Arusha watawala Ruaha Half Marathon 2012
Na Mwandishi Wetu, Iringa
WAKAZI wa mjini Iringa
mwishoni mwa wiki walishuhudia kwa mara ya kwanza wanariadha zaidi ya 320
wakichuana katika mbio za barabarani za Ruaha Half Marathon huku wanariadha
kutoka mkoani Arusha wakitawala.
Katika mbio hizo,
zilizoanzia mnara wa saa karibu na ofisi za Manispaa ya Iringa na kuelekea njia
ya kwenda Ruaha National Park na kurudi hadi uwanja wa Samora ambako zilihitimishwa, kwa upande wanaume
Alphonce Felix kutoka sekondari ya Winning Spirit alishika nafasi ya kwanza
akitumia saa 1:03.09 huku kwa wanawake, Mary Naali kutoka klabu ya Skytel
akishinda kwa saa 1:13.01.
Alphonce alifuatiwa na
Dickson Marwa wa klabu ya Mbui ya jijini Dar es Salaam 1:03.29 huku nafasi ya
tatu ikikamatwa na Saidi Makula wa Winnig Spirit 1:03:29 mshindi wa nne Getuni
Tsekeway pia wa Arusha 1:04.06 wakati aliyefunga tano bora alikuwa ni mwenyeji,
Moses Mwadeni aliyetumia saa 1:11:18.
Naali ambaye kwa muda huo
kaweka rekodi kwa wanawake hapa nchini, alifuatiwa kwa mbali na Stephancy
Perkins kutoka Australia aliyetumia saa 1:32.55, Natali Struble wa Marekani
alishika nafasi ya tatu kwa saa 1:38.50 huku nafasi ya nne ikienda kwa Yoko
Imamura wa Japan 1:59.00 wakati Mia Mjengwa wa Iringa alifunga tano bora akitumia
saa 2:03.00.
Mbio hizo, ambazo
zimepangwa kufanyika kila mwaka Jumamosi ya mwisho wa Mei, kwa mwaka huu wa
kwanza zilishirikisha wanariadha chipukizi wengi kutoka Iringa na mikoa za
jirani na baadhi wa kimataifa wa hapa nchini na kutoka nje.
Ruaha Half Marathon,
iliratibiwa na kudhaminiwa na shirika lisilo la kiserikali
la Mindset Empowerment
(ME), lenye makao yake makuu mjini Iringa, zikiwa na ujumbe wa kulinda na
kuboresha mazingira, ambapo kauli mbiu yake ikiwa ni ‘Mazingira bora kwa utalii
endelevu, okoa mto Ruaha’.
Lowassa apewa heshima
Tamasha la Upendo Radio
Na
Mwandishi Wetu
MBUNGE
wa jimbo la Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, atakuwa mgeni wa heshima
katika tamasha la kuhitimisha mpango wa kuchangisha fedha za kuiwezesha Upendo Redio
FM ya jijini Dar es Salaam kupanua
usikivu wake.
Wakati
Lowassa akipewa heshima hiyo kama muumini wa Kanisa la KKKT –Mashariki na Pwani
na mwasisi wa redio hiyo iliyoanzishwa
mwaka 2004, Askofu wa Kanisa hilo, Dk. Alex Malasusa, atakuwa mgeni rasmi.
Tamasha hilo la aina yake litakalopambwa na waimbaji mahiri kutoka
ndani na nje ya Tanzania ,
litafanyika Mei 27 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, likilenga kukusanya sh mil.
220 kusaidia upanuzi wa masafa ya redio hiyo.
Kwa
mujibu wa mmoja wa wadau wa tamasha hilo, siku hiyo itakuwa ni hitimisho la
tamasha hilo lililozinduliwa Februari 19 na Askofu Msaidizi wa Dayosisi ya
Mashariki na Pwani, George Fupe.
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, baada ya tamasha hilo
kuzinduliwa siku hiyo kwenye kanisa la KKKT-Magomeni, michakato mbalimbali ya
kulifanikisha iliendelea ikiwemo kugawa kadi za michango, ambayo itakabidhiwa
siku hiyo.
Chanzo
hicho kilidokeza kuwa, mkakati uliopo ni kuongeza usikivu wa redio hiyo kutoka
mikoa mitano ya sasa hadi 12. Mikoa ambayo Upendo Radio inapatikana, ni Dar es Salaam , Pwani, Morogoro, Zanzibar
na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Iringa na
kuongeza kuwa kama mambo yatakwenda vizuri kupitia tamasha hilo , mikoa zaidi itafikiwa.
Kati ya
waimbaji ambao watapamba tamasha hilo la aina yake, ni Faraja Ntaboba kutoka DR
Congo, Sarah K kutoka Kenya, Jennifer
Mgendi, Jackson Benti na Joshua John Mlelwa wa Tanzania.
Aidha
kwa wale ambao hadi sasa hawajapata kadi rasmi kupitia katika makanisa ya DMP, zitapatikana
getini siku ya tamasha hilo ,
huku wito ukitolewa kwa wadau kujitokeza kwa wingi kufanikisha shughuli hiyo.
