|
||
|
|
||
|
JK ahofia CCM kuanguka
2015
·
Asifu wapinzani kutembelea
wananchi
Mwenyekiti wa CCM taifa Rais Jakaya Kikwete, amekiri kuwa CCM itaanguka
katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutokana na kukithiri kwa rushwa miongoni
mwa watendaji wa chama hicho.
Kikwete alisema kuwa kwa sasa chama hicho kikongwe kimepoteza
matumaini kwa watanzania kutokana na vitendo visivyo vya kiungwana vinavyofanywa
na watendaji ndani ya chama.
Alisema hata kama itatokea kwa chama hicho kushinda uchaguzi mkuu
wa mwaka 2015 kama tabia walizonazo watumishi na viongozi hazitabadilika ni
wazi hakitapita kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Rais Kikwete, alitoa onyo hilo juzi usiku, alipofunga mafunzo maalum ya
siku nne kwa makatibu wa mikoa, makatibu na wenyeviti wa wilaya wa
chama hicho nchini mkoani Dodoma.
“Kama hatutabadilika katika suala la rushwa mwaka 2015 tutakuwa na
wakati mgumu sana na kama mwaka huo tutafanikiwa kuishika Serikali basi
mwaka 2020 hatutarudi tena madarakani.
“Najua rushwa ipo na mnaendelea kupokea shilingi laki mbili za airtime
(muda wa mawasiliano). Jueni kwa mtindo huu hatutafika ama wengine watavuka na
wengine kukwama.” Alisema na kuongeza;
“Viongozi wa chama ndiyo mmekuwa mawakala wa kusambaza rushwa bila hata
aibu, nawaombeni tubadilike kama tutaendelea hivi hali yetu itakuwa ngumu sana
katika chaguzi mbalimbali nawaambieni,”alisema.
Mbali na hilo alisema kuwa inasikitisha kuona kuwa wapo baadhi ya watu
ambao wameanza kujipitisha katika viongozi wa chama na kuwapatia hela kwa ajili
ya kuwapigia debe ili wawachague katika nafasi mbalimbali za urais ama ubunge.
Alisema kuwa kimsingi kwa sasa wapo watu
ambao wameisha anza kuzunguka na kujinadi kutafuta nafasi mbalimbali za
kugombea huku wakipenyeza rushwa jambo ambali linaendelea kukishushia adhi
chama hicho.
Akizungumzia chuki ndani ya chama alisema
watanzania kwa sasa wana akili zao na hawataki kudanganywa.
“Wapo badhi ya viongozi ndani ya chama
hawajui hata Ilani ya chama chao wakipanda kwenye majukwaa wanaanza kuzungumzia
ujenzi wa daraja la Mkapa ama lile la Malagarasi, watu hawataki kusikia hayo
mtu wa Ngara anataka kujua daraja lake limeishaje siyo la Mkapa” alisema
Hata hivyo alisema wazi kuwa kwa sasa
vyama vya upinzani vinafanya kazi kubwa zaidi ya kuwatembelea wananchi na
kusikiliza kero zao tofauti na ilivyo kwa chama cha mapinduzu kwani kwa sasa
CCM viongozi wake wapo mbali na wananchi.
“Nataka niwaambie vyama vya upinzani
vinafanya kazi kubwa na wanafika hatua ya kuaminika kwani wanapokwenda kwa
wananchi wanaambia kuwa CCM inafanya kazi za maendeleo kwa shinikizo la vyama
vya upinzani na wananchi wanaamini.
“Wananchi kwa sasa wanataka maendeleo na
kusikilizwa. Kwa sasa ukienda polisi umwambie RPC akuoneshe ratiba za mikutano
utaona orodha ndefu ya mikutano ni ya
vyama vya upinzani CCM hawapo mnafikiri hapo mtashinda.
“’Wapo watu ambao wanadai kuwa chama
kitafia mikononi mwangu nataka niseme kuwa chama hakifii mikononi mwangu
kitafia mikononi mwenu” alisisitiza Mwenyekiti wa chama hicho taifa.
Kikwete alisema kuwa siku hizi watu wana mbadala wa vyama vingine na
siyo CCM peke yao.
“Tuna vijana wengi kutoka katika vyuo mbalimbali ambao wanaweza kufanya
kazi kwa uadilifu wa hali ya juu hivyo hatuna budi kuachana na hawa wala rushwa
ambao watatupotezea sifa yetu kwa wananchi.
“Tukipoteza Urais ndiyo tumekwisha na chama kinaweza kufa.”
Katika hatua nyingine Kikwete aliwaonya
viongozi ambao wanajihusisha na uuzaji wa mali za chama kama vile viwanja na baadhi
yao kuingia mikataba yenye utata.
“Kuna watu wanapoingia mikataba sijui
wanakuwa wamelewa...kwanza unashindwa hata kuelewa...kwa mfano utakuta mtu
alipangishwa jengo la CCM kwa miaka 264 sasa unawaza huu mkataba wa aina gani
kwa sisi tuliopo hapa miaka 50 ijayo hakuna atakae kuwepo duniani sasa mmiliki
wa lile jengo atakuwa nani,?” alisema
Hata hivyo, aliwataka makatibu hao na
wenyeviti wa wilaya na mikoa kuhakikisha wanawatembelea wanachama wao na kutafuta
wanachama wapya kwa ajili ya kujiimarisha kwa chaguzi mbalimbali zijazo.
“Viongozi wengi hatuna tabia ya
kuwatembelea wanachama wetu na kuwatatulia kero zao hali ambayo inatugharimu
wakati wa uchaguzi kupata kura kidogo tofauti na idadi ya wanachama tulionao,”
alisema na kuongeza kuwa;
“Wenzenu wakiendelea kutembelea wanachama
na kutisha mikutano, nyie mnabakia kuimba wembe ni ule ule ushindi, shauri yenu
mtakatwa,”alisema.
Alisema wapinzani wanarikodi ya
kufanya vizuri kwa kufanya mikutano kuliko viongozi wa CCM.
Aidha, alisema iwapo hawatafanya kazi vizuri chama
hakitaweza kufanikiwa na kuwataka kutumia maarifa waliyopata katika mafunzo
hayo kuhakikisha chama kinakuwa imara na chenye uwezo wa kuongoza.
"Lazima muendelee kuongeza wanachama
sio kupanda majukwaani na kuimba iyena iyena...Utendaji mpya wa kuongeza
wanachama na kuwatambua na kuwapa majukumu,"alisema.
Mwisho
M
awakili wanaomtetea Kilewo kesi ya ugaidi wageuka walimu wa sheria katika kesi ya ugaidi Tabora
awakili wanaomtetea Kilewo kesi ya ugaidi wageuka walimu wa sheria katika kesi ya ugaidi Tabora
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kinondoni Henry
kileo ameunganishwa katika kesi ya kigaidi iliyofunguliwa katika mahakama ya
hakimumkazi mkoa wa Tabora.
Kilewo ameunganishwa na washitakiwa wengine 4ambao awali walifunguliwa kesi ya kumweagia mtu Tindikali wilayani igunga.
Hata hivyo kizungumkuti kilikuwa mapema asubuhi ya juni 24 ambapo washitakiwa hao kwa pamoja walifutiwa mashitaka ya awali na kasha kukamatwa tena na kufunguliwa upya mashitaka ya kigaidi ambapo walisafirishwa hadi Tabora Mjini kuunganana Kilewo.
Ndani ya mahakama ya hakimu mkazi mawakili wanaowatetea washitakiwa wakili msomi Petre Kibatalas na profesa Abdallah Safari waligeuka walimu wa vifungu vya sheria baada ya kupinga hoja zilizowasilishwa hapo na kuifanya kesi hiyo kuwa ya kigaidi.
Wameshitakiwa kwa makosa mawili moja la kigaidi la kumteka nyara Musa Musa Tesha na kosa la pili kuwa walimdhuru kwa kumwagia tindikali.
.
Mawakili waliomba mahakama kuona kama kweli kosa hilo ni la kigaidi pia mawakili waliiomba mahakama hiyo kurudisha kesi mahali ambapo washitakiwa wamekamatwa na wakashitakiwe huko.
Hakimu anayesimamia kesi hiyo hakimu mkazi Joktani Rushuera aliileza mahakama hiyo kuwa anaahirisha kesi hiyo hadi July 8 ndipo atakapotoa maamuzi kama kesi hiyo inalingana na ugaidi ama laaa, na kilichobaki hapo ni busara za hakimu kwani upande wa mawakili wa washitakiwa umeonesha wazi kupinga kesi hiyo kuwa ya kigaidi kwa vifungu vya sheria .
Washitakiwa wote watano wameshitakiwa makosa mawili moja la kula njama za kuteka ambalo linaingizwa katika kosa la kigaidi na lingine ni kumwagia tindikali Mussa Tesha mkazi wa igunga .
Hii ni kesi ya pili kufunguliwa dhidi ya CHADEMA kuhusu agaidi ambapo ya kwanza ilimuhusu mkurugenzi wa usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatale ambapo mahakama kuu ilitupilia mbali kesi ya ugaidi iliyoletwa mahakamani hapo kutokea mahakama ya Kisutu.
Kilewo ameunganishwa na washitakiwa wengine 4ambao awali walifunguliwa kesi ya kumweagia mtu Tindikali wilayani igunga.
Hata hivyo kizungumkuti kilikuwa mapema asubuhi ya juni 24 ambapo washitakiwa hao kwa pamoja walifutiwa mashitaka ya awali na kasha kukamatwa tena na kufunguliwa upya mashitaka ya kigaidi ambapo walisafirishwa hadi Tabora Mjini kuunganana Kilewo.
Ndani ya mahakama ya hakimu mkazi mawakili wanaowatetea washitakiwa wakili msomi Petre Kibatalas na profesa Abdallah Safari waligeuka walimu wa vifungu vya sheria baada ya kupinga hoja zilizowasilishwa hapo na kuifanya kesi hiyo kuwa ya kigaidi.
Wameshitakiwa kwa makosa mawili moja la kigaidi la kumteka nyara Musa Musa Tesha na kosa la pili kuwa walimdhuru kwa kumwagia tindikali.
.
Mawakili waliomba mahakama kuona kama kweli kosa hilo ni la kigaidi pia mawakili waliiomba mahakama hiyo kurudisha kesi mahali ambapo washitakiwa wamekamatwa na wakashitakiwe huko.
Hakimu anayesimamia kesi hiyo hakimu mkazi Joktani Rushuera aliileza mahakama hiyo kuwa anaahirisha kesi hiyo hadi July 8 ndipo atakapotoa maamuzi kama kesi hiyo inalingana na ugaidi ama laaa, na kilichobaki hapo ni busara za hakimu kwani upande wa mawakili wa washitakiwa umeonesha wazi kupinga kesi hiyo kuwa ya kigaidi kwa vifungu vya sheria .
Washitakiwa wote watano wameshitakiwa makosa mawili moja la kula njama za kuteka ambalo linaingizwa katika kosa la kigaidi na lingine ni kumwagia tindikali Mussa Tesha mkazi wa igunga .
Hii ni kesi ya pili kufunguliwa dhidi ya CHADEMA kuhusu agaidi ambapo ya kwanza ilimuhusu mkurugenzi wa usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatale ambapo mahakama kuu ilitupilia mbali kesi ya ugaidi iliyoletwa mahakamani hapo kutokea mahakama ya Kisutu.
Na Charles Misango
Udhalilishaji wa dini nyingine?
NIANZE kwa
kuungana na wananchi wote duniani walioweza kutamka, kusikitika na kulaani
filamu ya mmarekani mmoja ambayo inaelezwa kukashifu imani ya dini ya Kiislamu.
Naungana nao
kwa sababu mimi ni miongoni mwa wanaoamini uhuru wa kuabudu na kuheshimu sio
mawazo tu, bali hata imani ya mwingine hata kama kwangu sikubaliani nayo.
Filamu hiyo imeleta
madhara makubwa katika baadhi ya nchi nyingi duniani. Kumefanyika maandamano
makubwa katika nchi hizo, lakini lililo baya zaidi, kumetokea vifo vya watu
wengi wasiohusika, wala hawakuwa na taarifa yoyote juu ya kuwepo kwa filamu
hiyo.
Waliokufa
wengine hata huyo mtengeneza filamu hiyo hawamjui wala hawajawahi kumwona.
Wameponzwa na kitu wasichokijua. Wamekufa! Wamekwenda! Hawatarudi tena!
Hapa nchini
tukio hilo halikupita bure. Viongozi
wengi wa Kislamu walitoa matamko ya kulaani filamu hiyo. Tumshukuru Mungu
kwamba, kwa busara za viongozi hao, walifanikiwa kufikisha ujumbe wao bila kuhamasisha
waumini wao kufanya vurugu na maandamano ambayo kwa namna yoyote yangeleta
balaa.
Narudia.
Nakubaliana na kuungana kwa dhati na wale wote waliolaani filamu hiyo, ingawa
nimesikitishwa sana na vifo vya watu wasio na hatia wala kuhusiana na
mtengenezaji kwa namna yoyote ile, kwa sababu maisha yao yamekatishwa bure.
Nasikitika pia juu ya uharibifu wa mali uliofanywa na wenzetu ambao
wamechukizwa na filamu hiyo. Nina uhakika, walioharibiwa, masikini ya Mungu
hawana mchango wowote na uwepo wa filamu ya kumkashifu Mtume Mohammed (SAW).
Ni tukio
jingine baya kama lile la kile kitabu cha AYA ZA SHETANI kilichotungwa na
Salmine Rushidde miaka ile ya 90. Wenye kumbukumbu njema wanajua kile
kilichotokea duniani kwa wake ule.
Bila
kujikomba kwa yeyote, kitabu, filamu, chapisho lolote lile ama hata mahubiri
yanayodhalilisha, kutukana na kukashifu imani ya dini ama dhehebu jingine,
hufanywa na mtu ama watu wasiojali imani za wengine. Hufanywa na watu waliokosa
staha, wabinafsi, wachoyo, wenye upeo mdogo wa kufikiri, na mbaya zaidi wasiosumbua
akili zao kuona madhara yatakayotokana na matendo yao katika jamii.
Suala la
imani ya dini ni zito kwa maana ya uzito! Linalogusa uhai wa mtu. Kucheza na
imani ya mtu ni kucheza na roho ya mtu, hivyo, kwa namna yoyote ile linahitaji
kuchukuliwa kwa uzito na kila mtu. Kila anayetambua kuwa ni muumini wa dini ama
dhehebu fulani, anajua kuwa kile anachokiamini ndicho bora, safi na sahihi
kuliko cha mwingine. Kwake, wale wasioamini kama yeye waliopotea.
