Abihudi M. Saideya, wilaya mpya ya   Momba, Khalid J. Mandia (Babati) na Anna Rose Nyamubi (Shinyanga).

Wapo pia Dani B. Makanga (Kasulu), Amina J. Masenza (Ilemela), Mercy E. Silla (Mkuranga), Christopher R. Kangoye (Mpwapwa), Lt. Edward O. Lenga, wilaya mpya ya Kalambo, Halima O. Dendego (Tanga), Lephy B. Gembe (Dodoma), Saidi A. Amanzi (Morogoro), Jackson W. Msome (Musoma), Elias C. B. Goroi (    Rorya), Benedict Kitenga, wilaya mpya ya Kyerwa, Erasto Sima (Bariadi), Nurdin H. Babu (Mafia) na Khanifa M. Karamagi, wilaya mpya ya Gairo.

Wakongwe wengine ni Gishuli M. Charles, wilaya mpya ya Buhigwe, Saveli M. Maketta, wilaya mpya ya Kaliua na Darry Rwegasira,Karagwe.

Awapa sharti la mitihani

Pinda aliwataka wateule hao kuripoti katika vituo vyao vipya na kuapishwa na wakuu wa mikoa, ambapo watalazimika kupata mafunzo ya ungozi hususan kwa wakuu wapya kabla ya kuanza kazi.

Kadhalika, alisema wakuu hao watalazimika kufanya mtihani, mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo ili kupima uwezo wao wa uelewa na utendaji wa kazi.

 “Tumelazimika kuandaa mafunzo maalum kwa wakuu wote wa wilaya na mikoa ya wiki mbili, yatakayojumuisha pia makatibu tawala wa mikoa. Wajue hii sio semina ni mafunzo na watawajibika kufanya mitihani ili kupima uwezo wako” alisema bila kufafanua watakaoshindwa watachukuliwa hatua gani.

Pinda: Kimolo alidanganya

Akizungumzia sakata la kujiuzulu kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo kwa madai  ya kukerwa na utendaji wa uongozi ngazi ya mkoa na wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Waziri Mkuu Pinda, alidai kuwa kiongozi huyo aliudanganya umma.

Pinda alidai kuwa, katika namna ya uungwana, Rais Kikwete alilazimika kuwataarifu wakuu wa wilaya aliokusudia kuwaacha na sababu zake, akiwemo Kimolo, hivyo walijua kuwa hawatakuwa katika uongozi mpya

“Nimesikitishwa na tamko la Kimolo kwamba amejiuzulu. Yeye aliishaambiwa kuwa hatakuwa miongoni mwa watakaoendelea, na hivyo suala la yeye kujizulu halikuwa na tija. Ajiuzulu kwa nafasi gani ambayo hana? Alishangaa Pinda.

Alisema rais anayo haki ya kuteua na kuacha pia, na akataka watendaji wasifanye kinyongo pale wanapoacha kuteuliwa.

“Rais akifikia hatua ya kumwondoa mtu jua kuna tatizo kubwa, maana mara nyingi huwa hapendi kufanya hivyo” alisema

Maswali ya waandishi yagomewa.

Kwa mara nyingine tena, jana waandishi wa habari hawakuweza kupewa nafasi ya kuuliza maswali jambo ambalo liliwakera baadhi yao.

Kama ilivyokuwa kwa Rais Kikwete majuzi wakati akitangaza majina ya baraza jipya la mawaziri Ikulu, Pinda naye alipomaliza kusoma majina hayo na kutoa maelezo ya utekelezaji wa kazi, alisimama na kuwashukuru waandishi ambao nao walilazimika kusimama  huku wengine wakibaki midomo wazi.

No comments:

Post a Comment