Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!

JAJI warioba; TUACHENI



Jaji Warioba: ‘Tuacheni’

Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba, amewacharukia watu wanaoanza kuisakama tume yake na wenye mipango ya kutaka kuingilia utendaji kazi wa tume yake, wakae pembeni na kuwaacha huru.

Jaji Warioba alitoa onyo hilo jana wakati wakikabidhiwa rasmi jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, mkabala na Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, litakalotumiwa kwa kazi ya tume hiyo

Mwenyekiti huyo alisema, taasisi zilizowapendekeza wajumbe waliofanikiwa kuteuliwa katika tume yake, zisijaribu kuingilia kazi zao, wala kuwapa shinikizo wajumbe wake ili kulazimisha watende wanayotaka.

“Ninaomba kwa dhati kabisa wale waliopendekeza watuache tufanye kazi. Tumepewa kazi na nchi, watuache tufanye bila presha yoyote. Na wale wanaosema tuna mtu wetu kule, hawana mtu wao, bali watanzania wana watu wao hapa,” alisema Warioba.

Warioba alisema kwa kuwa jukumu la tume yake ni zito na nyeti, watajitahidi kufanya kazi kwa uwezo wake wote ili watekeleze yale waliyokabidhiwa na rais kwa niaba ya watanzania wote.

Alisema watapanga ratiba kamilifu kuhakikisha wanakuwa na utaratibu utakaowawezesha kuwafikia wananchi wengi.

Alisema watatoa nafasi ya kutosha kwa kila mwananchi wakitambua kuwa wana hoja zao kuhusu uzuri na upungufu wa katiba ya sasa, na wataomba mapendekezo ili iandikwe katiba itakayokidhi matakwa ya taifa.

Naye, Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani alisema kuwa, ushirikishaji wa wananchi katika ujenzi wa katiba ni jambo muhimu na la lazima katika kupata katiba inayokubalika na walio wengi.

“Wanazuoni wanatufundisha kuwa mamlaka ya taifa lolote yapo mikononi mwa wananchi wa taifa hilo na inapohitajika kujenga katiba basi ni lazima wananchi hao washirikishwe katika mchakato mzima kwa kutoa maoni na hatimaye kuihalalisha katiba ya taifa lao,” alisema.

Alisema, kufanikiwa kwa mchakato huo kutategemea zaidi uelewa wa wananchi wa katiba yetu ya sasa ya mwaka 1977, kwani ni ukweli usiopingika kuwa wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu katiba ya nchi yao.

Alikiri kuwa, kiwango kidogo cha uchapishaji na ukosefu wa utamaduni wa kusoma miongoni mwa wananchi, ndiyo sababu ya uelewa mdogo  wa wananchi kuhusu katiba.

Alisema, serikali imewapatia mahali pazuri pakufanyia kazi na vifaa vipya vya ofisi, pia inakamilisha ununuzi wa magari mapya kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo.

Kombani alisema, serikali itaendelea kutenga fedha za kutosha katika bajeti ili tume iendeshe mchakato huo kwa ufanisi na uharaka kwa kadri itakavyokuwa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema kuwa, Rais Jakaya Kikwete amemwagiza wafanye kila liwezekanalo kuiwezesha tume ifanye kazi yake katika mazingira stahiki, kwa uhuru, utulivu, salama na amani.

Alisema katika kufanya maandalizi hayo serikali ilizingatia uhuru na utulivu wa kufanya kazi, ulinzi na usalama, utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka, mawasiliano, bajeti ya tume na usafiri wa wajumbe.

Pia, vitendea kazi muhimu, umeme, watumishi na nyumba kwa wajumbe wote walio nje ya  mkoa wa Dar es Salaam, ambazo zitakuwa na samani.

mwisho

Magufuli, Mkulo watishana
·      Wagombea fedha za barabara

Ratifa Baranyikwa na Datus Boniface

HALI ya utendaji kazi ndani ya Baraza la mawaziri imeendelea kuwa tete baada ya mmoja wa mawaziri waandamizi kumpa mwenzake muda wa siku saba kutekeleza matakwa yake, vinginevyo watafikishana mbali.

Akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi, na daraja lililopo eneo la Tangibovu jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, alimshambulia hadharani Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo na kutishia kumshitaki kwa Rais Kikwete ikiwa hataruhusu kutolewa kwa vifaa vya ujenzi mali ya kampuni ya Strabag ya Ujeruman vilivyozuiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA)

Lakini Waziri Mkulo aliiponda kauli ya waziri Magufuli, akidai kuwa amekwenda kinyume na utaratibu wa kazi kwa kutishana kupitia magazetini, na kwamba namna pekee ilikuwa kufuata taratibu.

Akizidi kuishutumu wizara ya fedha, Magufuli alidai kuwa hawezi kubebeshwa lawama za kuchelewa kwa ujenzi wa barabara hiyo, na hatakubali kuadhibiwa kwa uzembe na makosa ya watendaji wengine wa serikali.

Kauli ya Magufuli ilikuja baada ya kukuta kazi za ujenzi zimesimama, na ndipo Meneja wa Kampuni hiyo ya ujenzi, Frank Rohde akamweleza kuwa kuna vifaa yakiwemo Makatapila vimezuiliwa kwenye bandari ya Dar es Salaam, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo Fedha.


No comments:

Post a Comment