Makambi ya mafunzo kwa 'Green
Guards' wa CCM yavunjwe - Dr Slaa
Katibu
Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amelitaka jeshi la polisi kuvunja mara moja
makambi yote ya CCM nchini yanayotoa mafunzo kwa vijana wanaoitwa Green Guards.Kiongozi huyo alikuwa akizungumzia vitisho vya jeshi hilo dhidi ya CHADEMA baada ya chama hicho kuamua kuandaa mafunzo ya ukakamavu kwa vijana wake yenye lengo la kulinda viongozi na mali za chama.
Dr Slaa amelitaka jeshi hilo kuvunja makambi ya CCM yaliyowekwa kote nchini ambapo vijana wa Green Guards wamekuwa wakipewa mafunzo ya namna ya kupambana na CHADEMA kwa kuwateka na kuwakata mapanga kama walivyowakata mapanga wabunge wa CHADEMA Highnes Kiwia na Joshua Nassari.
Kiongozi huyo ambaye ni tishio kuu kwa utawala wa CCM amesema matendo yote haramu yanayofanywa na kikundi hicho cha Green Guards yamekuwa yakiripotiwa polisi lakini hatua zozote hazichukuliwi.
Tamko la CHADEMA kuwafundisha vijana wake ukakamavu kukabiliana na vitendo haramu vya Green Guards limeonekana kutikisa jeshi la polisi lakini cha kushangaza wametoa vitisho kwa CHADEMA na kufyata mkia kwa kikundi cha Green Guards.
No comments:
Post a Comment