VATICAN CITY
MAKAO Makuu ya Kanisa
Katoliki Duniani (Vatican), yamewaonya maaskofu kutofanya mageuzi ya haraka
kabla ya kupata baraka za kiongozi wao, Baba mtakatifu Francis.
Onyo hilo lilitolewa juzi,
baada Dayosisi ya Ujerumani kusema kuwa wanandoa walioachana na kuoa tena,
kanisa hilo sasa litawaruhusu kupokea sakramenti ya ekaristi na sakramenti
nyingine.
Msemaji wa Vatican, Padri
Federico Lombardi, alisema kuwa Papa Francis atafanya sinodi maalum ya maaskofu Oktoba mwaka 2014, kujadili masuala yanayoikabili familia.
Alisema kuwa hatua ya
makanisa kujitangazia mageuzi yao wenyewe
yanaweza kusababisha mkanganyiko siku za usoni.
Inavyoonekana Papa
Francis anaweza kuyatilia maanani changamoto zinazojitokeza kwa mujibu wa sheria
za kanisa, hasa kuhusu watu waliooa kwa mara ya pili kuruhusiwa kupokea
sakramenti ya Ekaristi
Papa Francis ameonekana
kukubali uwezekano wa mabadiliko katika sheria za kanisa, zinazowakataza watu
walioowa au kuolewa kwa mara ya pili kutoruhusiwa kupokea sakramenti kwa
kuzingatia kuwa vifungo vya ndoa havitenguliwi, jambo ambalo Maaskofu wengi
wanaliona kuwa tatizo kubwa katika majimbo yao.
Jimbo kuu la Freiburg nchini ujerumani, wiki
hii limetoa kitabu cha mwongozo kwa ajili ya mapadre wanaofundisha watu
Wakatoliki waliooa mara ya pili (mitara) kuelezea masitikiko kama njia ya toba
kwa kushindwa kuendelea na ndoa ya kwanza ili waruhusiwe kupokea Sakramenti ya
Ekaristi Takatifu na Sakramenti zingine
Akiongea Vatican, Msemaji
wa Papa Askofu Kardinali Lombard alisema Papa Francis hakuzungumzia mwongozo wa
kitabu hicho cha jimbo kuu la Freiburg, lakini alisisitiza kuwa Papa alifanya
majadiliano na Maaskofu wake kuhusu namna ya kufanya mabadiliko katika Kanisa.
Papa huyu, mzaliwa wa
Agentina amelitikisa Kanisa tangu kuchaguliwa kwake mwezi machi mwaka huu kwa
kuelekeza mabadiliko zaidi kwenye masuala ya msamaha kuliko masuala ya utoaji
mimba na ndoa za jinsia moja mahali ambapo ndio kuna changamoto za wazi kwenye
mafundisho ya Kanisa hilo kongwe duniani.
Hata hivyo anaonekana
kupokea ushauri wa wasaidizi wake kwa karibu na wamesisitiza mara kuwa
mabadiliko hata kama yatatokea yatachukua muda kufikiwa.
Katika hali
isiyotarajiwa, Askofu Mkuu wa Freiburg Robert Zollitsch, ambaye pia ni Rais wa
Baraza la Maaskofu nchini ujeruman alipokea mitazamo miwili tofauti wiki hii
iliyojihusisha hasa na hoja ya
Kuonesha namna gani watu
wapo makini katika maisha yao ya imani wanaweza pia kutumia muda wao kushiriki
katika maisha ya Kanisa, alisema Alis Glueck Rais wa Kamati kuu ya wakatoliki
nchini Ujerumani
Kardinali wa Munich,
Reinhard Marx mmojawapo kati ya makardinali nane walioteuliwa kama washauri wa
Papa alikiita kitabu hicho cha mwongozo cha Freiburg kuwa ni “mchango katika
mjadala usiokwisha” na kusisitiza kuwa suala hilo litatatuliwa kwa manufaa ya
Kanisa zima ulimwenguni.
Maaskofu nchini Ujerumani
wamekuwa wakitoa maombi mara kwa mara kuiomba Vaticani iruhusu watu kutengana
na watu kuruhusiwa kuoa au kuolewa mara ya pili katika miaka ya hivi karibuni
kufuatia waumini waliooa mara ya pili au kutoolewa mara ya pili kuhudhuria misa
lakini wakiwa hawaruhusiwi kupokea sakramenti ya Ekaristi.
Kitabu hicho cha mwongozo
kimesisitiza kuwa Wakatoliki wanapaswa kukubali kuwa kuna ndoa ambazo
hazijafanikiwa, zimeshindikana hivyo wanapaswa kuzijadili na mapadre wao lakini
waonyeshe kwa imani kuwa watakuwa waaminifu kwa ndoa zao za pili na ni haki wao
kuwa na familia za aina hiyo, maana ndoa hizo pia zina roho wa Mungu kwani
zinategemea imani binafsi ya mtu kwa mwenzake na ushiriki wao kwenye maisha ya
Mama Kanisa
No comments:
Post a Comment