Pinda ametoa agizo hilo jana, ikiwa ni siku
chache tangu Waziri Magufuli alipoweka msimamo na kuagiza wasafirishaji
watakaokaidi agizo la kulipa asilimnia tano ya uzito unaozidi kwa mujibu wa
kanuni namba 7 (3) ya Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 2001, wasiingize
magari yao barabarani.
Hata hivyo, agizo la Magufuli limezua mtafaruku
mkubwa, baada ya karibu wasafirishaji wote nchini kusimamisha shughuli zao,
kiasi cha kuzusha hofu ya kuanguka kwa uchumi nchini. Hadi sasa kiasi kikubwa
cha mizigo kimekwama bandarini na sehemu nyingi za nchi kufuatia mgomo huo.
Pinda, katika agizo hilo ambalo limepokelewa kwa
shangwe kubwa, alisema mwaka 2006 aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Basil Mramba
aliandika waraka wenye kumbukumbu namba CKA/16/419/01Julai 19/2006 ambao iliyotoa
msamaha wa tozo ya magari kwa uzito uliozidi asilimia tano ya uzito
unaokubalika kisheria.
amewataka watendaji wa serikali kuhakikisha
wanawashirikisha wadau kila wanapotaka kufanya mabadiliko ya jambo fulani kwa
manufaa ya nchi na kuepusha ghasia na migogoro isiyo ya lazima.
“Mramba alizingatia maombi ya wadau wa usafiri,
ingawa ni kinyume cha sheria. Naye alifanya kwa nia njema,” alisema Pinda na
kuongeza kuwa sheria anayoikazania Magufuli haitekelezeki kirahisi kutokana na
hali halisi ya barabara zetu na mizani kulalamikiwa kuwa na matatizo katika
upimaji hivyo kutaka wadau hao kupewa muda kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa
sheria hiyo.
“Baada ya kelele hizi niliamua kukutana na Waziri
Uchukuzi, Ujenzi, Wakala wa Barabara (Tanroads) na watendaji wa Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu kwa ufafanuzi zaidi wa kisheria, na nikakutana na wadau wa
usafirishaji TATOA na TABOA katika kikao hicho nao walisema yao nikawaelewa.
Nikaona tatizo ni utekelezaji wa sheria yenyewe,” alisema.
No comments:
Post a Comment