Social Icons

NDOA YANGU, Ningejua!

NDOA YANGU, Ningejua!

"Sitasitisha ruzuku kwa vyama vya siasa"



Msajili wa vyama vya siasa,Jaji Mutungi amekataa agizo la Mwenyekiti wa PAC,Zitto Kabwe la kumtaka kusitisha ruzuku kwa vyama vya siasa,
Zitto alitoa agizo hilo wiki iliyopita kufuatia madai yake kuwa hesabu za vyama karibu vyote hazijakaguliwa kwa takribani miaka mine sasa.
Hata hivyo, agizo hili limezua tafrani kubwa ambapo karibu vyama vyote vilivyotuhumiwa vimekana madai ya Zitto vikidai kuwa, hesabu zao zimekaguliwa kwa mujibu wa sheria na hivyo, hakuna sababu ya kunyimwa ruzuku.
Mutungi amesema hatafanya hvyo mpaka hapo atakapofahamu ni sababu gani iliyofanya mhusika wa kusimamia ukaguzi huo, ambaye ni Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)  hakufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment