Uchaguzi Arusha
Ni Chadema
Yanyakua ushindi mnono
·
Mwigulu
Nchemba atimua mbio
·
Hofu yakimbiza
wapiga kura
·
Waangalizi
wa kimataifa waja
·
Mamia ya
polisi watanda jijini
Na Waandishi
wetu, Arusha
LICHA ya hujuma ya Chama Cha Mapinduzi na ufanisi mdogo wa Tume ya Uchaguzi wa Taifa, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimeibuka na ushindi mnono katika uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata nne za jijini Arusha.

Katika kata ya Elerai, mgombea wa Chadema Injinia
Jeremia Mpinga alimbwaga Emanueli Laizer wa CCM kwa kura 2,123 dhidi ya 1,569 Katika kata hiyo ambayo ilikuwa na wapiga kura
23797 waliyojiandikisha na vituo 55 vya kupigia kura, lakini idadi kubwa ya wananchi hawakujitokeza. Matokeo
ya kura yalitangazwa chini ya ulinzi mkali wa askari polisi wenye silaha zaidi
ya 40, na kupokelewa kwa shangwe kubwa na wafuasi na mashabiki wa Chadema.
Katika
kata ya Kaloleni, mgombea wa Chadema, Emmanuel Miliare alimshinda kwa mbali
mgombea wa CCM.
Akitangaza matokeo katika Kata ya Themi, msimamizi
wa uchaguzi Editha Mboye alimtangaza mgombea
udiwani wa Chadema Mallance Kinabo kuwa mshindi kwa kupata kura 674, akimwacha
mbali mgombea wa CCM Victor Mkolwe aliyepata kura 326, huku yule wa CUF Lebora
Ndervai akipata kura 307
Kata ya Kimandolu Chadema wameibuka na ushindi
mkubwa na kuiacha vibaya CCM.
Majina ya wapiga kura yatoweka
Dosari kubwa
iliwakumba wapiga kura baada ya majina, picha na maelezo kukosekana kwenye
daftari la wapiga kura karibu katika kata zote. Makamu Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi, Hamid M Hamid alikiri tatizo hilo na kudai kwamba tayari
alishawasiliana na wataalam wake wa mifumo ya kompyuta (IT) ili wayashughulikie
kwenye kila kata iliyokuwa ikiendelea na uchaguzi.
Hata hivyo alisema kuwa yeye si mchawi kuweza kubaini chanzo cha hitilafu hizo zilizojitokeza. Baadhi ya mapungufu yaliyobainika ni baadhi ya watu kuandikishwa zaidi ya mara moja. Kata ya Kaloleni kwenye kituo cha AICC Nursery B mpiga kura Michael Laurence alikuwa ameandikishwa mara tatu kwenye daftari la wapiga kura akiwa na namba 48674955, 444666858 na 13142914.
Hata hivyo kwenye majira ya saa saba mchana wataalam wa komputa wa tume walifika na kuanza kuwasaidia wananchi waliokuwa wamejazana kwenye kituo cha kata hiyo ambapo mmoja wa wataalam hao, Siif Mtezo aliwaeleza waandishi wa habari kuwa tatizo hilo lilisababishwa na watu kujiandikisha zaidi ya mara moja.
Alisema kilichowafanya wengi washindwe kuona majina yao ni hofu kama ile inayowakumba wanafunzi wanaoenda kuangalia matokeo, na kwamba tume ililazimika kuwapigia simu wananchi wengi waliokuwa wameondoka, na wakarudi kupiga kura.
Wakala wa Chama Cha Wananchi (CUF), Malik Abbas kwenye kituo hicho aliwaeleza waandishi wa habari kuwa wananchi wengi walifika lakini majina yao hayakuonekana na wakaondoka huku akionyesha baadhi ya picha ambazo hazionekani vizuri kutokana na kufifia kwenye daftari hilo.

Mgombea
udiwani wa kata hiyo kwa tiketi ya CUF, Abbas Darwesh alisema wananchi wengi
walishindwa kupiga kura akiwemo mtoto wake , Omary Othman ambaye pamoja na kuwa
na kitambulisho chake namba 32479962 jina lake halikuonekana kwenye orodha.
“Inawezekana kweli kuna mchezo mchafu umefanyika kubadili daftari la wapiga kura kama ambavyo tetesi zilikuwa zimezagaa kwa sababu mtoto wangu mwenyewe alipiga kura kwenye kituo hiki katikauchaguzi wa 2010, lakini leo naambiwa jina lake halipo” alilalamika Darwesh.

