Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!

ZITTO AIRARUA SERIKALI MABILIONI YA USWISI




Wakati shinikizo la Dunia sasa limeelekea kumaliza tatizo la ukwepaji kodi na Utoroshaji wa fedha kutoka nchi za Kiafrika, serikali ya Tanzania imekuwa ikusuasua kuchukua hatua za haraka kupambana na hali hiyo

Imedaiwa kuwa, Tanzania imekuwa ikishindwa kutumia njia bora ya mfumo wa kupashana taartifa (automatic exchange of tax information) ambao unasaidia kupata taarifa za makampuni makubwa ya kimataifa(MNCs) yanayokwepa kodi.

Hayo yameelezwa na Waziri Kivuli wa Fedha Zitto Kabwe jana kutoka Geneva, ambaye alisema kutokana na shinikizo la nchi mbalimbali, hivi sasa nchi zinazoitwa "secrecy jurisdictions" (tax havens) Zimeanza kuweka sahihi makubaliano ya kutoa taarifa. Tanzania mpaka sasa haijaweka sahihi na serikali haijatoa taarifa yeyote kwa Umma.

Alisema nchi za Ghana, Afrika Kusini na Nigeria nchi zinazotegemea sana rasilimali kama Tanzania zimeweka saini mkataba huu tayari. Asilimia 44 ya fedha za kigeni nchini zinatokana na mauzo ya madini nje. Makampuni ya madini ndio yanaongoza kukwepa kodi.

“Tanzania inapoteza jumla ya dola za kimarekani kati ya milioni 500 na bilioni 1.25 kwa mwaka kutokana na Makampuni makubwa ya kimataifa kukwepa kodi. Hii ni sawa na kusema Tanzania inapoteza dola takribani milioni mbili kila siku kwa uporaji huu.

“Naitaka serikali kutoa taarifa kwa nini haichuki hatua kuzuia mwanya huu wa mapato ya Umma. Serikali ichukue hatua mara moja kuhakikisha Tanzania inaingia makubaliano ya kupashana taarifa za kikodi. Huu sio wakati wa kuvuta miguu katika suala nyeti la umma. Badala ya kukimbilia kutoza kodi wanyonge, tuhakikishe makampuni makubwa yanayonyonya rasilimali zetu yanalipa kodi inayotakiwa’ alisema.

No comments:

Post a Comment