Kumbe, mtu
makini anayejali wengine, sharti awe mwangalifu na mwenye staha anapojaribu
kugusa imani ya mtu mwingine. Watu
waliojaliwa kuwa na upeo wa kufikiri, wenye kujali utu na hadhi ya wengine,
kamwe huwasikii katika kutangaza imani zao wakigusia kwa namna ya kudhalilisha
na kuudhi imani za wengine. Daima watazama kuhubiri, kufundisha na kutangaza
kile wanachoamini wao. Wataonesha uzuri wa dini zao, watanogesha tunu ya dini
zao, na watatoa matumani ya baadaye yanayopatikana kwa wale waliondani ya dini
zao na watakaojiunga nazo baadaye.
Wakati sote
tunaungana kulaani filamu hiyo inayoudhalilisha uislamu na Mtume Mohammed
(SAW), hapa nchini na hususan katika jiji la Dar es Salaam, kwa miaka kadhaa
sasa kumeibuka kundi la watu ambao bila woga, wala kujali na kuheshimu uhuru wa
kuabudu na imani ya dini nyingine, wamekuwa wakiendesha mahubiri dhidi ya dini
nyingine kwa lugha zilizojaa matusi, kejeli, dhihaka na udhalilishaji wa hali
ya juu.
Kundi hili,
limefanya hivi mchana kweupe na wanaendelea hadi nyakati za usiku, wakitumia
vipaza sauti vyenye nguvu kubwa na hivyo, matusi yao husikika kwa umbali
mkubwa. Watu hawa ambao huendesha mambo yao kwa mtindo wa maswali, ni mabingwa
wa lugha chafu zilizojaa mafundisho ya uongo wa kutisha! Wanatukana
wanavyotaka! Mathalani, wanadiriki hata kuita kuwa watu wa dini hiyo ni wajinga
na ndio maana kengere zao hulia…’wajinga njoo, wajinga njoo’ wameitwa makafiri
mara nyingi mno!
Swali la
kujiuliza, nani kawapa mamlaka ya kutukana na kudhalilisha dini za wengine?
Jeuri ya kufanya haya yote bila kujali, inatoka wapi? Hivi ikiwa wao hawako tayari kuona mtu yeyote
anadhalilisha dini, imani na kiongozi wao mkuu, na wako tayari kupambana hata
kumwaga damu kutetea imani hiyo, iweje kwao iwe ruksa kusema, kuhubiri na
kuendesha mihadhara inayotukana dini za wengine?
Hivi kama
sio busara na uvumilivu wa wale wanaotukanwa, ama leo hii nao wakasema yatosha
na wakaamua kutetea imani yao kwa njia yoyote dhidi ya wale wanaowatukana, je,
itakuwa nchi ya kukalika tena? Kwa nini
basi, wale viongozi makini, wanaojali na kuheshimu uhuru wa dini ya wengine;
kwa nini viongozi wa serikali walio na wajibu wa kulinda uhuru wa watanzania
wote wakae kimya wakiwaacha watu wachache WASIOJALI kutamba kwa matusi dhidi ya wengine? Nyote hakuna asiyejali hali
hii?
mwisho
Kwa heri Askofu Dk Paschal William Kikoti
ASKOFU wa Jimbo la Mpanda, Dk Paschal William Kikoti (55) aliyefariki Agosti 28, 2012 anazikwa leo jimboni kwake, huku mamia kwa maelfu ya waamini, watanzania na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakitarajia kuhudhuria mazishi hayo.
Miongoni mwa
watu mashuhuri wanaoshiriki mazishi hayo ni pamoja na Mwakilishi wa Baba
Mtakatifu nchini, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali
Polycarp Pengo na maaskofu karibu wote wa Tanzania, huku serikali ikiwakilishwa
na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Taarifa ya kifo
cha Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda mkoani Katavi, Dk Paschal William Kikoti
(55), zilipotangazwa usiku wa Agosti 28 na Makamu wa askofu Padri Patrick
Kasomo mbele ya waamini waliofurika ndani ya kanisa kuu la Mt Imakulata Mpanda,
zilipokelewa kwa mshituko mkubwa na baadhi ya watu walianguka na kupoteza
fahamu.
Kifo chake kimeacha simanzi na gumzo kubwa, na haikuwa ajabu kwa mji wa Mpanda na vitongoji vyake kuzizima kwa simanzi kubwa baada ya Padri Patrick Kasomo ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Karema iliyoko mwambao wa Ziwa Tanganyika kutoa taarifa hiyo kuwa kipenzi chao, kiongozi wao na mzazi wao aliyewatumikia kwa upendo mkubwa hayupo tena duniani.
Kifo chake kimeacha simanzi na gumzo kubwa, na haikuwa ajabu kwa mji wa Mpanda na vitongoji vyake kuzizima kwa simanzi kubwa baada ya Padri Patrick Kasomo ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Karema iliyoko mwambao wa Ziwa Tanganyika kutoa taarifa hiyo kuwa kipenzi chao, kiongozi wao na mzazi wao aliyewatumikia kwa upendo mkubwa hayupo tena duniani.
Mhashamu Askofu
Kikoti alifariki dunia baada ya kupatwa ghafla na ugonjwa wa shinikizo la damu jumapili
iliyopita saa moja asubuhi wakati akioga baada ya kuanguka, kisha kupoteza
fahamu. Aligunduliwa baadaye na mapadri
na watawa waliotoka kwenye ibada ya misa ya kwanza saa mbili na nusu asubuhi,
ikiwa ni saa nzima na nusu tangu alipofikwa na janga hilo.
Katika jitihada
za kuokoa maisha yake, uongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),
ulitafuta usafiri wa ndege siku hiyohiyo na kumsafirisha hadi Bugando kwa
matibabu zaidi, na ikabainika kuwa shinikizo la damu lilipanda kufikia 240 hadi
260, hali iliyomsababishia kifo.
Juzi jimboni Mwanza, hayati Askofu
Kikoti alifanyiwa
misa ya kumwombea ambayo ilifanyika katika Kanisa Kuu la Epifania, Bugando,
kabla ya mwili wake kusafirishwa kwa ndege majira ya mchana kuelekea mpanda.
Maisha yake jimboni Mpanda
Maisha yake jimboni Mpanda
Maisha ya
utumishi katika jimbo lake yanaelezwa kuwa ya kutukuka kutokana na tabia yake
iliyowavuta hata maadui zake. Haikushangaza basi, kuona umati wa watu
ukimiminika kwa siku mbili juzi na jana kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho
kwa marehemu.
Alikuwa ni mtu
aliyependa watu wa rika, kabila na imani zote, aliyejitolea kuwatumikia bila
kubagua. Zipo taarifa kwamba, hata ugonjwa wa shinikizo la damu ulichangiwa kwa
kiwango kikubwa na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika.
Baadhi ya
mapadri ambao hawakupenda kutaja majina yao, wamekiri kupoteza kiongozi
mashuhuri, makini na aliyekuwa jasiri katika kusimamia maadili mema, na
hakusita wala kuingiwa na wote kukemea na kuonya kwa upendo pale mmoja wa
mapadri alipokwenda kinyume na kiapo chake.
“Tumepoteza baba” ndivyo alivyosikika akisema padre
mmoja kwa majonzi, huku akikwepa kutaja jina lake. Hakuwa peke yake. Wenzake
walimuunga mkono huku wakielekea katika ndege ndogo kuupokea mwili wake
ulipowasili ukitokea Mwanza.
Kauli
ya Askofu Ruwa’ichi
Akihubiri wakati wa Misa ya
kumwombea Askofu mkuu wa jimbo la kuu Katoliki la Mwanza, Yuda Thadeus
Ruwa’ichi aliwataka waamini na wale watanzania wengine, kuiga mfano wa hayati
Kikoti ya kuishi katika uaminifu na kutokuwafanyia watu wengine mambo mabaya.
Askofu Ruwa’ichi aliwataka waumini
kujiuliza maswali ambayo yatatoa tafakari ya maana ya maisha yao hasa kwa
mkristo na kuwataka kuwa tayari kwa sababu hawajui siku wala saa ambayo mauti
itawakuta.
Alisema Mungu anasiri kubwa kwa
wanadamu na huwa inajidhihirisha kidogo kidogo katika mtiririko matukio yanayowakuta
binadamu na kwa mtazamo huo binadamu wanatakiwa kuishi kwa ushuhuda na kufanya
matendo yaliyo mema.
Aliwaomba waumini hao kuwaombea
maaskofu wao kutokana na kwamba wamekuwa wakibeba mizigo mkubwa ili wasiweze
kukata tamaa ya kuwatumikia.
Alisema kuwa maaskofu wanahitaji
ushirikiano mkubwa kwa waumini wao kutokana na kazi kubwa wanayoifanya ya
kutumia kanisa pamoja na watu wake.
Kikwete
amlilia
Naye Rais Jakaya Mrisho
Kikwete katika salamu za rambirambi kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania, Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, alisema pamoja na kupokea
kwa mshituko mkubwa taarifa ya kifo hicho, alikiri kuwa msiba huo ni pengo
kubwa la kiuongozi sio tu kwa Kanisa Katoliki hapa nchini, bali pia Jumuiya ya
Waamini wa Kanisa hilo kote duniani”. Rais Kikwete amekiri kutambua jitihada kubwa za hayati Askofu William Pascal Kikoti enzi za uhai wake katika kuwatumikia waumini wa Kanisa lake, na hususan wa Jimbo Katoliki la Mpanda, tangu alipopata Daraja la Upadre mwaka 1988, kuteuliwa kwake kuwa Askofu wa Kwanza wa Jimbo Katoliki la Mpanda mwaka 2000, na hatimaye alipowekwa Wakfu na Kusimikwa kuwa Askofu wa Jimbo hilo mwaka 2001.
“Kutokana na msiba huo mkubwa, ninakutumia wewe Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Salamu zangu za Rambirambi, na kupitia kwako kwa Kanisa Katoliki na kwa Waumini wote wa Kanisa hilo hapa nchini hususan wa Jimbo Katoliki la Mpanda, kwa kumpoteza mmoja wa Viongozi muhimu na wa ngazi ya juu wa kiroho, Marehemu Baba Askofu William Pascal Kikoti”, ameongeza kusema Rais Kikwete.
Historia yake
Askofu Kikoti alizaliwa Machi 3, 1957 huko Ihimbo, Parokia ya Nyabula, Jimbo Katoliki la Iringa. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Ihimbo, Iringa, kuanzia mwaka 1967 hadi 1973. Alisoma masomo ya Sekondari kidato cha Kwanza hadi cha Nne katika Seminari ya Mafinga kuanzia mwaka 1974 hadi 1977 na akaendelea na maomo ya kidato cha Tano na cha Sita katika Seminari ya Nyegezi Mwanza kuanzia mwaka 1978 hadi 1980.
Marehemu Askofu Kikoti alijiunga na jeshi la
Kujenga Taifa katika Kambi ya Makutupora kuanzia mwaka 1980 hadi 1981. Mwaka
1982 hadi 1983 alisoma Elimu ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Ntungamo na
baadaye akjiunga na Seminari Kuu ya Kipalapala kwa Masomo ya TaaliMungu
(Theolojia) kuanzia mwaka 1983 hadi 1988.
Alipata daraja la Upadri tarehe 29 Mwezi Juni 1988.
Kwa upande wa theolojia, alisoma Seminari Kuu ya
Kipalapala, Tabora na mwaka 1988 alipata daraja la upadri. Baada ya upadrisho
wake, alifanya kazi jimboni Iringa na kati ya mwaka 1989- 1990 alikwenda
masomoni Rome, Italia katika
Chuo Kikuu cha Urbaniana kuanzia mwaka 1989 hadi 1996 ambako alisomea Historia ya Mababu wa Kanisa na
Theolojia na kupata Udaktari wa Falsafa (PhD).
Mwaka 1997alirudi nchini na kufundisha katika Seminari ya Peramiho na Novemba
4, 2004, aliteuliwa na Baba Mtakatifu kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo la Mpanda.
Aliwekwa wakfu Januari 14, 2001. Kitaifa alikuwa Mwenyekiti wa Idara ya
Katekesi ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) tangu mwaka 2009 akisaidiwa na
Katibu Mtendaji, Padri Raphael Madinda.
Mbunge adai CCM ilipanga kumuua
*Spika ampa siku saba kuthibitisha
Na Martin Malera,Dodoma
Mbunge wa Ilemela Highness Kiwia (Chadema), amedai kuwa baadhi ya wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza walitaka kumuua.
Alisema anashangazwa na serikali kulifumbia macho suala hili licha taarifa zake kufikishwa mikononi mwa vyombo vya usalama.
Akichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa mwaka 2012/2013, Kiwia alisema mpango huo uliandaliwa siku nyingi na alipata taarifa hizo muda mrefu, akazipuuzia.
Mbunge huyo alisema kuwa wafuasi wa CCM walimteka na kutaka kuitoa roho yake wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo uliofanyika jimboni kwake katika Kata ya Kirumba jijini Mwanza.
“Wafuasi hao walitaka kuniua lakini kwa kuwa mimi nimefinyangwa kwa mikono ya Mwenyezi Mungu sitaweza kufa hadi hapo Mungu atakapotaka. Kutokana na maumivu niliyoyapata nililazimika kwendaIndia kwa ajili ya matibabu”
alisema Kiwia.
Mbunge huyo alisema kuwa mabadiliko na maendeleo ya wana Ilemela hayawezi kuondoka kwa wafuasi wa CCM kukatisha uhai wake.
Aidha alisema serikali imekuwa ikifumbia macho mambo ya kinyama ambayo yamejitokeza kwa baadhi ya watu kuwateka wengine na kuwafanyia vitedo vya kinyama.
Mbunge huyo alisema vitendo hivyo vinaonyesha kuwa serikali inapanda mbegu mbaya kwa vizazi vijavyo jambo ambalo ni hatari.
Baada ya kumaliza kijadili hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge), William Lukuvi aliomba mwongozokama tuhuma alizozitoa Mbunge ndani ya bunge kuwa wafuasi
wa CCM walitaka kumuua ni za kweli na atoe ushahidi.
Naibu Spika Job Ndugai alimtaka mbunge huyo kutoa ushahidi wa tuhuma hizo ndani ya siku saba na Kiwia aliomba kupewa muda ili aweze kuwasilisha vielelezo likiwemo gari la mbunge wa Viti Maalum Mariam Hewa ambalo lilikuwa katika tukio.
Z'bar imegeuzwa ‘mwanasesere’
Na Dauson Kaijage,Dodoma
MBUNGE wa Konde, Khatibu Said Haji (CUF),ametoa mpya Bungeni baada ya kudai kuwaZanzibar
imegeuzwa mwanasesere.
Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo aliwataka wabunge wote kutokaZanzibar kutounga mkono Bajeti ya Waziri Mkuu kama haitatengewa fedha za rada.
Akichangia mjadala wa hotuba ya Bajeti ya ofisi wa Waziri Mkuu na taasisi zake, Mbunge huyo alisema serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi kufanya sherehe za muungano ambazo hazina matunda wala faida kwa wazanzibari.
Alisema mambo mengi ambayo wanzazibar wanataka kuyafanya huwa yanapigwa chenga na kudharauliwakama mwanasesere.
