MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa(MAUWASA)iliyoko
wilayani Maswa mkoa wa Simiyu inadaiwa kiasi cha shs milioni 650 na Shirika la Umeme nchini Tanesco.
Meneja wa MAUWASA,Mhandisi Edmund Mahugi aliyasema hayo jana wakati
akitoa taarifa fupi ya mamlaka hiyo kwa wadau wa maji waliokuwa
wanahudhuria semina ya siku moja katika ukumbi wa halmashauri ya
wilaya hiyo.
Alisema kuwa wamekuwa na deni kubwa la umeme kutokana na Wizara ya
Maji yenye jukumu la kulipa kuchelewa kulipa na hivyo kusababisha
Tanesco kuwakatia umeme na wao kushindwa kusukuma maji kwa wateja.
“deni hili ni kubwa tunalodaiwa na Tanesco lakini mamlaka yetu imekuwa
ikilipiwa umeme na wizara ya maji siye tunachokifanya ni kuwa
tunapoletewa tu gharama tulizotumia za umeme haraka tunazituma
wizarani ili zilipwe lakini wanapochelewa kulipa ndipo tunapokatiwa na
hivyo hatuwezi kutoa huduma”alisema.
Aliendelea kueleza kuwa suala hilo limekuwa ni moja ya changamoto
kubwa inayoikabili mamlaka hiyo na hivyo wateja wao kutupa lawama kwa
mamlaka jambo ambalo limekuwa likiwanyima raha katika utendaji wa
kazi.
Awali akifungua semina hiyo Mkuu wa wilaya ya Maswa,Luteni Abdalah
Kihato ambaye hotuba yake ilisomwa na Diwani wa Kata ya Binza,Aron
Mboje aliitaka Mamlaka hiyo kuwaelimisha wateja wao kulipia Ankara zao
za kila mwezi ili iweze kumudu gharama za uendeshaji na matengenezo na
hata uwekezaji mdogo kwa kuendeleza mtandao wa maji pale ambapo
haujawafika kwa wananchi.
Mamlaka hiyo inahudumia zaidi ya watu 80,000 na mifugo ipatayo 50,000
katika mji wa Maswa na vijiji nane ambavyo ni
Buyubi,Dodoma,Mwashegeshi,Mwabayanda,Sola ,Nghami,Zanzui na Malita..
MWISHO.

No comments:
Post a Comment