Mwisho
Big brothe Stargame
Watatu
wang’oka mjengoni
WASHIRIKI
watatu kati ya wane waliokua kwenye
hatari ya kutoka kwenye shindano la Big Brother Stargame, Luke, Yadel (Liberia) na Dalphin (Siera
Lione) waliondolowa ndani ya jumba hilo
baada ya kupata moja moja
kila mmoja huku Zainab wa Siera Lione, alinyakua kura 13, kati ya kura
15 zilizopigwa..
Kwa
hatua hiyo, Luke alimuacha mpwe mshiriki mwenzake, Jesica (Namibia ) ambae
alikua na mahusiano nae, awali washiriki hao waliweza kukaa kwa muda mrefu na
kujadiliana ikiwemo mipango ya kuooana hapo baadae ambapo walipigana mabusu ya
mwisho mwisho.
**
ambae alikua na mahusiano na mshiriki
mwenzake, Jesicca, akiponea tundu la sindano
baada yausiku wa kuamkia jana waliliaga jumba hilo kufuatia kupata kura
chache za kuwawezesha kubaki ili kuwania kitita ha dola za kimarekani 300000.
Washiriki
walioaga ndani ya jumba hilo ni Luke,
Yadel (Liberia) na Dalphin (Siera Lione) hata hivyo mbali ya kutolewa kwa
washiriki hao ambao katika hatari ya kutoka wawilikua nne akiwemo Zainab (Siera
Lione) yeye aliponea tundu la sindano na kuamishiwa kwenye jumba la Upville
ambalo linakariwa na washiriki maalum kutoka nchi saba za afrika wakiwemo
wasanii,wanamitindo na wacheza filamu nyota.
Hata
hivyo, mshereheshaji wa shindano hilo, IK alipomwita jukwaani Zanab na
kumweleza kua amebahatika kubakia ila
kwa jumba la Upville, alisshukuru huku akisema kua alipokua ndani ya
jumba la Downville, wengi walimchukulia kama mkosaji ikiwemo vitendo vuya
kugombana mara kwa mara ikiwemo na mshiriki mwenzake, Seydou (Angola).
Katika
kura zilizopigwa Zainab alipata jumla ya kura, 13, Yadel na Luke, kila mmoja
waliambulia kura moja moja huku Dalphin akiambulia patupu kwa kukosa kura hata
mopja kati ya kura 15 zilizopigwa.
Mambo
ndanio ya jumba hilo yanazidi kunoga kwa nyumba
zote mbili, huku safari hii washiriki walio jumba la Upville ndio zamu yao ambapo wanatakiwa
kuingizwa kwenye hatari ilikupigiwa kura. IK aligeukia kwa washiriki wa jumba hilo na kuwatangazia juu ya kujiandaa ambapo zoezi hilo la kuwapendekeza
lilitarajia kuanza mapema jana.
Shindano
hilo ambalo
linarushwa moja kwa moja kila siku katika ving’amuzi vya Dstv chaneli 198.
Small augua
MWIGIZAJI mkongwe wa vichekesho nchini Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amelazwa katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam baada ya kuugua ghafla.
Mzee small anayesumbuliwa
na maradhi ya shinikizo la damu kiasi cha kushindwa kuongea, aliugua ghafla
juzi jioni muda mfupi baada ya kutoka Mwanza alikokwenda kwenye shughuli za
kisanii.
Akizungumza na Tanzania Daima mwigizaji mwenzake
Chausiku maarufu kwa jina la Bichau alisema kabla ya kuugua mzee small alikua
mwenye afya njema hadi walipoachana kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) waliporejea kutoka Mwanza.
Kwa mujibu wa bi chau walikwenda
Mwanza Ijumaa iliyopita kusherehesha shughuli ya walemavu wa ngozi
iliyoandaliwa na Madaktari wa Hospitali ya Bugando jijini humo.
“Tuliondoka Dar es Salaam
na ndege ya jioni Ijumaa tukalala Mwanza jumamosi tukafanyakazi iliyotupeleka
ilikua ni shughuli ya walemavu wa ngozi pale Bugando hospitali iliandaliwa na
madaktari wa chuo cha Bugando.
“Jumapili jioni tuliondoka
Mwanza sasa kabla sijafika nyumbani kwangu Magomeni nikapokea simu kutoka kwa
binti yake mzee small akanipa taarifa za ugonjwa… nilishtuka nikawaambia
wampeleke hospitali,” alisema bi chau swahiba wa nguli huyo wa vichekesho.
Kwa upande wake mke wa
mzee small alisema bado hali ya mumewe haijatengemaa hivyo kuomba dua za
watanzania.
“Analo tatizo la presha na
huwa anajikuna na kuvimba lakini safari hii amevimba shavu moja na kadri muda
unavyokwenda hali yake inazidi kuwa mbaya,” alisema mke wa mzee small akiwa
nyumbani kwake Tabata Kimanga kabla ya kumpeleka hospitali.
Katika maelezo yake mke
wa mzee small alisema juzi usiku walimpeleka mumewe hospitali ya KLM iliyopo
Tabata ambapo alipewa dawa ya kupunguza shinikizo la damu kisha kuruhusiwa kurudi
nyumbani.
Hata hivyo hali ya msanii
huyo iliendelea kuwa mbaya hadi alipokimbizwa hospitalli ya amana jana mchana.
Mwisho…
No comments:
Post a Comment