Alidai kuwa kwa muda mrefu Waznzibari wamekuwa wakitaka kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu (OIC) na kuondoa mafuta katika suala la Muungano lakini mambo hayo hayajafanyika jambo alilosema kuwa ni kuwacheleweshea maendeleo.
“Hoja za msingi zaZanzibar
huwa hazifanyiwi kazi lakini hoj yasiyo ya msingi yanapewa kipaumbele,"
alisema.
“Sisi fedha za mfuko wa jimbo za kila mbunge zinatusaidia nini wala suala la malipo ya umeme. Nitawalipia bili wazanzibari wote lakini msikubali kupitisha bajeti ya waziri mkuu kama hawatatenga fedha za rada kwa ajili ya maendeleo yaZanzibar ” alisema Haji.
*Spika ampa siku saba kuthibitisha
Na Martin Malera,
Mbunge wa Ilemela Highness Kiwia (Chadema), amedai kuwa baadhi ya wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza walitaka kumuua.
Alisema anashangazwa na serikali kulifumbia macho suala hili licha taarifa zake kufikishwa mikononi mwa vyombo vya usalama.
Akichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa mwaka 2012/2013, Kiwia alisema mpango huo uliandaliwa siku nyingi na alipata taarifa hizo muda mrefu, akazipuuzia.
Mbunge huyo alisema kuwa wafuasi wa CCM walimteka na kutaka kuitoa roho yake wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo uliofanyika jimboni kwake katika Kata ya Kirumba jijini Mwanza.
“Wafuasi hao walitaka kuniua lakini kwa kuwa mimi nimefinyangwa kwa mikono ya Mwenyezi Mungu sitaweza kufa hadi hapo Mungu atakapotaka. Kutokana na maumivu niliyoyapata nililazimika kwenda
Mbunge huyo alisema kuwa mabadiliko na maendeleo ya wana Ilemela hayawezi kuondoka kwa wafuasi wa CCM kukatisha uhai wake.
Aidha alisema serikali imekuwa ikifumbia macho mambo ya kinyama ambayo yamejitokeza kwa baadhi ya watu kuwateka wengine na kuwafanyia vitedo vya kinyama.
Mbunge huyo alisema vitendo hivyo vinaonyesha kuwa serikali inapanda mbegu mbaya kwa vizazi vijavyo jambo ambalo ni hatari.
Baada ya kumaliza kijadili hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge), William Lukuvi aliomba mwongozo
Naibu Spika Job Ndugai alimtaka mbunge huyo kutoa ushahidi wa tuhuma hizo ndani ya siku saba na Kiwia aliomba kupewa muda ili aweze kuwasilisha vielelezo likiwemo gari la mbunge wa Viti Maalum Mariam Hewa ambalo lilikuwa katika tukio.
Z'bar imegeuzwa ‘mwanasesere’
Na Dauson Kaijage,
MBUNGE wa Konde, Khatibu Said Haji (CUF),ametoa mpya Bungeni baada ya kudai kuwa
Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo aliwataka wabunge wote kutoka
Akichangia mjadala wa hotuba ya Bajeti ya ofisi wa Waziri Mkuu na taasisi zake, Mbunge huyo alisema serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi kufanya sherehe za muungano ambazo hazina matunda wala faida kwa wazanzibari.
Alisema mambo mengi ambayo wanzazibar wanataka kuyafanya huwa yanapigwa chenga na kudharauliwa
Alidai kuwa kwa muda mrefu Waznzibari wamekuwa wakitaka kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu (OIC) na kuondoa mafuta katika suala la Muungano lakini mambo hayo hayajafanyika jambo alilosema kuwa ni kuwacheleweshea maendeleo.
“Hoja za msingi za
“Sisi fedha za mfuko wa jimbo za kila mbunge zinatusaidia nini wala suala la malipo ya umeme. Nitawalipia bili wazanzibari wote lakini msikubali kupitisha bajeti ya waziri mkuu kama hawatatenga fedha za rada kwa ajili ya maendeleo ya
Nape: Magamba lazima yavuliwe
Na Angelica Sullusi, Mbeya
CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) kimesema bado kinaendelea na mchakato wa kuwaondoa
madarakani wanachama wake wenye tuhuma za ufisadi na wale wasiokuwa na maadili
mazuri kwa jamii, maarufu kwa jina la kuvua gamba.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu wa CCM, Nape
Nauye Jijini Mbeya juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini hapa.
Nape
alisema kuwa dhana ya kujivua gamba ilipangwa kuwa na awamu tatu, ambapo awamu
ya kwanza iliwataka watuhumiwawawajibike wenyewe ingawa ilikuwa na mwitikio
mdogo.
Kwa
mujibu wa Nape awamu ya pili ya kujivua gamba ilipangwa kufanyika kupitia
uchaguzi wa ndani ya chama hicho, na kuwa awamu hiyo ndio sasa inaendelea.
Alisema
awamu ya tatu ni ya kuwawajibisha wahusika kupitia vikao vya chama, ambapo
mpaka sasa tayari vikao vya kuwajadili viongozi wa juu wa chama hicho wenye
tuhuma za ufisadi vimeanza na vitakapokamilika umma utashuhudia mageuzi makubwa
ya uongozi wa chama hicho kikongwe nchini.
Akizungumzia
kuwavua gamba viongozi wa ngazi za juu za chama, Nape alisema kuwa kuna orodha
ndefu ya viongozi wanaojadiliwa kwenye vikao na kuwa wale ambao
wataonekana hawafai, chama kitawalazimisha kujiuzulu au hawataruhusiwa kuchukua
fomu za kuwania uongozi katika mwaka huu wa uchaguzi wa ndani ya chama.
Hata
hivyo Nape hakuwa tayari kutaja majina wala idadi ya watu wanaojadiliwa na
vikao vya maadili vya CCM kwa madai kuwa hilo
bado ni suala la ndani la chama ambalo halina sababu ya kuelezwa hadharani kwa
ajili ya ustawi wa chama hicho.
“Watu
wanadhani kuwa mchakato wa mageuzi ndani ya chama umekwisha na hakuna lolote
lililofanyika, lakini napenda kuwahakikishieni kuwa unaendelea na utazidi
kufanyika mpaka pale tutakapoona wale wote wasiostahili wameachia madaraka
ndani ya chama,” alisema Nape.
“Wanachama wanaojitambua kuwa wanatuhuma au
jamii haiwakubali kutokana na kutokuwa na maadili, wasijisumbue kuchukua fomu
za kuwania madaraka ndani ya chama kwa sababu majina yao hayatarudi,” alisema Nape.
Mahakama yakataa ombi la
mwanaharakati
na Grace Macha, Arusha
MAHAKAMA ya Haki Binadamu ya
Afrika(AfHCRC) imetupilia mbali maombi yaliyoletwa mbele yake
na mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka nchini Nigeria , Femi Falana akipinga
mkataba wa Umoja wa Afrika (AU) unaotaka nchi wanachama waridhie mashirika
yasiyo ya kiserikali (NGO’s) au wananchi wake kufungua mashauri
kwenye mahakama hiyo vinginevyo makundi hayo hayaruhusiwi.
Uamuzi wa shauri hilo namba 001/2011 ulitolewa jana
na majaji 10 wa mahakama hiyo na kusomwa na Rais wake
, Gérard Niyungeko ndiye katika hukumu iliyochua dakika 45 kwenye
ukumbi wa mahakama hiyo iliyopo, jijini hapa.
Jaji Niyungeko alisema kuwa walifikia uamuzi huo
baada ya kupitia hoja za pande zote mbili na kuridhika kuwa AU ni taasisi ya
kimataifa yenye sifa za kuweza kushitaki na kushitakiwa pekee lakini haiwezi
kushitakiwa kwa niaba ya nchi mwanachama kama ilivyokuwa kwenye shauri hilo jambo alilosema kuwa kisheria mahakama haina mamlaka
ya kusikiliza shauri hilo .
Alisema kwa mujibu wa katiba ya AU ambayo iliridhiwa
na nchi wanachama, mkataba huo hauwezi
kufanywa katika jumuiya ya kimataifa, na kwamba sio mwanachama katika mkataba huo.
Awali Jaji Niyungeko
akisoma hoja za Falana alisema kuwa mwanahakati huyo aliieleza mahakama hiyo
kuwa kutokana na nchi yake kutousaini mkataba huo namba 34(6) inawanyima haki
wananchi na NGO’s kufika kwenye mahakama hiyo jambo alilodai kuwa ni kuwabagua.
Hata
hivyo Falana hakuwepo mahakamani hapo wakati hukumu hiyo ikisomwa.
Majaji wengine waliosikiliza na kufanya uamuzi juu
ya shauri hilo ni pamoja na makamu wa Rais wa mahakama hiyo, Sophia Akuffo,
Jean Mutsinzi, Bernar Ngoepe, Modibo Guindo, Fatsah Ouguergouz, Augustino Ramadhan, Duncan Tambala,
Elsie Thompson na Sylvain Ore ambapo Jaji Joseph Mulenga
hakuwepo mahakamani hapo kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kiafya.
Chadema yaiumbua
CUF
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimegeuza mashambulizi yake na safari hii kimekishutumu Chama cha wananchi (CUF) kwa kile walichosema kuwahadaa watanzania kiasi cha kuaminika kuwa ni wapinzani wa kweli.
Mbowe akifungua tawi la chadema katika eneo la Mihuta
wilayani Tandahimba alisema mwanzoni walidhani CUF kilikuwa na dhamira ya kweli
ya kuwakomboa wananchi na ndiyo maana waliwaachia mikoa ya kusini kwa ajili ya
kuendeleza kazi hiyo.
Aliongeza kuwa dalili za wazi za CUF kushindwa kuwatumikia watu wa kusini zimeonekana wazi baada ya kuamua kufunga ndoa ya mkeka baina yake na ccm.
“Ninachoweza kuwaambia wana Mihuta ni kwamba Chadema, CUF na CCM si baba yenu wala mama yenu nakama mtaona vyama hivi
haviwasemei achaneni navyo, na kwa kuwa Cuf na CCM mlishawapa dhamana hiyo
wakashindwa mviache sasa”alisema.
Aliongeza kuwa dalili za wazi za CUF kushindwa kuwatumikia watu wa kusini zimeonekana wazi baada ya kuamua kufunga ndoa ya mkeka baina yake na ccm.
“Ninachoweza kuwaambia wana Mihuta ni kwamba Chadema, CUF na CCM si baba yenu wala mama yenu na
Mbowe, amewataka wananchi wa wilaya ya Tandahimba
kuihukumu serikali ya CCM kwa vile haitetei maslahi ya watanzania hususan
wakazi wa Tandahimba na sasa inatumia mabavu kuwatisha hata katika haki
zao za msingi hususan pale wanapodai kulipwa kulingana na nguvu zao
zilizotumika
“Jamani Tanzania inasifika kwa kutajwa kuwa nchi inayofuata haki na sheria za binadamu lakini leo wanatandahimba mnapigwa mabomu na askari
wanaotumia kodi zenu kwa ajili ya kudai fedha za korosho ambazo kwa makusudi serikali imeamua kuwakopa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani” alisema Mbowe
Alibainisha kuwa hakuna haja ya wakazi wa Tandahimba na Mtwara kwa ujumla kwa kulazimishwa mazao yao kuuzwa kupitia stakabadhi ghalani wakati mikoa mingine haifanyiwi hivyo na wanauza mazao kwa matajiri wanaowataka na bei wanayoitaka
Dk Slaa atoboa siri ya CUF
“Jamani Tanzania inasifika kwa kutajwa kuwa nchi inayofuata haki na sheria za binadamu lakini leo wanatandahimba mnapigwa mabomu na askari
wanaotumia kodi zenu kwa ajili ya kudai fedha za korosho ambazo kwa makusudi serikali imeamua kuwakopa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani” alisema Mbowe
Alibainisha kuwa hakuna haja ya wakazi wa Tandahimba na Mtwara kwa ujumla kwa kulazimishwa mazao yao kuuzwa kupitia stakabadhi ghalani wakati mikoa mingine haifanyiwi hivyo na wanauza mazao kwa matajiri wanaowataka na bei wanayoitaka
Dk Slaa atoboa siri ya CUF
Naye Dk Slaa alitoboa siri ya namna CUF kilivyoamua kuwa
sehemu ya utawala, baada ya kufichua barua mbili zikiomba fedha kwa ajili ya
kuhudumia chama na safari za kifamilia za Makamu wa Kwanza
wa Rais Zanzibar.
Alisema barua ya kwanza ya Katibu Mkuu wa Cuf Maalimu Seif kwenda serikalini inaomba kuwezeshwa kufanyika kwa mkutano wao chama kwa siku tatu katika eneo la Bagamoyo kwa gharama za sh. milioni 34.
Dk Slaa alisema barua ya pili ni ile inayoomba dola za kimarekani 10,000 kwa ajili ya nauli ya kwenda Nairobi Kenya kwa mke wa Maalim Seif kwa safari ya
kifamilia, ikiwa ni sawa na dola 1,000 kwa siku.
Aidha Dk Slaa alisema katika taarifa hiyo inaonyesha pia kuna fedha za dharura kwa ajili ya matumizi ya makamu wa Rais ambayo ni dola 3000 na kudai kuwa huo ni ufisadi usioweza kuvumiliwa na wapenda haki.
Alisema kwa mfumo huo wa CUF kutegemezi hata katika mikutano yake ya chama fedha za serikali, ni ushahidi wa wazi wazi kuwa inafanya kila kitu kwa kuongozwa na
serikali ya ccm.
Alisema barua ya kwanza ya Katibu Mkuu wa Cuf Maalimu Seif kwenda serikalini inaomba kuwezeshwa kufanyika kwa mkutano wao chama kwa siku tatu katika eneo la Bagamoyo kwa gharama za sh. milioni 34.
Dk Slaa alisema barua ya pili ni ile inayoomba dola za kimarekani 10,000 kwa ajili ya nauli ya kwenda Nairobi Kenya kwa mke wa Maalim Seif kwa safari ya
kifamilia, ikiwa ni sawa na dola 1,000 kwa siku.
Aidha Dk Slaa alisema katika taarifa hiyo inaonyesha pia kuna fedha za dharura kwa ajili ya matumizi ya makamu wa Rais ambayo ni dola 3000 na kudai kuwa huo ni ufisadi usioweza kuvumiliwa na wapenda haki.
Alisema kwa mfumo huo wa CUF kutegemezi hata katika mikutano yake ya chama fedha za serikali, ni ushahidi wa wazi wazi kuwa inafanya kila kitu kwa kuongozwa na
serikali ya ccm.
Mgeja awashukia wasomi
Na
Mwandishi wetu, Kahama
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga na
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicvho, Hamis Mngeja amewashukia wasomi hapa
Nchini kwa kuendekeza mambo ya semina, makongamano,warsha pamoja na tafiti
mbalimbli huku wakiicha nchi ikiendelea kudidimia kiuchumi.
