Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!

MTOTO ANAOMBA MSAADA WAKO HARAKA


 Huyu ni mtoto RUKIA AMBAYE AMEUNGUA KWA MAJI YA MOTO



Ndugu zangu kwa heshima kubwa na upendo, naomba msaada wenu wa hali na mali kumchangia mtoto Rukia ambaye ameungua vibaya mwilini kwa maji ya moto, na kwa bahari mbaya wazazi wake hawana uwezo wa kugharimia matibabu. Waweza kutumia mchango wako kupitia kwangu kwa namba 0756-219342, au 0713235593 (Charles Misango- Mhariri Tanzania Daima) nami nitaziwasilisha kwa wazazi wake ili waweze kusaidia kumkimbiza Muhimbili kwa matibabu mazito. ASANTE KWA WOTE MLIO TAYARI. TUJITOE KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYU


Mtoto huyo na wazazi wake wanaishi wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi. Leo Juni 4, kwa fedha chache zilizopatikana, mtoto amepelekwa zahanati ya kijiji cha jirani kupata matibabu madogo chini ya usimamizi wa msamalia mwema

2 comments:

  1. asanteni sana wale wote ambao hadi sasa mmechangia kwa hali na mali matibabu ya mtoto Rukia. Hadi jioni hii, nimepata jumla ya sh 155,000 kutoka kwa watu 10 na kwamba jitihada zimefanyika za kumpeleka mtoto huyo katika hospitali ya Nyangao mkoani Lindi ambako amelazwa na anaendelea na matibabu chini ya usimamizi wa ndugu Victor na Abdulazizi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwanza samahani sana kwa ukimya wa muda mrefu. Hii ilitokana na kutokea kwa matatizo ya kiufundi katika Blog yangu, na hasa baada ya watu wenye nia mbaya kubaini pass yangu, na hivyo kulazimika kuisitisha kwa muda.

      Napenda kuwafahamisha kuwa, mtoto huyo Rukia alifariki wiki mbili zilizopita kutoka na ugonjwa wa malaria. Hadi anafikwa na mauti, alikuwa akiendelea vema na matibabu ya majeraha yake ya moto, na kwa kweli yalikuwa ni maumizi makubwa kwetu.
      Tunaandaa taarifa rasmi kwa kila mmoja na tutachapa kaadri tuwezavyo mapato na matumizi.

      Delete