Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!

KUTOKA MIKOANI


WAZIRI wa Nishati  na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema  kuwa  watu ambao wataingia mikataba  mibovu katika  Wizara  yake watafukuzwa kazi pamoja na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria.
Muhongo aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC),alisema kuwa watu ambao wataingia mikataba mibovu watashitakikwa pamoja  na  kufukuzwa ili  kuleta  ufanisi wa kazi na usimamiaji wa miradi.
Alisema  kuwa kilio chake ni  mikataba ambayo  inatakiwa  kupitishwa  kwa  vigezo vilivyowekwa kwa  maslahi ya  taifa  na sio  kuwafurahisha  wawekezaji ambao wanataka  faida nyingi  huku taifa  likishindwa  kunufaika na uwekezaji.
Muhongo alisema kuwa kwa mtu yeyote ambaye  atahusika na  fununu za rushwa katika Wizara  hii mtu  huyo atafukuzwa  kazi baada  ya  kujiaminisha  kutokana  na  fununu  katika  kujenga  Tanzania iliyosalama.
Waziri alisema kuwa bodi ambazo ziko katika wizara yake lazima  zifanye  kazi kwa uhakika katika kusimamia mikataba ambayo imekuwa  ikilalamikiwa na wananchi kuwa ni mibovu.
Muhongo alitataka bodi  ya TPDC kupitia mikataba yote ambayo imeombwa na  ameibaini kuwa na mapungufu hali ambayo inahitaji  kuangaliwa  kwa umakini kwa maslahi ya taifa katika  mali ghafi ya gesi na mafuta.
“Bodi isiwe kama sehemu ya  kujipatia posho na wanaotaka posho na kushindwa kwenda na  kasi hii ni bora wajitoe ili kupata watu wengine ambao  ni waadilifu katika kufanya kazi ya usahuri”.alisema Profesa Muhongo
Alisema  kuwa katika  mambo mengine ambayo  ni mzigo katika baadhi taasisi ni  kuwa na  kesi ambazo haziishi na kuwa mradi kwa makampuni ya uwakili sasa  zifike mwisho katika  kuokoa  fedha za wananchi.
Muhongo alisema  makampuni ambayo yanashindwa kufikia asilimia 8 yasipewe usimamiaji ili  kupewa watu wengine ambao wataweza kuendesha kesi hizo ambazo zinakuwa mzigo na watu katika miradi.
Aliitaka  bodi  bodi  hiyo  kutopokea mikataba minginea mpaka watakapokamilisha  iliyopo ambayo baada  ya  kupitia  kulionekana kuna  upungufu ambapo ni kazi ya bodi kushauri serikali na kupata wawekezaji wenye sifa.
“Wawekezaji  wamekuwa na kauli  nyingi juu ya kuangalia masilahi yao hivyo  ni bora kujiaminisha na vitu ambavyo wanataka kuvifanya na si kukubali gesi ikatoka tutakwa hatujafanikiwa tunachotaka”.alisema Profesa Muhongo
Alisema  kuwa lazima shirika liwe na miradi ya gesi na mafuta ili kuzuia  mchezo wa wafanyabiashara ambao wanaweza kusema mafuta  yameadimika ili kupandisha bei ya mafuta.
mmmmmmmmmmmmmmmmmm

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limeshangazwa na kitendo kilichofanywa na madaktari wanaofanya kazi chini ya usimamizi wa madaktari bingwa (interns), na kusema kuwa hatua waliochukua inaweza kuleta vurugu ndani ya nchi.
Madaktari wanaofanya kazi chini ya usimamizi wa madaktari bingwa (interns), ambao walisimamishwa wakati wa mgomo wa madaktari juzi walijitokeza na kuomba radhi kwa wananchi na serikali kwa kushiriki migomo na kusababisha madhara makubwa kwa baadhi ya wananchi.
Madaktari hao ambao walikusanya saini zaidi ya 200 kutoka kwa wenzao, walienda mbali zaidi na kuapa kwamba hawako tayari kushiriki tena kwa namna yoyote katika migomo inayoweka rehani maisha ya wananchi.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholaus Mgaya, alisema kuwa, hatua iliyochukuliwa na madaktari hao ni cha kushangaza kwa kuwa bado madai waliyokuwa wakihitaji yameshindwa kutekelezwa jambo linaloweza kuchangia kuwepo kwa vurugu.
Mgaya, alisema kuwa Tucta alielewi ni kitu gani kimewasibu madaktari hao hadi kufikia hatua ya kuomba radhi.
Alisema kuwa inawezekana madaktari hao sio wanachama wa vyama vya wafanyakazi hivyo wameshindwa kujua sheria za kuitisha kwa mgomo.
“Sasa inatupa mashaka juu ya mgomo wao…maana hawajapata walichogomea wanaanza kuomba radhi hapa ni lazima ‘system’ imefanyakazi yake na inawezekana kulikuwa na mamluki wengi katika mgomo ule,” alisema.
Katibu Mkuu huyo, alisema kuwa Tucta imejipanga kukutana na viongozi wa madaktari hao ili kuweza kuwaelewesha maana ya mgomo na kuacha kutoa matamko yasiyo kuwa na tija.
Alisema madaktari hao wakiingia katika vyama vya Wanyakazi wataweza kujua sheria za kuitisha mgomo na kuhakikisha wanasimamia na kupata kile walichokuwa wanakihitaji kuliko wanavyofanya sasa.

“Hawa waliotoa tamko hilo inaelekea hawapo katika chama cha wafanyakazi, hivyo wakiingia katika vyama wataacha kutoa matamko ya aina hiyo maana wanaonekana hawaelewi na wanajifunza,” alisema

Hata hivyo Mgaya alisema kuwa inaonyesha madaktari hao kama wametishwa na kulazimika kutoa tamko hilo.

“Hapa kuna jambo limefanyika kwa kuwa hata Dk Steven Ulimboka hatumsikii tena, lazima kuna kitu kinafanyika lakini hatua waliyoifanya watapata hasara zaidi kwani hawawezi kukutana tena na serikali …kwa kifupi wamekalia kuti kavu,” alisema

Mwisho





-->
askofu
-->ASKOFU KIKOTI KUZIKWA KESHO


Mwili wa Mhashamu Askofu William Paskali Kikoti wa Jimbo la Mpanda, aliyefariki  Agosti 28 2012 katika Hospitali ya Rufaa Bugando kwa shinikizo la damu, utazikwa kesho katika Kanisa Kuu la Mt Imakulata jimboni humo. MIsa ya mazishi itaanza saa 4:00 asubuhi

Misa ya kumwombea na kuaga mwili wa Marehemu kule Mwanza ilifanyika janakatika Kanisa Kuu la Epifania kuanzia saa 6:00 Mchana na mara baada ya Misa mwili wa Marehemu Askofu Kikoti ulisafirishwa kwa ndege kwenda Jimboni Mpanda jana 30 Agosti 2012 saa 8:00 mchana.

Marehemu Askofu Paskal Kikoti alizaliwa tarehe 3 Mwezi Machi 1957 katika kijiji cha Ihambo, Parokia ya Nyabula Jimbo katoliki la Iringa.

Alipata elimu ya msingi huko Ihimbo kuanzia mwaka 1967 hadi 1973.


Alisoma masomo ya Sekondari kidato cha Kwanza hadi cha Nne  katika Seminari ya Mafinga kuanzia mwaka 1974 hadi 1977  na akaendelea na maomo ya kidato cha Tano na cha Sita katika Seminari ya Nyegezi Mwanza kuanzia mwaka 1978 hadi 1980.

Marehemu Askofu Kikoti alijiunga na jeshi la Kujenga Taifa katika Kambi ya Makutupora kuanzia mwaka 1980 hadi 1981.

Mwaka 1982 hadi 1983 alisoma Elimu ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Ntungamo na baadaye akjiunga na Seminari Kuu ya Kipalapala kwa Masomo ya TaaliMungu (Theolojia) kuanzia mwaka 1983 hadi 1988 .

Alipata daraja la Upadri tarehe 29 Mwezi Juni 1988.

 RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI- AMINA

-->


Madaktari: Kuna kikosi cha kumuua Ulimboka
*Wadai kutishiwa maisha, waomba ulinzi UN
*Wasema Ulimboka alimtambua afisa aliyemteka

Na Irene Mark

BAADA ya kutekwa, kupigwa na kutelekezwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, viongozi wa vyama vya madaktari wamedai maisha yao yako hatari hali iliyowalazimu kuomba ulinzi Umoja wa Mataifa na makundi mbalimbali ya kutetea haki za binadamu.

Madaktari hao wamesema hawana imani na maofisa wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, wanaotishia usalama wa maisha yao kwa namna tofauti hasa baada ya tukio la Dk. Ulimboka la Juni 27 mwaka huu.

Barua ya madaktari hao kwenda kwa Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini ya Julai 7, 2012, madaktari wameeleza namna maofisa wa serikali wanavyotishia usalama wa maisha yao hao na kuwaeleza namna walivyowatuma wenzao Afrika Kusini kuhakikisha Dk. Ulimboka anapoteza maisha.

Pia barua hiyo yenye kumb. Na.MAT/UN/SU/01, imetumwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi, Shirika la Human Rights Watch na Amnesty International.
Taasisi nyingine zilizopelekewa nakala ya barua hiyo ambayo Tanzania Daima ina nakala yake ni Kituo cha Haki za Binaadam (LHRC), SIKIKA Tanzania, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).

“Hata hivyo, watu kutoka serikalini waliihakikishia MAT kwamba timu ya wasaidizi wao imeenda Afrika Kusini kuhakikisha Dk. Ulimboka anarudi nyumbani akiwa maiti.

“Kwa kuongezea hapo, viongozi wa MAT tunapokea vitisho kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu na wakati mwingine tunapigiwa simu na namba zisizopatikana tukitishiwa maisha,” ilieleza sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Dk. Mkopi.

Aidha, barua hiyo imeuomba Umoja wa Mataifa kuwahakikishia madaktari usalama wa Dk. Ulimboka kwenye hospitali anayotibiwa na kuwalinda madaktari wengine hasa viongozi wa vyama na jumuiya ya madaktari.
Kadhalika barua hiyo imeuomba umoja huo kuushauri mfumo wa sheria za Tanzania kutokubali kutumika kwa faida za kisiasa na kulitaka Bunge kubaki na majukumu yake ya Kikatiba ya kuiwajibisha serikali kwa vifo vya watu kama matokeo ya mgomo unaoendelea.
Katika barua hiyo madaktari hao wameeleza namna Dk. Ulimboka alivyoteswa na watekaji hao kwa kung’olewa kucha, meno na kuumizwa sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimtambua ACP Msangi kuwa miongoni mwa watekaji hao.

Walieleza namna polisi wa kituo cha Bunju walivyoshindwa kuwapa ushirikiano kwa haraka ili kumuwahisha majeruhi huyo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili na jinsi walivyokuwa wakizuiwa na magari ya askari kwa lengo la kumchelewesha asipate huduma za kitabibu.

“Akiwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI), Dk. Ulimboka licha ya maumivu makali aliyokuwa nayo alimtambua ACP Msangi kuwa ni miongoni mwa waliomteka na kumtesa,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo na kubainisha kwamba ACP Msangi ni kiongozi wa tume iliyoundwa kuchunguza suala hilo.

Ikulu yasononesha viongozi wa dini

Baadhi ya viongozi wa dini waliojitolea kusuluhisha mgogoro baina ya madaktari na serikali, wameeleza kusononeshwa na jibu la Ikulu la kukataa kuonana nao huku wakibainisha kwamba jukumu lao kubwa ni kuhakikisha amani inatawala.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi hao, Msemaji wa Kamati ya Vijana wa Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata), Said Mwaipopo, alisema licha ya jibu hilo wanaendeleza juhudi za kuhakikisha mgogoro huo unamalizika kwa njia za amani.

“Hatukatishwi tamaa na jibu la Ikulu kazi yetu kubwa ni kuhakikisha amani inakuwepo… ndiyo maana jana tulikutana na viongozi wa madaktari tukawaeleza kwamba njia bora ya kufanya ni kuandika barua na kuieleza jamii kupitia vyombo vya habari kwamba wanaomba msamaha kwa Rais, wananchi na serikali.

“Kitu kinachotusikitisha vijana wale walikataa ushauri wetu tukagundua kwamba inawezekana nyuma yao kuna siasa zinaingia,” alisema Mwaipopo.

Akijibu suala hilo Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Edwin Chitage, alikiri kukutana na viongozi hao jana na kueleza kwamba walichokubaliana ni kusubiri barua rasmi kutoka Ikulu ikiwataka madaktari hao kuandika barua kuomba msamaha kwa Rais, Watanzania na serikali.

“Ni kweli lakini alichokisema Mwaipopo ni kwamba alipigiwa simu na watu waliodai kwamba wako Ikulu, hivyo wakawaambia viongozi hao wa dini watuambie madaktari tuandike barua ya kuomba msamaha.Tunaomba msamaha kwa nini,” alihoji.

Dk. Mkopi aliongeza kuwa madai yao hayajatekelezwa licha ya kuwepo kwa muda mrefu tangu mwaka 2005 na kwamba kama serikali haina dhamira ya kweli ya kumaliza mgogoro huo utaendelea hata baada ya miaka 10.

 Kukutana na Dk. Mwinyi

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk. Godbless Chale alisema walipokea simu kutoka kwa Waziri mpya ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi ikiwataka kwenda kumweleza sababu za mgomo wao.

“Kweli Dk. Mwinyi alitupigia simu akatuita alisema hajui madai yetu hivyo twende tukamweleze hivi kwa akili ya kawaida kweli ofisi inakosa nyaraka za kumbukumbu?!! Tunaona hayupo ‘serious’.

“Kabla hajatuita wizara yake iliteua wajumbe watatu Naibu Katibu Mkuu, Naibu Mganga Mkuu Dk. Donald Mbando na Mkurugenzi wa Rasilimali tukaketi nao kuwaeleza siku chache baadaye waziri anasema hajui madai yetu hii tumeona ni ‘kamchezo’ wanataka kutufanyia,” alisema Dk. Godbless.
Mwisho






Dk. Slaa, Mnyika, Lema wabanwa
*Nchimbi awaagiza polisi kuwahoji
*Adai Chadema ni wazee wa tuhuma

Na Salehe Mohamed, Dodoma

SIKU moja baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kudai kimebaini mikakati ya makusudi ya usalama wa taifa kutaka kuwadhuru baadhi ya viongozi wake, Waziri wa Mambo ya Ndani, Emanuel Nchimbi, ameliagiza Jeshi la Polisi liwahoji.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Waziri Nchimbi alisema licha ya jeshi la polisi kusita kuwahoji viongozi hao kwa madai ya kutoaminika, lakini sasa ameliagiza liwahoji na kuzifanyia uchunguzi tuhuma zao.

Alisema kama tuhuma hizo zitathibika si za kweli watachukuliwa hatua kulingana na sheria za nchi.
Juzi, Chadema kupitia kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, ilieleza kubaini mkakati wa makusudi wa kuwadhuru viongozi wakuu wa chama hicho, na kudai kuwa mpango unaratibiwa na baadhi ya vigogo katika idara ya usalama wa taifa, kwa lengo la kudhoofisha harakati za kufichua ufisadi na kudhoofisha serikali na chama kinachotawala.

Viongozi wanaolengwa katika mkakati huo ni Katibu Mkuu Dk. Willibrod Slaa, Mbunge wa Ubungo John Mnyika na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbles Lema.

Freeman Mbowe, alisema taarifa za uhakika zilizoangukia mikononi mwa intelijensia ya chama hicho zinathibitisha dhamira ya vigogo hao kuwadhuru viongozi wao na kuwataka wananchi wasisite kupigania haki yao, hata kama dhamira hiyo chafu itafanikiwa.

Alisema mpango huo unaratibiwa na mmoja wa viongozi wa juu kutoka Idara ya Usalama wa Taifa (jina linahifadhiwa). Vile vile, alimtaja mmoja wa watu wanaofuatilia nyendo za Mnyika na kwamba mkakati wa kwanza wa kumdhuru mbunge huyo ni kumuwekea sumu au kuvamiwa na watu watakaodhaniwa kuwa ni majambazi.

Hata hivyo katika hilo, Nchimbi alisema viongozi wa Chadema kwa muda mrefu wamekuwa na tabia ya kuvichonganisha vyombo vya dola na wananchi ili visiaminike.
Alisema suala la kuwalinda raia limesemwa kwenye Katiba na sheria kuwa ni jukumu la jeshi la polisi, hivyo mtu yeyote anayesema hana imani na jeshi hilo ana matatizo.

Alibainisha kuwa ingawa viongozi wa polisi walimuambia hawawezi kuwahoji viongozi wa Chadema waliosema hawana imani na jeshi hilo, amewaagiza wahojiwe bila kujali walichokisema.

“Ninyi Chadema …wazee wa tuhuma kwa miaka minne mmekuwa mkitoa tuhuma kwa JWTZ, polisi na usalama wa taifa, sasa tukiwachagua kuongoza nchi itakuwaje?” aliuliza Nchimbi.
Alisema iwapo itatokea siku moja jeshi la polisi likatangaza kupumzika kwa muda wa saa nne bila kukamata wala kuhoji jambo lolote nchi itakuwa kwenye hali mbaya hivyo ni vema wanasiasa wakajiepusha na kauli zenye lengo la kubomoa.

“Hawa viongozi wa Chadema wanajitafutia umaarufu wa kisiasa, wao wanajua sehemu za kupeleka taarifa zao na zinavyofanyiwa kazi, sasa kwa nini wanatumia njia zisizostahili?” alihoji.
Nchimbi aliongeza kuwa Chadema imeshajenga tabia ya kuvituhumu vyombo vya dola na imeshafanya hivyo kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), usalama wa taifa na sasa polisi.

Alibainisha kuwa tabia hiyo inaonyesha namna viongozi wa chama hicho wasivyo makini katika kupigania matatizo ya wananchi na kugeuka kuwa walalamikaji wa mambo yao binafsi.
Nchimbi pia alitumia fursa hiyo kukemea tabia ya viongozi wa kisiasa kuvishutumu vyombo vya dola hadharani bila kufikisha malalamiko yao ndani ya utaratibu unaostahili na kusema kuwa unavivunja moyo.

Waziri huyo alisema serikali haifanyi kazi kwa fitna, visasi au majungu kwani kama ingekuwa inafanya hivyo ingewakamata viongozi wa Chadema waliokuwa wakihusishwa na kifo cha kada mwenzao marehemu Chacha Wangwe.

Alisema pamoja na viongozi wa Chadema kutajwa sana kwenye ajali hiyo serikali iliyapuuza madai hayo na dereva wa marehemu Wangwe alifikishwa mahakani na kushtakiwa.

“Tutafute majukwaa ya kunufaika kisiasa kwa njia zilizo bora si hili linalofanywa na Chadema, wanachokifanya ni kulibomoa taifa badala ya kulijenga.
Nchimbi aliwataka wananchi na wanasiasa  waondoe hofu iliyoanza kujengwa kuwa polisi haiaminiki na badala yake washirikiane na jeshi hilo kikamilifu.



Madaktari bingwawamjibu Kikwete


  • Sasa waitaka serikali iwatimue na wao pia
  • Waliofukuzwa wasema Rais amepotoshwa
  • Bunge lachafuka kupigwa kwa Ulimboka


Na waandishi wetu, Dodoma, Dar

AGIZO la Rais Jakaya Kikwete kuwataka madaktari wanaoendelea na mgomo kua chakazi limechukua sura mpya baada ya madaktari bingwa ambao awali hawakuhusika kabisa na mgomo huo, kutoa tamko wakimtaka kiongozi huyo wa nchi kuwatimua wao kwanza kabla ya wale wa ngazi ya chini.

Badala yake, Madaktari bingwa ambao walitangaza kujiunga na wenzao juzi, baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa Dk Steven Ulimboka, walisema wataendelea na mgomo wao hadi hapo serikali itakapowarejesha kazini madaktari na madaktari wanafunzi wote waliofukuzwa .


Akitoa tamko la madaktari bingwa waliokutana kwa dharura jana na kamati ya jumuiya ya madaktari kujadili hotuba ya rais Kikwete, kiongozi wa mabingwa hao Dk. Catherine Mng’ong’o alisema huo ni msimamo wa madaktari wenzake, huku akitaka kufunguliwa kwa meza ya majadiliano ya dhati yenye nia ya kumaliza mgogoro wao.


“Madaktari bingwa hatuwezi kuyfanyakazi bila madaktari wa chini yetu… kama serikali imedhamiria kuwafukuza kazi hawa na interns (waliopo kwenye mafunzo ya vitendo) ianze na sisi.

“Tupo tayari kufukuzwa iwapo madai yetu ya msingi hayatatekelezwa na kama kuondoka waanze kutufukuza sisi kwanza,” alisema Dk. Mng’ong’o baada ya kumalizika kwa kikao cha madaktari bingwa kilichoketi kwa zaidi ya saa tano kwenye viunga vya hospitali hiyo.

Alisema hata wao hawana sababu ya kuendelea kufanyakazi katika mazingira magumu na kuwaona watanzania wakifa kwa kukosa vifaatiba na dawa.

Dk. M’ong’o alisema madaktari hapa nchini wamefanyakazi katika mazingira magumu kwa muda mrefu hivyo wakati wa kubadili hali hiyo umefika na kuwasaidia watanzania maskini wanaotibiwa kwenye hospitali hizo.

Jumuiya yasema JK kadanganywa

Kwa upande wao viongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini wameelezea masikitiko yao, ya namna  Rais Kikwete alivyopewa taarifa za uongo na wasaidizi wake.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la watoto kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Katibu wa Jumuiya hiyo Dk. Edwin Chitage alisema wapo tayari kumweleza ukweli rais kwa kuwa wasaidizi wake wameshindwa kufanya hivyo.

“Rais hajapata taarifa sahihi… tupo tayari kumweleza ukweli kwa sababu wasaidizi wake wanamdanganya, tunasikitika kuona watanzania wakidanganywa.

“Wanaelezwa hoja dhaifu za kuonyesha kwamba madaktari hatuna uzalendo wakati madai yetu pia ni kwa maslahi ya wagonjwa wote hasa pale tunapodai mazingira bora ya kazi.

Katibu huyo alisema moja ya madai yao yalikuwa kuomba kila hospitali ya wilaya ipate mashine moja ya X-ray kwa vile, haiwezekani nchi nzima kukosa mashine ya CT-Scan wakati bei yake ni sawa na gari aina ya shangingi moja la kiongozi wa serikali,” alisema Dk. Chitage.

Katibu huyo alikiri kwamba posho ni sehemu ya madai yao huku akisisitiza kwamba hawang’ang’ani nyongeza hiyo badala yake kuwepo kwanza na mazingira bora ya kazi ili kutoa tiba sahihi kwa mgonjwa.

Dk. Chitage alisema hawapendi kubishana na mamlaka ya rais huku akisisitiza uwezo wa kumaliza hili ni Kikwete kukaa nao meza moja kwa ajili ya kuzungumza badala ya kutoa vitisho.

Waomba kukutana na Rais

Madaktari hao walisema kuwa sasa wanaomba kukutana na rais ili kujadili hatima ya mfomo huo.

“Tunamheshimu rais na mamlaka zote ila tunachoamini ni kuwepo kwa meza huru ya majadiliano kati yetu na yeye kwa sababu nafasi ya kumaliza kero hii anayo,” alisema.

Naye Makamu Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Dk. Godbless Charles alihoji sababu za kuwepo kwa taarifa tofauti kuhusu ongezeko la mishahara wakati waliishauri serikali kuwa wazi kuhusu nyongeza hiyo.

“Kumekua na majibu tofauti mfano Waziri wa Afya na UStawi wa Jamii aliliambia Bunge kwamba nyongeza ya mishahara ni asilimia 15. Hotuba ya rais Kikwete inasema nyongeza hiyo ni asilimia 20 wakati ripoti ya wataalam iliyokutana na kamati ya Waziri Mkuu ilipendekeza asilimia 25 je, nia ya serikali iko wapi?

“Wakati viongozi wa serikali wakitoa taarifa zinazotofautiana ripoti ya ufafanuzi wa madai na hoja za madaktari iliyotokana na majadiliano ambapo tulikua wajumbe hatukutoa pendekezo lolote juu ya ongezeko la mshahara,” alisema Dk. Godbless.

Alisema tangu kuanza kwa mgogoro kati ya madaktari na serikali jumla ya vikao sita viliketi kati ya hivyo vikao vinne vilijadili juu ya uboreshaji wa huduma za afya kwa watanzania.

“Ni masikitiko yetu kuwa ripoti ya ufafanuzi wa hoja na madai yetu iliyotolewa Juni 31 mwaka huu, taarifa ya waziri wa afya, taarifa ya waziri mkuu ndani ya Bunge na hotuba ya rais haikuzungumzia kwa jinsi gani serikali itaboresha huduma za afya kwa watanzania,” alisisitiza Dk. Godbless.

Katika hotuba yake kwa wananchi rais Kikwete aliwataka madaktari wote waliogoma kuchakazi kwa kuwa viwango vikubwa vya mishahara wanaoyitaka serikali haiwezi kuilipa.

Kipigo cha Dk. Ulimboka

Akizungumzia kutekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye msitu wa Pande alikofanyiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania Dk. Steven Ulimboka alisema wameshtushwa na kauli ya rais Kikwete.

Kwa mujibu wa Dk. Godbless kauli ya rais Kikwete kwamba serikali yake haihusiki na kitendo hicho kimeingilia uhuru wa tume hiyo ambayo tangu awali madaktari na wanaharakati waliipinga.

“Tume imeundwa kuchunguza suala hilo na mpaka sasa hakuna mwenye uwezo wa kudhibitisha kwamba serikali inahusika… je ni sahihi kwa rais kutangaza waziwazi kwamba serikali yake haihusiki?

“Kauli hiyo haitoi uhuru kwa tume kueleza ukweli wa tukio kwa sababu tume hiyo imeundwa na serikali yenyewe,” alisema makamu mwenyekiti huyo na kuongeza kwamba madaktari hawana imani na tume hiyo.

Awali alisema madaktari wanahasira kwa kitendo cha kinyama alichofanyiwa mwenzao hali inayowafanya waishi kwa hofu huku wengine wakiandika barua za kuacha kazi na wengine wakiendeleza mgomo.

Bunge lachafuka, kupigwa Ulimboka

Katika hatua isiyokuwa ya kawaida, hali ndani ya bunge jana jioni ilichafuka, baada ya mwenyekiti wa bunge, kushishwa kabisa kuongoza kikao hicho kufuatia kuzuka kwa malumbano makali baada ya Mkuu wa mkoa wa Iringa, Stella Manyanya kukituhumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kuwa vinara wa mgomo wa madaktari.

Manyanya alisema kuwa, chadema wamebainika kuchochea mgogoro huo, hali iliyomfanya Mbunge wa Ubungo kusimama na kuomba mwongozo akimtaka Manyanya kuthibitisha ama kukanusha tuhuma hizo.

Lakini katika hali ya kushangaza, Mbunge wa Iramba mashariki Mwigulu Mchemba alisimama na kunukuu hotuba ya kambi ya upinzani, ambayo ilitamka bayana kuwa inaunga mkono madai ya watumishi wa serikali, na kwamba kwa kauli hiyo inadhihirisha bayana kuwa ndio wakuu wa mgomo huo.

Badala ya kutoa mwongozo, Mabumba hakumtaka Manyanya kukanusha ama kuthibitisha tuhuma hizo nzito, badala yake alimruhusu Mchemba kuendelea kurusha makombora mazito dhidi ya Chadema, safari hii akidai kuwa ni vimbelembele kutoa matamshi ya kulaani kupigwa kwa Ulimboka huku, wakimwacha mmoja wa viongozi wake bila kumhudumia wala kumjulia hali.

Katika kujichanganya kwa wabunge hao wa CCM, wakati Mchemba akidai kuwa Chadema ndio wachocheaji wakubwa wa mgogoro huo kwa kuwatumia madaktari, mwenzake Manyanya alitoa hoja asafari hii akidai kuwa, ndio waliohusika na tukio la kumvamia na kumteka na kisha kumpiga Dk Ulimboka.

Hata pale Mnyika aliposimama na kuomba tena mwongozo wa mwenyekiti, huku akiweka bayana jinsi inavyoelezwa ushiriki wa maafisa wa polisi, na hata Dk Ulimboka mwenyewe kuwataja wengine kwa majina, alimtaka mchangiaji kuthibitisha ushiriki wa Chadema kumjeruhi ama sivyo afute kauli yake.

Lakini kwa mara nyingine tena, Mabumba hakumtaka Manyanya wala Mchemba kuthibitisha kauli ama kufuta kama inavyofanywa kwa wabunge wa upinzani, badala yake alimruhusu mkuu huyo wa mkoa wa Iringa kuendelea na mchango wake bila kufuta kauli wala kuithibitisha.

Kushindwa huko kwa waziwazi kwa Mwwenyekiti wa kikao hicho cha bunge, kuliwachefua wabunge wengi wa upinzani, huku wale wa CCM wakionekana kufurahia jambo hilo.




Vigogo wa Jeshi kortini
Na Happiness Katabazi
MKURUGENZI wa Shirika Jeshi la Kujenga Taifa  (SUMA JKT) Kanali Ayoub Mwakang’ata na maofisa wenzake sita wa jeshi hilo jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka saba ya kula njama na  matumizi mabaya ya madaraka.
 Mbali na Kanali Mwakang’ta washitakiwa wengine ni Luteni kanali Mkohi  Kichogo,Luteni Kanali Paul Mayavi, Meja  Peter Lushika, Sajenti John lazier,Meja Yohana  Nyichi na Mkurugenzi wa Miradi ya Matrekta wa SUMA JKT-Luteni Kanali Felex Samillan.
Mawakili toka ofisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa(TAKUKURU), Dominsian Kessy na Ben Lincoln walidai mbele ya Hakimu Mkazi Alocye Katemana katika kosa la kwanza maafisa hao wote wanashitakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Wakili Kessy alidai kuwa Machi 5 mwaka 2009  katika chumba cha mikutano cha ofisi ya  SUMA JKT  Dar es salaam,wakiwa ni wajumbe wa bodi na Bodi ya Tenda ya SUMA JKT  kwa makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kutoa maamuzi ya bodi hiyo ambayo yalionesha yametolewa na TAKOPA  kwa madhumuni ya kununua magari na vifaa vya ujenzi  bila kupata idhini ya Bodi ya ya Wakurugenzi ya  TAKOPA.
 Wakili Kessy alidai kosa la pili pia ni la matumizi mabaya ya madaraka ambalo linawakabiliwa washitakiwa wote  kuwa Machi 12 mwaka 2012 ,washitakiwa hao wakiwa ni wajumbe wa bodi  ya Tenda ya SUMA JKT walitumia madaraka yao vibaya kupitishia maazimio  ya kununuliwa kwa magari na vifaa vya ujenzi ambavyo vilikuwa vimeishatumika kinyume na kifungu  cha 58( 3) cha Sheria ya Mamunuzi ya Umma ya mwaka 2005.
Aidha shitaka la tatu ni la matumizi mabaya ya madaraka linalomkabili mshitakiwa wa pili na wa saba (Kichogo, Samillan) ambapo  Machi 16 mwaka 2009  wakiwa wajumbe wa bodi ya Tenda ya SUMA JKT wanadaiwa kuhamisha  Sh Bilioni 2,744,432,545 kupitia hundi Na.000010 kutoka  akaunti ya TAKOPA  Na.011103031753 kwa  SUMA JKT akaunti Na.01110307094 ambazo zote  zipo Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kufuata matakwa ya kifungu cha  156 cha Sheria ya Fedha ya Umma na Kanuni zake ya mwaka 2001.
Shitaka la nne alidai linalowakabili washitakiwa wa pili na watatu  ambalo pia ni la matumuzi mabaya ya madaraka wanalodaiwa kulitenda Aprili 3 mwaka 2009,wakiwa wajumbe wa bodi hiyo  ambapo walihamisha  sh milioni 489,677,879.30 kupitia hundi Na.000011 kutoka TAKOPA akaunti Na.011103031763 kwa  akaunti Na. 011103017094 ya SUMA JKT bila kufuata kanuni na matakwa ya kifungu cha 156 cha Sheria ya  Fedha za Umma ya mwaka 2001.
Shitaka la tano ambalo linawakabili tena washitakiwa hao wawili ni matumizi mabaya ya madaraka  ambapo inadaiwa Aprili 4 mwaka 2009 wakiwa ni wajumbe wa bodi hiyo  walihamisha  Sh milioni 269,519,093.60 kupitia hundi  Na.000012 kutoka akaunti ya TAKOPA  Na.011103031753 kwa SUMA JKT akaunti Na.011103017094 bila kuzingatia masharti ya kifungu cha 156 cha Sheria ya Fedha za umma na kanuni zake ya mwaka 2001.
Katika shitaka la sita linlowakabili washitakiwa hao wawili tena pia ni la matumizi mabaya ya madaraka  ambapo Mei 4 mwaka 2009 wakiwa ni wajumbe wa bodi hiyo,walihamisha  shilingi 350,000,000,000 kupitia hundi Na.000015 kutoka akaunti ya TAKOPA Na.011103031753 kwa SUMA JKT akaunti Na. 011103017094  bila kufuata matakwa ya kifungu hicho cha sheria ya Fedha za umma.
Hata hivyo alidai shitaka la saba linawakabili washitakiwa wote ambalo ni la kula njama  kinyume na kifungu cha 32 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007, ikidaiwa kuwa kati ya Machi na Mei  mwaka 2009  wakiwa wajumbe wa bodi hiyo jijini Dar es Salaam, walikula njama na kuamisha  mradi kutoka akaunti ya TAKOPA Na. 011103017094 bila kufuata matakwa ya kifungu cha 156 cha Sheria ya Fedha ya umma na kanuni zake ya mwaka 2001.
Hata hivyo washitakiwa  wote walikana na Hakimu Katema aliwaachia kwa dhamana baada ya kila mmoja kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika ambao watasaini bondi ya sh milioni 25 kila mmoja. Kesi imeahirishwa hadi Agosti Mosi huu, itakapotajwa tena.

Ma DC, RC wazuiwa kuuliza maswali bungeni

 Na Mwandishi Wetu, Dodoma

ATHARI za wabunge walioteuliwa kuwa mikoa na wakuu wa wilaya, zimeanza kuonekana Bungeni jana baada ya kuzuiwa kuuliza maswali kwa madai kuwa ni sehemu ya Serikali.
Wabunge waliokumbwa na kisanga hicho ni Martha Umbulla ambaye kwa sasa ni mkuu wa wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara na mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Subira Mgalu.
Mwenyekiti wa Bunge, Jenister Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, aliwazuia wabunge hao wakati waliposimama kutaka kuuliza swali.
Mhagama alilazimika kusimama na kutumia kanuni ya kudumu ya Bunge ya 2(2) ambayo inasema “iwapo jambo au shughuli yoyote haikuwekewa masharti katika kanuni hizi, Spika ataamua utaratibu wa kufuata katika jambo au
shughuli hiyo.
“Kwa kuzingatia Katiba, Sheria nyingine za nchi, Kanuni
nyingine zilizopo, maamuzi ya awali ya maspika wa bunge pamoja na mila na desturi za uendeshaji bora wa shughuli za bunge na uamuzi huo utaingizwa katika kitabu cha Maamuzi ili kuongoza mwenendo wa baadaye wa uendeshaji wa shughuli za bunge.”   
Baada ya kusoma kanuni hiyo, Mhagama alisema wabunge hao ambao wamekuwa wakuu wa wilaya ni sehemu ya serikali, na kutokana na sheria hiyo, alizuia kuulizwa kwa maswali yao yaliyokuwa yamepangwa katika orodha ya shughuli za bunge jana katika swali namba 113 na 114.
Swali namba 113 lilikuwa liulizwe na Subira Mgalu
likielekezwa katika Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo alitaka kujua viwanda vingapi vimejengwa na ni kiasi gani cha fedha kimetumika kuwekeza kwenye viwanda hivyo kutokana na ahadi ya Rais katika kipindi cha kampeini ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 hadi leo.
Martha Umbulla, pia alielekeza swali lake Wizara hiyo hiyo akitaka kujua serikali ina mpango gani wa kujenga viwanda vya kusindika mazao ya kilimo ili kukuza soko la ndani na kuwezesha kilimo chenye tija kwa wananchi”.
Mbunge mwingine ambaye pia ni mkuu wa wilaya ni Lucy
Mayenga (Uyuhi, Tabora). Wabunge viti maalum ambao ni wakuu wa mikoa ni Injinia Stella Manyanya, (Rukwa) na Christina Ishengoma (Iringa).
Wakati huo huo, Spika Bunge, Anna Makinda hataendsha shughuli za bunge kwa siku kadhaa kutokana na kufiwa na mlezi wake, Zena Stephano.

JK: Hatuwalipi
·        Asema wasiotaka waondoke
·        Madaktari nao wamgomea
·        Mnyika naye amjia juu

Na Mwandishi Wetu

HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete amewataka madaktari wote wanaoona hawawezi kufanya kazi serikalini hadi walipwe kiasi cha sh milioni 3.5, waache kazi na kutafuta sehemu nyingine itakayowalipa vizuri.
Aidha, Kikwete ameweka bayana kuwa serikali haitaweza kulipa kima hicho cha chini cha mshahara na nyongeza za posho zitakazomfanya daktari wa ngazi ya chini kulipwa jumla ya sh milioni 7.7 kwa mwezi.
Wakati Rais Kikwete akitoa tamko hilo, Katibu wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Edwin Chitage, ameweka bayana msimamo wao wa kutorejea kazini na kuitaka serikali kuwaleta haraka madaktari kutoka nje kujaza nafasi zao, kama ilivyotangazwa juzi.
Katika hotuba yake kwa taifa jana, Kikwete alisema kuwa haoni sababu ya madaktari hao kugoma na kugombana na mwajiri ili ashinikize kulipwa mshahara huo, badala yake amewataka kuondoa usumbufu huo wa kuondolewa kwa nguvu, kwa wao kuacha kazi kwa amani, na kutafuta sehemu itakayokubali kulipa kiasi hicho.
Rais Kikwete amedai katika tamko hilo la kwanza tangu kuanza kwa mgomo huo wa madaktari wiki iliyopita, kwamba hakukuwa na haja ya madaktari hao kufikia uamuzi wa kugoma, hivyo kuleta madhara makubwa yakiwamo ya vifo kwa wagonjwa hata baada ya serikali kujitahidi kutimiza matakwa yao kwa kiwango kikubwa.
Kikwete ambaye alitumia kigezo cha nyongeza ya mshahara katika hotuba yake kuitetea serikali katika mgogoro huo, alisema itakuwa kuwadanganya madaktari hao na Watanzania kuwa inao uwezo wa kulipa kiasi hicho cha mshahara kutoka kima cha chini cha sh 957,700 cha sasa hadi sh milioni 3.5
“Mwaka 2004/2005, mshahara wa kuanzia wa daktari ulikuwa shilingi 178,700, mwaka 2005/2006 tuliupandisha na kuwa shilingi 403,120. Tuliendelea kuupandisha mwaka hadi mwaka mpaka kufikia shilingi 957,700 wanazolipwa sasa.
 “Kiasi hicho ni mara mbili ya mishahara ya watumishi wa taaluma nyingine wenye shahada ya kwanza wanaoanza kazi ambao kwa wastani hupata shilingi 446,100.
Kwa sasa hatuwezi kuwaahidi kuwa tunao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa shilingi 3,500,000 na posho zote zile. Tukifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa shilingi 7,700,000.  Kwa hakika kiasi hicho hatutakiweza. Si vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama walivyo madaktari,” alisema Kikwete.
Kikwete alisema Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi Machi, 8, 2012, kwa mujibu wa Sheria ya Mahusiano Kazini, Namba 6 ya mwaka 2004 ilitoa zuio la mgomo pamoja na kuagiza kuwepo mazungumzo baina ya pande mbili.
Aliongeza kuwa kati ya Aprili, 10, 2012 na 30 Mei, 30, 2012, vilifanyika vikao sita vya majadiliano kati ya Serikali na Chama cha Madaktari, kujadili madai 12 ya madaktari, ikiwa ni nyongeza ya mshahara kutoka kima cha sasa hadi sh 3.5 milioni. Posho ya kuitwa kazini (on call allowance) asilimia 10 ya mshahara.
Madai mengine ya madaktari yalikuwa kulipwa posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (Risk allowance) asilimia 30 ya mshahara, madaktari wapatiwe nyumba daraja A au posho ya makazi ya asilimia 30 ya mshahara, na posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu nayo asilimia 40 ya mshahara.
Kikwete alisema madai mengine ya madaktari ni posho ya usafiri ya asilimia 10 ya mshahara au wakopeshwe magari, madaktari wapatiwe Green Card za Bima ya Afya, kuondolewa kwa watendaji wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, viongozi wa kisiasa kulazimisha kupewa rufaa nje, madaktari waliofukuzwa warudishwe kazini, kuboresha huduma za afya na posho ya uchunguzi wa maiti iongezwe.
Alisema hadi sasa serikali imekubali kutoa Green Card za Bima ya Afya, kuchukuliwa hatua za kinidhamu dhidi ya watendaji wakuu wa Wizara ya Afya.
“ Lakini, jambo la kustaajabisha hata Waziri mpya wa Afya alipowataka waonane kuzungumzia hoja walikataa kumuona.  Kwanza walisema hawaoni sababu kwa vile wameyazungumza na kamati yake kwa miezi mitatu bila ya mafanikio.
“ Kuhusu viongozi kulazimisha kupewa rufaa ya kutibiwa nje, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwataka wazingatie maadili ya kazi zao na kukataa kutoa rufaa kwa mtu asiyestahili, awe kiongozi au asiwe kiongozi. Pili, walikubaliana kuwa hospitali zilizopo ziboreshwe ili viongozi watibiwe hapa nchini.  Ukweli ni kwamba kufanya hivyo ndiyo sera ya Serikali,” alisema. 
Aliongeza kuwa serikali pia ilikubali madaktari waliofukuzwa, na wale Interns waliokuwa wamerudishwa wizarani kutoka Muhimbili na kupangiwa hospitali za Temeke, Ilala, Mwananyamala na Lugalo.
Aidha, alisema pande zote walilokubaliana ni kuhusu kuongeza posho ya uchunguzi wa maiti. 
“Hili ni jambo jipya halikuwepo mwazoni.  Hata hivyo, serikali imelikubali na posho hiyo imeongezwa kutoka shilingi 10,000 hadi kufikia shilingi 100,000 kwa daktari na shilingi 50,000 kwa wasaidizi wake,” alisema.
Serikali iliwaeleza kuwa watumishi wa kada zote za afya watapatiwa chanjo dhidi ya maambukizi ya Hepatitis B na fedha zimetengwa katika bajeti ya 2012/13.
“Serikali imeeleza dhamira ya kurudisha posho ya mazingira hatarishi kwa watumishi wa umma wanaostahili.  Utekelezaji wake utafanyika baada ya uchambuzi wa kina wa kubainisha mazingira hatarishi ni yepi, viwango stahiki viwe vipi na nani hasa wahusika.  Madaktari wamekataa hili la kufanya uchambuzi, wanataka kiwango kiwe kama wanavyotaka wao, yaani asilimia 30 ya mshahara na kianze mara moja,” alisema.

Mambo yaliyoshindikana

Hata hivyo, Kikwete alikiri kuwa kuna mambo mawili hayakufikiwa muafaka kabisa kati ya pande zetu mbili, nayo ni posho ya kuitwa kazini (on call allowance).
“ Kwanza sina budi kueleza kuwa serikali imekubali kuongeza posho hiyo.  Tangu Februari, 2012 posho iliongezwa kutoka shilingi 10,000 hadi shilingi 25,000 kwa daktari bingwa (specialist), shilingi 20,000 kwa dakari mwenye usajili wa kudumu (Registrars) na shilingi 15,000 kwa madaktari waliohitimu ambao wapo katika kipindi cha mafunzo kazini (Interns). Viwango hivyo vya posho vinatumika hivi sasa. 
“Madaktari kwa upande wao hawakukubali uamuzi huo wa serikali na kusisitiza walipwe asilimia 10 ya mshahara.  Ugumu wa kukubali pendekezo la madakari ni kuwa sharti la malipo haya ni mtu kuitwa kazini.  Ukitaka ilipwe kiwango cha mshahara ina maana kuwa hata kama daktari hakupangwa kuitwa au alipangwa na hakutokea aendelee kulipwa.  Hili haliwezi kuwa sahihi kufanya.  Linaweza kuwafanya baadhi ya madaktari kutokutimiza wajibu wao kwa vile wana hakika mwisho wa mwezi malipo yako pale pale,” alisema.
Alidai jambo la pili ambalo muafaka haukufikiwa baina ya serikali na madaktari ni kuhusu mshahara wa kuanzia kazi wa daktari, ambao wanataka uwe shilingi 3,500,000 wakati serikali imesema kiasi hicho hawakiwezi, badala yake ipo tayari kuongeza mshahara kwa kati ya asilimia 15 mpaka 20 kama ambavyo itafanya kwa watumishi wote wa umma katika mwaka huu wa fedha.
“Kwa kiwango cha sasa cha mshahara wao, daktari ataanzia kati ya shilingi 1,100,000 na 1,200,000 kutegemea kiwango kipi hatimaye kitaamuliwa.  Madaktari wamekataa katakata na wameng’ang’ania shilingi 3,500,000,” alisema.

Jumuiya yashupalia mgomo

Wakati hali ya wasiwasi ikiwa hivyo, Katibu wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Edwin Chitage ameitaka serikali kuwaleta haraka madaktari kutoka nje huku akisisitiza kwamba hawapo tayari kurejea kazini.
Dk. Chitage alisema iwapo serikali itaendelea kupuuza madai yao hawatarudi kazini licha ya kupewa siku ya mwisho kuwa leo wawe wamerejea kazini.
Kwa mujibu wa katibu huyo, uamuzi wa serikali kutaka kutumia sh bilioni 200 kuwaleta madaktari kutoka nje ya nchi kabla ya kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma ni jambo la kuhuzunisha.
“Wakitaka wawalete hao madaktari hata leo lakini sisi msimamo wetu upo palepale… tunataka madai yetu yafanyiwe kazi kwanza,” alisisitiza Dk. Chitage.
Madaktari bingwa nao juzi walitangaza mgomo huku wakisisitiza kuungana kwa mabingwa wa hospitali za Muhimbili, MOU, MUHAS na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

MAT waukana mgomo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi, alisema katiba ya chama chao hairuhusu mgomo hivyo tamko la serikali kuwataka waliogoma kurejea kazini haliwahusu.
Akizungumza kwa kifupi sana, Dk. Mkopi alisema MAT haijawahi kuitisha mgomo na kwamba madaktari waliogoma wanafanya hivyo kwa sababu zao.
“MAT haijawahi kugoma kwa sababu katiba ya chama haituruhusu kufanya hivyo sasa kama kuna daktari aliyegoma ebu muulize.

TUCTA yahoji bil. 200/-

Katibu wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicholous Mgaya, aliitaka serikali kutafakari upya uamuzi wa kutumia sh bilioni 200 kuwaleta madaktari kwa sababu unaathiri wataalamu wa sekta nyingine.
Alisema lazima wananchi waelezwe fedha hizo zinatoka wapi kwa sababu hazipo kwenye bajeti iliyosomwa hivi karibuni na Waziri wa Fedha, William Mgimwa.
“Hivi wameshindwaje kutumia japo nusu ya fedha hizo kutatua sehemu ya matatizo ya madaktari?  Hao watakaokuja watakaa kwa kipindi gani? Kwa nini wameshindwa kuwatimizia madai madaktari wetu?” alihoji.

TEC yanena

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limeitaka serikali kukaa meza moja na madaktari ili kumaliza tatizo hilo.
Rais wa baraza hilo anayemaliza muda wake, Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi, alisema mgomo huo wa madaktari hauna matokeo mema kwa wananchi ambao ni  waathirika wakubwa katika jambo hilo.

Mnyika amkosoa JK

Naye Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, amekosoa hotuba hiyo, akidai Rais Kikwete hakueleza kabisa mchango wa serikali katika kusababisha hali hiyo.
“Hivyo, kwa kuwa pande zote mbili zinachangia katika athari zinazoikumba nchi na wananchi kutokana na mgomo; ni muhimu chombo cha tatu kikaingilia kati kuwezesha ufumbuzi kupatikana na chombo hicho ni bunge ambalo ndilo lenye wajibu wa kuisimamia serikali.
“Jitihada za kuwalazimisha madaktari kurejea kazini bila majadiliano ya pande mbili mbele ya chombo cha kuisimamia serikali kushughulikia chanzo cha mgogoro huo zinaweza kuleta ufumbuzi wa muda mfupi na athari za muda mrefu,” alisema.
Alisema hata madaktari wakisitisha mgomo wa wazi kutokana na amri ya mahakama na agizo la rais, migogoro katika ya serikali na watumishi wa umma wenye kusababisha migomo baridi ya chinichini ina madhara ya muda mrefu kwa taifa.
“Mathalani, kutokana na migomo baridi na huduma mbovu katika sekta ya afya wananchi wa kawaida wamekuwa wakifa kutokana na magonjwa yanayotibika. Migomo ya chini kwa chini ya walimu na mazingira mabovu yamekuwa yakisababisha kudidimia kwa elimu katika shule za umma; mwanafunzi aliyehitimu masomo yake bila kujua kusoma na kuandika hana tofauti na mgonjwa anayekufa kwa kukosa huduma.
“Hali hii ya kugoma kusiko kwa wazi imeanza kujipenyeza mpaka kwa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuachia mianya ya ufisadi na kushindwa kusimamia utawala wa sheria kama ivyodhihirika kwa kuongezeka kwa vitendo vya biashara haramu katika taifa letu’ alisema Mnyika.
 
Awashauri madaktari

Hata hivyo, Mnyika alikwenda mbali zaidi na kuwaomba Madaktari kuueleza umma msingi wa madai yao na kwa kiwango gani walikuwa tayari kushuka kutoka katika madai yao ya awali, kinyume na hayo itaonekana kwamba waliingia katika majadiliano wakiwa na msimamo wa kutaka madai yao pekee ndiyo yakubaliwe wakati ufumbuzi wa mgogoro wa pande mbili hupatikana kwa usawa.
“Ni vizuri ikafahamika kwamba katika majadiliano, pande zote  mbili huwa na mapendekezo yake; hivyo upo uwezekano kwamba yapo madai ambayo madaktari wameyatoa ambayo serikali haina uwezo wa kuyatimiza kwa kiwango walivyopendekeza na yapo ambayo serikali imeyakataa wakati ambao ina uwezo wa kuyatekeleza hata ikiwa kwa kiwango pungufu ya kile kilichopendekezwa na madaktari,: alisema.






UJUMBE WA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA KWA WAAMINI WAKATOLIKI NA WATU WOTE WENYE MAPENZI MEMA
Sisi Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania tumekutana katika Mkutano wetu Mkuu wa 65 wa kawaida tangu tarehe 23 – 30 Juni 2012 uliowajumuisha Wakuu wa Mashirika ya Kitawa, wakuu wa Idara, Tume na Taasisi za Baraza pamoja na wawakilishi Walei.  Lengo la Mkutano huu lilikuwa kutathmini shughuli na kazi zetu za Kichungaji na za huduma za jamii kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita (2009-2012) na vile vile kupanga mikakati ya kuboresha shughuli hizo za Kichungaji na za huduma za Jamii katika Nyanja za Afya, Elimu, Maji, misaada kwa wasiojiweza, utetezi na ushawishi, kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo (2012-2015).
Pamoja na kufanya tathmini ya kina ya utendaji wa Baraza letu katika kipindi hicho kilichopita, na kupanga mipango kabambe kwa ajili ya utendaji wa Baraza kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo,  Mkutano wetu Mkuu umekuwa fursa ya kujadiliana na kushirikishana baadhi ya matukio/mambo ambayo, kwa hakika, yameitikisa jamii yetu ya Watanzania na kuidhalilisha  mbele ya Jumuiya ya kimataifa.
Kwa namna ya pekee kabisa, tumetafakari juu ya vuguru za kidini za hivi karibuni zilizotokea katika Visiwa vya Zanzibar kuanzia 26-28 Mei, 2012 na kupelekea kuchomwa moto kwa baadhi ya Makanisa Visiwani humo pamoja na uharibifu mkubwa wa mali na uvunjifu wa amani. Bila kupenda kurudia matamko ya Wadau mbali mbali waliyoyatoa katika nyakati tofauti kulaani bila kusita hali hiyo ya kutisha na kusikitisha iliyojitokeza Visiwani humo, tunaunga mkono kwa nguvu zote kauli na jitihada za wale wote wenye mapenzi mema walioguswa na vitendo hivyo na hivyo kuvilaani. Tunatoa pole na kueleza mshikamano wetu wa kindugu kwa wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na vitendo hivyo vya vurugu ambavyo vimefanya sehemu ya jamii ya wakazi wa Visiwani humo, hasa Wakristo, kuishi kwa wasi wasi mkubwa kutokana na vitisho vinavyoendelea kutolewa na baadhi ya vikundi pamoja na hali ya kutopewa ulinzi wa kutosha na vyombo husika.  Tunaendelea kuwaahidi Sala na mshikamano wetu katika kipindi hiki kigumu.
Pamoja na hayo, tunapenda kuwakumbusha Watanzania wenzetu, hasa mamlaka husika kutafakari na kuzingatia busara ya wahenga waliosema kwamba “mwanzo wa makubwa ni madogo” na kwamba “mdharau mwiba mguu huota tende”. Kumbu kumbu zinatwambia kwamba, chuki za wazi za kidini zilianza kuinyemelea nchi yetu miaka ya 1990, pale mihadhara ya kashfa za kidini ilipoanza kuruhusiwa.  Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, kwa kuongozwa na busara ya kichungaji, kwa nyakati tofauti, liliandika barua kuziomba na kuzihimiza Mamlaka husika kuingilia kati na kuhakikisha kwamba mihadhara kama hiyo haipati nafasi ya kuendelea katika nchi yetu kwani kamwe haiwezi kuwa na tija isipokuwa kuamsha  hisia kali za kidini, jazba na kujenga chuki miongoni mwa waamini wa dini tofauti. Kwa bahati mbaya, ushauri huo wa Baraza la Maaskofu ulipuuzwa na mamlaka husika.
Hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko kubwa la vyombo vya habari ambavyo vimeanzishwa na ambavyo badala ya kuzingatia malengo mazuri ya vyombo vya habari ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, vimeonyesha malengo ya wazi ya kueneza uzushi, kashfa, chuki na uchochezi.  Bado kuna CD/DVD na Kanda chungu nzima zilizozagaa mitaani zenye malengo kama hayo ambapo, kwa mshangao mkubwa wa raia wema wa nchi hii, licha ya wahusika kufahamika na kuonekana wazi wazi, hakuna hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi yao. Tunachelea hata kudhani kwamba mamlaka za dola zinawakingia kifua wadau wa harakati hizo.
Mkusanyiko wa mambo yote haya ndio uliotufikisha hapa tulipo.  Kwa upendo tulio nao kwa nchi yetu na kwa kuzingatia historia ya mlolongo wa matukio yaliyotufikisha hapa tulipo, tunahofu, lakini kwa uwazi tunapenda kuziambia mamlaka husika, watu wote wenye mapenzi mema na Watanzania wote kwa ujumla kwamba, iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa mara moja ili kurekebisha  hali hii, baada ya miaka michache, hakika kwamba nchi yetu inaweza kuingia katika machafuko makubwa ya kidini.  Ili kuepuka hali hiyo isitokee, kwa moyo wa unyenyekevu kabisa, tunapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:-
·       Sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania tutaendelea kusali ili kuiombea nchi yetu amani.  Licha ya sala na maombi ya kawaida kwa ajili ya lengo hilo, Mkutano Mkuu umeamua kwamba, tutakuwa na siku moja ya kusali kitaifa kwa ajili ya kuomba amani;
·       Tutaendelea kutumia sauti yetu ya kinabii kuonya, kukemea na kukaripia vitendo vyote vile vinavyoashiria kueneza chuki miongoni mwa watu wa dini mbali mbali;
·       Kwa kutumia Tume na Idara zetu, tutaendelea kujenga na kueneza mazungumzano na Waamini wa dini mbali mbali tukiheshimu tofauti zilizopo. Hii ni kwa sababu tunaamini kwamba, suala la dini ni wito na hiari ya mtu na hakuna mtu yeyote aliye na haki ya kumlazimisha mwingine ajiunge na dini yake.
Kwa upande wa wadau wengine na hasa kwa Serikali yetu pamoja na vyombo vyake vya usalama tunapendekeza yafuatayo:-
·       Mihadhara, makongamano na mikutano yenye  lengo la kutoa kashfa na kuchochea chuki miongoni mwa dini mbalimbali ipigwe marufuku;
·       Vyombo vya habari vinavyoeneza uzushi, kashfa na uchochezi vidhibitiwe kwa kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufungiwa;
·       Uzushi na uongo unaoenezwa na vyombo vya habari na watu wenye lengo la kuwachonganisha Watanzania na waamini wa dini mbali mbali utolewe ufafanuzi mara moja na Wizara na vyombo vingine vinavyohusika;
·       Kuweko na mpango kabambe wa kutoa elimu ya uraia yenye kina na upana katika nafasi zote, itakayowawezesha vijana wetu kuwa wazalendo kwa nchi yao na kuepuka propaganda za kuwagawa Watanzania kwa misingi ya kidini;
·       Suala la ukosefu wa ajira, hasa miongoni mwa vijana, liangaliwe kwa makini kwani linaweza kuwa moja ya sababu zinazowafanya vijana wengi kujiingiza katika vikundi vya kidini vinavyojenga chuki na kutoa matumaini ya uongo;
·       Lakini, zaidi ya yote, iwapo Serikali yetu na mamlaka husika inataka kuwa na imani mbele ya jamii kwamba ina nia thabiti ya kuhakikisha kwamba vurugu za kidini hazipati nafasi katika Nchi yetu, wale wote wanaohusika na vurugu hizo wachukuliwe hatua za kisheria mara moja! Ni vigumu kuamini kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 2001 mpaka sasa, Makanisa 25 yamekwisha chomwa moto Visiwani Zanzibar lakini  hakuna aliyekamatwa na kuchuliwa hatua za kisheria!
Tumefanya mkutano wetu katika mazingira ya kuwepo mvutano kati ya madaktari na serikali na kwa bahati mbaya sana, kama tulivyokwisha kutamka huko nyuma, mvutano huu unaleta athari kubwa kwa raia wasio na hatia, athari ambayo haiwezi kurudishwa. Uhai wa raia wa Tanzania unaangamia kwa kukosa ulinzi wa tiba.  Katika hili tunapenda kukumbusha kuwa kila mmoja ni mdau.  Hakuna hata mmoja anayeweza kulikwepa hili.  Tunapenda kurudia himizo letu la awali kwamba ni bora ikapatikana njia nyingine iliyo mwafaka zaidi ya kudai haki na mazingira yanayofaa ya kazi bila kuleta madhara ya kupoteza uhai ambao ni haki msingi ya kila mwanadamu.
Tunaiasa Serikali yetu ikae tena pamoja na madaktari na kuchambua hoja zitakazowekwa mbele yao.  Uwazi na ukweli vikitawala hakuna pande itakayokataa kuridhia eti kwa sababu ya kukataa tu bila hoja.  Taifa letu limejipatia aibu mbele ya macho ya ulimwengu ya jinsi tunavyoshindwa kuishi kile tunachosema kwenye majukwaa.
Mwisho, tunaendelea kuwaalika Watanzania wenzetu, hasa viongozi wa dini mbalimbali kuwahamasisha waamini wao wawe raia wema wa nchi hii kwa kuungana pamoja kuhamasisha upendo, haki, amani na maridhiano miongoni mwa Watanzania wote. Licha ya tofauti zetu, tuzingatie hasa yale yanayotuunganisha: ubinadamu wetu na uraia wetu wa nchi yetu Tukufu ya Tanzania ambamo tutake tusitake, ni lazima wote tuishi! Tuepe ushindani ambao hauna tija isipokuwa kutupeleka katika kujenga chuki na hali ya kudhaniana vibaya miongoni mwa Waamini wetu.  Iwapo kuna sababu ya kushindana, tushindane katika kubuni mbinu za kujenga Upendo na Amani miongoni mwa Watanzania katika kutafuta njia za kuwaletea maendeleo yatakayowatoa kutoka katika Umaskini, Ujinga na Maradhi ambao ndio adui wetu sote.
Tunaiombea Nchi yetu Amani na Usalama.
+Jude Thaddaeus Ruwai’chi
RAIS: BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA/
ASKOFU MKUU JIMBO LA MWANZA



Hali ya Dk Ulimboka tete
HALI ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini Dk. Steven Ulimboka juzi usiku ilibadilika na kuwa tete kiasi cha kuwatia wasiwasi madaktari wanaomtibu.
Baadhi ya madaktari wanaomhudumia mwenyekiti huyo wameliambia Tanzania Daima jana kuwa, Dk Ulimboka hali yake ilibadilika ghafla juzi usiku, na hivyo kulazimika kumfanyia uchunguzi mpya na kumwongezea uangalizi.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la Kitengo cha Mifupa (MOI) cha hospitali ya Taifa Muhimbili kiongozi wa jopo la madaktari wanaomtibu Ulimboka, Profesa Joseph Kihamba alisema uchunguzi mpya umebaini matatizo mengine makubwa ya kiafya.
Alisema vipimo imebaini kuwa kiongozi huyo ameumizwa zaidi sehemu za shingo, taya, mbavu, hivyo, kukiri kwamba huyo ameumizwa sehemu kubwa ya mwili.
“Kuna vipimo vinahitajika ninachoweza kusema ni kwamba tumegundua ameumia sana kwenye singo, taya, ubongo wake, mbavu… kwa kifupi naweza kusema amejeruhiwa sehemu kubwa ya mwili wake,” alisema Profesa Kihamba.
Kutokana na mabadiliko hayo, sasa madaktari wameanzisha mchakato wa kukusanya fedha za kumsafirisha nje ya nchi kutokana na kukosekana kwa kipimo maalum ambacho kitaweza kugundua madhara mengine.
Maktari bingwa nao wagoma
Mgomo huo sasa umechukua sura nyingine baada ya madaktari bingwa kutangaza kujiunga nao huku wakiwataka madaktari wengine kote nchini kushiriki.
Akitoa tamko la madaktari hao waliokuwepo kwenye kikao kwa zaidi ya saa nane ndani ya majengo ya MOI, Dk. Catherine Mng’ong’o alisema uamuzi wa kikao hicho unatokana na ukatili aliofanyiwa Dk. Ulimboka.
Kwa mujibu wa Dk. Mg’ong’o mgomo huo wa mabingwa utahusisha hospitali za MOI, Muhimbili, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na MUHAS zote za jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kutoa tamko hilo alisema madaktari wote nchini wamefadhaishwa na kupata hofu kuhusu usalama wa maisha yao hivyo kuitaka serikali iweke bayana mustakabali wa wataalam wa sekta hiyo muhimu.
“Madaktari tumefadhaishwa, tumesikitishwa pia tumepata hofu kuhusu usalama wa maisha yetu tunaiomba serikali itamke mustakabali wa usalama wetu.
“Tunalaani ukatili aliofanyiwa Dk. Ulimboka ambaye hali yake inazidi kuwa mbaya… tunalaani juhudi zinazofanywa na wadhalimu wanaoitendea mabaya sekta ya afya kwa kutudhuru,” alisema Dk. Mg’ong’o.
Aidha mabingwa hao wameiomba serikali kuwarejesha kazini madaktari waliosimamishwa kazi na kunyimwa mshahara wao wa mwezi wa sita kwa sababu kufanya hivyo ni kuwadhalilisha wataalam hao.
“Hakuna mahali waliposema hoja za mgomo sio za msingi sasa kwa nini wawasimamishe kazi na kuwanyima mshahara wao wakati suala hili lipo mahakamani,” alisema kwa niaba ya timu ya madaktari bingwa huku akisisitiza kwamba huduma kwenye hispitali zilizotajwa zimesitishwa.
Polisi watishia kukamata madaktari
Jeshi la polisi nchini limetishia kuwakamata na kufikisha katika vyombo vya sheria madaktari watakaoendelea kukaidi amri halali ya Mahakama ya kusitisha mgomo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Kamishina wa Operesheni nchini, Paul Chagoja kwa wandishi wa habari, akisema hawatakuwa tayari kuona yeyote akitendewewa kinyume na matakwa ya sheria hivyo aliwataka madaktari kuheshimu viapo vyao vya kazi vinavyosisitiza kwamba udaktari ni wito.
Alisema ikiwa madaktari hawakuridhishwa na mwenendo wa mahakama wangefuata sheria kwa kukata rufaa mahakama za juu kuliko kuchukua uamuzi wa kibabe wa kugoma na kusababisha wagonjwa kukosa huduma za afya na kusababisha wengine kupoteza maisha.
Akizungumzia kuhusu Jeshi la polisi kuhusishwa katika tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka alikana chombo hicho cha usalama kuhusishwa kwa namna yoyote na tukio hilo kwa sababu wanatambua suluhu ya mgomo kamwe hauwezi kutatuliwa kwa kumuondoa Daktari huyo bali njia pekee ni ya mazungumzo.
Aliwaonya wale wanaosambaza uvumi wa kulihusisha jeshi la polisi na tukio la kujeruhi kwake anayachukulia kama maneno ya kuwakatisha tamaa ili washindwe kufanya uchunguzi wao kikamilifu.
Chagonja pia aliwataka wananchi na madaktari kuwa na imani na jopo la wapelelezi walioteuliwa kufuatilia suala hilo, na  kwamba watafanya uchunguzi kwa kina na kwa haki.
Kumetokea sintofahamu baina ya polisi na watu wa kada mbalimbali kutokana na kuwepo kwa tuhuma zinazolihusisha jeshi hilo na tukio la kutekwa, kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa Dk Ulimboka.
Aidha, kutokana na hali hiyo, watu wengi wamependekeza kuundwa kwa chombo huru kitakachofanya uchunguzi wa haki kwa sababu tayari jeshi hilo, limekwishachafuka kwa kuhusishwa na tuhuma hizo.
Mwisho  


Uchunguzi ufisadi wa bilioni 300 za gesi
waanza


*Pinda atangaza neema Mtwara, Lindi, Bajeti yake yapita


Serikali  imeanza uchunguzi wa tuhuma za mafisadi wanaodaiwa kupora sh bilioni 300 za miradi ya gesi, madini na petrol na kuzihifadhi kwenye akaunti nchini Uswizi.

Akizunguza wakati wa kufanya majumuisho ya  hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kuwa tayari Serikali imeanza uchunguzi wa tuhuma hizo.

"Taarifa hizi tumezipata kupitia vyombo vya habari
na tumeshafanya mawasiliano na vyombo vya dola kwa ajili ya uchunguzi, wakibainika wataenda mahakamani," alisema Pinda.

Taarifa za ufisadi huo uliibuliwa mwishoni mwa wiki ambapo inadaiwa kuwa  Watanzania sita  wamepokea hongo kutoka makampuni yanayotafiti gesi, madini  na petrol na kuweka pesa zao Uswizi.

Akizungumzia ugunduzi wa gesi katika mikoa ya Lindi na Mtwara, Pinda alisema mikoa hiyo itanufaika zaidi na fursa hiyo.

"Niwaambie tu kwamba sasa Lindi, Mtwara kumekuja. Wajipange kwa fursa hiyo na serikali tumejipanga kuhakikisha wananufaika na gesi," alisema.

Akizungumzia posho za madiwani, Pinda alisema wameongezewa kutoka sh 120000 hadi 250000 na posho hiyo itaendelea kuongezeka kadri ya uwezo wa serikali itakavyokuwa.

Bunge limepitisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa  mwaka 2012/2013 ambapo aliomba kuidhinishiwa sh trilioni 3.2

Kati ya fedha hizo, sh trilioni 2.7 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh bilioni  544.1 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Katika Bajeti hiyo, aliomba kuidhinishiwa sh bilioni 176.7 kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake.

Kati ya fedha hizo, sh 68,522,866,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh 108,271,972,000  kwa ajili ya Mpango wa Maendeleo.

Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Asasi zake ziliombewa na kupitishiwa sh.186,891,598,000, kati ya hizo, sh.164,614,726,000)  ni  kwa  ajili  ya  Matumizi ya Kawaida na sh 22,276,872,000  kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo.

Ofisi za Wakuu wa Mikoa ziliombewa na kupishiwa sh 173,276,761,000), kati ya hizo, sh.146,552,262,000 kwa matumizi ya kawaida na sh bilioni  26,724,499,000 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Ends


Pinda ayumba tena
* Akwama kutoa kauli ya serikali
* Atakiwa kujiuzulu, yeye ang’aka
* Kipigo cha Ulimboka chamtesa

Na Martin Malera, Dodoma

Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa mara nyingine tena jana katika hali isiyotarajiwa na wengi, aliyumba na kushindwa kutoa tamko zito kuhusu mgomo wa madaktari kinyume na alivyokuwa ameahidi mbele ya bunge juzi mjini Dodoma.

Pamoja na kushindwa kwake, Pinda pia alijikuta katika wakati mgumu kuelezea ukweli wa kile kinachodaiwa kuhusika kwa serikali katika tukio la kutekwa, kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa kiongozi wa jumuiya ya madaktari nchini, Steven Ulimboka.

Akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Chadema) katika kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, ambaye alitaka kujua hatua ya serikali ya kutotoa tamko wakati juzi alitoa kauli nzito  ya ‘liwalo na liwe’ kuhusu mgomo wa madaktari na kuibua hofu kubwa kwa wananchi, Serikali inalieleza nini taifa kuhusu hali hiyo na inafanya nini kumaliza mgomo huo.

Akijibu swali hilo, Pinda kwanza alikiri kuahidi kutoa tamko la Serikali akitumia neno la “liwalo na liwe’, lakini akadai kuwa serikali haitaweza kutoa tamko hilo tena baada ya kupata ushauri wa kisheria kwa kuwa jambo hilo liko mahakamani.

"Kwa bahati mbaya sana kauli yangu ya 'Liwalo na Liwe' imetafsiriwa kwa namna tofauti. Hata dada yangu Halima Mdee nilimsikia akitilia shaka kauli hiyo na kuhusisha na tukio la kutekwa kwa Dk. Ulimboka.

"Nilichoaminisha ni kwamba hili jambo liko mahakamani, lakini tungetolea tamko la Serikali bila kujali kwamba suala hilo liko mahakamani ndo maana nikasema Liwalo na Liwe"

Alisema baada ya mashauriano na wataalamu wa serikali jana usiku waliona si vyema kuendelea na tamko hilo hadi kesi iliyopo mahakama itakapomalizika.

Kuhusu tukio la kutekwa, kupigwa kwa Ulimboka, Waziri Mkuu Pinda alisema Serikali imeguswa na kushitushwa na tukio hilo, na akadai kuwa amesikitishwa na kuwepo kwa taarifa zinazoituhumu serikali kuhusika na unyama huo.

Waziri Mkuu  aliliambia bunge kuwa madai hayo ya kuituhumu serikali yanashangaza kwa sababu, yeye mwenyewe alipata taarifa ya kufanyiwa vitendo hivyo akiwa bungeni na hata wakati alipoahidi kutoa tamko la Serikali  hakuwa anajua chochote.

"Dk. Ulimboka tumekuwa naye kwenye vikao vya ndani vya majadiliano, tuko naye mahakamani. Leo Serikali ihusike kumteka, kumpiga na kumtesa kwa kiasi kile ili iweje,?"

Alisema Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi ameshatoa kauli juu ya tukio hilo, hivyo alisisitiza kuwa Serikali itafanya uchunguzi wa kina kuwanasa waliohusika.

Akijibu swali la nyongeza la Mbowe aliyetaka kujua hatua za dharula zilizochukuliwa na Serikali kumaliza mgomo huo hasa baada ya kusitisha tamko lake Bungeni, Pinda alisema Serikali itaendelea na majadiliano na madaktari hao ili kufikia muafaka.

"Hatua nyingi ya dharura tuliyochukua Serikali ni kuzungumza na hospitali ya Lugalo na  zingine ndogo kubeba jukumu hilo kwa sasa, pia tumeagiza madaktari wastaafu wote warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo," alisema Pinda.

Lissu amtaka ajiuzulu

Majibu ya Pinda yalimkoroga Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyesimama na kumuuliza sababu gani zinazomfanya aendelee kushikilia wadhifa wake huku akitambua kuwa ameshindwa kumaliza mgogoro huo.

"Mheshimiwa Waziri Mkuu, Februali mwaka huu wakati wa mgomo wa madaktari uliahidi kwamba mgomo huo hautatokea tena, leo mgomo umerudi tena, je, kwanini usijiuzulu?" Alihoji Lissu.

Pinda alidai kuwa tangu kuanza kwa mgogoro huo, amefanya jitihada za kutosha kujaribu kunusuru mgomo huo, na kwamba anaamini amefanya kazi kubwa kuufikisha hapo ulipo.
Hata hivyo, Lissu alisimama na kumwambia waziri mkuu, kwamba hapo alipoufikisha ni pabaya zaidi na haoni sababu ya yeye kuendelea kuwepo madarakani, kauli iliyoonekana kumkera Pinda ambaye alidai kuwa yapo mambo ambayo yanaweza kumfanya akajiuzulu, lakini sio katika sakata la mgomo wa madaktari.

"Mheshimiwa Lissu hii sio lugha nzuri ya kusema, nakuheshimu sana," alisema Pinda na kuzima swali hilo.

Naye Mbunge wa Viti Maalum, Martha Mlacha (CCM), alihoji endapo serikali inajua kama kuna kikundi cha watu kinachochochea  mgomo huo kwa kuwapa fedha. Akijibu hoja hiyo, Pinda alikiri kupata taarifa hizo na akadai kuwa serikali inafanya uchunguzi kubaini ukweli, ikiwa ni kweli wahusika watachukuliwa hatua.

Juzi Pinda aliahidi kutoa kauli ya Serikali wakati akijibu mwongozo Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Dhambi (CCM) aliyetaka kujua msimamo kuhusu mgomo wa madaktari.

Madaktari waikataa tume ya polisi

Jumuiya ya Madaktari nchini imesema haina imani na tume iliyoundwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuchunguza unyama aliofanyiwa Dk. Ulimboka huku wakisisitiza kuwepo kwa chombo huru zaidi.

Licha ya kutaka tume huru, madaktari hao wamesema wataendelea na msimamo wao wa kuhakikisha wanatetea maslai yao pamoja na mazingira magumu ya kufanyia kazi yanayowakabili kwa sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la MOI Katibu wa Jumuiya hiyo Dk. Edwin Chitage alisema madaktari nchini wanahitaji chombo kilichohuru kitakachochunguza tukio hilo kwa undani zaidi kuliko jeshi la polisi.

Alisema hawana imani na tume hiyo kwa sababu si huru kitakachopatikana kwa utaratibu unaoeleweka, kuliko polisi tu  hasa wakizingatia mazingira ya kutekwa na kupigwa kwa mwenzao ingawa hawawezi kusema kama jeshi la polisi linahusika.

“Tutaendelea kupigania masuala ya mazingira bora ya kazi kwani hatufurahii kuona msongamano wa wagonjwa wodini, mgonjwa akilala chini, watoto wachanga kulala zaidi ya watano kitanda kimoja na kukosekana kwa dawa na vifaatiba,” alisema.

Awali aliwataka madaktari wote nchini kuwa watulivu hasa katika kipindi hiki kigumu na kusisitiza kwamba tukio hilo limewaimarisha na kuwazidishia mshikamano.

Afya ya Ulimboka yaimarika

Hali ya afya ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini Dk. Steven Ulimboka inaendelea kuimarika licha ya maumivu makali yanayomkabili.

Akizungumza kwa tabu na waandishi wa habari kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kwenye Kitengo cha Mifupa (MOI) Dk. Ulimboka alisema; “Namshukuru Mungu naendelea vizuri tofauti na nilivyofikishwa hapa jana…bado nina maumivu makali naomba kama kuna watu wanataka kuja kuniona wasije ili nipumzike,” alisema.

Awali Ofisa Uhusiano wa MOI Jumaa Almas alisema hali ya Dk. Ulimboka inaendelea vizuri tofauti na alivyoletwa juzi asubuhi kwa kuwa sasa ana uwezo wa kutambua watu wanaofika kumjulia hali na kuzungumza kidogo.

Almas alisema madaktari wameshauri mgonjwa huyo kupumzika na kutaka idadi ya watu wanaofika kumjulia hali mgonjwa huyo ipingie ili kumwepusha na maambukizi zaidi.

“Kwa sasa hali yake ni nzuri na yupo chini ya uangalizi wa jopo la madaktari linaloongozwa na Profesa Joseph Kahamba,” alisema.

Kuhusu mgomo katika kitengo hicho Almas alisema ni huduma za dharura pekee zinazotolewa huku zile za kawaida zikiwa hazifanyiki kabisa.

Dk. Ulimboka alifikishwa hospitalini hapo baada ya kutekwa na watu wasiojulikana kisha kumpiga, kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kutupwa kwenye msitu wa Pande, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mwenyekiti huyo ambaye amekua akiratibu mgomo ya madaktari unaoendelea, aliokotwa na msamaria mwema akiwa amefungwa mikono  akiwa amejeruhiwa vibaya.
Vyama vyaendelea kulaani

Kutoka Mkoani Mwanza, Sitta Tumma anaripoti kuwa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti nchini (RAAWU), Kanda ya Ziwa kimelaani vikali kitendo cha kinyama cha kupigwa na kuumizwa vibaya, alichofanyiwa Dk. Steven Ulimboka, na kuelekeza tuhuma hizo kwa Serikali.

