Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!


Waislamu walipuka
·        Wachoma, wavunja makanisa, wapora vifaa vya ibada
·        Wavamia polisi kumteka aliyenajisi kitabu cha Kurani
·        Ilikuwa wamuue kwa kumchinja mchana hadharani
Na Happiness Mnale
KUNDI kubwa la waislamu wenye imani kali, jana lilizusha vurugu kubwa zilizoambatana na kuchomwa moto na kuharibiwa kwa makanisa manne ya kikristo Jijini Dar es Salaam, katika kile kilichoelezwa kuchukizwa na kitendo cha kijana mmoja wa kikristo aliyedaiwa kukimwagia haja ndogo kitabu kitakatifu cha Kurani.
Waislamu hao waliokuwa na jazba kubwa, walichukua hatua ya kufanya uharibifu huo, baada ya kushindwa kwa jaribio la kukiteka kituo kidogo cha polisi cha Mbagala kwa nia ya kumchukua kijana anayetuhumiwa kufanya tukio hilo Emanuel Josephat(14)ili wamuue kwa kumchinja hadharani kama adhabu kwa kosa hilo.
Vikosi vya polisi wenye silaha na mabomu ya machozi na maji ya kuwasha walipambana na waislamu hao ambao walizidi kuongeza kila dakika, hivyo kufunga shughuli zozote za kijamii katika barabara ya Kilwa, eneo lote la Mbagala.
Wakiwa na silaha za mawe, kundi hilo lilivamia mitaani na kuchoma kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Mbagala Zakhem, na lile la Assembly of God (TAG), huku wengine wakiharibu Kanisa la Anglican,kuvunja vioo katika kanisa la Wasabato, na kuchukua vifaa vya muziki na ibada na kuviunguza hadharani.
Waislamu hao waliyaponda mawe na kuyaharibu magari ya polisi namba T142 AVV,PT 0966 na T 325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka Clouds.
Jitihada za kamanda wa polisi wa mkoa wa Polisi wa Temeke, David Misime kujaribu kuzuia kuenea kwa ghasia hizo kwa kuwatumia viongozi wa kiislamu zilionekana kugonga mwamba kutokana na viongozi hao kuwatetea waumini wao.
viongozi wa dini hiyo akiwemo Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa kikao na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka wa kuwatuliza wasialamu hao lakini hali iliendelea kuwa mbaya.
Chanzo cha vurugu hizo, ni ubishani wa kitoto uliozuka baina ya mtoto Emmanuel na rafiki yake Zakaria Hamis (12) anayesoma shule ya msingiChamazi siku ya jumatano wiki hii.
Inadaiwa kwamba mtoto Zakaria alimwambia rafiki yake ambaye pia ni majirani, kwamba msahafu huo ni mtakatifu na kwamba mtu yeyote ambaye angekiharibu kwa jambo lolote iwe ni kukichana kwa makusudi, kukitemea mate ama kukikojolea angekufa pale pale, au kugeuka mnyama.
Katika ubishi huo, mtoto Emmanuel aliamua kukojolea msahafu huo, akitaka kuona kama kweli angekufa ama kudhirika jambo ambalo halikumpendeza rafiki yake ambaye alikwenda kuwaeleza wazazi wake.
Baba mzazi wa Zakaria, aliwaambia waandishi wa habari kwamba, kutokana na tukio hilo alilazimika kwenda kwa wazazi wa Emmanuel na kisha kwenda kwa mjumbe ambaye aliwalekeza kwenda kituo cha polisi kuandikisha maelezo na kisha kushikiliwa kwa muda.
Wazazi wote walikubaliana kuyamaliza mambo hayo, kwa kumwonya mtoto huyo, lakini habari za kuaminika zinasema kuwa baadhi ya viongozi wa kiislamu hasa msikiti wa Chamazi, waling’aka na kutaka jambo hilo lifikishwe ngazi za juu za uongozi wa kiislamu.
Viongozi wa kikristo
Katika hatua nyingine, viongozi wa kikristo walikataa kuzungumza jambo lolote kutokana na vurugu hizo na kuchomwa kwa makanisa yao. Jitihada za kuwapata askofu wa KKKT, Anglikani, TAG na Sabato hazikuweza kuwafanya wazungumze lolote hasa kila mmoja kudai kwamba jambo hilo ni zito na lingetolewa maamuzi kamili kesho jumamosi (leo)
Hadi tunakwenda mitamboni zaidi ya waislamu 100 walikuwa wamekamatwa, huku vurugu ziliendelea  kupinga kukamatwa kwa wenzao na jeshi la polisi, licha ya kuombwa na viongozi wao kuwa watulivu kwa kuwa jambo hilo sasa linashughulikiwa na mamlaka za juu.

No comments:

Post a Comment