Mngeja
ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali la Mzalendo
Foundation, aliliambia Tanzania Daima kuwa baadhi wasomi wameshindwa kutumia utaalamu wao kulisaidia
taifa hususan kuinua maisha ya wakulima ambao sasa wanakandamizwa.
Alisema
mfumo wa bei za mazao ya wakulima katika masoko hauelweki na kusababisha
kuyumba kwa bei ya mazao kila wakati na kusababisha mkulima badala ya kunufaika
na bei inamdidimiza.
Mgeja
alimwomba Waziri wa Kilimo Christopher Chiza kusikia kilio cha wakulima
wa mazao hususan yale ya Biashara ambayo yamekumbwa na mtikisiko wa kuporomoka
kwa bei mara kwa mara.
Aliitaka
Serikali kujielekeza katika kulinda viwanda
na kutumia malighafi za ndani badala ya kupeleka nje ya nchi jambo
linalowanufaisha mataifa mengine.
Alisema
kuwa ikiwa taifa litawekeza kwa wingi katika viwanda vya ndani uchumi wa nchi
utakuwa imara na thamani ya kilimo itapanda na kupendwa na kila mtu kwa sababu
ndio njia pekee anayoamini itawasaidia wananchi kuondokana na umasikini
walionao.
Mwisho
THE HAGUE, Uholanzi
RAIS wa zamani wa Liberia , Charles Taylor jana
amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela na
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
Mwezi uliopita Taylor
alipatikana na hatia ya makosa 11 ya kufadhili na kusaidia waasi nchini Sierra Leone
ili apate madini ya almasi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo
mwaka 1991-2002.
Awali kabla ya hukumu hiyo, waendesha mashtaka
walikuwa wakipendekeza Taylor
ahukumiwe kifungo cha miaka 80 jela ambapo upande wa utetezi ulipinga kwa madai
kuwa adhabu hiyo ni kali mno.
Wakati akitoa hukumu hiyo, Jaji
Richard Lussick alisema kuwa uhalifu uliofanywa nchini Sierra ni wa
kustaajabisha katika historia ya binadamu.
Mwezi Aprili
Taylor alipatikana na hatia ya makosa 11, ikiwa ni pamoja na mauaji na
ubakaji.
Awali akijitetea, Taylor aliushutumu upande wa mashitaka
kuwalipa na kuwatisha mashahidi katika kesi hiyo.
Pia aliwaambia majaji katika kesi hiyo
wazingatie umri na afya yake wanapotoa hukumu dhidi yake, akisema'' yeye sio
tishio kwa jamii''.
Baada ya kesi hiyo kusikilizwa The Hague kwa hofu kwamba ingeendeshwa nchini Sierra Leone
ingesababisha vurugu. Serikali ya Uholanzi ilikubali kuendesha kesi hiyo nchini
humo lakini ikataka kifungo akatumikie nchi nyingine, hivyo atakwenda kutumikia
nchini Uingereza.
Aidha Waendesha mashtaka nao awali walisisitiza
kuwa afya ya Taylor
au kuwa kwake na familia, isiwe sababu ya kupunguza kifungo au kutofungwa.
Katika nyaraka zilizoandikwa kwa hisia,
waendesha mashtaka walisema kuwa kifungo cha miaka 80 walichokiomba awali kitawasilisha
ukali wa uhalifu na kule Taylor
kuhusika kwake kufadhili vita nchini Siera Leone.
"Uhalifu wa makusudi wa ukatili ni pamoja
na watu kunyongwa na kukatwa viungo vyao, vichwa vilivyokatwa katwa
vilionyeshwa katika vituo vya kukaguliwa...wanawake na wasichana wadogo
walibakwa hadharani na watu walichomwa wakiwa hai ndani ya nyumba zao,"
aliandika mwendesha mashtaka Brenda Hollis.
Hata hivyo mawakili wake wa utetezi walisema
kifungo hicho ni "dhahiri kisicho na uwiano wa kupindukia ", na
kwamba Taylor
alipatikana na hatia ya kuhusika ambako si kwa moja kwa moja.
Walisema kuwa mteja wao hapaswi kushutumiwa peke
yake kwa kile kilichotokea katika vita ya Sierra Leone .
BBC
MWISHO.
Nape ni
gamba- Maige
Katibu
wa Itikadi na uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye ametajwa kuwa gamba namba moja
linalotakiwa kuvuliwa, kwa kile kilichodaiwa kutoa matamshi mengi ambayo
yamekivunjia heshima na kukidhohofisha chama hicho.
Nape
pia ameshutumiwa kwa kushindwa kwake kubuni mbinu za kuingiza wanachama na
zaidi kupambana na wimbi la kuhama kwa viongozi, makada na wanachama wa CCM.
Shutuma hizo nzito
zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga,
Ezekiel Maige (CCM) jana wakati akizindua matawi mawili ya wakereketwa wa
chama hicho ambao ni wajasiriamali, katika kijiji cha Isaka wilayani Kahama.
Maige alisema kuwa
Nape amekuwa akitoa kauli ambazo si za msingi, zisizojenga bila kujua kuwa
zinakidhohofia chama hicho tawala.
Mbunge huyo ambaye
amepata kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema kwa sasa kuna wimbi kubwa
la wana CCM wanaohamia vyama vya upinzani, ambalo ilitegemewa kuwepo kwa juhudi
za makusudi za kuzuia chini ya usimamizi wa katibu huyo wa Itikadi na Uendezi.
“Kitendo cha CCM
kupoteza wanachama zaidi ya 1,000 kwa wakati mmoja mkoani Arusha na sehemu
nyingine wanachama 3,000, kinashitua, na ilitegemewa Nape kusimama imara na
kuhakikisha chama hakiendelei kupoteza wanachama wake, lakini ndio kwanza
anasema hajali na eti hao ni makapi” alisema kwa kushangaa.
Nape akihutubia
vijana mjini Bukoba siku chache zilizopita alidai kuwa hata kama
wanachama wote watahama, yeye (Nape) atabaki peke yake na CCM haitakufa.
Alidai kuwa kasi ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) haiwezi kupuuzwa na kiongozi
makini, na kuongeza kuwa zinahitajika busara na bidii za kuwapa moyo waliopo
ili nao wasiondoke na sio kuwasimanga.
“Jamani Nape
anachokifanya sasa ndani ya chama mimi ninaweza kuamini kwamba anatumika na
kukidhi matakwa ya waliomtuma na si manufaa ya chama”
“Ninalolisema hapa
lisitafsiriwe kwamba nalilia uwaziri, hapana, ila ni uchungu nilio nao kwa
chama changu kuona kila siku tunavyopoteza idadi kubwa ya wanachama,
tuliyemkabidhi jukumu la uenezi anasema hajali, sasa huyu si atupishe mapema
kabla mambo hayajaharibika?”
Maige alimwomba Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja kutumia nafasi yake kuwashauri wajumbe wa
halmashauri kuu ya Taifa (NEC) kuchukua hatua za haraka dhidi ya Nape
Wakati Maige akitoa
maneno hayo mazito, Mgeja alikuwa ameinamisha kichwa chake chini, lakini mamia
ya wana CCM pamoja na wananchi wengine walishangilia kwa nguvu.
Katika hatua nyingine
Maige aliwalaumu viongozi wa CCM katika ngazi ya wilaya na Kata ambao wamekuwa
na tabia ya kutowatembelea wananchi ma kusikiliza kero zao wakisubiri mpaka
viongozi wa kitaifa. Alisema tabia hiyo ni
moja ya chanzo cha wananchi kuichukia CCM.
“Jamani inakuwaje
kiongozi mwenezi wa CCM kata ama wilaya anakaa kimya kabisa hakuna kazi yoyote
ya uenezi anayoifanya hata kama katika kata
ama wilaya yake itakuwa imetembelewa na wapinzani na wakamwaga sumu, wao
hawajibu, wanasubiri mbunge ama diwani aitishe mkutano na wao hujitokeza,”
Alisema ili
kukabiliana na wimbi la mabadiliko ni vizuri wana CCM wakakaa chini na
kujipanga vizuri kwa kuwa kitu kimoja badala ya kugawanyika kutokana na maslahi
binafsi.
Mwisho
MUUNGANO NA HATIMA YA TANZANIA
Ni hivi majuzi tu mwezi uliopita Muungano wetu umetimiza miaka 48, kama
kawaida tulifanya Sherehe. Lakini ukweli ni kwamba kwa Sasa Muungano
wetu unahitaji kuadhimishwa kwa kitu kingine zaidi ya Maonesho kwenye
viwanja vya mipira, magwaride ya majeshi na hotuba zilizojaa nukuu za
Nyerere na za Karume.
![]() |
Kuzaliwa kwa Muungano |
Muungano wetu umedumu kwa miaka yote hii katika mazingira ya usiri na
ulinzi mkuwa mkubwa wa "mada" hiyo. Lakini ukweli ni kwamba, zama hizo
zimepita.
Maswali kuhusu Muungano
![]() |
Sheikh Karume |
Muungano huu ni wa nchi mbili ambazo kabla ya kuungana zilikuwa huru.
Katika mazingira ambayo hayafahamiki vizuri kwa Watu wa Nchi hizi mbili
mpaka sasa - hususan vijana - nchi hizi ziliungana na kuunda Nchi Moja
iliyokuja kuitwa Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania. Maswali mengi
yaliyobaki tangu kuundwa kwa Muungano huu hadi leo ni pamoja na:
- Majadiliano baina ya Nchi hizi mbili ili ziungane yalifanyika wakati gani na kwa muda gani?
- Ni wajumbe wapi na wapi walioziwakilisha nchi hizi mbili katika majadiliano hayo?
- Ni yapi yaliyokuwa makubaliano ya mwisho baina ya pande hizi mbili?
- Makubaliano ya majadiliano ya pande hizo mbili yalijadiliwa na Wananchi wa Nchi husika (moja kwa moja au kupitia mabunge yao) na kuridhia kuunganishwa kwa Nchi zao?
- Nakala ya Mkataba/Makubaliano baina ya nchi hizi mbili yalifikishwa kwa wananchi na kusambazwa kwa uwazi ili waelewe misingi ya kuunganishwa kwa nchi zao?
- Nani anayenufaika Zaidi na Nani anayepoteza Zaidi kwenye huu Muungano?
Maswali haya yote - pamoja na mengine mengi - inawezekana katika nchi
hii kuna watu wana majibu yake, lakini ukweli unabakia kuwa walio na
hayo majibu ni wachache (kama wapo kweli). Kwa misingi hiyo Muungano
tangu zama hizo mpaka leo umebakia ni kama kitendawili ambacho wananchi
wengi hawawezi kukitegua. Na wengine wamefikia hatua ya kuamini kuwa
Siri ya Muungano alikuwa nayo Nyerere na Karume (ambao walikuwa marais
wa Tanganyika na Zanzibar kwa wakati huo) na sio Watanzania wote!
Mwisho wa Zama Umefika
Wanasiasa na viongozi wa Serikali kwa ujumla walijitihidi sana kwa
miaka kuutunza, kuudumisha na kuulinda Muungano kwa njia mbali - kubwa
ikiwa ni kutoruhusu ujadiliwe - na walifanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Lakini ni wazi kwamba Zama hizo za "Giza" kuuhusu Muungano zinapita kwa
kasi - kama sio kwamba zimeshapita kabisa mpaka sasa!
Zanzibar: Wanawake Barabarani kutaka Muungano Upigiwe Kura! |
Zama za kuulinda na Kuudumisha Muungano kwa kutumia mbinu ya kuuficha usijadiliwe waziwazi zimefikia mwisho wake sasa.
Mapinduzi ya Uarabuni Yamewaamsha Watanzania!
Watanzani wa leo - hususan baada ya kushuhudia "Mapinduzi ya Umma"
katika nchi kadhaa za Kaskazini mwa Afrika na Uarabuni - leo hii wengi
wao nao wanaamini kwamba jambo lolote linawezekana kwa nguvu za Umma,
hata hapa Tanzania - NA INAWEZEKANA WAKO SAHIHI! Na huu ni ukweli
usiopingika kwamba Hakuna Nguvu Duniani hapa inayoweza kuishinda Nguvu
ya Umma - hata Serikali na Majeshi haziwezi kuzima nguvu ya Umma - Umma
uliojiunga na Kusimama pamoja!
![]() |
Mubaraka: nguvu ya Umma ilimng'oa |
Ukiwa unaongoza watu kama hao, ni wazi kwamba unapaswa kuwa makini sana
na mambo ambayo wao wanayataka au kuyaona ni ya kipaumbele na kuyapatia
nafasi stahiki - badala ya kudhani unaweza kuwanyamazisha kwa
"kujifanya" unashughulikia mambo mengine ambayo kwako ndiyo ya muhimu
zaidi - UTAKUWA UNAJIDANGANYA!
Maswali yanayobaki
Utaratibu huu wa sasa wa "kuulinda na kuudumisha" Muungano unaweza
kudumu iwapo tu Nchi ingeendelea kutawaliwa na CCM kwa Asilimia 100
siku zote (kutokana na sababu zinazojulikana). Lakini hilo kwa sasa
hilo halipo tena! CCM Inazidi kupoteza majimbo na Ushawishi miongoni
mwa raia kwa kasi kubwa kila kunapokucha. Vyama vyenye Upinzani
vilivyojawa na hamu ya kuhoji kila Sera ya CCM ndivyo vinazidi kupata
mvuto na kusikilizwa zaidi Nchini!
![]() |
Sera za CHADEMA zinamaswali mengi kuhusu Muungano! |
MOJA: Kwa Mfano, Iwapo CHADEMA Itachukua dola mwaka 2015 na ikaamua
kuigawa nchi katika Majimbo kama sera yake inavyoelekeza kwa sasa,
ZANZIBAR Itakuwa katika jimbo Lipi? Je, Itabakia ba hadhi yake ya Sasa
ambayo hata hivyo haijulikani Vizuri - au kutakuwa na Badiliko?
PILI: Iwapo Jumuiya ya Afrika Mshariki Itaanzisha Shirikisho la Kisiasa
(kuwa na rais Mmoja wa AM), Zanzibar itakuwa mgeni wa Nani chini ya huo
Mfumo? (maana muundo wa Muungano wa Sasa hauko wazi katika hilo
pia)!... na mengine mengi!
Dalili kutoka Zanzibar
Zanzibar Leo! - Tatizo ni Muungano! |
Mambo yanayoendelea kwa sasa visiwani Zanzibar - kwa hakika ni ishara
kubwa sana kwamba zama za kuulinda na kuudumisha Muungano kwa mbinu ya
Ukimya imepitwa na wakati. Vurugu zinazoendelea kwa sasa huko Zanzibar
- hususan zinapoanza kuhusisha hisia za Ubaguzi dhidi ya "wabara", ni
wazi kwamba Siku sio nyingi zitaweza kuigia bara, na kundi la kwanza
kutafutwa wanaweza kuwa Makamu wa Rais na Mawaziri kutoka Zanzibar -
kabla ya kuingia mitaani na kuwageukia wapenmba waliojazana kwenye miji
ya Tanganyika!