 RAAWU imesema, ushahidi wa mazingira unaonesha dhahiri  kwamba Serikali imehusika kwa namna moja au nyingine kumdhuru kiongozi huyo wa madaktari nchini, ikiwa ni lengo la kutaka kuzima mgomo wa madaktari unaoendelea katika kudai maslahi na huduma bora ya matibabu kwa Watanzania.

Katibu wa RAAWU Kanda ya Ziwa, Ramadhani Mwendwa, ameliambia Tanzania Daima ofisini kwake kuwa kuna haja ya serikali kujisafisha kwa sababu mazingiora ya tukio hilo inaiweka katika hali ya kutuhumiwa

Mwendwa ambaye pia ni Katibu wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Mkoa wa Mwanza, alizidi kudai kuwa, manyanyaso na ukandamizwaji mkubwa unaofanywa na Serikali inaonesha wazi kwamba viongozi wa Tanzania wanawapeleka wananchi wao katika machafuko.

"Tusifike huko kama nchi nyingine zinavyopigana. Viongozi wa wafanyakazi tuweni wamoja na wafanyakazi wote katika kutetea maslahi ya taifa. Tusirudi nyuma", alisema Mwendwa.

CUF, Chadema wanena

VYAMA vya CUF na Chadema, vimelaani kitendo cha kutekwa na kupigwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka, huku vikiitaka serikali kuunda tume huru ya uchunguzi.

Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganizesheni wa Chadema, Benson Kigaila, alisema kuwa kitendo hicho jitihada za serikali kuwanyamazisha watetezi wa maslahi ya umma.

Akizungumza jijini Dar esSalaam jana, alisema hizo ni dalili za wazi za serikali ya CCM kushindwa kuhimili demokrasia ya wengine.

“Tumeshuhudia hali hii ikiwakumba wengi, kumbukeni tukio la mhariri wa Mwanahalisi Sued Kubenea kumwagiwa tindikali, mauaji ya Masudi Mbwana kule Igunga na hata kuuawa kwa mwenyekiti wa Chadema kule Arumeru ni katika njia za kutaka kuwanyamazisha na kuwatisha wengine,”alisema Kigaila

Alisema katika mgomo wa kwanza wa madaktari Rais Jakaya Kikwete aliuhakikishia umma kuwa watayashughulikia matataizo ya madaktari na kwamba suala la mgomo kwao litakuwa ni ndoto.

Kwa upande wao CUF, Naibu Mkurugenzi  wa Itikadi na Uenezi, Abdul Kambaya, alilitaka jeshi la polisi kuacha kuchunguza tukio hilo kutokana kutolitilia maanani tangu awali walipopewa taarifa.

Akizungumza  jana  na Tanzania Daima, alisema  kuwa kitendo alichofanyiwa Dk.Ulimboka  ni  aibu  kwa  taifa  kwa  kushindwa  kufanya ulinzi wa  viongozi watu wake.

Alisema uchunguzi  huo wa   tukio unatakiwa kufanywa na taasisi  zingine huru ili kutoa kutoa  majibu sahihi  kwa  wananchi lakini si jeshi la polisi.

 “Serikali  haiwezi  kujitoa katika tukio hili la kinyama alilofanyiwa Dk.Ulimboka hasa ukizingatia ni katika kipindi kifupi ambacho madaktari wako kwenye mgomo na huyu ni kiongozi wao,” alisema  Kambaya.





MBUNGE AMWAGA CHOZI MAUAJI YA ALBINO

MBUNGE wa Viti Maalum, Alshaymaa Kweigir (CCM) jana aliangua kilio Bungeni na  kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kupinga  Bajeti ya Ofisi ya  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa mwaka huu wa Fedham

Mbunge huyo alipinga Bajeti hiyo kwa madai kuwa  Waziri Mkuu ameshindwa kukabiliana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na kwamba  haungi mkono hoja.

Mbunge huyo alisema anasikitishwa na Serikali kutochukua hatua dhidi ya watu wanaowaua albino  bila hatia.

Alisema  idadi ya vifo vya albino nchini imeongezeka na kufikia 80 katika kipindi ambacho hakufafanua.

Alisema Albino wengi wamepoteza maisha, lakini wauaji wa watu hao wapo lakini hawakamatwi.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu wewe ndio mtu wakutusaidia sisi walemavu wa ngozi lakini umekaa kimya, hivi karibuni aliuwawa Faru ambaye alikuwa anaitwa George na mtu aliyehusika na mauaji hayo alikamatwa kwanini wauaji wa albino hawakamatwi,"

"Hivi karbibuni kauwawa albino huko Arumeru  na walemavu hawa wamekuwa wakiuwawa kwakukatwa viungo vyao mbalimbali vya mwili vikiwemo viungo vya sehemu za siri kwa kweli napata uchungu siungi mkono  hoja," alisema Mbunge huyo na baadaye
akaanza kulia.

Wakati akiendelea kulia,  Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Adam Malima aliinuka kwenye kiti chake na kwenda  kumchukua na kumtoa nje ya ukumbi wa Bunge huku akimbembeleza.

Awali akichangia bajeti hiyo Mbunge huyo aliishauri Serikali kuweka alama za barabarani ambazo ni maalum kwa ajili ya walemavu wasioona, wasiosikia na walemavu wa viungo  ili  kuwasaidia wakati wa kuvuka.

Mbunge huyo alifafanua kuwa walemavu hao wamekuwa wakipata taabu mara wanapotaka kuvuka barabara hivyo ni vyema Serikali ikaliangalia suala hilo kwa kina.

Aidha alisema kumekuwa na alama  za barabarani ambazo ni maalum kwa ajili ya walemavu lakini  hazitumiki.


Kiongozi wa madaktari atekwa, aumizwa

  • Aokotwa Mabwe Pande akiwa mahututi
  • Madaktari wazusha vurugu kubwa Muhimbili
  • Chadema waishukia serikali, wataka maelezo
  • Waziri Mkuu Pinda kutoa msimamo mzito leo



WATU wasiojulikana, juzi usiku walimteka kisha kumpiga na kumjeruhi vibaya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk. Steven Ulimboka.
Ulimboka ambaye amelzwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi inadaiwa alitekwa na watu hao akiwa na daktari mwenzake aliyetajwa kwa jina la Deo, eneo la kinondoni baada ya kupigiwa simu na watu hao.
Kiongozi huyo ameng’olewa meno na kucha na watu ambao haijajulikana, huku baadhi wakidai ni watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa, huku wengine wakisema ni majambazi.
Ulimboka alifikishwa Muhimbili majira ya saa 04:54 asubuhi na kupelekwa moja kwa moja katika Kitengo Cha Mifupa (Moi) na kupokelewa na Dk Cuthbert Mcharo.
“Tumempokea Dk Ulimboka ambaye hali yake si nzuri tumempeleka katika chumba cha dharura ili kumfanyia vipimo na uchunguzi,” alisema Dk Mcharo.
Baadhi ya madaktari walishindwa kuhimili na kuangua vilio vilivyoongeza simanzi huku wengine wakisema kauli ya liwalo na liwe iliyotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda imeanza kutekelezwa.
Ulimboka anena
Akizungumza kwa taabu baada ya kufikishwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Dk. Ulimboka alisema akiwa na rafiki zake alipigiwa simu na mtu anayemfahamu na ambaye walishawahi kukutana akimtaka wakutane.
Ulimboka alisema mara baada ya mtu huyo kufika walipokuwa, walianza mazungumzo, lakini wakiwa katikati yule mtu aliwasiliana kwa njia ya simu na watu asiowafahamu, na baada ya muda mfupi kabla ya kuagana liliwasili gari moja lenye rangi nyeusi likiwa halina namba.
“Wakashuka watu kama watano hivi wakiwa na bunduki wakawaambia wale wenzangu na yule niliyekuwa naongea nae kuwa wako free (huru),  wakaniingiza kwenye gari lao kwa nguvu” alisema Dk. Ulimboka
Naye Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Dk Godwin Chitage alisema juzi wakiwa na Dk. Ulimboka walipigiwa simu na mtu wa usalama wa taifa (jina limehifadhiwa) akamtaka wakutane usiku huo.
“Walitoka Ulimboka na Dk. Deo wakaenda maeneo ya Kinondoni Sterio walipokutana naye akaanza kupiga simu likaja gari jeusi, wakashuka watu wanne wakiwa na silaha, na kumtaka Dk. Deo aondoke, ndipo yakaanza malumbano kabla ya kumzidi nguvu na kumwingiza kwenye gari kisha kuondoka naye”
“Tulipopata taarifa kutoka kwa Deo tukaanza kupiga simu ya Dk. Ulimboka ikawa haipatikani tena.Tulienda Oysterbay polisi kutoa taarifa lakini hatukupata ushirikiano wa kutosha tukaenda ‘Central’ (kituo cha Kati) tukaambiwa tusubiri hadi kesho hapo ilikua saa saba tangu saa tano walipomteka.
Alisema asubuhi walipata taarifa kutoka kwa msamaria mwema kwamba Ulimboka amepigwa sana na ametelekezwa kwenye msitu wa Pande, na walifuatilia ingawa anadai walikosa ushirikiano kwenye kituo cha polisi Bunju.  
“Kitendo alichofanyiwa mwenyekiti wetu kimetufanya kuwa imara zaidi katika kupigania haki zetu. Tutasimama kwa pamoja kwa gharama yoyote hata kama ni kutoa uhai wetu.
“Nawaomba watanzania wote wanaoitakia amani Tanzania walaani kitendo hiki, tunawalaani wote waliofanya juhudi za kumchelewesha Dk. Ulimboka kufika hospitali ili lengo lao la kumtoa uhai litimie,” alisema Dk. Chitage. 
Kauli ya MAT
Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimelaani kitendo alichofanyiwa Dk. Ulimboka na kusema kimewafadhaisha na kimewavunja moyo katika utendaji kati yao na serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la MOI alikolazwa Dk. Ulimboka, Mwenyekiti wa MAT Dk. Namala Mkopi alisema wamesikitishwa zaidi na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyoitoa bungeni jana baada ya kuulizwa kuhusu mgomo huo akisema liwalo na liwe.
“Kazi ya MAT ni kulinda na kutetea haki za watumishi wa sekta ya afya hususan madaktari kuhakikisha wanakuwa na mazingira bora ya kazi kwa manufaa ya wananchi.
Mkuu wa Polisi Salenda apigwa
Katika tukio lisilo la kawaida mtu mmoja anayedaiwa kuwa mkuu wa kituo kidogo cha polisi daraja la Salenda alipata kipigo kikali kutoka kwa kundi la madaktari, baada ya kuhisiwa kuwa ni mmoja wa watu waliohusika na kumtekaji nyara Dk Ulimboka.
Inadaiwa polisi huyo ambaye alihisiwa kuwa mtumishi wa usalama wa taifa, alichepuka baada ya kumwona Ulimboka na kisha akasikika akizungumza na wenzake kwa njia ya simu kwamba, alikuwa(ulimboka) hajafa.
Afisa huyo aliokolewa askari wanaolinda hospitali hiyo na kupelekwa kwenye chumba kidogo kilichopo jirani na lango la kuingilia hospitalini hapo, ambapo baada ya muda askari polisi zaidi waliwasili wakiwa katika gari lenye namba za usajili T226 AMV wakiingia na kutoka katika chumba hicho.
Majira ya saa 05:20 asubuhi gari aina ya Toyota lenye namba za usajili T716 BKZ ililiwasili na kumchukua afisa huyo ambaye alidai kupoteza “Redio call” na bastola yake katika shambulio hilo.
Kova aunda Tume ya Uchunguzi
Katika hatua nyingine, kamanda wa polisi wa Kanda Maalum ya dare s Salaam, Seelema Kova ameunda tume maalum ya wataalam wa jeshi hilo, kuchunguza kwa makini tukio zima la kushambuliwa kwa kiongozi huyo wa madaktari nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kova alisema tume hiyo itaongozwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ahmed Msangi, na kwamba wahusika watakaokamatwa watafikishwa mahakamani bila kujali ni akina nani.
Akizungumzia kupigwa kwa polisi Muhimbili, Kova alisema waliohusika walitenda kosa baada ya kudhani kuwa ni mmoja wa watu waliohusika kumpiga Ulimboka.
“Huyu alikuwa katika kazi ya operesheni kuwasaka waliohusika na tukio hilo. Na alifika pale kuhakikisha kama kweli amepatikana na ndio maana akachepuka pembeni kutuarifu kuwa alikuwa Ulimboka. Sasa wao wakachukua sheria mkononi na kuanza kumshambulia” alisema Kova

 Pinda kutoa tamko leo


KIPIGO alichokipata kiongozi wa madaktari, Dk. Ulimboka na kauli nzito aliyoitoa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu mgomo wa madaktari, kimelivuruga Bunge.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), ndiye aliyechafua hali ya hewa jana baada ya kutilia shaka kauli ya Waziri Mkuu Pinda na kipigo cha daktari huyo.
Jana asubuhi wakati Waziri Mkuu akijibu mwongozo wa Mbozi Mashariki, Godfrey Dhambi (CCM), aliyetaka kujua msimamo wa serikali kuhusu mgomo huo, alisema  leo Serikali itatoa uamuzi mzito kuhusu mgomo wa madaktari na 'Liwalo na Liwe'
Mbunge huyo alisema wakati madaktari walipotoa tishio la mgomo wiki mbili zilizopita, Waziri wa Afya, Dk. Hussein Mwinyi alitoa kauli ya Serikali Juni 22 kwamba Serikali imetekeleza madai ya madaktari na kuongeza posho.
Kwa mujibu wa Zambi licha ya kauli hiyo, madaktari katika baadhi ya hospitali ikiwemo Muhimbili walianza mgomo.
"Mheshimiwa Spika, leo nimepigiwa simu kutoka Mbeya, Dar es Salaam, Moshi nimeambiwa mgomo unaendelea. Naomba mwongozo wako, hatua gani Serikali itachukua kuwaokoa wagonjwa?"
Akijibu mwongozo huo, waziri mkuu Pinda alikiri kuwa kweli Serikali imeenda mahakamani kupinga mgomo huo na mahakama iliwazuia madaktari kugoma na kuwataka watangaze kwenye vyombo kwamba wamesitisha  mgomo.
Kwa mujibu wa Pinda, madaktari walikaidi amri hiyo na jana Serikali ilikimbilia tena mahakamani na mahakama ilikazia uamuzi wake wa awali.
"Tunafikiri sio vizuri kuingilia kazi ya mahakama lakini pia tulidhani madakatari wataheshimu amri ya mahakama.
"Kesho (leo) serikali itatangaza hatua za kuchukua. Maana wakati mwingine waswahili wanasema ' Litakalo  na Liwe,' alisema Pinda na kushangiliwa na wabunge wote.
Chadema yataka tamko
Hata hivyo, kauli ya Pinda imeleta tafrani baada ya wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee ambaye ni mbunge wa Kawe na Mbunge wa Ubungo John Mnyika kutaka maelezo yakinifu kuhusiana na mambo ya kutatanisha katika mgogoro huo.
Mdee alimtaka Waziri Mkuu Pinda kutoa maelezo ya serikali kuhusiana na tukio la kuvamiwa, kutekwa na kisha kupigwa vibaya kwa Ulimboka, akitiliwa mashaka kauli ya kiongozi huyo mkuu wa shughuli za serikali bungeni aliyedai kuwa sasa ‘liwalo na liwe’.
Mbunge huyo alidai kuwa kauli ya Pinda inaleta mashaka na hisia kuwa serikali inahusika na tukio la kinyama alilofanyiwa Dakta Ulimboka.

Naye Mnyika kukamatwa na kushambuliwa kwa kiongozi wa madaktari Ulimboka Steven utachochea zaidi mgogoro kati ya madaktari na serikali

“Udhaifu wa serikali kuharakisha kwenda mahakamani kabla ya bunge kupewa fursa ya kujadili madai ya madaktari na kuisimamia serikali umelifikisha taifa hapa tulipo” alisema.

Mbunge huyo aliliambia Bunge kuwa serikali inajikanyaga katika sakata hilo kwa sababu imekishitaki Chama cha Madaktari nchini (MAT), lakini iliyotangaza mgomo ni Jumuiya ya Madaktari.
Pia Mnyika aliomba Bunge liruhusiwe haraka kujadili hoja za madai ya madaktari ili kuisimamia serikali kwa mujibu wa ibara ya 63 (2) ilio kupitisha maazimio kupata suluhu wa mgogoro huo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametoa maelezo bungeni kuwa kesho tarehe 28 Juni 2012 Serikali itatoa kauli bungeni kuhusu suala la mgomo wa madaktari, hata hivyo kauli hiyo itatolewa kwa mujibu wa kanuni ya 49 (1) hivyo bunge halitaruhusiwa kujadili kauli husika na hivyo kukoseshwa fursa ya kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi.
Alisema bunge linakoseshwa fursa ya kusikiliza upande wa pili wa madaktari na wahudumu wengine wa afya ambao walipewa nafasi ya kuwasilisha maelezo na vielelezo vya upande wao kwenye kamati ya bunge ya huduma za jamii.
Mnyika alidai kumeshangaa Naibu Spika Job Ndugai kudai kuwa tayari kamati ya huduma za jamii imewasilisha taarifa bungeni wakati wabunge hawajapewa nakala husika na wala haijawasilishwa kwenye bunge kwa ajili ya kujadiliwa
“Ikumbukwe kwamba jana tarehe 26 Juni 2012 niliomba muongozo kuhusu kauli za mawaziri kwa mujibu wa kanuni ya 49 (2) na 116, hata hivyo niliruhusiwa kuomba kutoa maelezo kuhusu kauli ya serikali juu ya utekelezaji wa madai ya madaktari na uboreshaji wa maslahi ya madaktari.

Mnyika alisema kuzembea ama kupuuza kuchukua hatua dhidi ya udhaifu uliojitokeza kutaleta madhara zaidi kwa kuwa hata serikali ikichukua hatua za kudhibiti mgomo kwa kutumia vyombo vya dola, madaktari na watumishi wa afya wataendelea na mgomo wa chini kwa chini, hivyo afya na maisha ya wananchi yataendelea kuathirika kwa muda mrefu zaidi.

“Ikiwa wabunge tutaelezwa ukweli na kupewa taarifa kamili tutaweza kuisimamia serikali na kuwaeleza ukweli madaktari kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani na nichukue fursa hii kuwaomba madaktari kufanya kila kinachowezekana kuokoa uhai wa wagonjwa katika kipindi hiki kigumu” alisema Mnyika

Zitto: sitaki kuamini Tanzania tumefika huko
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ameeleza kuchukizwa kwake na tukio la kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dk Ulimboka, akidai mambo kama hayo yanatokea kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla
“Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko.
Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia ina wajibu kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake.
“Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa Chadema kufuatilia suala hili kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake” alisema Zitto.
Nchimbi asema serikali haihusiki

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi amesema kuwa serikali haihusiki na wala haijatoa maelekezo ya kumshambulia Ulimboka.
Aliahidi kuwa itafanya uchunguzi wa nguvu kuwanasa wahusika na kuwafikisha katika mikono ya dola.
Alisema daktari huyo alitekwa na watu wasiojulikana hadi katika msitu wa pande ambako alipigwa hadi kupoteza fahamu na baadaye kuokolewa na msamari




‘Madudu’ Wizara ya Fedha

*Katibu Mtendaji PPAA akalia ofisi miaka 8 kinyume

Na Edson Kamukara

KATIBU Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA), Bertha Grace Malambugi, anatumikia wadhifa huo kwa uteuzi batili kwa mujibu wa sheria za Manunuzi ya Umma, uchunguzi wa Tanzani Daima imebaini.

Malambungi ambaye alikuwa Mhadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IMF) jijini Dar es Salaam, alianza kuongoza chombo hicho tangu mwaka 2001 na kasha kupandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Mamlaka hiyo mwaka 2004.

Uchungizi wa Tanzania Daima ulibaini kuwa Malambugi aliteuliwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha kwa wakati huo, Gray Mgonja kwa barua yenye kumb: Na. C/JA 26/425/01 ya Novemba 2, 2004.

Hata hivyo, uteuzi wake huo ulikiuka sheria ya mamlaka hiyo ya mwaka 2004 kifungu cha 2 (c) na marekebisho yake ya mwaka 2011 kifungu 89 (1) kwa vile Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2001, ilifutwa sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2004 ambayo ilianza kutumika mwaka 2005.

Kabla ya mabadiliko hayo, mamlaka ya uteuzi wa Katibu wa PPAA yalikuwa kwa Waziri wa Fedha lakini baada ya hapo alipewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo Malambugi ameendelea kushikilia wadhifa huo bila uteuzi wake kuthibitishwa na Rais kama sheria inavyosema.

Vyanzo vyetu vya habari vinabainisha kuwa watendaji wenzake katika taasisi zilizoanzishwa chini ya sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2004 kama vile Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), walifanya jitihada kuhakikisha uteuzi uliofanywa kwa sheria ya mwaka 2001 unapata baraka na kuhalalishwa na Rais.

Alipotakiwa kufafanua utata wa uteuzi wake, Malambugi alisema kuwa habari hizo ziko kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, kwani ndiye mwenye mamlaka ya kujua kama una shida au hapana.

“Hata kama uteuzi wangu una utata mimi ningefanyaje, siwezi kuhoji mamlaka ya uteuzi, wewe kama unaona kuna makosa yalifanyika watafute wahusika Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na wengine waliopelekewa nakala za barua yangu,” alisema Malambungi.

Tanzania Daima ilimtafuta Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhan Khijja, ambaye alikiri utata wa uteuzi wa Katibu Mtendaji huyo na kusema kuwa wanaliangalia jambo hilo ili kupata ushauri wa kisheria.

“Nimezungumza naye nikiwa Dodoma baada ya wewe kumpigia simu, hivyo jambo hilo tunaliangalia kupata ushauri wa wanasherika maana alianza kabla ya sheria kubadilishwa sasa tunasubiri tuone watasemaje kama jina lake lipelekwe kwa Rais au namna gani.

Khijja alifafanua kuwa kwa vile sheria ilikuja ikakuta tayari Malambugi ameteuliwa, hivyo kisheria yeye kama katibu mkuu hawezi kulitolea uamzi, hivyo wanasubiri kuona Mwanasheria Mkuu atasemaje.

PPAA ilianzishwa kwa sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2001 (sheria Na 3) chini ya Wizara ya Fedha kama chombo huru cha kusikiliza malalamiko kutoka kwa wazabuni.




Mramba, Yona kujibu mashitaka
 
Na Happiness Katabazi

HATIMAYE Mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imewaona aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja wana kesi ya kujibu katika shauri la matumuzi mabaya ya ofisi ya umma  na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7
 
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Sam Rumanyika anayesaidiwa na Jaji John Utamwa na Saul Kinemela alisema jopo lao baada ya kupitia  ushahidi wa mashahidi 12 walioletwa na upande wa Jamhuri uliokuwa ukiwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali marehemu Stanslaus Boniface, Ben Lincoln wa Takukuru na vielelezo17 mahakama imewaona washitakiwa wote wana kesi kujibu.
Jaji  Rumanyika alisema kutoka na uamuzi wao washitakiwa wote sasa watapata fursa ya kujitetea ili mahakama nayo isikie utetezi wao.
Jaji Rumanyika aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 22,mwaka huu, ambapo siku hiyo washitakiwa wote wataanza kujitetea.

Siri vifo vya Wahabeshi 42 yajulikana

Na Martin Malera, Dodoma

SIRI ya vifo vya raia wa Ethiopia 42 waliofariki dunia kwa kukosa hewa kwenye roli la mizigo wakisafiria kwenda nchini Malawi, imejulikana.

Habari ambazo gazeti hili imezipata kutoka kwa majeruhi wa tukio hilo, zilisema kuwa waliopoteza maisha walikosa chakula baada ya kukaa kwenye gari kwa miezi mitatu mfululizo.

Mmoja wa majeruhi 72 walionusurika, aliliambia gazeti hili kuwa tangu walipoanza safari hadi siku waliyokutwa kwenye roli wilayani Kongwa, Dodoma walikuwa wamemaliza miezi mitatu wakiwa wameishiwa chakula walichohifadhi.

Alisema wametumia muda huo kwani walikuwa wakisafiri kwa kutumia njia za polini ambazo haziwezi kulifanya gari likimbie.

"Tulikuwa tunapita porini, hakuna barabara na mara nyingi tulisafiri usiku na mchana tunaegesha gari kusubiri giza ndo maana hadi jana tulipokamatwa tulikuwa na miezi mitatu," alisema.

Habari zaidi kutoka katika hospitali ya mkoa wa Dodoma zilikohifadhiwa maiti hizo, zilisema kuwa miili yao imeanza kuharibika kutokana na uwingi wa maiti ambao hauendani na uwezo wa kuhifadhi.

Kwa sasa vyombo vya usalama vina msaka wakala anayehusika na biashara ya kuwasafirisha wahamiaji haramu ambaye anadaiwa kuwa yupo nchini Kenya.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi alisema kuwa serikali inafanya mawasiliano na ofisi ya ubalozi wa Ethiopia nchini Kenya kwani hapa nchini hawana ofisi.

Taratibu za mazishi ziko chini ya ubalozi wa Ethiopia na serikali inaendelea kufanya mawasiliano kupatia ufumbuzi suala hili

Raia 45 wa Ethiopia walikutwa  wamekufa na wengine 72 kuwa taabani baada ya kukosa hewa katika lori walilokuwa wakisafiria kwenda Malawi.

Maiti za watu hao na wenzao ambao wako katika hali mbaya, waligundulika juzi asubuhi katika msitu wa Chitego wilayani Kongwa, Dodoma.

Usafirisha watu hao umekuwa  mchezo wa kawaida kwani Watanzania wanadaiwa kuwa ndio wanaosaidia kuwasafirisha.







