Kufa
na kupona leo Arusha
*Mkuu
wa mkoa, Polisi wapigwa ‘stop’
*
Ujumbe mzito Tume ya Uchaguzi watua
David Frank na Ramadhani Siwayombe, Arusha
Uchaguzi mdogo wa Madiwani katika Kata nne za
Halmashauri ya Jiji la Arusha unafanyika leo huku Tume ya Taifa ya uchaguzi
[NEC] ikiwapiga marufuku Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo na Kamanda wa
polisi wa mkoa na jeshi la kutojihusisha na usimamizi wa uchaguzi huo.
Ujumbe mzito wa watendaji wakuu na Maafisa wa tume
ya Taifa ya Uchaguzi ukiongozwa na
Mwenyekiti wake, jaji mstaafu Damian Lubuva ‘wamehamia” jijini hapa kwa ajili
ya kuratibu mwenendo mzima wa uchaguzi huo uliotawaliwa na hofu ya kutokea tena
kwa vurugu.
Msafara
wa viongozi hao wa tume toka makao makuu jijini Dar es Salaam umezua
sintofahamu miongoni mwa wananchi wakiwemo waandishi wa habari waliohudhuria
mkutano wa maandalizi ya uchaguzi huo.
Akizungumzia
hatua hiyo na msimamo wa tume yake, Jaji Lubuva alisema watendaji hao wa
serikali hawana mamlaka ya kusimamia uchaguzi huo, isipokuwa tume yenyewe tu.
Amedai
kuwa wameamua kuweka ‘kambi’ ya muda katika uchaguzi huo kwa kuwa mkoa wa
Arusha umekuwa historia haswa kufuatia tuko la mlipuko wa bomu uliotokea wakati
wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa Chadema eneo la Soweto ambapo watu wanne
walifariki na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.
“Tumekuja
hapa kwani tukio hilo limeacha historia kwani halijawahi kutoka hapa nchini
hivyo tupo kufuatilia kwa karibu mwenendo mzima wa uchaguzi… na zaidi tutatoa
ushauri utakapohitajika’ alisema.
Mbali
na jaji Lubuva, wengine waliowasili jijini hapa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti
Hamid Mohamed Hamid na Mkurugenzi wa Uchaguzi Julius Malaba, na maafisa wengine
wapatao kumi.
Jaji
Lukuva akizungumzia Maandalizi ya Uchaguzi na kusema yamekamilika na kuwaomba
wananchi kushiriki uchaguzi huo bila hofu kwani usalama umeimarishwa na kutoa
onyo kwa baadhi ya watu kutowazuia wanaokwenda kutumia haki yao ya kikatiba.
Alisema
vituo vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa waa 10:00 jioni na kuongeza
kwamba idadi ya wapiga kura ni 60, 123 katika Kata zote zitakapofanyika
uchaguzi huo za Kaloleni, Themi, Elerai na Kimandolu .
Vituo
vilivyotengwa kwa ajili ya kupiga kura ni 136 ambapo Kaloleni ina vituo 27,
Elerai 56, Kimandolu 39 na Themi ina vituo 15 katika uchaguzi huo unasubiriwa kwa hamu.
Alisisitiza
kuwa watakaoruhusiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura ni wasimamizi wa
uchaguzi ,makarani,wapiga kura mjumbe wa tume kwa kibali maalum,askari polisi
na wakala wa chama.
Alisema kuwa karatasi za kupigia kura zimebadilishwa rangi kutoka zile zilizoandaliwa awali katika uchaguzi ulioahirishwa kutokana na hofu ya udanganyifu katika kura.
Alisema kuwa karatasi za kupigia kura zimebadilishwa rangi kutoka zile zilizoandaliwa awali katika uchaguzi ulioahirishwa kutokana na hofu ya udanganyifu katika kura.
Wagombea
udiwani katika Kata ya Kaloleni waliopitishwa na vyama vyao kwenye mabano ni
pamoja na Emmanuel Milliani (CCM) Kessy Lewi (Chadema), Ngilisho Paulo
(Democrasia Makini) na Darwesh Mkindi (CUF).
Katika
Kata ya Kimandolu ina wagombea wawili tu ambao ni Edna Saul (CCM) na Rayson
Ngowi (Chadema) ambapo katika Kata ya Themi wagombea ni Malance Kinabo
(Chadema), Victor Mkolwe (CCM) na Lebora Ndarvoi (CUF).
Uchaguzi
katika Kata ya Elerai unawajumuisha wagombea ambao ni pamoja na John Bayo
(CUF), Injinia Jeramia Mpinga (Chadema),
Emmanuel Laizer (CCM), na Boidefi
Shirima (TLP)
Chadema
yaonya
Wakati huohuo chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] kanda ya Kaskazini kimewataka viongozi wa kimila la kimasai (Laigwanan) kutokubali kutumiwa na wanasiasa kuvuruga nchi.
Wakati huohuo chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] kanda ya Kaskazini kimewataka viongozi wa kimila la kimasai (Laigwanan) kutokubali kutumiwa na wanasiasa kuvuruga nchi.
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini Israel
Natse alisema viongozi hao wasikubali kutumiwa na wanasiasa kwa malengo ya
kisiasa na kuharibu heshima yao katika jamii
ambayo ni kubwa .
‘’Sisi kama Chadema hatuna ugomvi na viongozi hao wa kimila, bali tuna ugomvi na viongozi wa chama tawala’ alisema
ambayo ni kubwa .
‘’Sisi kama Chadema hatuna ugomvi na viongozi hao wa kimila, bali tuna ugomvi na viongozi wa chama tawala’ alisema
Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema aliwataka wwa Arusha kujitokeza kupiga kura na wao kama chama wamejipanga vyema kulinda kura zao.
‘’Tumejipanga vyema kulinda kura zetu na nawaomba wana chadema wawe watulivu kesho (leo) hata kama watapata msukosuko wawe wavumilivu lakini ikifikia hatua ya manyanyaso kupindukia wamuombe Mungu awaongoze katika maamuzi’’alisema Lema.
No comments:
Post a Comment