Katiba Mpya SIO Jibu!
Wakati vuguvugu la kudai katiba mpya lilipoanza kushika kasi mwishoni
mwa mwaka juzi (wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu) na hatimaye Serikali
ikazidiwa nguvu na Upinzani na kukubali Madai ya CHADEMA ya kuundwa kwa
katiba mpya (ikumbukwe CCM haikuwa na Mpango wa Kuunda Katiba Mpya
Tanzania wakati wa Awamu ya Pili ya Kikwete Madarakani), binafsi
nilidhani kwamba hii ndiyo ingekuwa fursa muhimu sana kwa Serikali
"kujivua lawama" za usiri na tatizo la Muungano kwa kuruhusu wananchi
waujadili Muungano huu wakati wanajadili katiba mpya na kuutolea
majibu! HAIKU WA HIVYO!
Uundaji wa Sheria ya Katiba Mpya bado ulighubikwa na "WOGA" ule ule wa
miaka neda rudi, na hatimaye Suala la Muungano kuondolewa kwenye
masuala yatakayojadiliwa! Ukweli ni kwamba hili NI KOSA, na kuna "mtu"
atalilipia hili kosa!
Nini Kifanyike?
Ushauri wangu kwa Rais Kikwete na Serikali kwa ujumla ni kutambua na kufanya yafuatayo:
- Kwanza, ni muhimu kwa Kikwete na Serikali yetu ya leo kutambua kwamba Watanzania wa leo sio wa miaka ile ya Uhuru - au enzi za Nyerere! Watanzania wa leo sio watu unaoweza kuwaridhisha kwa "maneno mepesi" huku ukikwepa kujibu maswali yao Magumu? Watanzania wengi wanataka waelezwe - kabla hawajashawishiwa kuendelea nao au kuuvunja - ni nani anayenufaika zaidi na huu Muungano na Nani anayepunjwa zaidi kwenye huu Muungano. Hili ni swali gumu ambalo linahitaji majibu magumu, zaidi ya zile hotuba ambazo tumezoea kuzisikia za kuuremba na kuupamba Muungano pasipo takwimu na Vielelezo!
- Serikali itafute njia nzuri ya kulileta Suala la Muungano katika mjadala wa Wazi wa Kitaifa. Kama nilivyosema hapo juu - Fursa kubwa ya kufanya hivyo ilikuwa ni Mjadala wa Katiba. Ninaposema "njia nzuri" ninamaanisha kwamba iwapo Serikali tayari ina mtazamo wake ambao isingependa ubadilishwe - hata na "wenye nchi" wenyewe (wananchi), basi ijipange kuuleta huu mjadala kwa namna ambayo itawavuta Watanzania wengi kuunga mkono matakwa ya Serikali ya kuudumisha!
Kinyume cha Hapo, kuendelea kuuficha-ficha na kuutetea Muungano kwenye
Hotuba pasipo kujibu maswali ya Msingi ya Wananchi, kutazidi kuongeza
idadi ya watu wanaotaka kujua kiini hasa cha "Usiri"huo, na hapo ndipo
tatizo litakuwa kubwa zaidi hata ya hapa lilipo leo!
![]() |
Watanzania kwa Sasa wanahitaji Majibu magumu Zaidi |
Kuendelea kukwepa kuujadili Muungano SIO kuulinda wala kuudumisha kama
ambavyo wanasiasa wetu wengi wanaweza kuwa wanajidanganya kwa sasa.
Kitendo hicho ni kuzidi kuongeza watu wanaouhoji na wale wanaotaka
majibu mazidi. Kwa kadri idadi ya watu wanaouhoji na kuutilia mashaka
Muungano itakavyoongezeka ndivyo Uwezekano wa Kuwapa Majibu Sahihi na
kuwaridhisha utakavyozidi kuwa mgumu - NA HUO NDIO UTAKUWA MWISHO WA
MUUNGANO!
DIWANI WA CCM KIZIMBANI KWA KUTISHIA KUUA
DIWANI wa kata ya Unyambwa (CCM) katika Halmashauri ya
Manispaa ya Singida Shaban Salumu Satu amepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya mwanzo Utemini kwa tuhuma za kutishia kumuua
mwandishi wa Habari wa kujitegemea wa gazeti la Tanzania Daima Mkoani
Singida,Bwana Josephath Isango kwa njia ya mtandao.
Kwa mujibu wa maelezo ya mashtaka yaliyowasilishwa Mahakamani hapo kwenye kesi ya jinai namba 338/2012 iliyofunguliwa may,29,mwaka huu,yanaeleza kwamba,diwani huyo kupitia CCM kata ya Unyambwa anashitakiwa kuwa may,10,mwaka huu saa 1:56 asubuhi kwenye maeneo ya Mtaa wa Mwenge,kata ya Majengo iliyopo Manispaa ya Singida kwa makusudi na bila halali alimtishia mlalamikaji Bwana Josephath Isango kwa njia ya mtandao kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0753 88 05 74 kuwa atamuua na kummeza ,kitendo ambacho ni kosa na kinyume cha sheria.
Hata hivyo mshitakiwa huyo baada ya kusomewa shitaka hilo alikana na yupo nje kwa mdhamana wa shilingi 300,000 za ahadi kwa mdhamini mmoja mwenye barua kutoka kwa afisa mtendaji wa mtaa hadi juni,05,mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Mlalamikaji licha ya kuwa mwandishi wa Habari vile vile ni Mwenyekiti wa vijana wa Chadema wa Mkoa wa Singida,lakini pia aliwahai kugombea nafasi ya kiti cha ubunge wa jimbo la Singida mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kwa mujibu wa maelezo ya mashtaka yaliyowasilishwa Mahakamani hapo kwenye kesi ya jinai namba 338/2012 iliyofunguliwa may,29,mwaka huu,yanaeleza kwamba,diwani huyo kupitia CCM kata ya Unyambwa anashitakiwa kuwa may,10,mwaka huu saa 1:56 asubuhi kwenye maeneo ya Mtaa wa Mwenge,kata ya Majengo iliyopo Manispaa ya Singida kwa makusudi na bila halali alimtishia mlalamikaji Bwana Josephath Isango kwa njia ya mtandao kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0753 88 05 74 kuwa atamuua na kummeza ,kitendo ambacho ni kosa na kinyume cha sheria.
Hata hivyo mshitakiwa huyo baada ya kusomewa shitaka hilo alikana na yupo nje kwa mdhamana wa shilingi 300,000 za ahadi kwa mdhamini mmoja mwenye barua kutoka kwa afisa mtendaji wa mtaa hadi juni,05,mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Mlalamikaji licha ya kuwa mwandishi wa Habari vile vile ni Mwenyekiti wa vijana wa Chadema wa Mkoa wa Singida,lakini pia aliwahai kugombea nafasi ya kiti cha ubunge wa jimbo la Singida mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Chadema yateka Mtwara
Na
Abdallah Khamis Mtwara
DHANA ya kuwa mikoa ya Kusini ni ngome ya Chama Cha Mapinduzi jana ilifutika vichwani mwa wakazi wa mikoa hiyo, baada ya umati mkubwa kujitokeza, kuulaki msafara wa viongozi na hatimaye kuhudhuria mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa Mkoani Mtwara.
Msafara huo wa Kitaifa ukiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, ulipata mapokezi ya vijana wakiwa katika msafara wa piki piki magari na baiskeli karibu na daraja la Mikindani na kuelekea katika uwanja wa mashujaa ambapo umati mkubwa watu ulifurika kupita kiasi.
Akihutubia katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe alisema ameshajiandaa kisaikolojia kufa kwa ajili ya kutetea haki na kwamba wananchi wasiogope kupigania haki zao.
Alisema ikitokea akafa akiwa katikati ya mapambano waliobaki wasihuzunike bali wahakikishe huo ndiyo unakuwa mwanzo wa ukombozi
“Nikifa katika mapambano haya uinueni mwili wangu uwekeni pembeni na kisha endeleeni na mapambano kwa kuwa haya si ya Mbowe peke yake bali ni ya watanzania wote”alisema Mbowe
Aliwaambia wakazi wa Mtwara kuwa hawakwenda pale kutafuta jimbo au Kata bali kuleta ukombozi wa kweli kwa kuwa ni wajibu wa kila mtanzania kuhakikisha nchi inakombolewa
Akizungumzia kuhusu udini, Mbowe alisema viongozi wa serikali wanaotumia udini, ukabila na ukanda kuwagawa watu wamekata tamaa ya kuwatumikia.
Alisema kuwa kwa hali ilivyo itakuwa ni hatari zaidi kwa ustawi wa Tanzania kama hata tone moja la mafuta yatapatikanahuku nchi ikiwa inaongozwa na serikali ya CCM kwa kile alichodai tayari wamemwaga damu kwa tamaa ya mali katika rasilimali zilzokwishaanza kupatikana
Naye Katibu mkuu wa Chadema Dk Willbroad Slaa aliwataka polisi kuacha kuwanyanyasa raia na kueleza hata yanayotokea Zanzibar kwa sasa ni udhaifu wa Rais Kikwete kutaka kuzuia watu wasitoe maoni
Alisema hatua ya kuwataka watu wasijadili suala la muungano wakati inawagusa haiwezi kukubalika na kwamba polisi wawe na akili ya kuambiwa na kisha kuchanganya na zao kwa ajili ya maslahi ya Tanzania
“Kikwete amesababisha hali hii ya Zanzibar, maana hakukuwa na haja ya kumkamata mtu aliyekuwa anatoa maoni juu ya mustakabali wa nchi yake”alisema Dk Slaa
Kuhusu bajeti ya 2012/2013 Dk Slaa alitaka zisimamishwe na mishahara ya wafanyakazi ziboreshwe
Kuhusu Korosho Dk Slaa alisema wakazi wa Mtwara wanafanywa masikini huku korosho zao zikienda kutoa ajira kwa wananchi wa India na wajanja wa chache wa hapa nchini
“Tanzania haitakombolewa bila mikoa ya Kusini kuwa huru, tunataka mtuunge mkono katika kila hatua ili tuchukue nchi 2015”alisema Dk Slaa
Mnyika adai bunge ni Kanyaboya
Mbunge wa Ubungo John Mnyika akihutubia umati huo alisema bunge la Tanzania halina nguvu ya kuiwajibisha serikali na kama itafanya hivyo Rais anaweza kuwatimua wabunge wote
Alisema hali hiyo nachangiwa kwa kiasi kikubwa na katiba liyopo ambayo alisema ni lazima watanzania wajitokeze na kuingiza mambo ya msingi wakati wa kutoa maoni
DHANA ya kuwa mikoa ya Kusini ni ngome ya Chama Cha Mapinduzi jana ilifutika vichwani mwa wakazi wa mikoa hiyo, baada ya umati mkubwa kujitokeza, kuulaki msafara wa viongozi na hatimaye kuhudhuria mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa Mkoani Mtwara.
Msafara huo wa Kitaifa ukiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, ulipata mapokezi ya vijana wakiwa katika msafara wa piki piki magari na baiskeli karibu na daraja la Mikindani na kuelekea katika uwanja wa mashujaa ambapo umati mkubwa watu ulifurika kupita kiasi.
Akihutubia katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe alisema ameshajiandaa kisaikolojia kufa kwa ajili ya kutetea haki na kwamba wananchi wasiogope kupigania haki zao.
Alisema ikitokea akafa akiwa katikati ya mapambano waliobaki wasihuzunike bali wahakikishe huo ndiyo unakuwa mwanzo wa ukombozi
“Nikifa katika mapambano haya uinueni mwili wangu uwekeni pembeni na kisha endeleeni na mapambano kwa kuwa haya si ya Mbowe peke yake bali ni ya watanzania wote”alisema Mbowe
Aliwaambia wakazi wa Mtwara kuwa hawakwenda pale kutafuta jimbo au Kata bali kuleta ukombozi wa kweli kwa kuwa ni wajibu wa kila mtanzania kuhakikisha nchi inakombolewa
Akizungumzia kuhusu udini, Mbowe alisema viongozi wa serikali wanaotumia udini, ukabila na ukanda kuwagawa watu wamekata tamaa ya kuwatumikia.
Alisema kuwa kwa hali ilivyo itakuwa ni hatari zaidi kwa ustawi wa Tanzania kama hata tone moja la mafuta yatapatikanahuku nchi ikiwa inaongozwa na serikali ya CCM kwa kile alichodai tayari wamemwaga damu kwa tamaa ya mali katika rasilimali zilzokwishaanza kupatikana
Naye Katibu mkuu wa Chadema Dk Willbroad Slaa aliwataka polisi kuacha kuwanyanyasa raia na kueleza hata yanayotokea Zanzibar kwa sasa ni udhaifu wa Rais Kikwete kutaka kuzuia watu wasitoe maoni
Alisema hatua ya kuwataka watu wasijadili suala la muungano wakati inawagusa haiwezi kukubalika na kwamba polisi wawe na akili ya kuambiwa na kisha kuchanganya na zao kwa ajili ya maslahi ya Tanzania
“Kikwete amesababisha hali hii ya Zanzibar, maana hakukuwa na haja ya kumkamata mtu aliyekuwa anatoa maoni juu ya mustakabali wa nchi yake”alisema Dk Slaa
Kuhusu bajeti ya 2012/2013 Dk Slaa alitaka zisimamishwe na mishahara ya wafanyakazi ziboreshwe
Kuhusu Korosho Dk Slaa alisema wakazi wa Mtwara wanafanywa masikini huku korosho zao zikienda kutoa ajira kwa wananchi wa India na wajanja wa chache wa hapa nchini
“Tanzania haitakombolewa bila mikoa ya Kusini kuwa huru, tunataka mtuunge mkono katika kila hatua ili tuchukue nchi 2015”alisema Dk Slaa
Mnyika adai bunge ni Kanyaboya
Mbunge wa Ubungo John Mnyika akihutubia umati huo alisema bunge la Tanzania halina nguvu ya kuiwajibisha serikali na kama itafanya hivyo Rais anaweza kuwatimua wabunge wote
Alisema hali hiyo nachangiwa kwa kiasi kikubwa na katiba liyopo ambayo alisema ni lazima watanzania wajitokeze na kuingiza mambo ya msingi wakati wa kutoa maoni
Aliongeza
wakazi wa Mtwara wanashindwa kufaidika na gesi iliyopo mkoani humo pamoja na
kukosa uwezo wa kumiliki ardhi kwa amendeleo yao .
