Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!

MAHUSIANO

HOJA NZITO WIKI HII:

WAPENDWA, KUPITIA KIPINDI CHA MARIDHIANO NINACHOKIRUSHA KUPITIA REDIO MARIA KILA JUMANNE, MSIKILIZAJI WANGU MMOJA ALILETA TATIZO HILI AMBALO NINALIWEKA KWENU NA NAMNA NILIVYOJARIBU KUMSAIDIA KUTATUA JAMBO HILI. SIO VIBAYA KWAKO KUCHANGIA, MAANA LENGO KUU NI KUSAIDIA NA KUWASAIDIA WENGINE.

"Ndugu Misango, mimi nimefunga ndoa miaka sita iliyopita, na tumejaliwa watoto wawili. Hivi majuzi nimepata tatizo kubwa baada ya kugundua kuwa mke wangu ana mahusiano na jirani yangu ya kimapenzi. niligundua hivyo, baada ya kuona simu ya mke wangu katika sehemu ya kupeleka ujumbe "send Iterm' ikimwomba mtu huyo hela za kumbatiza mtoto wetu. Nimeumia sana, na kwa kweli baada ya kumuuliza mke wangu amekataa katakata, ingawa uchunguzi na baada ya kuwashirikisha wazazi, imebainika kuwa ni kweli wana uhusiano.

Kinachoniumiza zaidi ni kupata uhakika kuwa hata huyu mtoto sio wangu ni wa yule jamaa. Je, hata kama ni ndoa ya Kanisa, kwa tukio hili siruhusiwi kumwacha aendelee na maisha yake, maana hata sasa mapenzi ya kweli na mtoto huyo yameisha!

3 comments:

  1. Pole sana ndugu yangu maisha yana vitu vingi sana ndani yake lakini waweza hakiki kwa vipimo vya DNA kama mtoto ni wako au la!

    ReplyDelete
  2. pole sana lakini iwapo tayari mapenzi yashakutoka na huyo dada basi we muache aende nawe ukaendelee na maisha

    ReplyDelete
  3. Maisha ya ndoa yanaitaji uvimilivu wa hali ya juu sana.. Mimi kwa upande wangu ni vizuri kumualika MUNGU Hawe hakimu kwa tatizo hilo

    ReplyDelete