Magufuli
agomea wamiliki wa Malori
WAZIRI wa Ujenzi Dk John
Magufuli amesema atahakikisha kuwa anasimamia sheria ili jitihada zinazofanywa
na serikali za kudhibiti uharibifu wa barabara hazidhoofishwi na watu wachache
wenye nia ya kujinufaisha binafsi bila kuja maslahi ya Taifa.
Kauli hiyo ni muendelezo
wa mvutano kati ya wizara hiyo na
Wasafirishaji wa mizigo ambao wanapinga sheria ya tozo ya asilimia tano
kwa Wasafirishaji wanaozidisha mizigo na kusababisha uharibifu wa barabara.
Akizungumza kwa niaba ya
waziri huyo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Wizara hiyo, Martin Ntemo alisema nia ya serikali sio kuwatoza faini
wasafirishaji hao bali anachokusudia nikuwaona wasfirishaji hao wanakuwa
wazalendo katika kulinda barabara nchini.
Alisema hivi karibuni
kumejitokeza wasafirishaji wasio waaminifu waliokuwa na mawasiliano ya karibu
na watendaji wa zamani waliokuwa wakishirikiana nao kupitisha mizigo kinyume na
taratibu.
“Mianya hiyo kwa sasa
imezidi kudhibitiwa na hali kwa sasa ni nzuri tofauti na awali kabla ya
kupitisha zoezi la kuwabadilisha wafanyakazi takriban 400 ambao ni sawa na
asilimia 85 ya watumishi wote katika vituo hivyo na kuajiriwa wapya”alisema.
Hatua hiyo ya
kubadilishwa kwa watendaji hao inaelezwa kuwa ni chanzo kingine cha malalamiko
kutoka kwa baadhi ya wasafirishaji hao wakishirikiana na watenaji wasiokuwa
waaminifu.
Aidha, Ntemo alizipongeza
baadhi ya kampuni za usafirishaji kuwa mfano wa kuigwa, kampuni hizo ni Dar
Express, Cargo Star, Hood bus, Coca Cola, BM Coach, Bakheresa (AZAM Transport),
TBL, Golden Coach, Kanji Lanji bus, Taqwa, Consolidated Logistic, Lamada na
Puma.
“Kumbukumbu ziliofanyiwa
uchambuzi kwa kipindi cha miaka kumi zimebainisha kuwa yapo makampuni ambayo
hayana rekodi ya kuzidisha mizigo wakati wote yanapopimwa katika vituo vya
mizani ya barabarani”alisema.
Wamiliki
WAMILIKI wa malori
wamemtunishia misuli Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, na kueleza kuwa wao
hawajagoma ila wameamua kupaki malori yao ili wasiendelee kuharibu barabara.
Wamiliki hao
walieleza kuwa Waziri huyo amerudisha tozo ya asilimia tano kwa maslahi yake na
amekuwa mtu ambaye haambiliki, ashirikiani na wadau pamoja na kujichukulia
sheria mkononi.
Wakizungumza jana
jijini Dar es salaam, wamiliki hao walieleza kuwa sheria hiyo iliyotangazwa na
Magufuli kuanza kutumika Oktoba mosi, wao walipatiwa barua Oktoba 2 na kueleza
kuwa tozo hiyo imeondolewa hali iliyosababisha msongamano.
Karim Radha ni
Mkurugenzi wa kampuni ya Consolidated Ltd alisema kuwa wanaomba sheria hiyo ifuate utaratibu wa
kwenda bungeni na kupitishwa .
“ Anasema
washafirishaji tunataka faida kubwa huo ni uongo na sheria ya tozo ipo nchi
nyingi hata kwenye muunganiko wa nchi za Afrika mashariki, na hata nchi zilizo
katika umoja wa SADC, aseme kuwa anaogopa barabara zake hazina viwango hivyo
zitaharibika ,”alisema.
Davis Mosha kutoka
Delina Group, alisema kuwa wao hawabishani na kiongozi ila waziri hana dhama ya
kuvunja sheria iliyopo miaka 40 iliyopita.
“ Hatutaki
kukurupuka kwenda mahakamani kama ambavyo waziri alisema, tunasubiri majibu,
pia sisi hatupo kisiasa wala hatutumiki, hatujagoma ila tumepaki vyombo vyetu,”
Ibrahim Ismail
alisema kuwa tozo hiyo ilikuwepo kutokana na mizani zote kutokuwa na viwango
sawa.
Alisema kuwa Dk.
Magufuli hapaswi kuwasukumia wasafirishaji mzigo kuwa wanaharibu barabara aseme
tatizo lililpo na ukweli uonekane.
Faisal Edha alieleza
kuwa wao kama watanzania wana uchungu na nchi na hawatakubali kuharibu barabara
hivyo ni vyema Waziri akasimamia ujenzi wa uhakika wa barabara zilizo imara.
“Kwa mfano sasa
baada ya kutengua tozo hiyo magari mengi yanayotoka Afrika kusini yamekwama
Tunduma wakiwa wanaleta mzigo mgodini, hayo ni madhara, lakini bandarini pia
mizigo inazidi kuongezeka, matokeo yake mchi inakosa maendeleo na hawatendei
haki watanzania”aliongeza.
mwisho
No comments:
Post a Comment