Mawazo abeba silaha
Aliyekuwa diwani wa ccm kata ya Arusha alphonce Mawazo aliwaambia wakazi wa Mtwara kuwa mabadiliko ya kweli huanza kwenye akili na mtu
akishafungua akili kila kitu chake kitaenda kwa ufasaha na kuwa huru
Huku akishangiliwa na umati wa watu uwanjani hapo Mawazo alisema wameenda Mtwara wakiwa na silaha za nguvu ya umma, na kuwataka wasitengane katika kutafuta mabadiliko ya kweli, na kuachana na waliowasaliti kwa kuwaingiza katika maisha magumu.
Aliwaeleza wakazi wa Mtwara kuwa wamefungwa na minyororo ya umasikini na kwamba minyororo hiyo ni mibaya kwa mustakabali wa maisha yao kuliko hata minyororo ya chuma waliokuwa wakifungwa watumwa enzi za ukoloni
Millya CCM wameshaanza kuaga
Kwa Upande wake aliyekuwa Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Arusha James Millya alisema harakati zilizoanzishwa na ccm hivi karibuni kutaka nafasi ya mgombea urais ihojiwe mahakamani ni baada ya kugundua mwaka 2015 hawatakuwa na nafasi ya kushinda hivyo kimbilio lao ni mahakamani.
“CCM wanatuaga na mkitaka kuamini hilo sasa wameanza kutaka nafasi ya urais ihojiwe mahakamni kwa kuwa huko ndiyo kimbilio lao lililobaki
kwa sasa”alisema Millya
Alisema CCM wanaichukia Chadema kwa kuwa inataka uhakika wa maisha hata kwa motto wa masikini ambaye hajui hatma yake ya maisha kwa siku zijazo.
Aliongeza kuwa ni wakati muafaka sasa kwa watanzania kuachana na watu waliowasaliti kwa kushindwa kusimamia wajibu waliokabidhiwa.
Mwisho
Mawazo abeba silaha
Aliyekuwa diwani wa ccm kata ya Arusha alphonce Mawazo aliwaambia wakazi wa Mtwara kuwa mabadiliko ya kweli huanza kwenye akili na mtu
akishafungua akili kila kitu chake kitaenda kwa ufasaha na kuwa huru
Huku akishangiliwa na umati wa watu uwanjani hapo Mawazo alisema wameenda Mtwara wakiwa na silaha za nguvu ya umma, na kuwataka wasitengane katika kutafuta mabadiliko ya kweli, na kuachana na waliowasaliti kwa kuwaingiza katika maisha magumu.
Aliwaeleza wakazi wa Mtwara kuwa wamefungwa na minyororo ya umasikini na kwamba minyororo hiyo ni mibaya kwa mustakabali wa maisha yao kuliko hata minyororo ya chuma waliokuwa wakifungwa watumwa enzi za ukoloni
Millya CCM wameshaanza kuaga
Kwa Upande wake aliyekuwa Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Arusha James Millya alisema harakati zilizoanzishwa na ccm hivi karibuni kutaka nafasi ya mgombea urais ihojiwe mahakamani ni baada ya kugundua mwaka 2015 hawatakuwa na nafasi ya kushinda hivyo kimbilio lao ni mahakamani.
“CCM wanatuaga na mkitaka kuamini hilo sasa wameanza kutaka nafasi ya urais ihojiwe mahakamni kwa kuwa huko ndiyo kimbilio lao lililobaki
kwa sasa”alisema Millya
Alisema CCM wanaichukia Chadema kwa kuwa inataka uhakika wa maisha hata kwa motto wa masikini ambaye hajui hatma yake ya maisha kwa siku zijazo.
Aliongeza kuwa ni wakati muafaka sasa kwa watanzania kuachana na watu waliowasaliti kwa kushindwa kusimamia wajibu waliokabidhiwa.
Mwisho
Chadema yazidi kutikisa
·
Yazoa wanaCCM kila kona ya nchi
Na
Waandishi wetu Tabora, Bukoba
WIMBI la viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo,(Chadema) limezidi kushika kasi kote nchini, ambapo zaidi ya watu 300 wamejiunga na chama hicho mwishoni mwa wiki.
WIMBI la viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo,(Chadema) limezidi kushika kasi kote nchini, ambapo zaidi ya watu 300 wamejiunga na chama hicho mwishoni mwa wiki.
Mkoani
Tabora, aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya Tabora mjini, na diwani katika
kipindi cha mwaka 2000 hadi 2005, Moses Singu Sangu, ametangaza kujivua
uanachama wa CCM na kujiunga na chadema.
Sangu alifikia hatua juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igundu, Kata ya Ifucha Manispaa ya Tabora, akiwa ni miongoni mwa wana CCM 100 waliotua Chadema, wakidai kuchoshwa na kukithiri kwa rushwa ndani ya CCM ambayo anaamini hakuna wa kuiondoa.
Sangu ambaye kadi namba CDM 0562559 alisema kundi kuhama huko kwa wana CCM mkoani Tabora ni mwanzo tu kwa madai kuwa kuna kundi kubwa zaidi la wanachama litamfuata.
Alisema rushwa imekithiri ndani ya CCM na kutoa mfano wa chaguzi za mwaka 2000 na 2005, ambapo alidai aliongoza katika kura za maoni katika kugombea kuteuliwa kugombea udiwani wa kata ya Itonjanda kwa kura 380 dhidi ya mpinzani wake aliyepata kura 101, lakini nusura jina lake liondolewe baada ya kufuatwa na mtoto wa kigogo mmoja ndani ya CCM mkoa akitakiwa atoa chochote ndipo jina lipite.
”Nilipofuatwa niligoma kutoa chochota na baadaye nilisikia jina langu limepitishwakama mshindi halali.... hapo baada ya muda
kwenda.” alisema.
Hata hivyo, mwaka 2005 jinalake
lilikatwa licha ya kuongoza
katika kura za maoni kwa alama 148 huku wa pili akipata kura 48 kwa sababu muhula
uliopita alikataa kutoa chochote kwa “mzee”.
Alisema hali ndani ya kata hiyo kwa sasa ni mbaya kutokana na kushamiri kwa rushwa kunakofanywa na watendaji wengi wa vijiji, vitongozi na kata kwani wananchi wamekuwa wakipigwa faini hadi sh milioni moja wanapotenda makosa.
Aliongeza kuwa kutowajibika kwa watendaji wa CCM na serikali, kumechangia kwa kiwango kikubwa kuwepo kwa ukosefu wa miundombinu, maji na huduma za afya.
Ameeleza kukerwa kwake na tabia ya serikali kuwathamini wananchi kipindi cha uchaguzi tu na baada ya hapo wanaachwa wakiwa hoi.
Mkutano huo uliondaliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema, (BAVICHA), Manispaa Tabora, Saimon Lameck,zaidi ya vijana 100 walijiunga na chama hicho
Sangu alifikia hatua juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igundu, Kata ya Ifucha Manispaa ya Tabora, akiwa ni miongoni mwa wana CCM 100 waliotua Chadema, wakidai kuchoshwa na kukithiri kwa rushwa ndani ya CCM ambayo anaamini hakuna wa kuiondoa.
Sangu ambaye kadi namba CDM 0562559 alisema kundi kuhama huko kwa wana CCM mkoani Tabora ni mwanzo tu kwa madai kuwa kuna kundi kubwa zaidi la wanachama litamfuata.
Alisema rushwa imekithiri ndani ya CCM na kutoa mfano wa chaguzi za mwaka 2000 na 2005, ambapo alidai aliongoza katika kura za maoni katika kugombea kuteuliwa kugombea udiwani wa kata ya Itonjanda kwa kura 380 dhidi ya mpinzani wake aliyepata kura 101, lakini nusura jina lake liondolewe baada ya kufuatwa na mtoto wa kigogo mmoja ndani ya CCM mkoa akitakiwa atoa chochote ndipo jina lipite.
”Nilipofuatwa niligoma kutoa chochota na baadaye nilisikia jina langu limepitishwa
Hata hivyo, mwaka 2005 jina
Alisema hali ndani ya kata hiyo kwa sasa ni mbaya kutokana na kushamiri kwa rushwa kunakofanywa na watendaji wengi wa vijiji, vitongozi na kata kwani wananchi wamekuwa wakipigwa faini hadi sh milioni moja wanapotenda makosa.
Aliongeza kuwa kutowajibika kwa watendaji wa CCM na serikali, kumechangia kwa kiwango kikubwa kuwepo kwa ukosefu wa miundombinu, maji na huduma za afya.
Ameeleza kukerwa kwake na tabia ya serikali kuwathamini wananchi kipindi cha uchaguzi tu na baada ya hapo wanaachwa wakiwa hoi.
Mkutano huo uliondaliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema, (BAVICHA), Manispaa Tabora, Saimon Lameck,zaidi ya vijana 100 walijiunga na chama hicho
Huko Mkoani
Singida takribani watu 298 akiwemo mjumbe wa kamati
ya utendaji ya jumuiya ya wazazi ya Wilaya ya Singida vijijini, Michael Wawa
wamejiunga na Chadema katika jimbo la Singida Kaskazini.
Kujiunga kwa wanachama hao kulitokana na
ziara ya siku tatu ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Chadema, Godbles Lema na
Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Manyara, Rose Kamili katika jimbo hilo
linalowakiliswa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Katika siku ya kwanza katika kata ya
Ilongero, Chadema kiliwanyakua wana CCM 27, ambapo katika kata ya Ngamu jumla
ya wana CCM 210 walijiunga na chama hicho akiwemo Wawa.
Idadi ya walioikimbia CCM iliongezeka
katika mkutano uliofanyika Kata ya Msange ambapo waliojiunga ni 35 na Kijiji
cha Mwanyonye wakaingia wanachama 26, na hivyo kufanya jumla ya wanachama wapya
waliojiunga na chama hicho kufikia 298.
Juzi jijini Dar es Salaam , zaidi ya wanachama na watu
mbalimbali 3,000 walijiunga na Chadema katika mkutano mkubwa wa hadhara
uliofanyika katika viwanja vya jangwani na kuhutubiwa na viongozi wakuu wa
chama hicho.
Sitta afichua siri nzito
* Alazimika kukimbilia kwa JK
Na Betty
Kangonga
WAZIRI
wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta ametoboa siri nzito, akidai kuwa mmoja wa
wabunge wa jumuiya hiyo, kutoka hapa nchini alitia saini mkataba wa mazingira
ambao ni hatari kwa taifa, kiasi cha kumlazimu yeye kukimbia kwa Rais Jakaya
Kikwete kumzuia asiukubali.
Bila
kumtaja mbunge huyo, Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo, alidai kuwa, mbunge
huyo wa Afrika Mashariki alikubali kusaini muswada wa sheria ya mazingira
(transboundary Equal System), unaoleta kuzitaka nchi wanachama kulifanya suala
la mazingira lisimamiwe na jumuiya jambo ambalo ni hatari kwa taifa.
Sitta alitoboa jambo
“Ukisema
suala la mazingira lisimamiwe na jumuiya ina maana suala la ardhi ni lazima
liingizwe katika jumuiya yetu jambo ambalo linaweza kusababisha athari katika
nchi,” alisema.
Waziri
Sitta, alisema kutokana na kutishwa kwa hatua ya mbunge huyo imemlazimu
kuwasiliana na kumshauri Rais Kikwete ili asikubali kuupokea na kuusaini.
Aliwaonya
wabunge wateule wa Bunge la Afrika Mashariki kuwa makini katika maamuzi
mbalimbali yanayohusu taifa kutokana na baadhi ya nchi za jumuiya hiyo kutumia
ujanja hasa katika suala la ardhi.
Aliitaja nchi moja (jina linahifadhiwa) kuwa inajaribu kwa kila njia kuhakikisha ardhi inaingizwa katika jumuiya kutokana naTanzania kuwa
na ardhi kubwa kuliko nchi nyingine za jumuiya hiyo.
Aliitaja nchi moja (jina linahifadhiwa) kuwa inajaribu kwa kila njia kuhakikisha ardhi inaingizwa katika jumuiya kutokana na
Hata
hivyo Waziri Sitta, aliwataka wabunge hao kuhakikisha wanaweka mbele vipaumbele
vya taifa ikiwa ni pamoja na kilimo cha uzalishaji ili kuifanya Tanzania kuwa
ghala la chakula na biashara kwa nchi za Afrika Mashariki.
“Kuna
mchezo unaoendelea ambapo wenzetu (anaitaja) wananunua mahindi yetu na
kuyasindika huku wakiyaweka katika mifuko ya sembe na kwenda kuyauza nchi ya
Sudan Kusini’
“Niwaombe
wafanyabiashara wa hapa nchini wajaribu kuweka kinu cha kusindika mazao maana
masoko yapo mengi ya uhakika,” alisisitiza.
Naye, Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, alisema kuwa kwa sasa watakuwa na kamati maalum ya kushughulikia masuala ya Afrika Mashariki kutokana na kuweka ushirikiano baina ya ofisi yake na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki baada ya kuunda kikosi kazi ili kuangalia namna ya kuimarisha uhusiano na wabunge wa EALA.
“Ushirikiano huo utaondoa baadhi ya kasoro zilizojitokeza za kukosa taarifa za mwaka zinazofanywa katika bungehilo ,
kutokuwepo kwa nyaraka za majadiliano,” alisema.
Naye, Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, alisema kuwa kwa sasa watakuwa na kamati maalum ya kushughulikia masuala ya Afrika Mashariki kutokana na kuweka ushirikiano baina ya ofisi yake na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki baada ya kuunda kikosi kazi ili kuangalia namna ya kuimarisha uhusiano na wabunge wa EALA.
“Ushirikiano huo utaondoa baadhi ya kasoro zilizojitokeza za kukosa taarifa za mwaka zinazofanywa katika bunge
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa EALA, Adam Kimbisa, alisema kuwa watajitaidi
kuangalia lipi halali na haramu huku wakitumia akili zao kuepuka kutumiwa na
baadhi nchi katika bunge hilo .
Mwisho.
Kafumu amkubali Jaji
Na Mustapha
Kapalata, Nzega
MBUNGE wa Igunga, Dk Peter Kafumu amefuta hoja yake
ya kumkataa Jaji Mery Nsimbo Shangali wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora,
aliyoitoa wiki iliyopita na sasa amekubali kuendelea na kesi yake.
Wakili
wa Kafumu, Antony Kanyama aliiambia mahakama hiyojana kuwa baada ya kujadili
kwa mapana na kutambua athari za kuahilisha kesi hiyo walifikia muafaka wa kukubali
jaji huyo aendelee kusikiliza kesi hiyo ambayo, imefunguliwa na aliyekuwa
mgombea ubunge kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Joseph
Kashindye, anayepinga ushindi wake.
Kutokana
na uamuzi huo, jana Mweka Hazina wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Mchemba alipanda
kizimbani kutoa ushahidi wake, akiwa ni shahidi wa 17 kwa upande wa utetezi.
Mwigulu ambaye ni mbunge wa
Iramba Maghalibi katika utetezi wake alikanusha mambo mbalimbali yakiwemo madai
ya kutoa matusi na kugawa fedha katika
baadhi ya mikutano ya kampeni wa jimbo hilo .
