Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!

Kuhanga ashauri benki kukopesha wanafunzi vyuo vikuu



 MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambaye ni mstaafu, Nicholus Kuhanga amekiri kuwa upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaoanza vyuo vikuu nchini ni tatizo, hivyo alishauri Tanzania kuingia kwenye mpango wa kuwakopesha kwa kupitia benki.

Kuhanga alisema hayo alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima kuhusu suluhu kwa wanafunzi wanaohitaji mikopo ambao wamekidhi vigezo lakini hawakupata.

Alisema, njia mojawapo ni kuingia kwenye mpango huo wa benki kama nchi za wengine ili kuondoa mgongano uliojitokeza baina ya serikali na wanafunzi hao.

“Kwa kutumia mfumo huu wa benki nafikiri kila mmoja ataweza kunufaika mkopo huo, watakapomaliza watatumia vitambulisho vyao ili kuanza kuzirejesha,” alisema na kuongeza kuwa wale ambao watakuwa hawana vigezo vya kupata mkopo benki, ndio hao wasaidiwe na Bodi ya Mikopo Tanzania (HELBS).

Alisema kuwa, serikali haina fedha ya kutosheleza kumlipa kila mhitaji, japo wazo la kuanzisha bodi hiyo lilikuwa serikali isaidie kuongeza idadi ya wanaokwenda vyuo vikuu kutoka katika familia za wasiojiweza.

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa UDSM, alisema bodi ina bajeti kwa idadi fulani, hivyo wale ambao hawakupata sasa ni jukumu la wazazi, ndugu na jamii kuwasaidia.

mwisho

No comments:

Post a Comment