Msimamizi wa uchaguzi Kata ya Kaloleni Anna Lebisa
amekiri kukosekana kwa majina ya wananchi katika daftari licha ya kuwepo katika
mbao za matangazo na kusema hawakuruhisiwa kupiga kura. Miongoni mwa waliokumbwa
na kadhia hiyo ni Omari Othmani na mtangazaji wa TBC Khalifa Mshana ambao alilazimika
kulifikisha suala lao kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji
mstaafu Hamid Mahmood ambapo alimuachia afisa wa tume kulishughulikia.
Mwenyekiti wa jukwaa la Katiba Deus Kibamba akiwa
na timu yake ya waangalizi wa uchaguzi huo alisema kura zimeanza kupigwa
taratibu na idadi ndogo ya watu kujitokeza akidai kumechangiwa na hofu kubwa
baada ya kuwepo kwa askari wengi katika vituo vya kupigia kura.
‘’Wingi wa askari wenye silaha za moto katika vituo vya kupigia kura umechangia kufanya baadhi ya wananchi kutojitokeza kwa hofu ya askari hao’’alisema Kibamba..
Wafuasi wa Chadema watekwa, wapigwa
Matukio ya kutekwa na kupigwa kwa wafuasi wa Chadema, yalijiri katika uchaguzi huo jana. Vijana wanaoaminika kuwa ni wa CCM, wakiwa ndani ya gari aina ya Landcruizer ambayo iliyoegeshwa kwenye uwanja wa AICC wa Soweto waliwakamata na kuwapiga baadhi ya wananchi waliokuwa wakielekea katika vituo vya kupigia kura eneo la Soweto.

Msimamizi wa uchaguzi wa kata hiyo, Anna Lebisa alikiri kuliona gari hilo majira ya saa tatu asubuhi ambapo aliwaelekeza polisi waliokuwa kwenye kituo hicho kuwafatilia lakini waliondoka kabla hawajakamatwa.
Aidha mwananchi mwingine, Hassan Noor ambaye alikuwa wakala wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye kituo cha AICC Nursery alishindwa kufanya kazi hiyo baada ya kunyang’anywa barua yake na vijana waliokuwa kwenye gari aina ya Landcruizer ya rangi ya maziwa ambayo namba zake hakuzishika.
Akiongozana na wenzake wawili kwenye mzunguko karibu na kituo hicho cha kupigia kura, Noor aliona gari hilo likisimama karibu yao na kuwataka waondoke eneo hilo ambapo aliwaeleza kuwa wao ni mawakala, ndipo walipomtaka awaonyeshe barua.
“Nilijua
ni askari, na nilipowapa wakaninyang’anya na kuichana. Alafu wakampiga mwenzangu Boniface Kimaro alipigwa
na kitu kama chuma kichwani na wakaondoka. tumeripoti kituo cha kati cha polisi”
alisema.
Katika
kata ya Kimandolu watu 6 walikamatwa wakiwa wamekaa katika gari moja na kupelekwa
polisi kwa mahojiano, hali hiyo ikajitokeza tena katika Kata ya Kaloleni pia,
ambako watu wasiojulikana walikamatwa wakiwa wamejificha ndani ya gari .
Ulinzi
mkali wa polisi
KAMANDA wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatusi Sabas jana aliongoza kazi ya ulinzi uliokuwa na idadi kubwa ya askari polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi.
Kamanda Sabas akitumia gari aina ya Toyota Land Crueser
TP 1715 alionekana akizunguka katika mitaa ya kata zote nne, zilizokuwa
zimesheheni idadi kubwa ya askari wengi
kutoka mkoani Kilimanjaro.
Washuhudiwa
na waangalizi wa kimataifa
Katika tukio la kwanza la kihistoria, uchaguzi wa
kata hizo, ulishuhudiwa na waangalizi wa kimataifa kutoka taasisi ya
Internationa Low and Policy Institute yenye makao makuu yake nchini Norway, na
wale wa ndani kutoka jukwaa la Katiba.
Kiongozi wa waangalizi kutoka Norway Sterling Roop,
akiongea na Tanzania Daima alisema kuwa idadi ndogo ya wapiga kura imejitokeza na
uwepo wa dosari kadhaa umewafanya baadhi ya wananchi kukosa haki yao ya kupiga
kura.
Roop alisema pamoja na wananchi kuwa na shahada halali ya kupigia kura na majina yao kuwepo, lakini hakukuwa na picha zao katika daftari la wapiga kura na hivyo, wakazuiwa kupiga kura. Katika vituo vingi hususani kata ya Kaloleni dosari kuu ilikuwa ni kukosekana kwa majina katika daftari la kupiga kura kwa wananchi ambao wana shahada na pia majina yao kubandikwa katika ofisi za kata kama wapiga kura halali.
Mwigulu Nchemba atimua
matokeo hayo ambayo yameonekana kuwasononesha viongozi na wanachama wa CCM, yalimfanya Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba, kuondoka kimya kimya jijini hapa kwa kutumia gari maalum.

Nchemba ambaye aliongoza kikosi cha CCM katika
kampeni za kimya kimya, majira ya jioni alionekana akielekea Moshi, huku
wasaidizi wake wakiwemo wabunge wakitoweka katika vituo vya kuhesabia kura.
Mapema, wabunge wa Chadema na wa CCM tangu asubuhi walikuwa wakizunguka katika kata
hizo, huku mbunge wa viti maalum (ccm) Catherin Mgige akitumia gari ndogo salon
yenye vioo vya giza alionekana akizunguka kata zote jana.
Chadema iliamua kumweka kila mbunge kusimamia katika
kata ambapo Godbles Lema alikuwa kata ya
Elerai, Joshua Nasari na Jamesi Milya, Kaloleni huku Alfonce Mwazo aliyekua
diwani wa Sombetini ccm kabla ya kuhamia Chadema akisimamia Kimandolu.
No comments:
Post a Comment