Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!

MDEE: Mangula hama Kawe



Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee, Chadema amemshauri Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Philip Mangula kuhama katika Jimbo hilo kama anaona ni vibaya kukaa katika Jimbo linaloongozwa na Chadema, kwani mkakati uliopo sasa sio kurejesha Jimbo hilo CCM bali kuhakikisha Wilaya nzima ya Kinondoni inaongozwa na Wabunge wa Chadema katika majimbo yote

Mdee pia amemshauri Mangula kama anataka mchango wa uzee wake utambulike aende kwanza Dakawa yeye na wana CCM wenzake wanapotuhumiwa kumiliki maeneo makubwa ya ardhi ya wananchi wanyonge waliyojipatia kinyume cha taratibu ili awe safi kutoa ushauri kama mzee.

Kauli hiyo ya Mdee inafuatia kauli iliyotolewa na Mangula akisema anajuta na anaona aibu kuishi katika Jimbo la Kawe linaloongozwa na Halima Mdee (Chadema), na kuwataka wanachama wa CCM kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2015 jimbo hilo linarudi kwao.

Mangula aliyasema hayo juzi alipozungumza na viongozi mbalimbali wa kata na wilaya zote za  jijini Dar es Salaam pamoja na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wa CCM.

“Ni aibu mimi ni mkazi wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, na Mdee ndiye Mbunge wangu sasa siku akisema anataka kuongea na wazee wa jimbo lake mimi ntafanyaje? siwezi kwenda nitasingizia naumwa ili nisiende” alinukuliwa Mangula.
Mdee amesema Chadema ina madiwani wachache kuliko wale wa CCM ambao huwa hawahudhurii hata vikao kubuni mapato ya Halmashauri, ndio maana tangu wawepo wabunge wa Chadema wilaya ya Kinondoni mapato sasa yameongezeka kutoka Bilioni 10 hadi Bilioni 25 na kuna uwezekano wa mapato hayo kuongezeka zaidi kadiri madiwani wa CCM wanavyopungua kwani madiwani wa Chama hicho bado wanalinda ulaji wao na wabunge wa chama chao.

Alimshangaa Mangula kwa kutaka majimbo yaliyoko Chadema yarudishwe CCM kwani wabunge wa Chama cha Mapinduzi hawahudhurii vikao na hawawakilishi wananchi wao na  kushindwa pia kuhudhuria mikutano muhimu ya maamuzi ya mapato na matumizi kwenye Halmashauri zao. 

Mdee vile vile alisema Mangula hana nia nzuri na maendeleo ya wananchi, angekuwa na nia nzuri asingependa majimbo yarudi CCM ambayo wawakilishi wake huwa hawaendi hata kwenye mikutano.
“Wazee wengi wa Chama cha Mapinduzi, kama Msekwa, Kinana, Magufuli hata Rais Kiwete Mwenyewe, makazi yao yapo Kawe, usalama wa Taifa makao yao yapo Kawe, Mawaziri wote wapo Kawe na wananipa ushirikiano wa kutosha kusaidia maendeleo ya Jimbo la Kawe kinachomsumbua Mangula mimi sikielewi anaendekeza siasa hata katika maendeleo, tutaiga nini kwa mzee huyu.

Aliongeza kuwa ameingia madarakani, amejitahidi kusimamia ujenzi wa barabara kuu na barabara ndogo maeneo ya Mbweni, Mabwepande na Bunju, maeneno ambayo yalikuwa hayana huduma za kijamii kama maji, umeme na barabara.

Mdee alisema, ni kutokana na utendaji mzuri wa wabunge wa Chadema, Wilaya ya Kinondoni sasa imepanda kimapato na pesa zinazopatikana asilimia 60 zinaenda kwenye shughuli za maendeleo, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo Wilaya yaTemeke ilikuwa inaongoza ikifuatiwa na Ilala.

Mdee aliongeza kuwa Mangula anachukizwa na utendaji bora wa wabunge wa Chadema kwani hauonyeshi matumaini kama CCM wanaweza kuyarejesha majimbo hayo siku za hivi karibuni.

“Jimbo la Kawe halitarudi CCM siku za hivi karibuni, akiona hawezi kuhama Kawe basi ahame Chama ili aweze kuwa huru, lakini Jimbo la Kawe litakuwa ndio chachu ya kusaidia majimbo mengine ya Wilaya ya Kinondoni yachague Chadema”.

MWISHO.


No comments:

Post a Comment