NDOA YANGU, Ningejua!
WAKAMATWA NA ATM 243 ZA BENKI YA NMB
Jeshi la Polisi mkoani Geita,limefanikiwa kuwakamata
watu wawili wakiwa na kadi 243 za watu mbalimbali wilayani Chato, zinazotumika
kutolea fedha kwenye ATM za Benki ya NMB kinyume cha sheria. Kamanda wa
polisi mkoani Geita, Leonard Paulo,aliwaambia waandishi wa habari ofisini
kwake,kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 7, usiku katika Kijiji cha Kitela
wilayani Chato. Aliwataja watuhumiwa hao kuwani Gidion Matiku (22) na
Seleman Hassan(30) mkazi wa Chato wote wakiwa wafanyabiashara wa duka la nafaka
pamoja na vifaa vya ujenzi. “Tunawashikilia watu hawa tukiendelea kufanya
uchunguzi zaidi kwa nini wanamiliki hizi kadi zote za ATM zilizotolewa na Benki
ya NMB wanazifanyia nini kwa sababu zina majina ya wateja mbalimbali, ambao
ndio wamiliki halali wanaotambuliwa na benki
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment