Polisi wakamia
Chadema, waihofia CCM
Na
Mwandishi Wetu
WAKATI
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Said Mwema leo anakutana na waandishi wa habari
kuzungumzia suala la vyama vya siasa kuwa na vikundi vya ulinzi, baada ya
msimamo wa Chadema wa kuendelea na hatua yake ya kuimarisha chama chao kwa
ajili ya mafunzo ya kujilinda, Jeshi limeendelea kuwa kimya kuhusiana na Chama
Cha Mapinduzi kumiliki kikundi cha vijana cha Green gurad.
Badala
yake polisi wameendelea kukikamia na kutoa vitisho zaidi kwa chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhusiana na jambo kama hilo.
Tangu
kutolewa kwa tamko la Chadema kutaka kuendesha mafunzo kwa vijana wake wa Red
Briged, Polisi wameendelea kusisitiza kuwachukulia hatua kali za kisheria
vbiongozi wa juu wa chama hicho kutokana na kile walichosema kuunda kikosi cha
kijeshi kinyume na sheria.
Juzi
msemaji wa polisi, Advera Senso aliweka wazi kuwa wiki hii watachukua hatua
kali za kisheria dhidi ya viongozi wa Chadema na kuwaonya vijana kote nchini, kukataa
kutumiwa na wanasiasa waliodaiwa kutaka kuhatarisha amani ya nchi.
Mbali
na polisi, mamlaka nyingine zilizokemea uamuzi wa Chadema ni pamoja na Rais
Jakaya Kikwete, ambaye alisema kinachotaka kufanywa na Chadema kimelenga
kuhatarisha amani. Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia naye juzi
alikaririwa akiishambulia Chadema kwa uamuzi huo aliyouita ni wa hatari.
Hata
hivyo, kwa makusudi ama kwa lengo la kukana ukweli, jeshi la polisi limekuwa
likikwepa mara zote kugusia kuhusiana na CCM kumiliki kikosi Green Guard,
ambacho baada ya kubanwa na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa UVCCM Martin
Shigela alikiri wiki iliyopitai kuwa kipo na kinafanya kazi ya kulinda usalama
wa viongozi na wanachama katika shughuli zao.
Kadhalika,
jeshi hilo limeonekana kupuuza na kutotaka kuzifanyia kazi taarifa za matukio
mabaya ya kupiga, kuteka na kujeruhi yaliyofanywa na Green Guard dhidi ya
viongozi na wanachama wa Chadema. Hadi sasa sio IGP Mwema, ama afisa yeyote wa
ngazi ya juu wa polisi aliyetamka waziwazi kuikemea CCM kama wanavyofanya kwa
Chadema.
Chadema
kimeripoti katika jeshi la polisi, matukio ya kikatili walivyofanyiwa na vijana
hao wa ccm katika mikoa ya Tabora, Dar es Salaam, Mwanza, Iringa, yakiwemo
mauaji ya Kada wake wa Arumeru mkoani Arusha.
Msimamo wa
Chadema
Kwa
upande wake, Chadema kimezidi kumtaka IGP Mwema kuweka wazi sababu za msingi
zinazomfanya hadi sasa apate kigugumizi na kushindwa kutamka ikiwa ni halali
kwa CCM kumiliki kikosi cha vijana kwa ajili ya ulinzi wao, lakini iwe nongwa
na dhambi kubwa kwa vyama vingine vya siasa.
Taarifa
ya Chadema kwa vyombo vya habari jana imelishutumu jeshi la polisi kwa
kushindwa kwake, kuichukulia hatua CCM ambacho kwa miaka mingi kimehodhi kikosi
hicho cha vijana ambacho wamedai kimehusika na matukio mengi ya kikatili.
“Jeshi
la Polisi wameshindwa kutoa kauli kwa CCM kumiliki kikundi cha ulinzi, ambacho
kimekuwa kikifanya mazoezi ya kijeshi kama kule Igunga, kikituhumiwa
kushambulia, kupiga, kuteka na kutesa wapinzani wa CCM.
“Kwa
mfano, wabunge Kiwia (Hainess) na Machemli (Salvatory) walishambuliwa Kirumba,
Peter Msigwa, akashambuliwa iringa, Mbwana Masoud akapigwa Igunga, na marehemu
Msafiri Mbwambo ambaye waliyomuua walitoroka mbele ya polisi wenye silaha
mahakamani” imesema taarifa ya Chadema.
Aidha, kimesema kuwa hadi sasa hakuna ripoti ya
kutekwa na kuteswa kwa Dk Stephen Ulimboka, Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri Absalon Kibanda, ukweli wa
waliolipua bomu Kanisa Katoliki la Olasiti na katika mkutano wa Chadema Soweto
mjini Arusha.
Chadema wamezidi kuongeza kuwa Green Gurad
wameshutumiwa pia kuwashambulia waandishi wa habari nchini, na kuwataja
waliofikwa na vipigo hivyo kuwa ni Frederick Katulanda wa Mwananchi, mwaka 2010
katika uchaguzi mkuu huko Kwimba, Munir Zakaria wa Channel Ten huko bububu
Zanzibar na Musa Mkama wa Dira katika uchaguzi mdogo wa Igunga.
No comments:
Post a Comment