WATUHUMIWA wa ujangili waliokamatwa hivi karibuni
katika Operesheni Tokomeza Ujangili mkoani Kilimanjaro, jana walifikishwa
mahakamani mjini hapa akiwamo Mohamed Hatiki, aliyekutwa na rundo la bunduki
na risasi.
Hatiki anadaiwa kumiliki bunduki sita bila leseni,
ambazo ni shotgun namba TZCAR86629, pistol glock namba RUW605, pistol
revolver namba TZCAR 59644, rifle 375 namba TZCAR93195, rifle 280 namba
TZCAR88522 na rifle 22 namba TZCAR37022.
Hatiki (26), mkazi wa Kata ya Bondeni, Manispaa ya
Moshi na Mohamed Sadiq wa Pasua walifikishwa juzi katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi, Sophia Massati, huku Sadiq akizirai akiwa kizimbani baada ya kupata
mshituko.
Hatiki, ambaye ni mshitakiwa wa kwanza anakabiliwa
na makosa 15 yanayoangukia chini ya sheria ya uhifadhi na uhujumu uchumi huku
katika shitaka la kwanza akidaiwa kupatikana na nyara za serikali ambazo ni
kwato mbili za kongoni zenye thamani ya sh milioni 1.04.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa
mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Omari Kibwana, akisaidiana na
mwendesha mashitaka kutoka Maliasili, Rusticus Mahundi, mshitakiwa huyo
anadaiwa kupatikana na nyara hizo Oktoba 23, mwaka huu, alfajiri katika Kata
ya Bondeni.
Shitaka la pili hadi la saba, mshitakiwa anadaiwa
kumiliki bunduki sita zilizotajwa hapo juu bila kuwa na leseni halali.
Shitaka la nane, Hatiki anadaiwa kupatikana na
risasi 23 za bunduki aina ya shotgun na katika shitaka la tisa anadaiwa
kupatikana na risasi saba za bunduki aina ya pistol glock yenye namba za
usajili RUW605 bila leseni.
Katika shitaka la kumi, Hatiki anadaiwa kupatikana
na risasi 56 za bunduki aina ya pistol revolver bila leseni, wakati shitaka
la 11 ni kupatikana na risasi nne za bunduki aina ya rifle 375 bila leseni.
Mshitakiwa huyo ambaye yupo nje kwa dhamana,
anashitakiwa pia kwa kosa la kukutwa na maganda ya risasi ya bunduki aina ya
rifle 375, risasi 15 za bunduki aina ya rifle 280, maganda 10 ya bunduki aina
ya rifle 280, na risasi 84 za bunduki aina ya rifle 22.
Naye mshitakiwa wa pili, Sadiq (67), anakabiliwa na
makosa tisa, likiwamo kumiliki silaha na risasi bila leseni, pamoja na
kukutwa na fuvu la nyati na mfupa wa tembo wenye thamani ya sh milioni 24.1
na tumbili hai mmoja Oktoba 22, mwaka huu, eneo la Pasua.
Silaha hizo ni rifle namba TZCAR 82048, rifle MK4,
rifle 22, risasi nne za silaha aina ya shotgun, 12 za bunduki aina ya rifle
303 na 11 za bunduki aina ya rifle 22.
Hata hivyo mshitakiwa huyo alishindwa kutimiza
masharti ya dhamana ya kuwa na watu wawili, mmoja aweke dhamana ya fedha
taslimu sh milioni 14, hivyo kurejeshwa rumande hadi Novemba 6, mwaka huu.
|
NDOA YANGU, Ningejua!
ABAMBWA NA SILAHA NA RISASI NYINGI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment