Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!

JELA KWA KUMNYANG'ANYA FEDHA MAMA YAKE



 
KIJANA mmoja Athuman Peter kwa jina maarufu mzee wa Genya (26), mkazi wa mtaa wa Nyamakokoto, mjini Bunda, mkoani Mara, aliyemnyang'anya sh. laki moja na simu moja ya mkononi mama yake mzazi kwa kutumia silaha, amehukumiwa na mahakama ya wilaya ya Bunda, kutumikia kifungo cha miaka 30 jela.

Hukumu hiyo imetolewa jana na hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya ya Bunda Said Hamad Kasonso, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakani hapo na upande wa mashitaka.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi, Masoud Mohamed kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo novemba 18 mwaka jana majira ya saa 1:30 jioni, katika mtaa wa Nyamakokoto, mjini Bunda.

Mohamed alisema kuwa siku ya tukio mshitakiwa huyo alimvamia mama yake mzazi aitwaye Pendo Mgasa, aliyekuwa nyumbani kwake na kumnyang'anya fedha tasilimu sh. laki moja, pamoja na simu moja ya mkononi aina ya Nokia yenye thamani ya sh. 20,000.

Alisema kuwa katika kufanya unyang'anyi huo mshitakiwa huyo alitumia panga alilokuwa nalo, akimtishia kumuua mama yake mzazi kwamba iwapo akikatalia fedha hizo au kufanya lolote atamutoa uhai wake kwa kumkata na panga hilo.

Akitoa hukumu hiyo hakimu Kasonso alisema kuwa ameridhika pasipo kuacha shaka yoyote juu ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na kwamba kwa jinsi hiyo anamtia hatihani mshitakiwa huyo kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela.

Alisema kuwa kitendo alichokifanya mshitakiwa huyo ni cha kinyama hasa kwa kumfanyia mama yake mzazi na kuongeza kuwa adhabu hiyo itakuwa fundisho kwake na kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo ya kutaka kujipatia fedha na mali kwa njia za unyang'anyi.

Hata hivyo mshitakiwa huyo alipotakiwa kujitetea alishindwa kufanya hivyo na badala yake alibaki kimya bila kusema lolote.

Mwisho




No comments:

Post a Comment