MADIWANI wa Manispaa ya
Kinondoni jana nusura wamuwajibishe mkurugenzi wa manispaa hiyo Fortunatus
Fwema kwa madai kuwa ameshindwa kusimaia kazi za
maendeleo alizopaswa kufanya katika robo ya tatu nya mwaka na
kuzitolea taarifa.
Kufuatia maazimio hayo ilimlazimu
Meya wa Kinondoni Yusuph Mwenda awaombe madiwani hao pasipo kujali vyama vyao
wampe muda mkurugenzi huyo, hadi kikao kijacho cha baraza hilo awe
ameandaa ripoti itakayoonyesha kazi aliyoagizwa asiamaie kupitia kamati mbali
mbali za baraza hilo.
Hali ya kutaka
kumuwajibisha Mkurugenzi ilianzia wakati madiwani wa manispaa hiyo waliokuwa
katika kikao cha kawaida kupitia muhtasari wa kikao kilichopita na kutaka kujua
manispaa imefanya nini katika maeneo ya wazi ambayo yalikubaliwa yalindwe na
taarifa zitolewe katika kikao kinachoendelea.
Mbali na taarifa hiyo pia
madiwani hao walitaka ufafanuzi wa ujenzi wa nyumba mbali mbali zinazoendelea
katika manispaa ya Kinondoni pasipo kuwa na vibali vya ujenzi huku manispaa
ikiwa haichukui hatua zozote za kushughulika au kuwawajibisha wahusika.
Diwani wa Ubungo Boniface
Jackob.(Chadema) alikuwa wa kwanza kuongea na kumuomba mwenyekiti wa kikao
hicho Yusuph Mwenda amuagize mkurugenzi kutoa taarifa ya maazimio ya kamati
mbali mbali juu ya kuyalinda maeneo ya wazi ya halmashauri ya manispaa ya
Kinondoni.
Abbas Tarimba diwani wa
Hananasifu (CCM)alisema katika ujenzi holela unaoendelea katika manispaa ya
Kinondoni ni wazi watendaji wanachangia kwa kuwa hawachukui hatua na kwamba ni
wakati muafaka kwa baraza la madiwani kuonyesha mfano kwa kuwawajibisha
watendaji wanaoshindwa kusimamia wajibu wao huku wakiendelea kupokea mishahara
ambayo ni kodi ya wananchi.
“Tusiwe wasemaji ambao
hatuna maamuzi tutoe mfano kwa kuwawajibisha watendaji hawa hatujui hawa
building Inspector (wakaguzi wa majengo) wanafanya nini kwa maana nyumba hizi
zisizo na vibali zinaendelea kujengwa kila siku na haifanyiki katika giza”
alisema Tarimba
Paschal Manota diwani wa
Kimara (Chadema)alisema kama kuwawajibishga watendaji ni lazima waanze na
mkurugenzi kwa kuwa ameshindwa kuhakikisha maagizo ya kamati yanatekelezwa huku
akieleza maagizo ya kamati mabli mbali yanayotakiwa kufanyiwa kazi yamekuwa ni
kama ngonjera katika masikioya watendaji.
Renatus Pamba ambaye ni
diwani wa Sinza(Chadema)alitaka baraza lifahamishwe ni lini na hatua
gani zitachukuliwa kwa maeneo ya wazi ya manispaa hiyo ambayo
yamejengwa na hayana nyaraka
Diwani wa Msasani Aisha
Sagamwiko (CCM)alisema licha ya kumtaarifu mkururugenzi juu ya ujenzi
unaoendelea wa nyumba ya ghoarofa tatu lkatika eneo lake pasipo kuwa na vibali
hakujafanyika jitihada zozote za kuzuia au kuangalia kama jengo hilo lipo
kihalali na matokeo yake wahusika wanamalizia bati pasipo kuulizwa uhalali wa
ujenzi huo.
Kwangu mimi pale
Msasani jengo la ghorofa tatu limanza msingi nikatoa taarifa kuwa
linajengwa na haionyeshi mtaalamu ni nani na muhusika ni yupi lakini mpaka leo
hakuna kinachofanyika sasa tunasubiri waje wahamie kwa matarumbeta huku
manispaa ikiwa imelala”alisema.
Kwa upande wake Ester
Samanywa, viti maalum Chadema alitaka kujua kama kuna mamlaka zaidi katika
kumiliki ardhi ya manispaa ya Kinondoni kwa kile alichoeleza majengo katika
maeneo ya Kawe Beach yanaendelea kujengwa huku wahusika wakiwa hawatekelezi
maagizo ya manispaa kusitisha ujenzi wa maneneo hayo.
Kufuatia hoja hizo madiwani
walisikika wakipaza sauti ya kutaka mkurugenzi awe wa kwanza kuwajibishwa na
kasha wafuatie watendaji wa chini yake.
Kutokana na hali hiyo
Mwenda alitaka majibu kutoka kwa mkurugenzi ambapo alisema maeneo ya wazi
yanatarajiwa kuwekewa vibao vya kuonyesha kuwa hayaruhusiwi kuvamiwa na kwamba
taarifa ya kamati mbali mbali atazitolea maelezo katika kikao kijacho.
Majibu hayo yaliamsha yowe
katika ukumbi huo wa manispaa ya Kinondoni kwa madiowani kupaza sauti kuwa
wanajibiwa kisiasa na kwamba hawaridhiki na majibu hayo, hali iliyomfany Mwenda
awaombe wawe na subira mpaka kikao kijacho ndipo wachukue hatua kama hakutakuwa
na utekelezaji.
“Tunatambua kuna
udhaifu katika kusimamia maeneo ya wazi katika maispaa yetu na hili
halifdichiki nianachoweza kuwaomba ni kutoa muda kwa mkurugenzi kama
alivyosema na hapo tutaangalia way forward(nini kitafuata)alisema
Mwenda
Mwisho
No comments:
Post a Comment