Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!

Kiwia afanyiwa upasuaji India




Hellen Ngoromera,Dar na Danson Kaijage, Dodoma

MBUNGE wa Jimbo la Ilemela Highness Kiwia(CHADEMA),amefanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa katika hospitali ya Apollo nchini India, Alhamisi iliyopita.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa Masuala ya Bunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)John Mrema alisema kutokana na upasuaji huo, hali ya mbunge huyo inaendelea vizuri.
“Mheshimiwa Kiwia alishafanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa tangu Alhamisi ya wiki iliyopita na kwa sasa anaendelea vizuri,” alisema Mrema.
Alipoulizwa kuhusu kureja nchini Mrema alisema ni mapema mno kueleza kwani hivi sasa anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
“Kuhusu kurejea lini nchini madaktari ndio watakaojua kwani kwa sasa anaendelea kuangaliwa pamoja na kufanyishwa mazoezi,” alisema Mrema.
Kiwia na mbunge mwenzake wa chama hicho, Salvatory Machemuli wa Jimbo la Ukerewe walijeruhiwa vibaya kwa mapanga na shoka na watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) katika eneo la Ibanda Kabuhoro mjini Mwanza.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Aprili mosi mwaka huu baada ya wabunge hao kudaiwa kuvamiwa na watu hao.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow aliwataja wengine walioshambuliwa kuwa ni Ahmed Waziri ambaye inasemekana kuwa ni kada wa UVCCM aliyekatwa kiganja chake cha mkono wa kulia.

Wengine ni Haji Mkweda (21), ambaye alijeruhiwa mguu wa kulia, Judhith Madaraka (26), aliyechomwa kisu kwenye titi lake la kushoto na mkono wa kushoto, Ivory Mchimba (26), aliyejeruhiwa kichwani na mdomoni.

Majeruhi wote ukiondoa wabunge hao na Waziri, wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure.

Awali, wabunge hao walilazwa katika Hospitali ya Rafaa Bugando lakini baadaye walisafirishwa kwa ndege kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam na baada ya siku kadhaa mbunge  Kiwia alihamishiwa katika hospitali ya Appolo, India.


UDOM wamshinikiza Kikwete
Kutoka Dodoma wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma ambao ni makamanda wa Chadema wamemtaka Rais kutoa kauli juu ya kupigwa na hata mauaji yanayoendelea dhidi ya viongozi wa upinzani nchini. 
Wakizungumza na Tanzania Daima jana, wanafunzi hao walisema kuwa inasikitisha kuona serikali ikiwa kimya juu ya kushambuliwa kwa viongozi na mauaji ya makamanda wa Chadema, huku jeshi la polisi likiwa halionyeshi juhudi zozote za kupambana na hali hiyo. 
“Tunamtaka  Rais Kikwete atoe tamko la mauaji hayo kwani yamekuwa yakiwahusisha wafuasi wa CCM jambo hilo linasababisha watu kuwa na hasira huku wakijiuliza ni kwanini serikali inaonekana kuwa kimya
“Tunajua zimetumika mbinu mbalimbali za kudhoofisha nguvu ya vyama vya upinzani hususan Chadema na sasa imefikia hatua ya kuwahua makamanda wa Chadema na wengine kutishiwa maisha jambo ambali ni hatari kwa taifa” alisema Mwenyekiti Mstaafu wa chadema katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), Robert Edwini.
Mbali na hilo wanafunzi hao wamesema kitendo cha CCM kuanzisha Mkoa Maalum kwa wanafunzi wa elimu ya juu ni ukiukwaji wa taratibu na sheria ya uendeshji wa siasa vyuoni.
Mwenyekiti mstaafu wa Chadema Chuo Kikuu cha Dodoma, Robert Edwin, alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa sheria ya kutoendesha siasa vyuoni lakini CCM kimekiuka sheria hiyo.
“Inasikitisha kuona kuwa chama cha Mapinduzi kimekuwa kikikinzana na kauli zake, maana awali walidai kutokufanya siasa vyuoni na wakati mwingi wana siasa wa chadema wamekuwa wakipewa adhabu hata kwa kuonekana wamevaa kombati chuoni..
“Lakini juzi CCM waliingiza basi la Shabiby pamoja na la chuo likiwa na bendera ya CCM kwa ajili ya kuwachukua wanachuo ambao ni wafuasi wao kwenda makao makuu kuzindua Blog ya chama” alisema.
Mbali na hili alidai  kitendo cha kunchagua Christopher Ngubiagai kuwa Katibu wa mkoa maalumu wa wanafunzi wa elimu ya juu na kuingia moja kwa moja katika NEC ni dalili za kutoa mwanya kwa wanavyuo wa kada ya CCM kufanya siasa vyuoni huku vyama vingine vya siasa vikinyimwa uhuru huo.
“Nataka niseme kuwa kama CCM wanaamua kutoa mianya ya kuendesha siasa vyuoni ni bora wakawa wazi ili vyama vingine vya siasa vipate nafasi ya kuendesha siasa na kufanya hivyo itaonekana kuwa hiyo ndiyo demokrasia ya kweli, alisema

Mwisho.



No comments:

Post a Comment