-->

-->
Polisi Tarime iache
kuvuruga wananchi

KATIKA ukurasa wa mbele wa gazeti hili, kuna habari ya vurugu zilizozushwa jana na Jeshi la Polisi kwenye Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya mkoani Mara.
Chanzo cha vurugu hizo kilielezwa kuwa ni baada ya jeshi hilo kutumia nguvu na kuwatisha kwa silaha wananchi waliokuwa wakiomboleza msiba wa Mgosi Magasi Chacha, aliyeuawa na askari kwa kupigwa risasi juzi katika mgodi wa North Mara.
Kwamba polisi hao waliokuwa wamejazana kwenye magari wakiwa na silaha, walizingira hospitali ya wilaya hiyo wakitaka kuuchukua kwa nguvu mwili wa Chacha ili kwenda kuuzika.
Licha ya ndugu wa marehemu wakiongozana na mkewe na wananchi wengine, kujaribu kuwazuia askari hao wasiuchukue mwili huo, wakitaka taratibu za kisheria zifuatwe juhudi zao ziligonga mwamba.
Tunawapa pole ndugu wa marehemu Chacha pamoja na wafiwa wote walioguswa na msiba huo, lakini tunalaani vikali hatua ya Jeshi la Polisi kutumia mabavu kuuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuuzika wakati ndugu zake wapo.
Tunasema hivyo tukiwa bado na kumbukumbu za jeshi hilo mwishoni mwa mwaka jana kuwaua kwa kuwapiga risasi raia watano na kisha kuvamia hospitali wakitaka kuchukua miili ya marehemu kwa madai ya kwenda kuizika.
Hata hivyo, miili hiyo baadaye ilikutwa imetelekezwa vichakani ikiwa kwenye majeneza, jambo ambalo lilizidisha hasira, simanzi kwa wafiwa na hivyo vurugu kubwa kuzuka.
Sisi tunahoji ni lini Jeshi la Polisi limepata jukumu la kuwaua wahalifu na kuwazika kwa nguvu wakati familia zao ziko tayari kuwachukua na kuwazika kwa heshima?
Matukio haya yameanza kujirudia mkoani Mara pasipo viongozi wakuu kutoa kauli za kuyakemea, hatua inayoashiria kuwa wanakubaliana nayo.
Maana inashangaza kuona askari wanampiga risasi na kumuua mtuhumiwa wa wizi halafu hao hao kabla ya hata uchunguzi kufanyika kuthibitisha kama aliyeuawa alikuwa mwizi kweli, wanakimbilia kumzika kwa nguvu. Je, huku si kutaka kuficha ukweli?
Na hata katika mila na tamaduni zetu za Kiafrika, maiti huwa inazikwa kwa heshima zote kulingana na taratibu za jamii husika, ndiyo maana wanafamilia wanaachiwa kusimamia jukumu hilo. Sasa ubabe huu wa polisi mkoni Mara unalenga kuwataka wananchi hao wafanyeje?
Maana lazima ieleweke kuwa hata kama aliyeuawa alikuwa mwizi, bado ndugu zake wana haki zote za kuchukua mwili wake na kuhifadhi tayari kwa mazishi vyovyote vile watakavyo.
Tunaamini kuwa Jeshi la Polisi mkoani Mara na uongozi wa kitaifa watajitathimini na kujirekebisha, na hivyo kujiepusha na vurugu zisizo za lazima, zinazotokana na ubabe wao wa kuzingira hospitali kwa nia ya kuwapora wafiwa maiti za ndugu zao ili wakazizike kwa nguvu.

Mwisho




Shinikizo la POAC lamrejesha Mbajo

Na Betty Kangonga

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe amesema kuwa kamati hiyo iliamua kutopitia taarifa za hesabu ya Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC) hadi pale Mkurugenzi wake, Methusela Mbajo, atakaporudishwa katika nafasi yake.

 Mbajo alisimamishwa mwishoni mwa mwaka jana kupisha uchunguzi ndani ya CHC ulitokana na maombi ya Bodi ya shirika hilo baada ya kuwapo tuhuma kwamba menejimenti yake ilihusika na vitendo vya ufisadi.

Akizungumza na waandishi wa habario jana jijini Dar es Salaam, Zitto alisema kuwa kamati ililazimika kutopitia na kujadili taarifa za CHC hadi pale Mbajo atakaporudishwa kazini kutokana na uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutomkuta na makosa.

“Tulikubaliana kama kamati kwanza Mbajo arudishwe katika nafasi yake...wakitekeleza hilo ndipo sasa warudi kwa ajili ya kupitia taarifa yao,” alisema.

Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema kuwa CHC wameweza kutekeleza agizo hilo na jana wamemrejesha kazini mkurugenzi huyo.

Alisema ripoti ya hiyo inatarajiwa kujadiliwa Juni 6 mwaka huu,  kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge.

Katika mkutano wa nne wa Bunge ambao ulishuhudia mvutano, Zitto aliapa kuwa kama ingebainika alihongwa yeye au wajumbe wake wa POAC, angejiuzulu na kumtaka aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo naye ale kiapo kama hicho, lakini aligoma.




Mkapa asema niacheni

Na Grace Macha, Arusha 
RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa, jana alisema kwa sasa hataki kusumbuliwa kwa namna yoyote, badala yake ameomba aachwe huru ili ashughulikie matatizo aliyonayo.
Bila kutaja aina ya matatizo hayo, Mkapa alikataa kuzungumza na waandishi wa habari akidai kuwa hataki kuongeza matatizo mengine, kwa vile aliyonayo kwa sasa yanamtosha.
Mkapa alitoa kauli hiyo baada ya kuombwa na kundi la waandishi wa habari mara baada ya kutoka kwenye mjadala maalum kuhusu uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji barani Afrika, ulioandaliwa na Taasisi ya Uwezeshaji na Uwekezaji (ICF).
Waandishi walitaka kufanya mahojiano na Rais huyo mstaafu  kuhusiana na mambo kadhaa yakiwemo aliyozungumza katika mkutano huo, ambayo yalikuwa mazito na ‘mwiba’ kwa watawala wengi wa serikali barani Afrika.
“ Niacheni , nina matatizo yangu ya kunitosha, sitaki kuongea kwa sasa” alisema na kisha akaondoka.
Rais Mstaafu Mkapa amekuwa akishambuliwa na viongozi mbalimbali wa siasa kwa madai ya kuuza mashirika ya umma, kutumia wadhifa wake na kujimilikisha kampuni ya uchimbaji madini, akishirikiana na baadhi ya waliyokuwa mawaziri katika serikali yake.
Baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipendekeza rais huyo wa zamani akamatwe kwa kuhusika na tuhuma za ufisadi, kama ilivyofanywa kwa baadhi ya mawaziri wake wa zamani kwa tuhuma za ubadhilifu.
Mkapa aliingia hivi karibuni katika mzozo mzito na familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, baada ya kukaririwa akisema Mbunge wa Musoma, Vicent Nyerere (Chadema) hakuwa mtoto wa Mwalimu, kauli aliyoitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, wakati akimnadi mgombea wa CCM, Sioi Sumari
Mapema akizungumza katika mjadala uliohudhuriwa na washiriki toka makampuni na taasisi mbalimbali za bara la Afrika, Mkapa alisema alifanikiwa wakati wa utawala wake kutokana na sera yake ya uwazi na ukweli, na pia kujikita katika utekelezaji wa mipango.
Alisema sio vema kwa  viongozi wa nchi za Afrika kuzungumzia  mipango na mikakati ya maendeleo kila kukicha, badala yake waingie kwenye utekelezaji.
Alisema kuwa sera yake ya uwazi na ukweli ilisaidia kuwapa wananchi taarifa sahihi kuhusu hali ya uchumi, fedha na changamoto zote zilizoikabili Serikali na wao kupata fursa ya kushiriki kuzitafutia ufumbuzi.
 Mkapa alisisitiza umuhimu wa serikali za Afrika kuwawezesha kiuchumi wanawake na vijana waweze kujiajiri kwa kuwa hayo ndio makundi makubwa kuliko makundi mengine katika jamii hivyo itaziwezesha nchi hizo kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka na kukabiliana na tatizo la umaskini wa kipato.
 Alisema kuwa tatizo la ajira limesababisha vijana wengi kughiribiwa na wanasiasa ambao huwapa matumani hewa ya mafanikio, na wengi kuamini kuwa njia sahihi ya kujinanusa ni kujiingiza katika siasa
 Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa ICF, Omary Issa alisema taasisi hiyo imefanikiwa kuboresha mifumo mbalimbali inayopunguza usumbufu kwa wafanyabiashara na wawekezaji huku akitolea mfano wa mpango kuboresha mfumo wa usafirishaji mizigo kutoka bandarini mpaka nchi jirani wanaoutekeleza kwa pamoja na mamlaka ya mapato nchini TRA na Jeshi la polisi ambao utawezesha kuondoa vizuizi vyote vya kodi barabarani.
Alisema kuwa ICF imesaidia  kuboresha mfumo wa usajili wa makampuni nchini Rwanda ambapo kwa sasa huchukua siku 2 kusajili biashara tofauti na awali ambapo ilikuwa mpaka siku 16 huku gharama zikipungua kutoka dola za Marekani 433 mpaka 25.

Issa alisema kuwa taasisi yake katika kuhakikisha shughuli za biashara zinafanyika kwa urahisi na ufanisi zaidi imesaidia kuboresha mfumo wa mahakama nchini Zambia kwenye mahakama 3 na kutoa mafunzo kwa majaji wapya 14 huku nchini Sierra Leone wakifanikiwa kuboresha mfumo wa mahakama ambapo kwa sasa huchukua miezi miwili tokea kufungua kesi za biashara na kupata uamuzi ambapo awali ilikuwa inatumia mpaka miaka sita.




Chadema yaiumbua CUF


CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimegeuza mashambulizi yake na safari hii kimekishutumu Chama cha wananchi (CUF) kwa kile walichosema kuwahadaa watanzania kiasi cha kuaminika kuwa ni wapinzani wa kweli.
Mashambulizi hayo yaliongozwa na viongozi wawili wa juu wa Chadema, Mwenyekiti Freeman Mbowe na katibu Mkuu, Dk Wilbroad Slaa wakati wa mikutano mikubwa waliyofanya jana mkoani hapa.

Mbowe akifungua tawi la chadema katika eneo la Mihuta wilayani Tandahimba alisema mwanzoni walidhani CUF kilikuwa na dhamira ya kweli ya kuwakomboa wananchi na ndiyo maana waliwaachia mikoa ya kusini kwa ajili ya kuendeleza kazi hiyo.

Aliongeza kuwa dalili za wazi za CUF kushindwa kuwatumikia watu wa kusini zimeonekana wazi baada ya kuamua kufunga ndoa ya mkeka baina yake na ccm.

“Ninachoweza kuwaambia wana Mihuta ni kwamba Chadema, CUF  na CCM si baba yenu wala mama yenu na kama mtaona vyama hivi haviwasemei achaneni navyo, na kwa kuwa Cuf na CCM mlishawapa dhamana hiyo wakashindwa mviache sasa”alisema.


Mbowe, amewataka wananchi wa wilaya ya Tandahimba kuihukumu serikali ya CCM kwa vile haitetei maslahi ya watanzania hususan wakazi wa Tandahimba na sasa inatumia mabavu kuwatisha hata  katika haki zao za msingi hususan pale wanapodai kulipwa kulingana na nguvu zao zilizotumika

“Jamani Tanzania inasifika kwa kutajwa kuwa nchi inayofuata haki na sheria za binadamu lakini leo wanatandahimba mnapigwa mabomu na askari
wanaotumia kodi zenu kwa ajili ya kudai fedha za korosho ambazo kwa makusudi serikali imeamua kuwakopa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani” alisema Mbowe

Alibainisha kuwa hakuna haja ya wakazi wa Tandahimba na Mtwara kwa ujumla kwa kulazimishwa mazao yao kuuzwa kupitia stakabadhi ghalani wakati mikoa mingine haifanyiwi hivyo na wanauza mazao kwa matajiri wanaowataka na bei wanayoitaka


Dk Slaa atoboa siri ya CUF

Naye Dk Slaa alitoboa siri ya namna CUF kilivyoamua kuwa sehemu ya utawala, baada ya kufichua barua mbili zikiomba fedha kwa ajili ya kuhudumia chama na safari za kifamilia za Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.

Alisema barua ya kwanza ya Katibu Mkuu wa Cuf Maalimu Seif kwenda serikalini inaomba kuwezeshwa kufanyika kwa mkutano wao chama kwa siku tatu katika eneo la Bagamoyo kwa gharama za sh. milioni 34.

Dk Slaa alisema barua ya pili ni ile inayoomba dola za kimarekani 10,000 kwa ajili ya nauli ya kwenda Nairobi Kenya kwa mke wa Maalim Seif kwa safari ya
kifamilia, ikiwa ni sawa na dola 1,000  kwa siku.

Aidha Dk Slaa alisema katika taarifa hiyo inaonyesha pia kuna fedha za dharura kwa ajili ya matumizi ya makamu wa Rais ambayo ni dola 3000 na kudai kuwa huo ni ufisadi usioweza kuvumiliwa na wapenda haki.

Alisema kwa mfumo huo wa CUF kutegemezi hata katika mikutano yake ya chama fedha za serikali, ni ushahidi wa wazi wazi kuwa inafanya kila kitu kwa kuongozwa na
serikali ya ccm.




Mgeja awashukia wasomi
Na Mwandishi wetu, Kahama
MWENYEKITI  wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicvho, Hamis Mngeja amewashukia wasomi hapa Nchini kwa kuendekeza mambo ya semina, makongamano,warsha pamoja na tafiti mbalimbli huku wakiicha nchi ikiendelea kudidimia kiuchumi.
Mngeja ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali la Mzalendo Foundation, aliliambia Tanzania Daima kuwa baadhi wasomi  wameshindwa kutumia utaalamu wao kulisaidia taifa hususan kuinua maisha ya wakulima ambao sasa wanakandamizwa.
Alisema mfumo wa bei za mazao ya wakulima katika masoko hauelweki na kusababisha kuyumba kwa bei ya mazao kila wakati na kusababisha mkulima badala ya kunufaika na bei inamdidimiza.
Mgeja alimwomba Waziri wa  Kilimo Christopher Chiza kusikia kilio cha wakulima wa mazao hususan yale ya Biashara ambayo yamekumbwa na mtikisiko wa kuporomoka kwa  bei mara kwa mara.
Aliitaka  Serikali kujielekeza katika kulinda viwanda na kutumia malighafi za ndani badala ya kupeleka nje ya nchi jambo linalowanufaisha mataifa mengine.
Alisema kuwa ikiwa taifa litawekeza kwa wingi katika viwanda vya ndani uchumi wa nchi utakuwa imara na thamani ya kilimo itapanda na kupendwa na kila mtu kwa sababu ndio njia pekee anayoamini itawasaidia wananchi kuondokana na umasikini walionao.
Mwisho





Kesi ya mauji ya mtoto wa Fundikila yaiva

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Juni 4-8 itaanza kusikiliza kesi ya mauji ya mtoto  wa Chifu Abdallah Fundikila, Swetu Fundikila inayowakabili MT 1900 Sajenti Roda Robert(42) wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha Mbweni na wenzake.

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya uendeshaji wa kesi za Mahakama Kuu ambayo gazeti hili imeiona nakala yake, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na Jaji Zainabu Mruke na jumla ya mashahidi tisa wa upande wa jamhuri watoa ushahidi katika kesi hiyo.

Mbali na Dorisi washtakiwa wengine ni  MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Kikosi cha Kunduchi na MT 85067 Koplo Mohamed Rashid wa JKT Mbweni.

Wakili wa serikili Dionisia   Saiga awali alidai mahakamani hapo kuwa Januari 23 mwaka 2010  kuanzia majira ya saa 6 usiku, kuwa marehemu akiwa na wenzake wawili wakitumia gari aina ya Toyota Corolla, wakitoka Mwananyamala walikutana na washtakiwa wakiwa kwenye gari lao wakitokea kwenye maegesho ya magari ya Baa ya Mango Garden.
Wakili Saiga alidai kuwa mshtakiwa wa kwanza alimwamuru dereva wa gari alilokuwemo marehemu, arudi nyuma na kwamba dereva huyo alitii.Alidai kuwa washtakiwa walilifuata gari hilo na kusimama pembeni na baadaye mshtakiwa wa kwanza alishuka na kumfuata dereva na kumuonya kuwa siku nyingine asipowaheshimu viongozi wa nchi atapata shida.

Aliendelea kudai kuwa baada ya hapo marehemu na wenzake waliondoka lakini walipofika kwenye makutano ya Barabara ya Kawawa na MwinyiJuma, walikutana tena na washtakiwa ndipo mshtakiwa wa kwanza akawatukana.
Alidai kuwa marehemu aliuliza sababu ya kuwatukana bila kosa, lakini mshtakiwa wa kwanza alimpiga dereva, jambo lililomlazimisha marehemu kuingilia kati kuamlia.
mwisho




Vurugu Z’ bar zina mkono wa vigogo

Betty Kangonga na Asha Bani


KANISA la Pentekoste Tanzania limedai kuwa vurugu zilizotokea visiwani Zanzibar na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali, zina msukumo wa baadhi ya viongozi wa siasa na dini.

Kiongozi mkuu wa Kanisa hilo, William Mwamalanga aliliambia Tanzania Daima jana kuwa baadhi ya viongozi wa siasa wanaouchukia Muungano, na wale wenye malengo ya kidini waliwatumia vijana kufanya vurugu hizo.

‘Kuna siri nzito iliyojificha katika vurugu hizo. Wapo baadhi ya viongozi nyuma ya vurugu hizo kwani muungano umetumiwa kama kigezo.

‘Chokochoko za muungano hazijaanza leo wala jana maana tunafahamu wazi kuwa wapo baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakiupinga muungano huo ndani ya Bunge na hata nje hivyo imefika wakati kwa watawala wetu kuwa wakweli juu ya suala hilo,’ alisema.

Mchungaji huyo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kupambana na dawa za kulevya, alisema kuwa kauli za baadhi ya viongozi zinazotolewa juu ya suala hilo zimekuwa chachu za vurugu hizo.

Alidai kuwa anaamini matatizo ya muungano haytamalizwa kwa kupatikana katiba Mpya bali kinachopaswa ni viongozi wanaofahamu umuhimu wa suala hilo kuweka wazi kwa wananchi ili waweze kuujua kwa undani.

‘Watawala wawaeleze vijana umuhimu wa suala hilo hata kama kuna mchakato wa katiba mpya bado itakuwa shida kwa kuwa vijana hawaelewi ulazima wa ushirikiano huo,’ alifafanua.

Alisema watawala wanapaswa waandae kipindi maalum ili kuujadili muungano huo na sio maana kwa sasa suala hilo limevuka mipaka na kutumiwa kama kigezo cha uhalifu na uvunjifu wa amani.

Hata hivyo alimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema kupata muda na kukutana na wazee wa visiwa hivyo pamoja na viongozi wa kisiasa ili kutafuta suluhu ya kudumu juu ya suala hilo.


Utalii haujavurugwa


Katika hatua nyingine, serikali imesema vurugu zilizotokea Zanzibar haikuathiri soko la utalii kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya Kenya na katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema mitandao na vyombo hivyo vinalenga havikusema ukweli na vinalengo la kuichafua Tanzania.

Alisema hali ya amani katika mji Mkongwe imetulia  na kwamba hakuna taarifa zozote za uharibifu wa maeneo ya vivutio vya utalii wala kuchmwa kwa hoteli yeyote ya kitalii mjini humo.

“Serikali inawahakikishia wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa hayo yalikuwa matukio ya kipekee nay a kupita na hatua zimechukuliwa na Jeshi la Polisi kuongeza usalama kwa wakazi na watalii,”alisema Nyalandu.

Hata hivyo alikiri kuwepo kwa matukio ya kuporwa kwa watalii na vibaka ambapo hivi karibuni watalii wanne wamefanyiwa vitendo hivyo katika maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam ambao yamefanywa na watu waliotumia magari na pikipiki.

Hivi karibuni katika mji wa Zanzibar kumetokea na vurugu zilizopelekea kuchomwa kwa makanisa pamoja na shule jambo ambalo viongozi mbalimbali wa serikali na wa kidini wametoa tamko.


Mwisho.
-->
-->
-->



Slaa amlipua Waziri Ghasia

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Chadema) Dk Willbroad
Slaa amemtaka Mbunge wa Mtwara vijijini Hawa Ghasia kuacha kutisha na kuwakamata wananchi wanaomuuliza maswali katika mikutano ya hadhara akidai amekashifiwa.

akihutubia umati wa wananchi katika Kata ya Mtimbwilimbwi na Nanyamba, Slaa alisema ni uvunjaji wa sheria na ubabe kukamata wananchi waliowapigia kura.

Slaa alisema hayo baada ya wananchi kumwelezea kuwa wamekuwa wakikamatwa na viongozi wa Serikali na CCM wanapouliza maswali, ndio maana wameingiwa woga.

Alisema Waziri Ghasia anafanya vitendo hivyo kwa kuwa ana uhakika wa kutogombea tena ubunge katika jimbo la Mtwara vijijini baada ya kutambua kuwa hawezi tena kushinda

Slaa alisema maisha ya wakazi wa Mtwara vijijini na umasikini unaowazunguka ni aibu kwa uongozi katika miaka 50 ya uhuru, ambapo akina mama wajawazito wanalazimika kwenda hospitali wakiwa na vifaa.

“Enzi za Mwalimu Nyerere hakukuwa na suala hilo leo hata mtoto mdogo anajua kuwa mama yake anakaribia kujifungua kwa kuwa ni lazima atakuwa anahangaika kutafuta vifaa vya kujifungulia.”alisema Dk Slaa

Alibainisha kuwa jimbo la Karatu ambalo wananchi wake hawakuwahi kuwa na waziri kwa miaka 15 sasa wanafikiria kuingiza maji ndani ya nyumba zao wakati Mtwara vijijini ambayo Mbunge wake ni waziri wananchi wanatafuta maji umbali wa zaidi ya kilometa 10 kufuata maji.

Katika hatua iliyoonesha kukithiri kwa umasikini, Dk Slaa alilishwa supu ya ngozi ya ng’ombe kama kitoweo, ambapo walidai wamefanya hivyo kwa kuwa hawana uwezo wa kununua nyama.

walisema hata hizo ngozi ni lazima aende mtu kuzifuata Mtwara mjini na siku inapokosekana wanajihesabia kama wamekosa nyama halisi

Kufuatia hali hiyo Dk Slaa aliwataka wananchi wa Mtwara mjini
kujiepusha na kuuza uhuru wao kwa gharama ya shilingi elfu tano na badala yake wasimamie ukombozi wa kweli

Mbowe kumbana Waziri Mkuu

Akizungumza katika mkutano aliyoifanya katika kata za Madimba na Tangazo, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe amesema kuanzia sasa atakuwa msemaji wa wakazi wa mkoa wa Mtwara kwa kuwa hawana msemaji wa shida zao hususan zao la korosho na gesi.

Alisema akifika bungeni swali lake la kwanza kwa waziri mkuu ni kumuuliza serikali ya CCM inatumia sera gani kuchimba gesi katika mkoa wa Mtwara.

Mbowe alishangazwa na kitendo cha serikali kuweka nguzo za umeme katika maeneo yenye nyumba za nyasi, na kukiita kama dharau, na kwamba ilipaswa kwanza kuhakikisha wananchi wake wana nyumba bora.


Wenje amvaa Mbatia

Mbunge wa  Nyamagana Ezekiel  Wenje (Chadema) amemshambulia Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Nccr Mageuzi, James  Mbatia akidai amefungishwa ndoa ya mkeka na CCMapinduzi, kwa kupewa ubunge
wa Viti Maalum na Rais Jakaya Kikwete ili kumsaidia kutekekeza ilani  isiyotekelezeka.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Majengo katikati ya mji wa Mtwara juzi,Wenje alisema  kitendo cha Mbatia kukubali ubunge wa viti maalum
kimeonyesha udhaifu wake mkubwa  kwamba sio mpinzani wa kweli wa kupinga ufisadi na ubadhirifu unaofanywa na Serikali ya CCM.
Hatua hiyo ya Wenje kumuita mbatia mbunge wa viti maalum iliibua mvutano katika mkutano huo baada ya makundi ya watu kutofautiana wengine wakisema hata Chadema kuna wabunge wa viti maalum

Kutokana na mabishano hayo ilimlazimu Wenje mwisho wa mkutano kutoa ufafanuzi jinsi wabunge wa viti maalumu wa chama wanavyopoatika na wabunge wanaoteuliwa na rais kwa mujibu wa mamlaka ya  ibara ya 66 (1)
(a) ya katiba ya nchi.

“Ndugu zangu hakuna  sababu ya kubishana hapa, wapo wabunge wa viti maalum wa chama husika wanaotokana na idadi ya wabunge halali waliochaguliwa kwa kura za wananchi, na wapo wabunge wa kuteuliwa na Rais kwa mujibu wa kifungu hicho,wote ni wabunge  lakini tofauti yao ni huyu ni wa Rais na huyu ni wa wabunge.







JK Tumepwaya

afichua kisa cha kuachwa Ma-DC

RAIS Jakaya kikwete amekiri kuwa watanzania wengi wamekosa imani na serikali yake kwa kile alichodai kuwa kimechangiwa na utendaji mbovu wa baadhi ya watumishi.

Kikwete ametamka hayo jana, alipokuwa akifunga semina ya mafunzo kwa wakuu wa mikoa na wilaya iliyokuwa ikifanyika mjini hapa, na kudai kuwa utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji wa serikali yake, umewafikisha wananchi wengi kuichukia serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Alisema taifa limekosa kukosa maendeleo kutokana na tabia ya baadhi ya watendaji, kujihusisha na rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma na uonevu, mambo ambayo yamewakatisha tamaa wananchi.
Aidha aliongeza kuwa tabia ya viongozi kuchelewesha maamuzi katika kutatua kero za watu, zimekuwa zikiwakasirisha wananchi, na kutoboa kuwa ndizo zilizomfanya kuwaacha baadhi ya waliokuwa wakuu wa wilaya.
Ameongeza kuwa baadhi ya wakuu hao wa wilaya, waliiuka maadili ya ya utumishi ikiwa ni pamoja na ulevi uliokithiri.
Kutokana na hali hiyo, Kikwete aliwaagiza viongozi hao kufanya kazi zao kwa uangalifu, kutotumia ubabe na kuheshimu mipaka na mgawanyiko wa majukumu yao ya kila siku.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amewataka viongozi na watendaji wa serikali kujiuzulu na kuwaachia vijana  wasomi nafasi hizo ili waweze kutumia elimu yao kujenga taifa.
Alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wazee kuwapisha vijana, watumie nguvu na elimu yao, na wao wabaki pembeni wakiwa washauri katika mambo mbalimbali, badala ya kunga’ang’ania madaraka hata katika umri huo mkubwa.
Semina hiyo ilikuwa na lengo la kutoa mafunzo kwa wakuu wa mikoa na wilaya, kabla ya kuanza rasmi kazi zao, kufuatia kuteuliwa kwao na Rais Kikwete hivi karibuni.