Mchemba
ambaye katika uchaguzi huo alikuwa Meneja wa kampeni wa CCM alisema chama hicho
kilitenga sh. ml 402 kwa shughuli nzima.
Akijibu
swali toka kwa wakili wa Kashindye, Prof. Abdallah Safari, aliyemtaka aeleze
madai kuwa September 16 mwaka jana aligawa fedha kwa walimu 70 katika shule ya
msingi Nkinga na kuwashawishi wakipigie kura chama chake ili kukinusuru
kisianguke, Mwigulu alikanusha kufanya hivyo kwa walimu hao wala taasisi yoyote
ya kiserikali na kuongeza kuwa shughuli za utoaji pesa hakuzifanya yeye.
’’Mimi
sihusiki na viji Petty Cash na husika na kusaini account kubwa hivyo viji petty
cashi vina wenyewe kama nilivyo taja hapo
mwanzo’’alisema Mchemba.
Mwigulu
alisema kuwa chama hicho hakiwezi kutetewa na kikundi cha walimu bali na
wanachama wa CCM waliopo sehemu mbalimbali nchini wakiwemo wa Igunga.
Mwigulu
alitamba kuwa CCM kinafedha nyingi na yeye ni bwana fedha ama mweka fedha wa
chama, kauli ambayo ilionekana kuwakwaza wananchi waliokuwa wakisikiliza
ushahidi wake.
Jaji Shangali
alimkea mbunge huyo kwa kutoiheshimu mahakama hasa kwa kutotumia lugha zisizostahili.
Katika
hatua nyingine, Mahakama hiyo ilikataa ushahidi wa shahidi wa 18 Fedrick Magaka
ambaye ni Afisa Mtendaji Kata ya Igunga, baada ya kubainika kuwa tayari alikuwa
amehudhuria baadhi ya vikao vya kesi hiyo. Kesi hiyo inaendelea leo.
Mwisho.
Shibuda: Nitatoboa siri za Chadema
Na
Danson Kaijage, Dodoma
MBUNGE
wa Maswa Magharibu, John Shibuda (Chadema) ametishia kutoboa kile alichokiita
siri za Chama hicho kwa madai kuwa ameishajizua zote.
Aidha
Shibuda amemtaka Mwenyekiti wa Baraza Vijana Chadema (BAVICHA), John Heche
amwombe radhi ndani ya siku tatu tangu leo (Jana) kutokana na kauli za
kumdahalilisha katika vyombo vya habari juu ya kutangaza nia yake ya kugombea
Urais 2015.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini hapa jana, mbunge huyo alidai alidai kuwa iwapo
Bavicha hawatamwomba radhi ndani ya siku tatu atatoa siri kubwa za vijana hao
zilizojifichika nyuma ya pazia.
“Niliingia
Chadema ili kuelewa mfumo na kanuni za chama, sasa nimeisha zijua siri zao
hivyo naweza kufanya jambo kwa wananchi wangu na watanzania kwa ujumla. Lazima
Heche anieleze ni kwanini ametoa matamko katika vyomba vya habari ambayo
yanalenga kunidhalilisha kwa wapiga kura wangu’ alisema.
“Sijui
kama ni kauli ya vijana au yake mwenyewe; na kama
Heche ni kiongozi au mlinda masilahi ya viongozi ndani ya chama wenye fikra za
ugandamizaji na ukabila ndani ya chama.”
Alisema
kuwa mwenyekiti huyo anatakiwa kueleza anaendesha baraza hilo kwa mawazo ya wajumbe au anatumia cheo
chake vibaya kwa lengo la kulida maslahi ya watu ambao ni wachache wenye fikra
hasi.
“Kwani
kuna nini mimi msukuma wa watu nikigombea urais au hao Bavicha wana siri gani
na wanamtaka nani awe rais’ alisema na kudai anatangaza rasmi kwamba atagombea
nafasi hiyo, na kama atapitishwa na Chadema,
atamteua Dk. Slaa kuwa meneja wake wa kampeni.
Mbunge
huyo alidai kuwa hawezi kutoka Chadema,
badala yake atapambana na kukabiliana na changamoto zote ndani ya chama
hicho.
“Mimi
sihami ndani ya chama lakini kama chama
kitanikataa basi nitapeleka mashitaka yangu kwa wananchi ili niweze kuwaeleza
kile kilichojificha nyuma ya pazia kwa watanzania.
“Nilitoka
CCM kwa lengo la kukataa kunyanyaswa nikategemea kuwa huku hakuna mambo kama hayo, hivyo hata huku siwezi kukubali kuburuzwa kwa
ajili ya maslahi ya watu wengine, na niliishamwambia Dk. Slaa kuwa siwezi
kuburuzwa na kukubali dhuruma kwa ajili ya watu wachache badala ya kuwatetea
watanzania’ alisema.
Alidai
kushangazwa na kauli ya Heche kutaka afukuzwe, akihoji itasaidia kuongeza
matawi mangapi ya Chadema nchini, akidai alikataa kukubali fikra hasi hata
alipokuwa CCM, hivyo hatakubali kufungwa mdomo kwa ajili ya watu wenye dhuruma,
na wanaoendekeza ukabila na ukanda ndani ya chama.
Aidha
alisema alipoulizwa ni kwa nini amekuwa akipingana na viongozi wenzake kwa
mambo mengi, na hivyo kuzua migogoro, alisema hana mgogorowowote ndani ya chama
na kutaka kama ipo iwekwe wazi.
Mwisho.
CCM: Hatuhofii mgombea binafsi
Na Tamali Vullu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)
kimesema hakihofii kuwapo kwa suala la mgombea binafsi katika uchaguzi kwa
madai kuwa suala hilo
ni kitanzi kwa vyama vya upinzani nchini.
Kauli hiyo ilitolewa jana
jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye
alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu semina iliyowakutanisha wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete
kuhusu mwongozo wa CCM katika kushiriki mjadala wa Katiba Mpya.
“Watu wanadhani CCM inaogopa
mgombea binafsi. Hapana, sisi hatuna tatizo. Inatupasa tuweke mfumo ambao
mgombea binafsi hatatumia madaraka vibaya…nadhani ni kitanzi kwa vyama vya
upinzani kwani kama suala hili lingekuwapo
kuna baadhi ya wabunge waliopo wasingeenda,” alisema.
Alisema kutokana na
umuhimu wa suala hilo , wameona na vema wananchi
wakapata fursa ya kutoa maoni yao kwa kadri kila
mmoja anavyoona kwa kuzingatia maslahi ya taifa katika suala hilo kabla ya kuingizwa katika Katiba mpya.
Suala la mgombea binafsi limekuwa likipingwa na
chama hicho kwa muda mrefu kwa hofu kuwa lingeweza kukiumiza pindi wanachama
wake wanaposhindwa kura za maoni, kwani wangeweza kusimama binafsi na kushinda.
Aidha, alisema mambo
mengine ambayo wamependekeza kuingizwa katika mjadala mpana ni suala la matokeo
ya uchaguzi wa urais kutohojiwa, ili kuondoa malalamiko yaliyojitokeza kila
baada ya uchaguzi mkuu.
Alisema baadhi ya vyama
vimekuwa vikilalamikia matokeo ya urais, lakini vimekuwa vikizuiwa na katiba
kwa kuwa imetamka matokeo hayo yakishatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) hayapaswi kupigwa mahakamani tofauti na ilivyo kuwa ubunge.
Alisema mambo mengine
ambayo chama hicho yamehitaji wananchi wapewe fursa ya kuchangia maoni yao ni utaratibu wa uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya
Muungano, utararibu wa uteuzi wa
mawaziri, waziri mkuu na utatibu wa uteuzi wa Tume huru ya uchaguzi.
Nape alisema mambo mengine
ambayo yanapaswa kuingizwa katika mjadala ni kero za muungano zilizopo husuasani
orodha ya mambo ya Muungano, nafsi ya rais wa Zanzibat katika uongozi wa
Serikali ya Muungano, mfumo wa mahakama na ukomo wa idadi ya wabunge.
Aidha walitaka uwepo wa
baraza la pili la kutunga sheria, muundo wa bunge/ baraza la wawakilishi na
aina ya wabunge/ wawakilishi.
Akizungumzia masuala
waliyokubaliana yabaki kwenye katiba ni kuendeleza sera ya kuwapo kwa usimamizi
madhubuti wa maadili ya viongozi kwa kuupa nguvu kikatiba.
Alisema kuwa suala hilo likiwa na nguvu ya
kikatibva litakuwa ni tiba kwa tatizo la viongozi kukosa uadilifu.
Alidai wanataka kubaki kwa
muundo wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano kuwa wa serikali mbili, kuendelea
kuwapo kwa mihitimu mitatu ya dola (Serikali, Bunge na Mahakama) na kuwapo kwa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
“Halmashauri Kuu ya CCM
ilijadili na kukubaliana misingi mikuu
ya taifa letu inabaki kwenye katiba ambayo ni kuendelea kuwapo kwa umoja wa
kitaifa, amani, utulivu, usawa na haki, kufanyika kwa uchaguzi wa mara kwa mara
katika vipindi maalum na kuendeleza uhifadhi
na ukuzaji wa haki za binadamu na kuheshimu usawa mbele ya Sheria.
“Mambo mengine ni kuendeleza
sera ya dola kutokuwa na dini rasmi na serikali kuendelea kuwa mmiliki wa
rasilimali kuu za nchi hususan ardhi,” alisema.
Alibainisha kuwa mambo
mengine ambayo wamependekeza kuendelea kubaki kwenye katiba ni kuimarisha
madaraka ya umma, kuhamasisha sera ya msingi ya kujitegemea, kusimamia usawa wa
jinsia na haki za wanawake, watoto na makundi mengine katika jamii, kusimamia
hifadhi ya mazingira na kuendelea kuwapo kwa rais mtendaji.
Alisema kuwa mapendekezo
hayo waliyokubaliana watayawasilisha kwa maandishi kwa Tume ya kuratibu maoni
kuhusu katiba mpya inayoongozwa na Jaji Mstaafu, Joseph Warioba.
Kwa muda mrefu kumekuwa na
shinikizo kutoka kwa watu wa kada mbalimbali, wakiwemo wanaharakati na
wanasheria wanaotaka kuwepo kwa mgombea binafsi jambo ambalo pia kiliwahi
kupigiwa debe na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mnamo mwaka 1995.
Moto wa kuwepo kwa mgombea
binafsi katika chaguzi za kisiasa ulianzishwa na Mchungaji Christopher Mtikila
alipofungua kesi ya kikatiba katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma mwaka 1993 akiiomba iruhusu kuwepo kwa
mgombea binafsi.
Katika hukumu iliyotolewa
Oktoba 24, 1994 na Jaji Kahwa Rugakingira, Mchungaji Mtikila aliibuka mshindi.
Hata hivyo, Serikali
ilikata rufaa Mahakama ya Rufani, lakini wakati rufaa hiyo ikisubiri
usikilizwaji na uamuzi, Serikali ilipeleka muswada bungeni na kufanya
marekebisho ya kikatiba na kuweka ibara inayotamka kuwa kila mgombea ni lazima
awe amependekezwa na chama cha siasa.
Februari 17, 2005,
Mchungaji Mtikila alifungua kesi nyingine Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam
akipinga marekebisho hayo ya Katiba ya mwaka 1994. Katika kesi hiyo alikuwa
akiiomba Mahakama hiyo pamoja na mambo mengine, iamuru kuwepo kwa mgombe
binafsi.
Katika hukumu iliyotolewa
Mei 5,2006, Mchungaji Mtikila aliibuka mshindi kwa mara nyingine baada ya
Mahakama Kuu kukubaliana na hoja na maombi yake na kuwepo kwa mgombea binafsi.
Hukumu hiyo ilitolewa na
na jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu wakiongozwa na aliyekuwa Jaji
Kiongozi, Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo.
Serikali ilikata tena
rufaa katika Mahakama ya Rufani, ikipinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu,
iliyosikilizwa na Jopo la Majaji Saba wa Mahakama ya Rufani Aprili 8, 2010.
Katika hukumu yake ya Juni
16, 2010, Mahakama ya Rufani ya Tanzania
ilitolewa na jopo la majaji hao saba walioongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania ,
Augustino Ramadhani, mahakama hiyo ilijifunga mikono baada ya kusema kuwa haina
mamlaka ya kutengua ibara ya Katiba.
Wengine katika jopo hilo
la majaji walikuwa Eusebio Munuo, Januari Msofe, Benard Luanda, Mbarouk
Mbarouk, Nathalia Kimaro na Sauda Mjasiri
Diwani CCM atishia
kumuua mbunge
- Polisi wamdaka na watoto wake
- Leticia Nyerere adaiwa kukamatwa
Mbunge Chadema
atishiwa kuuawa
- Polisi wamshikilia diwani na watoto wake
- Leticia Nyerere adaiwa kukamatwa Marekani
Na Mwandishi Wetu, Iringa
SIKU moja baada ya kundi
la vijana wanaoaminika kuwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwacharanga
mapanga wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mbunge wa Iringa
Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, sasa ametishiwa kuuawa.
Habari zinasema kuwa
Diwani wa Kata ya Nduli, Idd Rashid Chonanga, jana asubuhi alimvamia Mchungaji
Msigwa ofisini kwake na kumtaka ajue kuwa siku zake zinahesabika, hata kama
juzi alinusurika, lakini atahakikisha ameuawa kwa njia zozote zile, hali
iliyomfanya mbunge huyo kukimbilia polisi kuomba msaada.
Diwani huyo, ndiye
anayetuhumiwa kusimamia kikamilifu tukio la kucharangwa mapanga kwa wafuasi
watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati wa mkutano wa
mbunge huyo uliofanyika katika uwanja wa kata ya Nduli na kuwajeruhi vibaya.
Katika mkutano huo ambao
ulifanywa na mbunge huyo, mwenyekiti, katibu, wajumbe sita wa CCM wa kata ya
Nduli na wanachama wengine takriban 90 walihamia Chadema, huku ikidaiwa kuwa
wengine zaidi ya 150 wangelikihama chama tawala wiki hii.
Akizungumza akiwa polisi,
Mchungaji Msigwa alisema kuwa kauli ya diwani huyo imemtisha kwa kuwa anajua
ina baraka za viongozi wake wa ngazi ya juu.
Mchungaji Msigwa
alilitaka Jeshi la Polisi lisifanye mzaha katika jambo hilo, kwa kile alichodai
kuwa ni jambo la hatari na lenye lengo mahsusi la kuwatisha viongozi wa vyama
vya upinzani na wananchi baada ya kuona kuwa CCM inazidi kupoteza maelfu ya
wanachama wake kila kukicha.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Iringa, Evarist Mangalla, alisema hadi muda huo alikuwa hajapokea taarifa hizo,
lakini akaahidi kulishughulikia jambo hilo kikamilifu, ili kulinda amani na
usalama wa kiongozi huyo na raia wengine.
