Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!

WAANDISHI WA HABARI WAMTIMUA WAZIRI NCHIMBI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, leo asubuhi ameonja joto ya jiwe baada ya kutimuliwa na waandishi wa habari, waliokuwa katika maandamano ya amani kupinga na kulaani mauaji ya Mwandishi wa kituo cha luninga cha Channel 10, Daud Mwangosi.

Nchimbi, aliwasili katika viwanja vya jangwani ghafla na bila kualikwa na wanahabari, na kupanda juu moja kwa moja katika jukwaa la muda la udongo, na hivyo kuonekana kana kwamba ndiye aliyepokea maandamano hayo.

Kitendo hicho, kilionekana kuwachefua waandishi na ndipo kelele za kumtaka aondoke, zilipoanza na kupasua anga. Mwandishi mkongwe na wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheele, alilazimika kupanda naye juu na kuhoji uhalali wa waziri Nchimbi kuwepo katika maandamano hayo, huku ikijulikana kuwa  wizara yake ndiyo inayohusika na mauaji hayo.

Kutokana na kelele hizo, kiongozi wa ratiba za maandamano hayo, Charles Misango, alilazimika kutuliza hasira za waandishi bila mafanikio, na ikalazimu kumwomba waziri Nchimbi aweze kukubaliana na ukweli wa kutotakiwa katika eneo hilo, hivyo aondoke.

Waziri Nchimbi alilazimika kukubaliana na hali hiyo, na kuondoka huku akiwa anasindikizwa na kelele za 'ondoka' ondoka'ondoka

No comments:

Post a Comment