-->

Nchimbi aonya vurugu Z’bar
·        30 wapandishwa kizimbani

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI  wa mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, ameliagiza jeshi la polisi nchini kumkamata mtu yeyote atakayechochea fujo na vurugu visiwani hapa bila kujali wadhifa wake.

Akizungumza na viongozi viongozi mbalimbali wakiwemo wanajumuia za maimamu (Jumaza) pamoja na mwakilishi wa mabalozi katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani Kilimani, katika mkutano uliohudhuriwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema. Nchimbi alisema, watanzania wanahitaji amani ambayo inatakiwa kulindwa na kila mtanzania.

Nchimbi ambaye alidai kuridhishwa na kurejea kwa utulivu katika viunga vya mji huu, alisema serikali haiwezi kamwe kunyamaza na kuwaachia watu wachache wakivuruga amani na kuhatarisha usalama wa wengi.

Bila kutafuna maneno, waziri huyo alikiri kutofurahishwa kwake na mwenendo mzima wa kikundi cha uamsho kinachotuhumiwa kushiriki vurugu kubwa zilizozuka kwa siku mbili zilizopita.

Alisema jumuia hiyo, ambayo kwa karibu mwaka mzima wamekuwa wakiitwa na kuonya na polisi dhidi ya matamshi mbalimbali yaliyolenga kuwagawa watanzania, lakini mara tu wanapotoka katika meza ya mazungumzo hurejea tena kuhubiri yaleyale, jambo alilosema sio la kiungwana.

“Hata katika mikutano na maandamano ya juzi walikuwa na haki ya kufanya maandamano, na walitakiwa kuomba kibali na kupatiwa ulinzi, jambo ambalo hawakulifanya” alisema.

Aliwaomba viongozi wa serikali kushirikiana na kuona wananchio wanarudi katika hali nyao za zamani na kusisitiza jeshi kutosita kuchukua hatua kwa yeyote akateyevunja sheria.

Nsaye sheikh kutoka msikiti wa Amir Tajo, Omar Mohamed Ali , alimtaka waziri huyo kuangalia kanda za jumuia za uamsho na kuona kama kuna uvunjifu wa amani, na kudai kuwa juzi walifanya matembezi ya hiyari bila kudhuru mtu, ambapo polisi walikuwa na habari ya matembezi hayo na badala yake, walimchukua sheikh wao kwa njia ya kumteka nyara hali iliyozua hisia tofauti kwa wananchi.

Katika hatua nyingine watu 30 wakiwemo viongozi watatu wa jumuiya ya Uamsho akiwemo  Mussa juma Issa wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe wakikabiliwa na tuhuma kukusanyika na kuandamana bila kibali na kufanya fujo

Viongozi na watu hao hata hivyo, wameachiwa kwa dhamana ambapo upelekezi wa kesi hiyo bado unaendelea.

Vurugu kubwa zilizuka juzi mjini hapa ambapo, kundi la watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa Uamsho  walifanya ghasia kubwa ikiwemo kuchoma magari, kushambulia nyumba ambapo kanisa moja la T.A.G Kariako lilichomwa moto na kuharibiwa vibaya kwa magari ya watu.

Aidha, katika vurugu hizo, inadaiwa kwamba watu wasiofahamika walianza kusaka nyumba wanazoishi watu kutoka Tanzania bara wakitishia kuwauwa.

Marekani yahuzunika
Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, ameeleza kusikitishwa kwake na vurugu zilizozuka mjini hapa, na amewataka viongozi wa makundi yote kuhakikisha kuwa wanasimamia amani na utulivu kwa nguvu zote.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Balozi huyo alisema vurugu hizo zimetia doa amani, umoja na mshikamano ambao umekuwepo tangu uchaguzi mkuu uliyopita, na kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Amesema ni vema kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kulinda amani kwa kuwa ghasia hizo zitaleta athari kwa uchumi wa nchi na kuwagopesha watalii na wawekezaji wa kigeni kuingia nchini.

Uamsho yakana kuchoma kanisa
Katika hatua nyingine, Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), imepinga kuhusika kuhamasisha kufanya machafuko yaliyotokea mji wa Zanzibar usiku wa Mei 26 na kusababisha kuchomwa moto kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) la Kariakoo ikiwa ni pamoja na kuharibu magari, miundo mbinu na mali nyingine.
 
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari imesema; “kama alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshima zenu ila kwa haki ya Uislamu (maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukumu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa, Mahekalu na sehemu nyingine za ibada) zisivunjwe wala zisiharibiwe”.

Jumuia hiyo ilitoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za Serikali, mali za Wananchi, Taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu.

Taarifa hiyo ilibainisha kwamba matukio hayo wanayachukulia kama njama za makusudi za wale wasioipendelea amani ya nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao.

“Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine kwani wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu,” ilisema taarifa hiyo.

Mwisho.






Zanzibar yachafuka
  • Makanisa, magari yachomwa moto
  • Vita ya mabomu, mawe yalindima
  • Raia wa Bara wawindwa, wapigwa
  • Kisa ni suala la kuwepo kwa Muungano

Na Waandishi wetu, Zanzibar


Machafuko makubwa yameukumbuka mji wa Zanzibar juzi na jana, ambapo Kanisa moja limelipuliwa na kitu kinachoaminika kuwa bomu la kurusha kwa mkono, huku kukiwa na madai kuwa watanzania wenye asili ya Bara wanaoishi na kufanya kazi visiwani hapa wakishambuli.

Mashuhuda wameliambia Tanzania Daima kwamba, watu ambao hadi sasa hawajajulikana lakini wakiaminika kuwa ni wafuasi wa kundi la kidini la uamsho, walilishammbulia na kulilipua Kanisa la Tanzania Assemblies Of God la Kariakoo, kuharibu magari, miundombinu na mali nyingine.

Taarifa hizo zilizothobitishwa na jeshi la polisi, zimesema kuwa wafuasi wa kundi hilo walianza vurugu hizo wakipinga kitendo cha kukamatwa kwa kiongozi wao, Mussa Juma kwa kosa la kufanya maandamano bila kibali cha polisi.

Habari zimedai kuwa baada ya kukamatwa kwa kiongozi huyo, wafuasi wake walianza kuhamasishana kwenda kituo cha polisi Madema, kilichoko wilaya ya Mjini Magharibi wakiwa na silaha za mawe, jambo lililowafanya polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Hata hivyo, habari zinadai kuwa baada ya kutawanyika majira ya saa mbili usiku wafuasi hao walianza kuziba barabara kwa mawe na magogo makubwa, kuchoma matairi katika maeneo ya michenzani, kabla ya kuyashambulia na kuharibu vibaya magari kadhaa.

Aidhaa mashuhuda wamedai kuwa baadhi ya wafuasi hao walianza kuzisaka nyumba za ibada na ndipo walipokwenda lilipo kanisa hilo, na kuanza kulishambulia kwa mawe, kabla ya kulilipua kwa kitu kinachoaminika kuwa bomu

Kadhalika, kuna madai kuwa wafuasi wengine wa kundi hilo, walijigawa na kuanza kuzifuatilia nyumba wanamoishi wafanyabiashara na wafanyakazi wanaotoka Tanzania Bara na kuzishambuli kwa mawe, huku wakitoa maneno ya vitisho.

Mmoja wa watanzania hao anayefanya kazi katika hoteli moja ya kitalii (jina linahifadhiwa) alikiri nyumba yao kushambuliwa vikali, na jana alilazimika kuhamia kwa rafiki zake ambao ni wenyeji wa visiwa hivi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishna Musa Ali katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari, amekiri kuharibiwa kwa kanisa hilo na kwamba hadi jana mchana watu saba walikuwa wakishikiliwa na jeshi hilo.

Kamishina Ali alisema, kundi hilo Mei 26 katika mwendelezo wake wa kufanya  mikusanyiko kwa ajili ya makongamano, mihadhara, dua na itkafu wakiwa katika viwanja vya Lumumba majira vya asubuhi kwa dhamira ya kusasababisha watu  wauchukie Muungano na kuitaka serikali iitishe kura ya maoni kuhusu kuendelea, au kutoendelea kwa Muungano na serikali zake.

Alisema pamoja na kufanya matendo mengine ya uvunjifu wa  amani kinyume na lengo la kuanzishwa kwa jumuia hiyo na katiba yao, majira ya saa za mchana viongozi wao waliwahamasisha watu waliokuwa watu katika kongamanao hilo kufanya maandamano bila kuarifu polisi.

Kamishna Ali alidai, kutokana na historia ya nyuma ya kundi hilo, polisi walilazimika kuyavunjwa kwa vile katika siku za karibuni jumuiya hiyo ilikwishaonesha dalili za uvunjifu wa amani kwa kuyfanya matendo mbalimbali ikiwemo kutoa lugha ya matusi kwa viongozi wa serikali na wananchi ambao hawakuwaunga mkono.

Alisema kundi hilo limekuwa likifunga barabara bila sababu, kutembea na ving’ora isivyo halali, kuwashambulia watu kwa silaha zenye ncha kali, kuharibu mali za watu kama magari, na vingine vya aina hiyo.

Kutokana na tukio hilo, Polisi wametangaza msako mkali wa kuwasaka viongozi na wanaokiwafadhili kikundi hicho kwa gharama yoyote waliohusika na furugu hizo na kwamba watakaopatikana watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka.

Kamishna huyo amesema polisi na vikosi vya usalama wameimarisha ulinzi kuhakikisha kuwa usalama wa maisha ya watu na mali za unadumishwa kwa gharama yoyote.

Chadema wailaumu Serikali

Jijini Dar es Salaam, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema Rais Jakaya Kikwete, Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na CCM wamesababisha  mivutano na vurugu Zanzibar kwa kutaka kudhibiti  mjadala kuhusu muundo wa  muungano na uhuru wa nchi katika mchakato wa katiba mpya kwenye suala hilo tete na tata.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaa, Mkurugenzi wa habari wa Uenezi wa chama hicho, John Mnyika ambaye alisema mivutano na virugu zinazoendelea Zanzibar ni matokeo ya serikali ya Muungano na ya Mapinduzi Zanzibar kutokuzingatia mapendekezo ya chama hicho kuhusu umuhimu wa uhuru wa mjadala kuhusu muundo wa muungamo katika mchakato wa katiba mpya.

Aidha, alisema mvutano huo umeshika kasi baada ya maamuzi ya NEC ya CCM bila ya maoni ya wanachama wake wa Zanzibar na bara kuminya mjadala kuhusu suala hilo.

“Maamuzi hayo ya NEC yaliyotanguliwa na kauli ya Rais Kikwete kudhibiti mjadala kuhusu hatma ya muungano. Jana na leo pamekuwapo na vurugu Zanzibar kati ya wafuasi wa kikundi cha uamsho na vyombo vya dola, kukamtwa ni matokeo tu,” alisema Mnyika

mwisho 







AJALI:

habari za kuaminika zinasema kuwa Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, Chadema, amepata ajali mbaya ambayo imesababisha kifo cha mama yake mzazi, Gloria Shao na wengine wawili.
ajali hiyo imetokea majira ya saa 12.45 jioni ya leo, katika eneo la Boma Ng'ombe wilayani Hai, mkoa wa Kilimanjaro wakati alipojaribu kumkwepa mwendesha pikipiki na ndipo gari lake likaacha njia na kupinduka.

Selesini akiongea nami kwa shida kutoka katika hospitali ya wilaya ya hai, alisema kuwa anajisikia maumivu makali kifuani na alikuwa hajui hali ya mama, mke wake na wengine

-->
 Mnyika ashinda
Na Happiness Katabazi
 HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemtangaza Mbunge wa Jimbo la Ubungo,John Mnyika (Chadema) kuwa ndiye mbunge halali wa jimbo hilo na matokeo ya uchaguzi ya jimbo hilo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Novemba mwaka 2010,yalikidhi matakwa ya kisheria.
Uamuzi huo ulisababisha jiji la Dar es salaam kuzizima kwa shangwe na nderemo na baadhi ya barabara zikifungwa kwa muda kutokana na umati mkubwa wa wafuasi na  wanachama wa Chadema waliokuwa wakishangilia ushindi wa mbunge huyo.
Akisoma hukumu hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa shauku kubwa ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na maelfu ya wafuasi wa vyama hivyo, Jaji Upendo Msuya alitupilia mbali hoja moja baada ya nyingine, kabla ya kuhitimisha na kufutilia mbali pingamizi lililowekwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Hawa Ng’umbi.
Akichambua dai la kwanza, la kwamba mdaiwa wa pili(Mnyika) aliingiza Laptop binafsi  katika chumba cha kujumlishia kura ambazo zilimuongezea kura hewa14,857 ambazo hazikuhesabiwa, jaji huyo alisema mashahidi wa tatu wa mlalamikaji walishindwa kuthibitisha dai hilo katika ushahidi wao.
“Hoja katika dai hili ni je Laptop hizo zilitumika kuongezea kura au la..lakini mahakama baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili umeona Ng’umbi ameshindwa kutoa vielezo au kuleta ushahidi wa kuunga mkono dai lake kwamba kompyuta hizo mali ya Mnyika ambazo kisheria hazikupaswa kutumika kujumlishia kula, zilitumika na kwa sababu hiyo mahakama hii inatupilia mbali dai hilo”alisema Jaji Msuya.
kuhusu hoja ya kura 14,857 zinazodaiwa kuwa hewa, jaji huyo alisema amelazimika kuzifanyia mahesabu idadi za kura walizopata ambapo alisema Mnyika alipata kura 66,742, Ng’umbi 50,554 jumla ya kura hizo ni 117,286 na wagombea wengine 14 toka vyma vingine walipa kura 15,210  kwa hiyo jumla ya kura zote walizopigiwa wagombea wote 16 ilikuwa ni 132,496.
“Kura 14,857 zinazobishaniwa na mdaiwa  zinaweza kuhesabiwa  kwa jumla ya wagombea 16  ambao walipata  132,496 ambapo kura halali zilizopigwa ni 117,639 ,kura zilizoaribika ni 2,184  unapata jumla  kura 14,857.
Alisema baada ya kufanya hesabu ya kura hizo alibaini kuwepo kwa tofauti ya kura 353 sawa na asilimi 0.3 ya jumla ya kura halali zilizopigwa.
“Katika akili yangu nimetafakari dai hili ,pia nimezingatia mazingira ya kujumlishia kura  yaliyoelezwa na pande zote katika kesi hii, nimezingatia muda wa kazi na kielelezo kilicholetwa na upande wa utetezi ni sahihi na dosari ya kura 14,857 haikuweza kufanywa na laptop hizo na Mnyika hakupinga kuingia nazo kwaajili ya kuhakiki kura ambazo zilishahesabiwa na maofisa wa NEC .
“Kwa maelezo hayo hapo juu mahakama hii inasema hata sheria  haikatazi wakala wa mgombea  kuingia na laptop  kwenye chumba cha kujumlishia kura na pia Ng’umbi ameshindwa kuleta wataalamu wa kompyuta waje kutoa ushahidi ambao ungeonyesha laptop hizo zilitumika kujumlishia kura na kwa maana hiyo ombi hilo nimelikataa ”alisema Jaji Msuya.
Kuhusu dai kuwa Mnyika aliingiza  watu zaidi ya nane ambao hawakustahili katika chumba cha kujumlishia kura, jaji huyo alisema Ng’umbi ameshindwa kutoa ushahidi na hata kama waliingia waliathiri vipi taratibu na kanuni za uchaguzi wa jimbo hilo.
 Kuhusu dai la Mnyika kwamba alimkashifu Ng’umbi katika mkutano wake wa hadhara alioufanya Septemba mwaka 2010 na kudaiwa alimuita ni fisadi kwasababu aliuza nyumba za UWT ,alisema pia mlalamikaji huyo ameshindwa kuthibitisha dai hilo kwani lilijikita katika misingi ya ushahidi wa kusikia ambao hautakiwi mahakamani.
“Kwa kuitimisha mahakama hii imetupilia mbali madai yote ya mlalamikaji na kwa kauli moja inamtangaza Mnyika kuwa ndiye mbunge halali wa jimbo la Ubungo na kwamba taratibu zote za uchaguzi zilifuatwa “alimaliza Jaji Msuya na kusababisha kulipuka kwa nderemo na vifijo toka kwa wafuasi wa Chadema.
Ng’umbi aondoka kwa huzuni
Muda mfupi mara baada ya kutolewa kwa hukumu, malalamikaji katika kesi hiyo, Hawa Ng’umbi, aliondoka mahakamani hapo kwa huzuni huku akisindikizwa na baadhi ya wanachama wa CCM waliofika hapo kusikiliza kesi hiyo.
Akizungumzia juu ya kama ana nia ya kukata rufaa, Ng’umbi alisema bado anatafakari ili aweze kupata majibu kama atakata rufaa ya kupinga hukumu hiyo.
Alisema atakaa na uongozi wa juu wa chama chake kwa ajili ya kuangalia kama kutakuwa na uwezokano wa kufanya hivyo, haraka iwezekanavyo.
”Hadi sasa siwezi nikasema lolote juu ya kukata rufaa, lakini nitatolea ufafanuzi juu ya hilo pindi nitakapokaa na uongozi wa juu na kulijadili suala hilo,”alisema Ng’umbi.
Katika kesi hiyo  Ng’umbi alitetewa na wakili wa kujitegemea Issa Maige, wakati Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitetewa na wakili Kiongozi wa serikali Justus Mulokoz. Mnyika alitetewa na Edson Mbogoro.
Chadema yafanya kufuru
Baada ya kumalizika kusomwa kwa hukumu hiyo, maelfu ya wanachama  wa Chadema walimbeba juu juu Mnyika na kumtoa nje ya viwanja vya mahakama kwa shangwe.
Wabunge wawili wa chama hicho, Ezekiel Wenje wa jimbo la Ilemela na Mchungaji Peter Msigwa wa Iringa mjini waliungana na umati huo na ndipo ukaanza msafara wa kuelekea katika ofisi za jimbo la ubungo huku wakiimba nyimbo mbali mbali za kusifu hukumu hiyo
Msafara ulipitia barabara ya Maktab, Bibi Titi, morogoro ambapo polisi waliokuwa wametanda kila eneo la mji, walijaribu kumzuia Mnyika wakitaka apande gari kuepusha msongamano, lakini wananchi waligoma na kutishia kufanya fujo hali iliyowalazimu askari kuusindikiza kwa amani.
Idadi ya watu ilikuwa ikiongezeka kila baada ya muda, na baadhi ya wafanyakazi na wenye biashara zao waliacha kwa kwa muda na kuungana na wafuasi hao kushangilia.
Katika eneo la magomeni magomeni mwembe chai wanafunzi wa shule ya Msingi Dk Omar waliungana na msafara huo sambamba na wanafunzi wengine wa shule mbali mbali za sekondari, na katika eneo la soko la Big
Brother wafanyabiashara walionekana wakiwa wamejipanga barabarani na kupunga mikono juu huku wakiwa wameshika bendera za Chadema.
Hata hivyo, mamia ya watu katika eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi walimzuia Mnyika wakitaka aingie ndani ya stendi hiyo kuhutubia jambo ambalo lilipingwa na viongozi wa Chama hicho kwa kuhofia uvunjifu wa amni.

Mnyika auhutubia
Akiwa katika eneo la ofisi za Chadema, Ubungo, Mbunge huyo alilazimika kuhutubia umati wa watu, ambapo alisema hukumu  hiyo ni ushindi wa wananchi wote dhidi
ya ufisadi unaofanywa na serikali ya CCM.
“Kwa sababu ya mfumo wa serikali yetu nilijua leo (jana) ingekuwa ni mwisho wa ndoto yangu ya kuwatumikia wananchi, lakini kwa sala zenu tumeshinda na sasa ni fursa nyingine ya kuwatumikia ninyi mlioniyuma pasipo kuwa na kizuizi chochote”alisema Mnyika na kushangiliwa.
Alisema mazingira ya kazi awali yalikuwa magumu kutokana na muda mwingi kufuatilia kesi mahakamani na kwamba sasa ana uhakika wa kuongeza nguvu juu ya kuzisemea shida za wananchi  bungeni na hata kuzitatua.
Aliitaka Taasisi ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURA) iwaeleze wananchi hatua waliyofikia baada ya aliyekuwa mshindani wake Hawa Ng’umbi kuwahi kukamatwa na taasisi hiyo kwa makosa ya rushwa.
Alisisitiza kuwa ni wakati wa wananchi kujua nini kinaendelea dhidi ya kesi hiyo na kwamba wasimuonee aibu kwa kuwa anatoka chama kinachotawala.
Akizungumzia masuala ya kitaifa Mnyika alisema anazo nyarak zinazoonyesha matumizi mabaya ya fedha katika benki kuu huku akisema hali hiyo inaiweka nchi katika hatari ya kukwama kiuchumi kutokana na ufisadi unaofanyika.
“Ninazo nyaraka za siri za benki kuu na ninatarajia kuziweka hewani muda wowote kuanzia sasa pale panafanyika ufisadi wa kutisha hali inayofanya mfumuko wa bei kuongezeka kila siku”alisema Mnyika
Kuhusu tatizo la maji katika jimbo la Ubungo na madudu ya wizara hiyo, alisema ataenda kupambana nae bungeni baada ya kuonyesha kiburi cha kutosikia kilio cha wananchi huku akisisitiza suala la Machinga kulifikisha bungeni
Mbowe: ni ushindi wa watanzania
Naye Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, amesema ushindi wa Mnyika ni wa Wananchi wa jimbo la Ubungo, Wanachama na Watanzania kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Mbowe alisema kesi za uchaguzi zinagharimu kiasi kikubwa cha fedha ambazo zingetumika kwa ajili ya shughuli zingine za maendeleo, hivyo suala hilo litawasilishwa bungeni kujadiliwa.
Mbowe alisema pesa za uchaguzi zinazopotea zingeweza kutumika kwa ajili ya kununua dawa hospitali, vitanda, madawati kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
“Wananchi kama mlivyoona wenzetu walikuwa na mashitaka matano, ambayo yametupiliwa mbali na Jaji kutokana na kukosa uthibitisho, hatua ya kukimbilia mahakamani kunakofanywa na baadhi ya Wabunge huku wakikosa vielelezo, sio nzuri”alifafanua
Alisema kama Mnyika angepoteza Ubunge huo, ni wazi kwamba Wananchi wasingepata mwakilishi mwenye uwezo kama wake.


   


-->
Mawaziri, wabunge wengi wanaishi na VVU

Na Nasra Abdallah
Baraza la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Nchini (TACOPHA) limedai kuwa wapo mawaziri na wabunge wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo, na limewataka wasiogope kujitangaza hadharani ikiwa ni pamoja na kuunda mtandao wao.

Mwenyekiti wa Baraza hilo,Vitalis Makagula, alitoa kauli hiyo wakati wa semina ya siku mbili ya waandishi wa habari kuhusu vvu/Ukimwi, Sheria na Haki za Binadamu, iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wanaoandika habari za Ukimwi(AJAAT), na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Makagula alisema kujitangaza kwa viongozi hao kutasaidia kuondoa woga kwa wananchi wengine ambao wanaogopa kujitokeza hadharani na kujitangaza, kwa vile watakuwa wameonesha mfano.

Mwenyekiti alidai kushangazwa na ukimya wa viongozi hao hata pale wanapolazimika kuzungumzia ugonjwa huo katika majukwaa yao ya kisiasa, husema kwa dakika chache na kurukia mambo mengine.

“Tunajua vema wapo mawaziri wanaoishi na ugonjwa huu. sasa badala ya kujificha na kuongea tu kwa maneno, ifike mahali viongozi wetu wafanye suala hili kwa vitendo,”alisema.

Alisema hadi sasa, makundi machache ndio yameonesha nia yakuwa na mtandao wa watu wanaoishi na ugonjwa huo wakiwemo,walimu waandishi na wananchi wa kawaida huku wataalam katika fani mbalimbali wakibaki nyuma jambo analosema bado jitihada za makusudi zinatakiwa kufanyika.

Naye Mwanasheria wa Taasisi ya Kudhibiti Ugonjwa wa Ukimwi (TACAIDS) Sam Komba, alisema pamoja na Ukimwi kuwa na mahusiano ya karibu na haki za binadamu, lakini bado wagonjwa wanakabiliana na unyanyapaa, na wengine wakilazimishwa kupimwa bila hiari yao kama vile akina mama wajawazito.

Awali akifungua semina hiyo,Mwenyekiti wa AJAAT,Simon Kivamwo,alisema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo waandishi katika kuandika habari za Ukimwi.

Kivamwo alisema katika semina hiyo waandishi wataweza kupitia sheria ya Ukimwi na kujua watu ambao wapo katika mazingira hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo.
mwisho.



Kagasheki akumbana na madudu Maliasili
·       Maofisa wake wafuja mamilioni ya fedha
·       Atishwa na utoroshaji wanyama hai

Na Asha Bani

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ameelezea kushtushwa kwake na ubadhilifu wa kutisha ulioko katika wizara hiyo, Idara ya wanyamapori unaodaiwa kufanywa na baadhi ya watendaji wake.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Jijini Dar es Salaam, waziri huyo alisema  idara hiyo inanuka kwa uozo unaotokana na wizi na ubadhilifu mkubwa ambao umeleta hasara kwa taifa

Kagasheki alidai idara hiyo inaongoza kwa ‘madudu’ ya kutisha, na ametangaza kuchukua hatua za haraka dhidi ya watendaji wanaotuhumiwa kuhusika na ubadhilifu huo mkubwa haraka iwezekanavyo, akidai fedha zilizotafunwa na wajanja hao ni nyingi.

“Jamani Idara ya wanyamapori ina fedha nyingi lakini zinaliwa na watu kwa maslahi binafsi na kama fedha hizo zingekuwa zinapelekwa serikalini kama inavyohitajika nchi hii kwa sasa ingefika mbali, mimi naogopa hata kutaja kiasi cha fedha hapa hadharani,”alisema Kagasheki.

Mbali na ufujaji huo,  Balozi Kagasheki amekiri kuwa usafirishaji wanyamapori nje ni mkubwa mno licha ya serikali kusitisha kuuzaji huo.

Alisema uchunguzi wa haraka umebaini kuwa biashara ya kusafirisha wanyama pori inafanywa kati ya wanfanyabiashara wa ndani na baadhi ya watendaji ambao hawajali na wanaonekana kutumia kila mbinu kufanikisha biashara hiyo.

Hata hivyo, katika hali iliyotarajiwa, Balozi Kagasheki alionesha hofu yake ya kukabiliana na wafanyabiashara na baadhi ya maafisa wa wizara hiyo, kiasi cha kuomba msaada kutoka taasisi nyingine vikiwemo vyombo vya habari kusaidia kupambana na ‘genge’ la wabadhilifu hao

“Katika idara kunahitaji usaidizi maana hapa ni vita na hata ninyi waandishi nafikiri mnaweza tukasaidiana kwa kuwa najua mtakuwa mnawajua sana wafujaji. Kuwaondoa hawa ni kutangaza vita ”alisema

Kutokana na hali hiyo, alisema atavunja uongozi wa idara hiyo na kuunda upya haraka iwezekanavyo, ingawa ni mapema sana kufanya hivyo.

Alisema ataagiza kufanyika kwa sensa kwa wanyama na kuweka wazi kila kitu, ili kunusuru kumalizika kwa wanayama wote.

“Tutawajulisha wananchi waelewe, hatutachelewa maana watu wameshajua, wasije kuwamalizia wanyama wote,”alisema Balozi Kagasheki.

Balozi Kagasheki alibainisha pia udhaifu mkubwa ndani ya wizara hiyo uliosababisha kushindwa kudhibiti uuzwaji wa magogo  nje ya nchi.

Alisema katika usimamizi wa mazao ya misitu mambo hayaendi vizuri lakini akadai kuyashughulikia haraka iwezekanavyo.

Akitoa hotuba yake kwa wajumbe wa bodi hiyo alisema rasilimali za misitu zinakadiriwa kuwa hekta 33.5 milioni, ambapo kati ya hizo hekta milioni 15.3 zimetengwa na kuhifadhiwa kisheria katika sehemu mbalimbali za nchi huku hekta milioni 9.7 za hifadhi ya maji ardhi na bioanuai na haziruhusiwi kuvunwa.

Alisema  kiasi cha hekta 2.3 milioni ni ya misitu ya hifadhi ya jamii, na wakala akisimamia mashamba 15 ya miti ya kupandwa yenye takribani hekta 85,000 za misitu iliyohifadhiwa.

Kagasheki alisema eneo la misitu takribani hekta milioni 18.2 zilizobaki ni eneo lisilohifadhiwa kisheria. Aidha alisema watumishi wa wakala wa huduma za misitu ni wachache ikilinganishwa na maeneo ya misitu yanayotakiwa kusimamiwa kulingana na takwimu zilizopo.

“Kuna wataalamu 1,756 sawa na asilimia 67.5 ya watumishi wanaohitajika ambao ni 2,600 huku wataalamu wanaosimamia na kutunza misitu ya asili  moja kwa moja ni 500 tu sawa na asilimia 19.2 ya wanaohitajika kusimamia misitu ya taifa iliyohifadhiwa kisheria,”alisema.

 Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo Lazaro Nyalandu alimtaka kila mtu kujenga utamaduni wa kupanda miti ili nchi iwe kijani, na kuongeza kuwa kuna soko kubwa la asali duniani linaloweza kuharibika kutokana na ufugaji wa nyuki unaofanyika karibu na kilimo cha tumbaku unaharibu ubora wake.

Kutokana na hali hiyo aliwashauri wafugaji wa nyuki kufanya shughuli hizo mbali na kilimo cha tumbaku.


Mwisho.


-->
-->

Kesi ya Lulu yapigwa kalenda
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana iliairisha tena kesi ya mauji inayomkabili msanii wa Filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ hadi Juni 4, mwaka huu kwa maelezo kuwa jalada la kesi hiyo limeitwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Mei 15 mwaka huu, Lulu kupitia mawakili wake Kenned Fungamtama, Peter Kibatara, Fulgence Masawe na Joaquine De- Melon waliwasilisha ombi Na.46/2012 chini ya hati ya dharura iliyokithiri Mahakama Kuu wakiomba mahakama hiyo iamuru Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulishughulikia ombi la msanii huyo la kutaka kesi hiyo isikilizwe katika mahakama ya watoto kwasababu mshtakiwa huyo ana umri chini ya miaka 18.
Mei 18 mwaka huu, uongozi wa Mahakama Kuu ukampangia Jaji Dk.Fauz Twaibu kusikiliza ombi hilo ambapo atalisikiliza Mei 28 mwaka huu mahakama hapo.
Kwa mujibu wa ombi la Lulu, anadai kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Augustina Mmbando Mei 7 mwaka huu, alikataa kutoa uamuzi la kutaka kesi hiyo ihamishiwe katika mahakama ya watoto kwasababu mshitakiwa huyo ana umri chini ya miaka 18 na badala yake hakimu huyo akasema mahakama hiyo haina mamlaka na kuwashauri mawakili hao kuwasilisha ombi hilo Mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa hati hiyo ya madai, Wakili Fungamtama alidai kuwa Hakimu Mmbando alijielekeza vibaya kwa kusema kuwa mahakama ile ilikuwa haina mamlaka ya kusikiliza ombi lao kwa hiyo wanaiomba Mahakama Kuu imwelekeze hakimu huyo asilikize ombi lao na alitolee maamuzi na kuwa endapo Mahakama Kuu itabaini vinginevyo basi mahakama hiyo ya juu itoe tafsiri ya umri kuhusu ombi hilo.
mwisho

TCRA: Simu za mkononi hazina madhara

Na Sitta Tumma, Kwimba.
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA), imesema kwamba mionzi ya mawimbi ya mawasiliano ya simu hayaleti madhara kwa watumiaji punde wanapokuwa wanawasiliana, tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya watu.
Imesema, katika kubaini ukweli huo imefanya utafiti kuhusiana na athari ambazo zinaweza kumkumba mtumiaji wa simu hizo, na kwamba hakuna athari zozote zinazoweza kujitokeza badala ya simu yenyewe kuchemka iwapo mtumiaji atatumia muda mrefu kuongea na mwenzake kwa wakati mmoja.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, Injinia Lawi Odiero aliyasema hayo juzi wakati alipokuwa akizungumza katika siku ya Mawasiliano na Teknolojia inayofanyika Mei 17 kila mwaka, iliyofanyika kwenye shule ya sekondari ya wasichana ya Bishop Mayala Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Kwa mujibu wa Meneja huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa, Watanzania hawana budi kuendelea kutumia mawasiliano ya simu, kwa maendeleo yao, na kwamba  Mamlaka hiyo imejizatiti kuhakikisha inaboresha na kutoa huduma nzuri za mawasiliano hapa nchini.
"Mionzi ya mawasiliano ya simu hayawezi kumdhuru mtumiaji kama ambavyo imekuwa ikielezwa. Isipokuwa mtumiaji anayeongea kwa muda mrefu kwa wakati mmoja simu anayotumia hupata joto tu!.
Suala la kwamba kuna athari kubwa siyo kweli, ila ipo athari kidogo sana labda na ile ya simu kupata joto wakati wa mawasiliano. TCRA imefanya utafiti wa uhakika katika hili na ndiyo maana tunasema hakuna madhara kwa mtumiaji", alisema Meneja huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa, Odiero.
Katika hafla hiyo, TCRA iliendesha pia maswali ya chemsha bongo, ambapo washindi waliweza kuzawadiwa TV yenye vifaa vyake vyote, Laptop mbili, kashine ya mahesabu pamoja na fedha taslimu kwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo ya Bishop Mayala iliyopo Kijiji na Tarafa ya Ibindo Kwimba.
Kwa upande mwingine, Meneja huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa, Odiero aliwahakikishia Watanzania kwamba, Mamlaka yake imejizatiti zaidi katika utoaji wa leseni za huduma, masafa, kuagiza bidhaa za simu na mawasiliano,leseni za kuuza vifaa hivyo vya mawasiliano nchini, pamoja na leseni ya mitandao nakadhalika.
Pamoja na mambo mengine alisema, Mamlaka hiyo imejiimarisha zaidi katika sula zima la kukuza na kulinda mawasiliano kwa maslahi ya watumiaji hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuendelea kutekeleza mikataba mbali mbali ya Kimataifa katika kuleta ufanisi bora wa huduma ya mawasiliani kwa Watanzania
Kwa mujibu wa Meneja huyo wa TCRA, Mamlaka hiyo ambayo ilianza kazi zake rasmi Novemba Mosi mwaka 2003, imefanikiwa pia kupiga hatua kubwa za kimaendeleo juu ya mawasiliano hapa nchini, hivyo kamwe haitarudi nyuma kuhakikisha kwamba Watanzania wengi wanapata huduma hiyo ya mawasiliano ya simu, intaneti na mawasiliano mengine yote yanayosimamiwa na TCRA.

Mwisho.

Dk. Kigoda msimamisha kazi bosi TBS
Marietha Mkoka na Happiness Mnale

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Abdallah Kigoda amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) Charles Ekerege kwa tuhuma za ubadhilifu.
Kusimamishwa kazi kwa Ekerege kumekuja baada ya kuwepo sintofahamu ya muda mrefu kuhusiana na kukabiliwa na tuhuma nzito za upotevu wa takairban sh bilioni 38 zinazotokana na ukaguzi wa magari nje ya nchi.
Kigoda alitangaza uamuzi huo jana, na kudai kuwa ni kwa ajili ya kutoa nafasi ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina juu ya tuhuma hizo, ambapo ameunda kamati maalum ya uchunguzi. Hata hivyo, waziri huyo hakutaka kuingia kwa undani kuhusiana na suala la mtendaji huyo mkuu wa TBS
Waziri huyo aliyeanzakazi wiki iliyopita, alisema ameamua kumsimamisha kazi Ekerege ili kulifanya shirika hilo lirudi katika hali yake ya kawaida ikiwemo kupisha bodi iliyoundwa kutimiza wajibu wake.
Tuhuma dhidi ya Ekerege ziliibuliwa na kamati mbili za kudumu za bunge, ya Mashirika ya Umma (POAC) na Hesabu za Serikali (PAC), ambapo wajumbe wa kamati hizo waliokwenda kufanya ukaguzi nje ya nchi walibaini madudu mengi, ikiwemo kutokuwepo kwa ofisi za ukaguzi kama ilivyodaiwa na shirika hilo, kiasi cha kusababisha upotevu wa sh bilioni 38.
Wajumbe wa kamati hizo walibaini malipo ya kampuni hewa za ukaguzi wa magari nje ya nchi.
Hatua ya kumsimamisha Ekerege, imekuja baada ya mtangulizi wake, Waziri Cyril Chami kushindwa kumchukulia hatua ikiwemo kumsimamisha, jambo ambalo pamoja na tuhuma nyingine dhidi ya mawaziri kadhaa, lililozua mzozo mkubwa bungeni kiasi cha kuwalazimisha wabunge kutishia kupiga kura ya kutokuwa na imani, na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Chami pia inadaiwa alikataa ushauri wa aliyekuwa naibu wake, Lazaro Nyarandu ambaye alitaka asimamishwe kazi kupisha uchunguzi, na akadiri kuendelea na msimamo huo hadi alipoachishwa uwaziri wa Viwanda na Biashara
Katika utetezi wake, Chami alidai kushindwa kumwondoa mkurugenzi huyo madarakani kwa kile alichodai kuwa mtendaji huyo ni mteule wa rais kama alivyo yeye. Kauli hiyo, na kubaki madarakani kwa Ekerege, kuliwashangaza wengi ambao waliamini kuwa, hakukuwa na sababu ya kutomwondoa kwa vile lengo lilikuwa kutaka tume ya uchunguzi ifanye kazi yake ikiwa huru. Aidha, inajulikana wazi kuwa kusimamishwa sio kufukuzwa, na hivyo angeweza kurudi kazini ikiwa ataonekana hana hatia.
Hata hivyo Dk. Kigoda ambaye ni Mbunge wa Handeni hakuwa tayari kuwataja wajumbe wa kamati hiyo na muda waliopewa kumchunguza Ekerege.
Katika hatua nyingine waziri huyo alisema atainua sera ya kukuza viwanda na biashara ikiwemo kuinua wafanyabiashara wadogo na ushirikiano baina ya serikali na viwanda vidogo.
“Tumepanga kuwasaidia wajasiriamali na kuangalia maeneo ambayo watu wakiwezeshwa watainua uchumi wao na kuboresha utendaji kazi,” alisema
Alisema kiwanda cha General Tyre kitahitaji kufufuliwa na viwanda vya Pamba na Korosho.
Pia alivisifu viwanda vinavyoiingizia serikali mapato kuwa ni kiwanda cha Saruji Twiga, Sigara (TCC) na viwanda vya bia kutaka viwanda vingine kuiga mfano ikiwemo kuongeza juhudi.
Akizungumzia uwekezaji katika nchi waziri huyo alisema kuwa suala la kupunguza gharama za umeme halijapata ufumbuzi hivyo juhudi zinahitajika kukabiliana na changamoto hiyo.

Mgomo mkubwa wa walimu wanukia
* Waipa serikali siku 13

Na Nasra Abdallah
CHAMA cha walimu Nchini(CWT),kimetoa siku 13 kwa Serikali kuwalipa malimbikizo ya madeni yao la sivyo wasilaumiwe kwa hatua ambayo wataichukua.

Akizungumza na waandishi wa habari,jijini Dar es Salaam,Rais wa CWT ,Gratian Mukoba, alisema madeni hayo yanayofikia sh. Bilioni 13 yanahusiana na mishahara na mengine.

Akiwa ameongozana na kamati tendaji ya CWT Mukoba alidai  tamko hilo  limetokana na kikao chao walichokaa Mei 14 hadi 18 mwaka huu ambapo mbali na mambo mengine ,kamati ilipokea taarifa ya ulipwaji wa madeni ya walimu yaliyohakikiwa mwaka 2011 na kubaini kuwa Desemba mwaka jana Wizara ya Fedha na Uchumi ilitoa jumla ya sh. Bilioni 22.5 kwa ajili ya kulipa madeni hayo.

Akifafanua zaidi, alisema hadi kufika Machi mwaka huu, kati ya fedha hizo zilizotengwa kuwalipa walimu,TAMISEM iIilikuwa imelipa jumla ya sh. Bilioni 16.6 na bado ilikuwa haijalipa sh. Bilioni 2.6

Hadi Aprili mwaka huu,Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufindi ilikuwa imewalipa jumla ya sh. Milioni 800 kati ya bilioni 3.2 zilizotengwa kwa kazi hiyo.

“Kamati inatoa rai kwa Serikali kutowabeza walimu kiasi hicho na inategemea kuona hatua za haraka zinachukuliwa ili kuepuka mgogoro wa kikazi kati ya walimu kupitia chama chao na serikali kama mwajiri”alisisitiza Mukoba.

Alisema serikali inapaswa kulipa madeni yote hayo ndani ya mwezi huu, kwa kuwa fedha hizo tayari zipo mikononi mwa Wizara ya Elimu na kinachofanywa sasa ni ucheleweshwaji wa makusudi.

Madai mengine chama hicho walimu wanayotaka kufanyiwa kazi mbali na madeni ni Serikali kuweka kwenye bajeti yake posho ya kufundishia asilimia 55 kwa walimu wa Sayansi na asilmia 50 kwa walimu wanaofundisha masomo ya sanaa.

Pia wameitaka Serikali iweke kwenye bajeti yake asilimia 30 ya mishahara ya walimu wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu kama posho ya mazingira na kuongeza kuwa Wilaya zinazohusika zilishatajwa na Serikali.


DK. Kafumu amkataa Jaji

Na Mustapha Kapalata,Nzega
 
KATIKA hali isiyo ya kawaida jana Mbunge wa Jimbo la Igunga Dk. Peter Kafumu alimkataa Jaji Mery Nsimbo Shangali kuendelea kusikiliza kesi ya kupinga matokeo yaliyo mpatia ushindi mbunge huyo katika uchaguzi mdogo wa Igunga uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
 
Akisoma barua ya Kafumu mbele ya mahakama hiyo, Wakili wake, Antony Kanyama alisema kuwa mteja wake hana imani na jaji huyo kwa kuwa baadhi ya maamuzi yanakwenda ndivyo sivyo.
 
Alisema imani na jaji huyo imetoweka kwa madai kwamba amekuwa akiwadhalilisha na kuwatukana mashahidi wa upande wa utetezi, na kutoa mfano wa shahidi(DW14), ambapo amedai alichukua nafasi ya mawakili wa mdai kwa kuwahoji maswali mashahidi wake badala ya kutaka ufafanuzi juu ya maelezo yao.
 
Aliitaja sababu nyingine kuwa ni tabia ya jaji huyo ya ukali pasipo sababu dhidi ya mawakili wa utetezi kila walipohoji mashahidi wa upande wa mdai.
 
Aliitaja sababu nyingine kuwa ni kile alichodai kuwa ni kitendo cha jaji huyo kuwanyima mawakili wa upande wa utetezi waliomba kupewa nakala ya mwenendo wa shauri hilo, mara tu usikilizaji wa kesi kwa pande zote ulipokamilika ili kuwasaidia kuandaa hoja za majumuisho.
 
Wakili Kanyama alidai kuwa kutokana na hali hiyo mashahidi wake muhimu wamekataa kuja kutoa ushahidi kwa kuogopa kudhalilishwa.
   
Hata hivyo, wakili Prof. Abdallah Safari anayemtetea mlalamikaji, Joseph Kashindye anayepinga ushindi wa Kafumu, alisema kuwa maombi hayo si ya msingi, na akatoa mifano mbalimbali ya kesi kama hizo na kuongeza kuwa kama wanaona hali ni mbaya wasubili wakate rufaa mara baada ya kesi hiyo kuhukumiwa.
 
Baada ya kupitia pande zote mbili na kusoma kwa muda jaji huyo alitupilia mbali ombi hilo la Kafumu na kusema kuwa kesi hiyo inaendelea kusikilizwa kwakufuata taratibu na kanuni za kimahakama.
 
Jaji Mery alisema hakuna sababu za msingi zilizotolewa na kwamba maelezo yanayolalamikiwa yanaweza kufanywa katika Rufaa.
 
Pamoja na kutupilia mbali ombi hilo, Wakili Kanyama aliiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo mpaka aongee na mteja wake kama ataendelea ama vipi.

Katika hatua nyingine, Jaji Mery ametaka mahakama iachwe uhuru na isiingiliwe katika mwenendo wake, kwa vile hadi sasa haijabainika nani atakuwa mshindi katika kesi hiyo kwani bado ushahidi unaendelea kusikilizwa kwa mjibu madai na upande wa serikali.
 
‘’Naomba muiachie Mahakama iendelee kusikiliza kesi hii na muheshimu mahakama kama jinsi tulivyo apishwa’’alisema jaji Mery.
HUU NDIO UNAODAIWA KUWA WARAKA WA MHE MAIGE
Ndugu zangu na rafiki zangu. Kwanza niwape pole kwa mshituko mlioupata
kwa haya yaliyojitokeza.

 Naomba msisikitike sana. Kila jambo alilopanga Mola hutokea kadiri ya
 mapenzi yake. Route ya maisha ya mwanadamu hupangwa na Mola mara tu
anapompulizia pumzi ya uhai. Hili lilipangwa hata kabla sijatokea
 duniani miaka 42 iliyopita!

 Mungu hakushindwa kumwokoa mwanawe Yesu asisulubiwe, tena kwa kuonewa!
 Hasha, tungeupataje ukombozi bila hilo kutokea? Wakati mwingine Mungu
 hutoa nafasi kwa mambomagumu kuwafika waja wake, si kwamba hawapendi,
 bali ili unabii utimie. Ilifika wakati hata Yesu akaona kama Mungu
 kamuacha! Hasa sisi kwa hili tunaweza kudhani Mungu katuacha! Hasha,
 ni njia ya kuufikia ukombozi wa kweli.

 Pili, kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa,yaliyotokea ni ushahidi
 kwamba maliasili ni ngumu. Kukabiliala na wabaya ni kazi ngumu. Wapo
 waliojipanga ukiwavamia ovyoovyo unaondoka wewe. Ndivyo ilivyotokea.

 Niwahakikishie, wazalendo wamepoteza mpambanaji.

 Nimepambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini
 ndani na nje ya nchi. Nilitumia kila aina ya uwezo wangu kulizawadia
 taifa langu utumishi uliotukuka. Sikubakisha chembe ya energy.

Waziri gani aliyesimamia sheria na kuwapa vitalu watanzania maskini
wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza? Waziri gani
aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake?
Watu wametumia records za matukio ya 2009/10 kuficha matendo na
maamuzi ya kishujaa ya maige ya 2011.

Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si
siku nyingi. Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu. Bado nasisisitza
hivyo, si Mungu wangu kama ilivyodhaniwa, bali Mungu wetu wa haki.

Waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai? Waziri gani
aliyeonyesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona
hawatendi sawa? Maige hakusita kuchukua hatua.

Maamuzi haya ni magumu na yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi
mkubwa. Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda. Nilisema
Bungeni, watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini. Muda
haukuruhusu, ila nitarudi Bungeni na nitasema.

Imesemwa issue ya nyumba. Nimefafanua na kutoa vielelezo. Kila mbunge
aliyetaka kukopeshwa shs 290m, wengine wameanzisha biashara na wengine
wamenununua magari na wengine majumba. Wapo walioficha, na tupo
tuliojiweka wazi! Mkopo wangu huo umekuwa my contribution na balance
kulipwa na benki na nyumba kuimortgage.

Nimetoa nyaraka zote kwa wanahabari na vyombo vyote husika. Nimesema
mwenye mashaka aende kwa Msajili wa hati wizara ya ardhi, au kwa
kamishna wa maadili, au CRDB Azikiwe na Dodoma nilikokopa au amtafute
muuzaji. Kote huko utapata rekodi ya bei na mode of payment. Wapo
wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei
tofauti na niliyonunulia.

Mwanasheria wangu anashughulikia hilo. Niwahakikishie, vita
nimepigana, imani na dhamana nimeilinda, muda wa kutuzwa na mwenye
kumbukumbu sahihi, Mungu utafika. Naamini nimejiwekea akiba isyooza
Mbiguni.

Yapo mengi yasiyo sahihi yaliyosemwa. Nitakuwa nafafanua kila nipatapo
fursa na muda utazidi kutufunua. Kwa kifupi, kwa suala la vitalu,
hakuna kampuni hata moja iliyopewa kitalu cha uwindaji bila kuomba,
kukaguliwa na kamati ya ushauri na hatimaye kupewa alama. Kampuni
zisizokuwa na sifa ni zile zilizopata chini ya alama 50.

Na kwa kampuni zilizokuwa kwenye biashara, passmark ni alama 40 kwa
mujibu wa kanuni ya 16(5) ya kanuni za uwindaji wa kitalii za mwaka
2010.

Hakuna kampuni iliyopata chini ya alama 50 iliyopata kitalu. Hakuna
kampuni ya kizalendo iliyopendekezwa na kamati ya ushauri ambayo
haikupewa kitalu.

Kwa upande wa report ya CAG, haikunigusa binafsi kwani ilikuwa
inaishia juni 2010 wakati mimi ilishika dhamana Novemba 2010.

Ka upande wa biashara ya wanyama hai, hakuna wanyama waliosafirishwa
kinyume cha sheria wakati wangu (2011), na matukio ya utoroshaji
tulipoyabaini,tulifungua mashitaka kwa watuhumiwa nakufunga biashara
hiyo.
Naanza kazi ya kuwawakilisha wananchi wa Msalala.
Nitawawakilisha kwa mujibu wa katiba na ahadi zangu kwao hadi 2015
watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo.

Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana. Kwa wakristo, naomba msome
Mwanzo 4:1-15.

Wasalaam.
-->
-->



Muleba yakumbwa na mafuriko

Na Ashura jumapili,Kagera

MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Kagera zimesababisha mafuriko katika maeneo mengi ya Wilaya ya Muleba na kubomoa nyumba zaidi ya 20, huku kata ya Muhutwe ikiwa imeathirika zaidi.
Mbali na kubomoa nyumba, mvua hiyo imesababisha vyoo vingi kufurika na kinyesi kutapakaa eneo kubwa la makazi ya watu, hivyo kuwepo na tishio la magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
Akiongea na Tanzania Daima kwa niaba ya wananchi wenzake Rajabu Juma mkazi wa Kijiji cha Bisore Kata Muhutwe alisema, nyumba yake ni miongoni mwa zilizoathirika baada ya kujaa maji, kiasi cha kumlazimu kubomoa matundu katika kuta za nyumba yaweze kutoka.
Diwani wa Kata hiyo Justus Magongo alisema hali ni mbaya na nyumba nyingi zimebomolewa na mafuriko, na huenda kukawa na maafa zaidi ikiwa mvua hizo zitaendelea kunyesha. Alisema uongozi wa kata umetoa taarifa kwa mkurugenzi na katibu tawala wa wilaya hiyo.
Alivitaja vijiji vilivyoathirika zaidi kuwa ni Bukoki,Kagondo senta, Muhutwe, Eibanga, Nshambya na Kagondo Eifo, na kwamba mvua hiyo imeaharibu pia miundo mbinu ya barabara, na karibu zote hazipitiki.
Kutokana na hali hiyo, uongozi wa shule ya msingi Nyarigamba ulilazimika kusimamisha masomo kwa siku ya jana wakihofia maafa kutokana na maji mengi kujaa madarasani, na hasa ikizingatiwa kuwa majengo yake hayajasakafiwa kwa saruji.
Hata hivyo alisema kuwa uwezekano wa nyumba kuendelea kubomoka ni mkubwa kwani kuna baadhi ya nyumba za matofali mabichi bado zimezungukwa na maji karibu robo ya nyumba kuta zimelowana.
Aidha diwani huyo alitoa wito kwa serikali ya wilaya ya Muleba kujiandaa kunyunyizia dawa katika maeneo yaliyobomoka vyoo na kusababisha kinyesi kusambaa ovyo ili kuepuka magonjwa ya milipuko.
Katibu Tawala Wilaya ya Muleba Projestus Lubanzibwa alipoulizwa jitihada zilizochukuliwa na halmashauri yake kuwanusuru wanachi hao alisema ofisi yake haina taarifa za mafuriko hayo.
“Mimi sina taarifa isipokuwa jana nilipita huko nikakuta maji yamejaa nika wasiliana na mtendaji wa kata hiyo leo amesema maji wameisha yaondoa kama kuna tatizo labada nifuatilie”alisema Lubanzibwa.
Naye afisa mtendaji wa Kata hiyo Ally Rajabu alipoulizwa alisema matukio hayo yametokea bado anaendelea na tathimini kwa kushirikiana na watendaji wa vitongoji.