Hata hivyo, Tanzania
Daima imethibitishiwa kukamatwa kwa diwani huyo na vijana wa CCM waliohusika
kuwakata mapanga watu watatu waliokuwa katika mkutano wa mbunge huyo juzi.
Mmoja wa maafisa wa
polisi alidai kuwa miongoni mwa vijana waliokamatwa, wawili ni watoto wa diwani
huyo na kwamba watu wengine wanne, akiwemo mfanyakazi wa diwani huyo, bado
wanasakwa na jeshi hilo kwa kuhusina na tukio la juzi.
Akizungumzia kutishwa kwa
maisha kwa mbunge Msigwa, aliyekuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Nduli, Ayub
Mwenda, alisema tangu jana amekuwa akipokea vitisho na kudai kuwa hali hiyo
haitakisadia chama tawala, badala yake kinasababisha kichukiwe na hata na wale
waliokuwa wakikipenda.
“Wananchi wengi
wamechukizwa sana na tukio la juzi, na wakisikia tena na hili alilofanya huyu
diwani leo, ndio itakuwa imezidi kujipalia mkaa. Hii ni nchi ya demokrasia ya
vyama vingi, na kila mtu anayo haki ya kujiunga na chama chochote, sasa
inashangaza kuona inakuwa nongwa kwao,” alisema Mwenda alipohojiwa na gazeti
hili.
Wakati huohuo, mmoja wa
watu waliojeruhiwa vibaya katika shambulizi la mapanga juzi, Osca Sanga bado
amelazwa katika hospitali ya mkoa, wakati wengine wawili waliruhusiwa jana.
Mganga Mfawidhi wa
hospitali hiyo, George Kabona, amesema Sanga anaendelea na matibabu, ingawa
alikiri kuwa hali yake bado haijawa ya kuridhisha.
Leticia Nyerere adaiwa
kukamatwa Marekani
Katika tukio jingine, kuna madai kuwa Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (Chadema-Kwimba), amekamatwa nchini Marekani akikabiliwa na makosa mawili ya jinai.
Katika tukio jingine, kuna madai kuwa Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (Chadema-Kwimba), amekamatwa nchini Marekani akikabiliwa na makosa mawili ya jinai.
Taarifa zilizosambaa
sehemu mbalimbali nchini, zimedai kuwa mbunge huyo, Machi 26, mwaka huu,
alitenda kosa la kupatikana na kadi ya kijani kwa njia ya udanganyifu akidaiwa
kudanganya kuwa alikuwa mmoja wa waathirika wa unyanyasaji wa kifamilia.
Hata hivyo, habari hizo
zinadai kuwa mbunge huyo aligundulika kusema uongo kwa vile hati yake ya
kusafiria ilionyesha amefika Tanzania mara kadhaa ambapo kwa mujibu wa maelezo
yake alikuwa akidai kunyanyaswa kifamilia.
Aidha mtoa taarifa huyo
anadai kuwa Leticia anatuhumiwa kujipatia dola 15,000 kutoka kwa mtu aliyetajwa
kwa jina la Cooper, na pia kushindwa kufika katika mahakama ya Maryland
Februari 10 kusikiliza shauri hilo.
Hata hivyo, uongozi wa
Chadema nchini Marekani umekanusha vikali tuhuma hizo na kuziita za uzushi
zilizolenga kumchafua mbunge huyo machachari.
Katika taarifa yao
iliyosambazwa katika vyombo kadhaa vya habari, uongozi huo umedai kuwa
aliyesambaza ujumbe huo ana lengo baya na ni moja ya mbinu za wapinzani wao
kutaka kukichafua chama hicho na viongozi wake.
“Tunapenda kuchukua
nafasi hii kukanusha vikali taarifa iliyosambazwa kupitia mitandano ya kijamii
ya kwamba Leticia Nyerere amekamatwa. Kwa kweli hizi sio taarifa za kweli, ni
za uzushi na kutaka kuchafuana. Tunamlaani vikali mtu yeyote aliyehusika
kusambaza taarifa hizo,” ilisema sehemu ya taarifa hizo.
Juhudi kadhaa
zilizofanywa na Tanzania Daima kutaka kuwasiliana na mbunge huyo kwa njia ya
simu, zilishindikana hadi tunakwenda mitamboni.
Mwingine CCM atua Chadema Arusha
Na Grace Macha Arusha
WIMBI la viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukimbia chama hicho limechukua sura mpya baada ya aliyekuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa, Ally Bananga kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Bananga ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la UVCCM na Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya UVCCM mkoani hapa alisema kuwa amefikia umuzi huo baada ya kuchoshwa kutumika kama karai la ujenzi au fagio la taka, huku akimtuhumu aliyemtaja kama ‘mtoto wa mkubwa’ kuvuruga umoja huo.
Akitangaza uamuzi huo jana mbele ya waandishi wa habari, alisema amefikia umuzi huo baada ya kuona anatumia nguvu kubwa kupigania mabadiliko ndani ya chama hicho lakini inashindikana hivyo akaamua kukihama.
Bananga alisema kuwa kwa namna ambavyo CCM inaendeshwa haimpi fursa mtoto wa mkulima na mfanyakazi kama yeye kutimiza malengo ya kutumikia wananchi kwa kuwaongoza kutokana na fursa hiyo kupewa watoto wa viongozi pekee.
“Usaliti na makundi ndani ya CCM yanatishia uhai wa chama hicho na tayari yamekwisha angamiza Taifa letu, hata nafasi ya watoto wa wanyonge inazidi kuwa finyu, labda ujipendekeze kwa wakubwa ili upate nafasi ya kutumikia jamii au chama.
“Nafsi yangu haiko tayari kusimamia uovu huu sasa nimeamua kusimamia ninachokiamini bila uoga wala unafiki, kwa mfano tazameni yanayoendelea ndani ya UVCCM Arusha , mikono ya mtoto wa mkubwa inaumaliza umoja huo” alisema Bananga bila kumtaja jina mtoto huyo.
Alisema kuwa hawezi kuendelea kukaa kwenye chama kinacholinda waovu huku akitolea mfano kuwa licha ya wabunge na wananchi kupigia kelele juu ya ubadhirifu mkubwa uliofanywa na mawaziri nane ambao umelipa Taifa hasara ya mabilioni ya fedha lakini hakuna hatua zozote wamechukuliwa mpaka sasa.
Kwa upande wake aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Katibu wa Chadema mkoa wa Kinondoni, Henry Kilewo walimkaribisha kwenye chama hicho huku wakimtaka avute subira mpaka wiki ijayo atakapokabidhiwa kadi na viongozi wa kitaifa kwenye mkutano mkubwa wa hadhara wanaotazamia kuufanya mjini hapa.
Kilewo aliwataka vijana wote nchini kujiunga kwenye harakati kutafuta mabadiliko (M4C) yatakayowezesha kubadili hali ya uchumi wa Taifa na mtu mmojammoja hivyo kuwa bora zaidi huku akiwahimiza kuacha kuangalia maslahi yao binafsi.
Katika hatua nyingine aliyekuwa diwani wa Sombetini, Alphonce Mawazo ambaye naye alijiunga na Chadema kiongea kwenye kikao hicho alisema kuwa ni unafiki mkubwa mtu yeyote anayedai anapigania maslahi ya wananchi kuendelea kubaki ndani ya CCM.
Akiongea kwa sauti kubwa ambayo ilionyesha dhahiri kuwafikia watu waliokuwa meza za jirani akiwemo Waziri wa Afrika Mashariki, Samweli Sitta , Mawazo alisema kuwa mtu yeyote mwenye dhamira safi ya kuwatumikia wananchi akiwa ndani ya CCM ni lazima atakufa kwa shinikizo la damu (pressure) kwa kufikiria maovu yanayofanywa na viongozi wa chama hicho kwa wananchi.
Hivi karibuni aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoani hapa , James Millya alikiama chama hicho na kujiunga na Chadema ambapo baada ya siku chache walijitokeza badhi ya viongozi wa umoja huo wakamtuhumu kuwa aliondoka na fedha za umoja huo hali ilimlazimisha Katibu wa mkoa, Abdallah Mpokwa kuingilia kati na kutoa ufafanuzi kuwa madai hayo si ya kweli .
Hata hivyo hatua hiyo ya Mpokwa inadaiwa kuwa haikuwapendeza viongozi wake wa juu hali iliyopelekea kupewa uamisho wa haraka ukimtaka akaripoti wiki ijayo makao makuu ya umoja huo jiji Dar Es Salaam .
Juhudi za kumpata katibu mkuu wa UVCCM taifa, Martin Shigela kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda kutokana na simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.
Amwita Ole Millya ‘Scraper’
Katika hatua ya kushangaza, Nape aliwaita vyuma chakavu (scraper) makada na wanachama waliokihama chama hicho na kujiunga na upinzani, huku akimtaja kwa jina aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoani Arusha, James ole Millya, aliyetimkia Chadema hivi karibuni.
Kauli hiyo ilitokana na swali aliloulizwa kama CC imejadili upepo wa kisiasa ndani ya chama hicho kufuatia wanachama wake kukihama kwa kasi.
“Wala hiyo haikuwa ajenda yetu, hao waliohama ni ‘scraper’ hazina umuhimu kwetu kwa hiyo hatuwezi kujadili watu hao. Na nendeni mkaandike hivyo kuwa Millya ni ‘scraper’,” alitamba Nape.
Tundu Lissu aibwaga CCM
Tundu Lissu aibwaga CCM
· Aangua kilio baada ya hukumu
· Ulinzi mkali watanda mahakamani
Na Jumbe Ismailly, Singida
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma imetupilia mbali madai ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki na kumtangaza kuwa Tindu Lissu alishinda kihalali katika uchaguzi mkuu uliofanyika Okt,30, mwaka 2010.
Katika kesi hiyo ya madai iliyoanza kusikilizwa tangu Machi 12, mwaka huu walalamikaji wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walitarajia kuleta mashahidi 51 lakini kwa sababu zisizofahamika ni mashahidi 24 na vielelezo saba viliwasilishwa kama ushahidi mahakamani hapo.
Katika kesi yao ya msingi walalamikaji walikuwa wakipinga ushindi wa mlalamikiwa namba moja ambaye ni Tundu Antiphas Lissu kuwa mbunge kwa madai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.
Walidai kuwa ukiukwaji huo uliufanya uchaguzi huo kutokuwa huru, wa wazi na haki na hivyo kumfanya mgombea wa CCM asiweze kupata ushindi katika uchaguzi huo.
Lissu ambaye alishinda kwa kupata kura 13,787 na kumzidi mgombea wa CCM Jonathan Njau kwa kura 1,626 alileta mashahidi wanne tu akiwemo yeye mwenyewe.
Akisoma hukumo hiyo,Jaji Moses Mzuna alizitaja hoja zilizowasilishwa katika mahakama hiyo kuwa ni pamoja na mlalamikiwa kuandaa barua zilizodai kuwa ziliandaliwa na vyama vya siasa vya kambi ya upinzani ambavyo havikuwa na wagombea katika uchaguzi huo.
Hoja zingine ni kuwa na mawakala nje na ndani ya chumba cha kupigia kura zaidi ya sheria inavyoagiza, kutoa hongo ya usafiri na chakula kwa mawakala wa vyama vyote isipokuwa CCM, askari katika baadhi ya vituo waliacha shughuli zao na kwenda kufanya kampeni.
Hata hivyo jaji Mzuna ambaye alikuwa akisoma hukumu hiyo huku akitoa mifano ya kesi mbalimbali zilizotolewa hukumu na Mahakama Kuu aliweka bayana kwamba mashahidi wote walifika kutoa ushahidi walionekana kujichanganya wakati wa maelezo yao.
Alisisitiza pia kwamba waleta maombi katika kesi hiyo walishindwa kuwaleta mashahidi muhimu ambao wangeweza kutoa ukweli juu ya hali halisi ya kesi hiyo licha ya kufahamika, jambo lililotafsiriwa kuwa huenda walifanya hivyo kwa kuhofia kuharibiwa kesi yao.
“Wao ndiyo waliopaswa kuthibitisha bila kuacha shaka yoyote juu ya dai lao hilo la msingi, kwani walitakiwa kuwaleta waliobaini tuhuma hizo zikitendeka kwani ni jukumu la mleta maombi kuthibitisha ”alifafanua.
Jaji huyo alisema kesi hiyo ilijikita zaidi kwenye kushuku na hivyo walalamikaji kujikuta wakishindwa kuthibitishia Mahakama hiyo kikamilifu.
“Jambo la kushangaza ni kwamba mashahidi walioitwa Mahakamani hapa walikuwa ni sawa na watu wanaovaa koti kwa kubadili nje ndani na ndani nje huku mawakili wa waombaji wakijigeuza kinyonga kila walipokuwa wakitoa maelezo yao.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo Jaji Mzuna alisema ni vema Mahakama zisibariki pale inapobaini kuna kila dalili za kuwanyima haki wananchi wa jimbo husika.
Aliamuru walalamikaji kumlipa Lissu gharama alizotumika katika kesi hiyo , kwa mujibu wa taratibu za kisheria kuhusu madai ya gharama za kesi hiyo .
Aangua kilio
Lussu na mkewe katika hali isiyokuwa ya kawaida waliangua kilio mara baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo, huku akisema kuwa amesikitishwa na waliomshitaki kwa kile alichosema walijua hawana ushahidi wowote zaidi ya kutunga na kuhisia.
“Nakubaliana na matokeo ya hukumu hii na ni kweli kabisa haki imechukua mkondo wake, kwani waleta maombi hawakuwa na ushahidi wowote zaidi ya kutunga, kuhisi, kufundishana uwongo lakini mengi zaidi nitaongea na wananchi kule Kijijini kwatu Ikungi muda mfupi baadaye’ alisema LIssu.
Hukumu hiyo, ilipokelewa kwa shangwe kubwa na mamia ya watu, kiasi cha kulazimisha kuwekwa kwa vipaza sauti ili watu waliokosa nafasi ndani kuweza kusikiliza.
Ulinzi mkali wa polisi
Tangu asubuhi jana, askari wengi wa polisi na wale wa usalama wa taifa walitanda kila kona ya eneo la mahakama hii, kinyume kabisa na hali inavyokuwa siku zote.
Ulinzi huo uliandamana na ukaguzi mkali ambapo kila aliyeingia ndani ya jengo la mahakamana alikaguliwa, huku askari wakilazimika kuwazuia wananchi waliozidi kufurika katika mahakama hiyo kila muda ulivyosonga mbele.
Hata hivyo, haikuweza kuelezwa sababu za msingi za kuimarisha ulinzi huo, ambapo afisa mmoja wa jeshi la polisi aliyehojiwa kwa sharti la kutotaja jina alisema ni wajibu wao kulinda amani katika matukio mazito kama hilo.
MWISHO.
·
No comments:
Post a Comment