Breack news
NYUMBA za wakazi wa kabila la barbaig Manyara, zimechomwa moto nyumba wakazi kwa madai ya kujenga katika shamba la mwekezaji.
wakazi hao walikuwa wanaishi katika eneo hilo ambalo lilikuwa shamba la serikali ambalo pia lilichukuliwa kwa wananchi.
Tukio la kuchoma moto nyumba hizo limeanza tangu saa tano asubuhi huku wafugaji jamii wa kimasai na barbaig wakipinga hatua hiyo.
Hali ni tete mno katika eneo hilo, kwani wafugaji hao wamejikusanya kwa silaha za kijadi wakisaidiwa na wakulima, na jeshi la polisi nao wamezidi kujiimarisha kukabiliana na mapambano hayo.
Hakuna aliyeruhusiwa kubeba mali zake, na hivyo nyumba zinazochomwa zina mali zote wanazomiliki wafugaji na wakulima wa eneo hilo.
Wananchi hao wanapinga kwa sababu hadi sasa hawajaambiwa mahali pa kwenda, na wanayakataa madai ya serikali ya kudai kuwa kila mtu atagawiwa ardhi ya kumtosha kama danganya toto.
No comments:
Post a Comment