Sakata la Bastora ya Rage laibukia tena

Na Mustapha Kapalata, Nzega.
 
SAKATA la bastora lililowahi kumfikisha polisi mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage na kupigwa faini ya sh laki moja na kamati ya maadili wakati wa kampeni za ubunge wa jimbo la Igunga, jana liliibuka tena jana wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo.

Akiwa mmoja wa mashahidi waliosimama jana katika Mahakama Kuu kanda ya tabora, Rage akijibu maswali kutoka kwa wakili wa mlalamikaji na aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chadema, Josephat Kashindye, alisema

 waziri wa Utawi wa jamii njisia na watoto Sophia Simba jana walipanda kizimbani kutoa ushahidi wa kesi ya kupinga matokeo yakumpatia ushindi Dk,Peter Kafumu katika Mahakama Kuu kanda ya Tabora.
 
 
Shauri hilo lilifunguliwa na mlalamikaji Joseph Kashindye dhidi ya Dk.Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi.
Akiwa shahidi wa kumi na tano kwa upande wa wajibu madai Adeni Rage alikili kushiriki kampeni hizo za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga akipangiwa kata ya Tarafa ya Igulubi wilayani humo.
 
Rage alitoa maelezo yote wakati akiulizwa maswali na wakili wa mjibu madai kwanyakati tofauti huku akiwa ameketi katika kiti kilichokuwa kimewekwa kizimbani.
 
Baada ya kutoa maelezo hayo wakili wa mlalamikaji alianza kumuuliza maswali shahidi huyo juu ya umiliki wa Bastora yake na kwanini alikuwa nayo katika mikutano mbalimbali ya kampeni ambazo alizoshiriki.
 
Mbunge huyo mambo yaliyo kuwa yakimkabili nipamoja na kutangaza kuwa mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Joseph Kashindye amejihudhuru kugombea kiti hicho haliambayo ilileta tafrani katika uchaguzi huo.
 
Wakati akijubu maswali hayo Rage alikili kumiliki Bastora hiyo pamoja na kushiriki nayo katika shuguli nzima za kampeni wakati huo.
 
Hata hivyo alisema upepo ulimponza hasa pale ulipo peperusha shati lake na Bastora hiyo kuonekana hadharani na vyombo vya habari kumpiga picha mara mmoja.
 
’’Pamoja na kufanya mikutano mbalimbali hata wakati nikipanda kwenye jukwaa kulikuwa na upepo mkali uliofunua shati langu na kusababisha Bastora kuonekana hadharani nandipo waandishi walianza kuniangalia na hatimaye walinipiga picha iliyoonekana kwenye gazeti la mwananchi’’alisema rage.
 
Rage alisema kuwa mara baada ya kutokea tukio hilo bastora hiyo ilichukuliwa na Jeshi la Polis kwa maagizo ya waziri wa  mambo ya ndani na yeye kuhojiwa pamoja na kupigwa faini ya laki mmoja na kamati ya maadili.
 
Akitumia muda mrefu kujibu maswali hayo zaidi ya masaa matatu alisema kuwa richa ya kuwa na batora katika majukwaa ya kampeni kamati ya maadili ya uchaguzi ilimpiga faini.
 
Wakati huo huo waziri wa Ustawi wa jamii na njinsi na watoto Sophia Simba akiwa shahidi wa kumi na sita kwa upande wa mjibu madai akitoa ushahidi wa kula chakula na wananchama wa CCM katika Hospitali ya Nkinga kata ya Inkiga.
 
Alikili kula chakula hicho na kudai kuwa alikuwa na mwaaliko wa chakula cha mchana na ndugu yake katika Hospitali hiyo hata hivyo alipoulizwa jina la ndugu huyo alishindwa kulitaja.
 
Richa ya kula chakula hicho alikili kula na watu zaidi ya 50 hali ambayo mawakili wa mlalamikaji waliendelea kumuuliza maswali mbalimbali ikiwepo na maneno aliyoyatamka kuwa msimchague kashindye kwani hana mke pia ni masikini hata hivyo waziri huyo alikanusha maneno hayo.
 
Kesi hiyo ikisilizwa na Jaji Mery Shangali inaendelea leo May 18 mwaka huu huku mashahidi wa mlalamikaji 22 wakiwa tayali wametoa ushahidi na sasa mashahidi 16 wa mjibu madai wanaendelea kutoa ushahidi huo ambapo upande wa serikali ukisubili kuanza kutoa ushahidi wake wa watu 10.
mwisho




Mawaziri wapya wagongana
* Mmoja asema, hakuna fedha, mwingine adai zipo


Irene Mark na Dunstan Bahai

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mawaziri watatu wapya wa serikali, wametoa matamshi yanayokinza, kuhusiana ukweli wa hali ya fedha ilivyo ndani ya serikali.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawamba akiwaambia wadai kuwa serikali haina fedha kiasi cha kushindwa kutoa fedha za mikopo ya wanafunzi wote walioomba mikopo ya elimu ya juu kutokana na ufinyu wa bajeti unaoikabili Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Kwa mujibu wa Dk. Kawambwa, mwaka wa fedha wa 2011/12 serikali imetenga bajeti ya sh. bilioni 317.8 kwa ajili ya ukopeshaji lakini hadi kufikia Machi 15,2012, kati ya wanafunzi 113,356, waliokopeshwa ni 94,092 wakiwemo 26,272 wa mwaka wa kwanza, 66,744 wanaoendelea na masomo, 772 wanaosoma nje ya nchi na 304 wanaosoma shahada za uzamivu nchini waliopata huku zaidi ya  wanafunzi 19,264 wakikosa.
Aidha, Waziri William Lukuvi juzi alionesha hofu yake ya serikali kuwa katika hali mbaya ya fedha, baada ya hatua ya wafadhili kuamua kutoipa serikali moja kwa moja fedha za maendeleo, badala yake kuamua kuziweka katika miradi iliyokusudiwa.
Hata hivyo, jana Waziri wa Fedha na Uchumi Dk. William Mgimwa amesema serikali inazo fedha za kutosha na kwamba wafadhili hawajajiondoa katika kuisaidia Tanzania, bali sasa fedha zao zilizokua zikitolewa katika bajeti hiyo zitaelekezwa kwenye miradi mbalimbali moja kwa moja..

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Dk. Mgimwa aliwaondoa wasiwasi watanzania kwa maelezo kwamba wafadhili bado wataendelea kuisaidia Tanzania na kwamba hadi sasa  Hazina ina fedha za kigeni kiasi cha dola bilioni 3.6 za Marekani zinazoweza kuilisha nchi kwa miezi minne hivyo si kweli kwamba Tanzania imefilisika.

“Naomba niwaondoe wasiwasi wananchi wahisani bado wanayo imani sana na sisi walichokifanya ni kuelekeza fedha hizo kwenye miradi moja kwa moja badala ya kuingiza kwenye bajeti kuu.

“…Tusisikilize maneno hayo wafadhili bado wapo wanaweza kutusaidia kupitia madirisha matatu, kwanza bajeti, pili miradi na kwenye kapu la maendeleo sasa wao wameamua kupeleka katika miradi, njia zote zinafaida yake,” alisema waziri huyo.

Hata hivyo Dk. Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Kalenga alishindwa kueleza baadhi ya miradi itakayofaidika na fedha za wahisani moja kwa moja baada ya kuwepo kwa taarifa rasmi kwamba hawatachangia tena kwenye Mfuko wa Ukimwi.

Aidha waziri huyo aliyewahi kuwa mtumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) alisema serikali itaongeza umakini kwenye utunzaji wa fedha na uwajibikaji.

“Katika bajeti ijayo ya serikali tutaongeza nguvu kwa kuishirikisha sekta binafsi kwa sababu tunaamini kwenye dhana ya Public, Private Partnership (PPP) na vipaumbele vyetu tutawaeleza tukishakua tayari,” alisema Mgimwa.


Hata hivyo, pamoja na utetezi huo, katika hali nyingine Waziri Kawambwa katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Kamishina wa Elimu wa Wizara hiyo, Mary Stella Wassene kwenye hafla ya uzinduzi wa Mpango Maalum wa kutoa elimu ya fedha ujulikanao kama NMB Financial Fitness shuleni uliofanyika kitaifa katika shule ya Sekondari ya Pugu na kufuatiwa na uzinduzi wa nakala 50,000 za vitabu vitakavyotumika kutoa elimu hiyo nchini, alisema serikali haina uwezo wa kuwapa mikopo wanafunzi wote waliokidhi vigezo kwa sababu ya ukosefu wa fedha.

Badala yake, aliwataka wazazi na watanzania kujifunza utamaduni wa kujiwekea fedha kidogo kidogo kwa ajili ya maendeleo ya elimu kwa watoto wao.

Wakati hayo yakiendelea, kumekuwa na malalamiko mengi karibu katika vyuo vingi, kupinga kucheleweshewa kwa posho na mikopo hata kwa wanafunzi walioteuliwa kupewa mikopo, huku mamia ya wengi wakiishia kulalamika kwa kuikosa.
Kawamba katika hafla hiyo jana ambayo Benki ya NMB inakusudia kutoa elimu ya fedha kwa wananchi, aliwahimiza watanzania wenye uwezo kuchangia sekta ya elimu.

“Hivi leo tunayo changamoto kubwa ya namna ya kugharamia elimu ya watoto wetu katika vyuo vya elimu ya juu. Pamoja na serikali kutenga fedha kila mwaka katika bajeti kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, bado mahitaji ya mikopo hiyo ni makubwa kuliko uwezo wa serikali wa kutenga fedha kwa ajili ya kukopesha,” alisema

 “Wito wangu kwa wananchi ni kwamba, pamoja na mchango mkubwa wa serikali katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii  hapa nchini, tujifunze utaratibu wa kujiwekea akiba kidokidogo kama tunavyo elekezwa na wenzetu wa NMB. Tukifanya hivyo wengi tutakuwa  na uwezo wa kujitegemea zaidi  katika kujiletea maendeleo yetu ikiwa ni pamoja na uwezo wa kugharamia pamoja na mambo mengine elimu ya vijana  bila kuisubiri serikali itenge fedha ambazo hazitoshelezi mahitaji ya kila mmoja,” alisisitiza. 
Dk. Kawambwa alisema mpango huo wa elimu ya fedha utasaidia jamii nyingi kuwa na nidhamu ya fedha lakini pia kuwa na mwamko wa kutumia huduma za benki ikiwa ni pamoja na kuhifadhi fedha zao huko.

Alisema utafiti uliofanywa na taasisi moja ya utafiti wa mambo ya fedha ya Financial Sector Deepening Trust (FSDT) unaonyesha kwamba,  ni asilimia 10 tu ya Watanzania   wanaotumia huduma za kibenki na kwamba moja  ya sababu zinazoelezwa kuwa  chanzo cha uwiano huu, ni uelewa mdogo wa masuala ya kifedha.

Kutokana na tatizo hilo, alisema kuwa  Benki ya NMB imetambua changamoto hiyo na kudhamiria kuanzisha mkakati huo, wenye lengo la kuongeza uelewa wa masuala ya kifedha kwa Watanzania hususani wanafunzi.

Naye Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing, alisema wamelazimika kuchagua uzinduzi huo kufanyika katika shule hiyo kutokana na kuwa ni ya kihistoria kwa kutoa marais wa Tanzania lakini pia viongozi kadhaa wa ngazi za juu serikalini na kwenye mashirika mbalimbali.

Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Meshark Ngatunga, alisema benki hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kufanya shughuli mbalimbali hasa za kijamii kama vile za elimu, afya na michezo na wameongeza huduma nyingine hiyo ya elimu ya fedha.

Alisema kwa mwaka jana pekee, benki hiyo imetumia zaidi ya sh. milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ya kijamii ikiwa ni pamoja na kukarabati madarasa katika shule ya sekondari ya Pungu na masuala ya michezo shuleni hapo.

Mwisho



-->



Arusha, Muleba wazidi kuikimbia CCM
Grace Macha Arusha na Antidius Kalunde, Muleba
KIMBUNGA cha Operesheni Vua Gamba, Vaa Gwanda ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezidi kutikisakote nchini, baada ya kumzoa mjumbe wa Halmashauru Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Arusha mjinia Emmanuel Temba.
Temba ambaye pia amewahi kuwa Diwani wa Kata ya Kimandolu, Emanuel Temba, alikuwa miongoni mwa wanaCCM 400) wa Kijiji cha Enduleni akiwemo Mwenyekiti wao, Pettey Kitaika waliohamia Chadema na kukabidhiwa kadi jana na katibu wa Chadema mkoani hapa, Amani Golugwa.
Wakati Mwenyekiti huyo wa kijiji hicho, Kaita akisema ataeleza sababu za yeye kujitoa ndani ya chama hicho tawala mwishoni mwa wiki kwenye mkutano mkubwa utakaofanyika kijijini hapo utakaowashirikisha viongozi wa Chadema mkoa, Temba yeye alisema viongozi wa CCM hawashauriki na wamemeacha misingi ya kuanzishwa kwa chama hicho kwa sasa wanajilimbikizia mali na familia zao.
Alisema kuwa kuna wanachama wengi wa CCM toka vijiji vya jirani ambao nao wanatarajia kujiunga na Chadema siku hiyo ya mkutano ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya na mkoa toka  Chadema.
Temba alisema kuwa amevutiwa na operesheni hiyo ya vua gamba vaa gwanda ambayo imekuwa ikiwahamasisha wananchi kujua haki zao na kuikataa CCM.
Alisema kuwa viongozi wa CCM wamesahau kuwatumikia wananchi ambao kila kukicha maisha yao yanazidi kuwa magumu kutokana na kupanda kwa gharama za maisha kunakosababishwa na mfumuko wa bei za bidhaa.
“CCM hawashauriki mimi nilikuwa nikiongea kwenye vikao lakini hakuna anayesikiliza, nimeamua kuja huku (chadema) ili niweze kuongea kwa sauti, sina nia ya kugombea uongozi wowote nitashirikiana na wanachama wenzangu kuendeleza operesheni Vua gamba Vaa Gwanda” alisema Temba.
Naye mwana CCM mwingine Lucas Eliahu ambaye alitangaza rasmi kukihama chama hicho alisema kuwa amechoka kudanganywa kila siku maisha bora kwa kila Mtanzania huku maisha yanazidi kuwa magumu.
“Nimechoka hata nikifa  acha nifie Chadema, ni bora kufia kwenye haki niweze kupumzika kwa amani kuliko kuendelea kukaa CCM ambayo haiwajali na inawakandamiza wananchi walio maskini kwa kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa yao” alisema Eliahu.
Kwa Prof Tibaijuka hoi
Huko Bukoba, Chadema kimeendeleza wimbo hilo baada ya kuvuna wanachama wapya 112 katika jimbo la Muleba Kusini ambalo mbunge wake ni Prof. Anna Tibaijuka.
Wanachama hao walipokelewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Msalaba Mwekundu mjini Muleba juzi join, ambapo pia ulifanyika ufunguzi wa ofisi ya chama jimbo, na kufuatiwa na mkutano wa hadhara uliyoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Kagera, Wilfred Lwakatare.
Wengine waliohudhuria mkutano huo uliyofurika mamia na wananchi ni Mbunge wa Viti Maalum, Conchesta Rwamulaza (Chadema), Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake mkoa (Bawacha), Anna Mukono na madiwani mbalimbali kutoka vyama vingine vya upinzani wilayani humo.

Katika idadi hiyo ya wanachama waliojiunga na chama hicho, 45 walirudisha kadi kutoka vyama vingine vya siasa na 67 ni wapya. Hao ni 21 kutoka CCM, 11 wa TLP, 7 wa CUF na 6 kutoka NCCR Mageuzi.

Mwisho







Jaji Mkuu awashukia mahakimu

Na Datus Boniface

JAJI Mkuu Othuman Chande ameshangazwa na hatua ya mahakimu nchini, kung’ang’ania adhabu ya kifungo gerezani kwa wahalifu badala ya kuwatumikisha kifungo cha nje.

Huku, akiwataka wajiulize ni wahalifu wangapi wamepewa adhabu zao kwenye jamii nje ya magereza, na kitu kipi kinazuia kufanya hivyo.

Aidha, Jaji amesema kitendo hicho kinaingiza nchi kwenye matatizo makubwa ya msongamano wa wafungwa mgarezani, hivyo taifa kutumia fedha nyingi.

Jaji Chande alisema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akifungua mafunzo ya mahakimu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu matumizi ya adhabu mbadala.

“Hebu tuyaache magereza yabaki kwa wale wahalifu hatari kama majambazi, wabakaji na wengine ambao tunaamini kwa hakika kuwa hawastahili kubaki kwenye jamii” alisema

Alisema miaka mingi mahakimu wamekuwa na mazoea kuona kuwa adhabu mbadala ya kifungo gerezani haitoshi katika kuwarekebisha wahalifu, na kupendekeza kutoa hukumu za vifungo vya magerezani pekee hata kwa makosa yanayostahili adhabu mbadala.

Katika maelezo yake, sheria za nchi zinatoa fursa kwa wafungwa kutumikia adhabu mbadala ya kifungo magerezani, lakini kwa bahati mbaya  na kwa mazoea mahakimu wamekuwa hawapendi kuzitoa adhabu hizo.

Kwa mujibu wa kauli ya Jaji Chande, litakuwa ni jambo la kushangaza na aibu, kung’ang’ania utaratibu wa kizamani uliozoeleka.

Hivyo, alitaka mahakimu hao kubadili mtizamo huo, na kuwa tayari kwenda sambasamba na mabadiliko ya Idara ya Mahakama nchini ikiwemo kutumia kifungo mbadala.

Alienda mbali zaidi na kusema, takwimu zinaonyesha kuwa nchi jirani ya Kenya mwishoni mwa Machi, walikuwa na wafungwa 50,000 ambao wanatumikia vifungo mbadala, wakati Tanzania inatoa adhabu hiyo kwa wafungwa chini ya 900.

Aliwataka mahakamu wajiulize kwa nini Idara ya Mahakama nchini iko nyuma kiasi hicho ikilinganishwa na Kenya.

Alisema, adhabu mbadala hasa ya kutumikia jamii bila malipo mfano kutunza mazingira, ujenzi wa shule, zahanati, barabara, zimeonekana kuleta manufaa makubwa kwa jamii.

Aliongeza kuwa, matokeo ya tafiti nyingi  zilizofanyika juu ya matumizi ya adhabu mbadala zinaonyesha wahalifu wanabadili tabia zao na kuwa watu wema kuliko wa wanaopelekwa magerezani.

Aliongeza, utafiti huo unaonyesha kwe upande mwingine kwamba, wahalifu wanaotoka magerezani wanakuwa wabaya kuliko walivyokuwa mwanzo, kutokana na kufundishwa tabia chafu magerezani.

Mwisho



JK kufukuza mawaziri
* NEC yanywea kwa shinikizo la wabunge

Na Edson Kamukara
BAADA ya vuta nikuvute ya muda mrefu ya wabunge kumtaka awawajibishe mawaziri wake, hatimaye Rais Jakaya Kikwete, amekubali kuwatimua wale wote waliotuhumiwa kwa ubadhilifu na kufanya mabadiliko makubwa katika serikali yake.
Katika kikao chake cha dharura kilichoketi jijini Dar es Salaam jana chini ya Mwenyekiti wake Rais Kikwete, Kamati Kuu ya CCM, iliafikiana na kubariki uamuzi wa kuwatimua mawaziri hao na maafisa wote wa serikali wanaotuhumiwa kwa ufujaji wa mali ya umma na kusuka upya kwa baraza hilo na taasisi zingine zilizoainishwa katika ripoti za Kamati za Kudumu za Bunge na ile ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).
Hatua hiyo inakuja zikiwa ni siku chache tangu Kamati ya Wabunge wa CCM katika kikao chake cha ndani kuwashinikiza mawaziri kadhaa waliotajwa moja kwa moja kwenye ripoti hizo kuachia ngazi.
Shinikizo hilo pia lilichagizwa zaidi na hatua ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), kuwasilisha kusudio la kutaka wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao hicho cha CC, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kikao hicho kimechukua uamuzi huo kutokana na ukweli kwamba suala hilo ni zito na linahitaji kuweka mfumo mzuri wa utendaji na uwajibikaji serikalini.
Hata hivyo, licha ya Nape kusita kuwataja kwa majina mawaziri wanaotakiwa kung’oka, mawaziri walioshambuliwa bungeni na kutakiwa kutimuliwa ni pamoja na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mstafa Mkulo, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Prof. Jumanne Maghembe, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu na Naibu wake, Athuman Mfutakamba.
Wengine katika orodha hiyo ni Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda na naibu wake, Dk. Lucy Nkya, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Cyril Chami, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima.
Alipoulizwa ni kwa nini Rais angoje shinikizo la wabunge wa CCM na wapinzani ndipo achukue hatua ya kuwaondoa watendaji wabovu, Nape alitetea akisema kuwa si kweli kuwa mkuu huyo wa nchi ameshinikizwa, bali huo ni uamuzi wake na wao wameuridhia.
Alisema kuwa chimbuko la vuguvugu hilo ni hatua ya Rais Kikwete kuweka uwazi wa kuruhusu ripoti hiyo ya CAG iwasilishwe na kujadiliwa bungeni kwani imetoa mwanya kwa wabunge kuchambua kwa kina na kubaini watendaji wabovu.
“Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi wa wabunge wa CCM juu kilichojitokea kwenye Bunge lililopita mjini Dodoma, taarifa hizo zimewasilishwa na kujadiliwa na CC,” alijigamba Nape na kuongeza kuwa;
Alisema kuwa Rais Kikwete aliwaeleza jinsi alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhilifu ulioanishwa na taarifa ya CAG, kamati za kudumu za Bunge na wabunge.
“Hivyo CC tumaridhia na kutaka uamuzi huo uchukuliwe mara moja, tuna imani kuwa Rais atafanya mabadiliko haraka iwezekanavyo maana alikuwa amebanwa na majukumu kidogo ya safari nje ya nchi, mazishi ya Rais Bingu wa Mutharika na sherehe za Muungano. Ila sasa wakati wowote atafanya,” alisema Nape.
Kuhusu ni funzo gani CCM imelipata kutokana na watendaji hao kugoma kujiwajibisha hadi mamlaka iliyowateua iwachukulie hatua, Nape alisema ziko aina mbili katika uwajibikaji yaani kujiondoa mwenyewe au kusubiri mamlaka ichukue hatua.
Hata hivyo alisisitiza kuwa chama hakijatikisika bali tukio hilo linaweka mfumo mzuri wa watu kujifunza utendaji wa uadilifu na kujiwajibisha pale wanapokuwa wamekwenda kinyume.
Wabunge CCM wapongeza
Baadhi ya wabunge wa chama hicho, wamepongeza hatua hiyo na kudai kuwa itarudisha heshima na nidhamu ndani ya serikali ambayo imeporomoka kiasi kikubwa.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, alisema kuwa kilio chake na cha wabunge wenzake, hakikuwa na lengo la kumkoa yeyote wala kuleta madhara kwa chama chao, bali kilitokana na uchungu mkubwa walionao kwa watanzania na mali zao.
Filikunjombe alisema kuwa ajenda yao katika suala hilo, ilikuwa kuhakikisha kuwa serikali ya CCM inatekeleza kikamilifu ilani yake ya uchaguzi ambayo imelenga kuleta maisha bora kwa kila mtanzania, na hivyo, iliwaumiza zaidi baada ya kuona kuwa wapo baadhi ya wenzao kwa kutumia madaraka yao wamelenga kuiangamiza nchi kwa kutimia kofia ya chama.
Hilo ndilo tulilotaka la kuhakikisha kuwa tunaisimamia serikali yetu iliyoaminiwa na watanzania kuwaongoza kwa kupambana na wenzetu waliotugeuka. Tutaendelea kupigania haki za watanzania, bila kuchoka” alisema mbunge huyo.
Mbunge mwingine ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini, alidai kuwa uamuzi huo wa CC umempa faraja kubwa na sasa anaweza kurudi jimboni kwake akiwa na amani kubwa
“Siamini unachosema ndugu mwandishi. Kwa sasa sitaki utaje jina langu, langu, lakini kama ni kweli wamekubaliana hivyo, naweza kurudi jimboni kwangu kwa amani” alisema mbunge huyo.
Makatibu watano wateuliwa
Kamati Kuu ya CC, imewateuwa makatibu watano kukaimu nafasi za ukatibu katika mikoa mitano ya Geita, Njombe, Simiyu, Katavi, Kaskazini Magharibi.
Nape aliwataja walioteuliwa kuwa ni Hilda Kapaya, Shaibu Akwilombe, Hosea Mpagike, Alphonce Kinamhala na Aziz Ramadhani Mapuri, ambapo vituo vyo vya kazi vitapangwa baadaye.
Mwisho 

No comments:

Post a Comment